ATIKA SCHOOL
  • Start
    • SITEMAP
    • KNEC Portal
    • ZERAKI HELP AND SUPPORT
    • Academic Environment
    • KNEC KCSE PROJECT INSTRUCTIONS
  • BLOGS
    • About Us? >
      • Learn more about us
    • CUSTOMER CARE >
      • PRICING
      • Help & Support
    • News and Opinions
    • JOBS IN KENYA AND ABROAD FOR KENYANS AND BEYOND
    • How its Done
  • OUR PRODUCTS
    • All Categories >
      • MORE PRODUCTS >
        • SECONDARY CRE NOTES
        • COURSE BOOKS
        • KCSE KISWAHILI SETBOOKS
        • Backed Up Files and Archives
        • FREE DOCUMENTS
        • PRIMARY 8-4-4 BASED RESOURCES
        • STANDARD 8 RESOURCES
        • HIGH SCHOOL RESOURCES >
          • Biology Paper 3 Exams
          • Secondary Examinations
        • PRIMARY CBC BASED RESOURCES
        • COLLEGE & VARSITY RESOURCES
      • PRIMARY RESOURCES CBC
      • PRIMARY RESOURCES 8-4-4
      • SECONDARY RESOURCES
      • NOTES & TUTORIALS
      • COLLEGE RESOURCES
      • NOVELS and OTHER BOOKS
    • EXAMINATIONS >
      • MOCKS AND JOINT EXAMS >
        • FORM 1 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 2 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 3 EXAMINATIONS, QUESTION PAPERS AND ANSWERS
        • FORM 4 MOCKS PAST EXAMS BY REGION
        • TOP SECONDARY EXAMS ALL SUBJECTS
      • KPSEA NATIONAL EXAMS
      • KCPE >
        • KCPE PAST PAPERS AND ANSWERS >
          • KCPE 2020 RESULTS, REPORTS, QUESTIONS AND ANSWERS
          • KCPE PAST PAPERS 2019 REPORTS, RESULTS, QUESTIONS AND ANSWERS
        • KCPE PAST PAPERS PER SUBJECT
      • KCSE >
        • KCSE PAST PAPERS BY SUBJECT
        • KNEC KCSE PAST PAPERS, MARKING SCHEMES, QUESTIONS & ANSWERS
        • Free KCSE Past Papers Mathematics
        • Free KCSE Biology Questions and Answers
      • QUESTIONS & ANSWERS >
        • SECONDARY >
          • LANGUAGES >
            • Secondary English Questions and Answers
          • TECHNICALS >
            • COMPUTER STUDIES >
              • COMPUTER STUDIES Q & A
              • kcse computer studies paper 2 AND 3 Questions & Answers
            • BUSINESS STUDIES QUESTIONS & ANSWERS
            • KCSE AGRICULTURE TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE HOME SCIENCE DIRECT QUESTIONS AND ANSWERS
          • SCIENCES >
            • KCSE Mathematics Topical Questions
            • KCSE Biology Topical Questions and Answers
            • CHEMISTRY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE Physics Topical Questions
            • KCSE physics Practical Sample Quiz
          • HUMANITIES >
            • C.R.E (CRE) QUESTION AND ANSWERS
            • ISLAMIC RELIGIOUS EDUCATION (IRE) QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE History Topical Questions and Answers
            • GEOGRAPHY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
        • PRIMARY >
          • Standard 4-8 Mathematics Topical Questions from Mocks and KCPE
          • Std 6 Mathematics Notes
    • TUTORIALS >
      • SECONDARY >
        • SCIENCES >
          • FOCUS MATHEMATICS TUTORIALS AND EXAMS FREE
          • KCSE BIOLOGY NOTES
          • FREE KCSE CHEMISTRY NOTES
          • KCSE PHYSICS NOTES, AUDIOVISUALS AND MORE
        • LANGUAGES >
          • ENGLISH >
            • A GUIDE TO SILENT SONG AND OTHER STORIES
            • English KCSE Set Books
            • ENGLISH POETRY QUESTIONS WITH ANSWERS FOR K.C.S.E CANDIDATES
            • ENGLISH GRAMMAR #KCSE
          • KISWAHILI >
            • Bembea ya Maisha
            • CHOZI LA HERI - MWONGOZO
            • KIGOGO - MWONGOZO
            • MASWALI NA MAJIBU YA TUMBO LISILOSHIBA
            • USHAIRI MASWALI NA MAJIBU
            • KCSE Kiswahili Fasihi
        • TECHNICALS >
          • HOME SCIENCE NOTES
          • KCSE BUSINESS STUDIES NOTES
          • COMPUTER STUDIES NOTES LATEST
          • kcse Computer Studies Notes
          • KCSE AGRICULTURE NOTES, SYLLABUS, QUESTIONS, ANSWERS, SCHEMES OF WORK AND OTHERS
        • HUMANITIES >
          • KCSE History Notes Form 1 to 4
          • FREE KCSE CRE NOTES
          • KCSE GEOGRAPHY NOTES
          • IRE NOTES, AUDIOVISUAL, QUESTIONS AND ANSWERS
      • PRIMARY >
        • STANDARD 4: SOCIAL STUDIES
        • NOTES >
          • KISWAHILI
          • SOCIAL STUDIES
        • EXAMINATIONS
        • DecaTurbo Online Series Examinations
        • KCPE Mathematics Notes
        • KCPE and Primary Level Compositions
      • Other Supportive Documents >
        • SYLLABUS >
          • Primary 8-4-4 based Syllabus, Objectives and Lessons
          • Primary Mathematics Syllabus
        • MASOMO VIDEOS
    • CURRICULUM >
      • NEW CURRICULUM DESIGNS >
        • PRIMARY >
          • PRE PRIMARY ONE CURRICULUM WITH SYLLABUS
          • PRE PRIMARY TWO CURRICULUM WITH SYLLABUS
        • SECONDARY >
          • KNEC KCSE SYLLABUS AND COURSE OUTLINES
        • COLLEGE >
          • Regulations for the TIVET Craft and Diploma Business Examinations
    • HIGH INSTITUTIONS >
      • EXAMINATIONS >
        • College and Varsity Past Papers online
      • TUTORIALS >
        • COLLEGE AND UNIVERSITY NOTES AND TUTORIALS
  • MEMBERS RESOURCES
    • Primary >
      • CBC AND 8-4-4 LATEST EXAMS
      • CBC PROFFESSIONAL TOOLS
      • CBC NOTES PRIMARY
      • CBC KPSEA EXAMS
      • Standard 8 (std) English Topical Questions
      • KCPE MATHEMATICS TOPICAL QUESTIONS FROM 1989 TO LAST YEAR
      • STANDARD 8 PAST PAPERS 8-4-4 BASED
    • Secondary >
      • FORM 1 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 2 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 3 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 4 EXAMS WITH ANSWERS
      • KCSE 2020 QUESTIONS AND ANSWERS
      • NOTES SECONDARY
      • MOCKS SECONDARY >
        • kcse form 2 mathematics questions
    • Free Schemes of Work
    • FOCUS A365 SERIES K.C.P.E EXAMINATIONS FOR PRIMARY
    • ALL GROUPS PRODUCTS
    • PREMIUM PRODUCTS 2

BEMBEA YA MAISHA 

TIMOTHY M.AREGE
​Bembea ya Maisha ni hadithi kuhusu Yona na mkewe Sara pamoja na Bunju na mkewe Neema. Wahusika hawa wanajikuta katika vuta n’kuvute inayochochewa na mitazamo ya kitamaduni, uhalisia wa mambo pamoja na matamanio ya wahusika binafsi. Baina yao kuna mitikiso inayotishia familia, ndoa na mahusiano ya kijamii. Kuna shutma, shaka, tuhuma na mivutano. Lakini pia kuna hongera, imani, ushirikiano, upendo, kutanabahi na mshikamano. Katika huu mseto wa mambo ipo sauti imara ya Sara inayosikika ikihimiza na kuzindua. Sauti inayoiona kila hali mfano wa bembea.  

MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA IN PDF DOWNLOADS

18/3/2023

0 Comments

 
bembea-ya-maisha-mwongozo_1.pdf
File Size: 561 kb
File Type: pdf
Download File


Read More
0 Comments

Wahusika wadogo

18/3/2023

0 Comments

 

​WAHUSIKA WADOGO

​Salome na Mina: Wahusika wadogo ambao wanatajwa tu. Hawashiriki moja kwa moja katika masuala ya tamthilia hii. Salome ni mwanawe Yona na Mina ni bintiye Bunju na Neema.

​Umuhimu wao

​Wanakamilisha idadi ya watoto wa Yona na Bunju mtawalia. Idadi hii ni dhihirisho la usasa ambapo wazazi hawapati watoto wengi kutokana na hali ibuka za kiuchumi na za kijamii. Pia, wanaendeleza malezi ya kisasa ambapo watoto hawaonani na wazazi wao kwa kuwa wanahudhuria masomo ya bweni au nje ya nchi.

​Ushauri muhimu kwa mtahiniwa

  1. Mtahiniwa sharti asome kitabu husika (Bembeaya Maisha) barabara na kukielewa.
  2. Mwongozo ni kurunzi ya kumulikia njia, kwa hivyo, mtahiniwa sharti aelewe aendako.
  3. Ni muhimu kusoma na kulielewa swali lililoulizwa. Ni vyema kujiuliza swali lifuatalo: Mtahini anataka habari gani kutokana na swali hili?
  4. Usitoke nje ya muktadha wa swali na kuandaa habari ambazo hazihusiani na swali uliloulizwa.
  5. Ikiwezekana, toa mifano kutoka kwenye tamthilia inayohusiana na jambo unalolifafanua ili kuweka jambo hilo wazi.

Read More
0 Comments

​Lemi

18/3/2023

0 Comments

 

​​Lemi

​Ni mvulana wa miaka kumi, mwanawe Bunju.

​Sifa zake:

  1. Mtiifu: Lemi anawatii wazazi wake na pia mlezi wake Bela. Anatii amri ya mama yake anapoambiwa aende akafue hanchifu.
  2. Mwenye shukrani: Lemi anamshukuru mama yake Neema wakati alikumbushwa kufua hanchifu yake (uk. 48).
  3. Mdadisi: Lemi anauliza mama yake maswali kuhusu mama yake na bibi yake. Lemi anauliza mama yake (uk. 30) kwa nini hana raha na maswali mengine mengi. Pia anataka kujua ni kwa nini bibi yake hajakuja kumsalimu.
  4. Mwenye vipawa: Lemi ana kipawa cha kuimba na kucheza nyimbo kwa miondoko na minenguo (uk. 22).

​Umuhimu wake

Lemi anawakilisha watoto wa baadhi ya wazazi ambao hawapati wakati mwingi wa kuingiliana na wazazi wao ambao mara mwingi wako kazini. Anawakilisha watoto ambao hulelewa na yaya.

Read More
0 Comments

​Bela

18/3/2023

0 Comments

 

​​Bela

​Ni mfanyakazi wa nyumbani wa Neema.

Sifa zake:

  1. Mwenye busara: Anazungumza na mwajiri wake, Neema, kuhusu matatizo anayoyapitia kwenye ndoa yake kwa busara na kumsihi kuvumilia.
  2. Mtu wa kutegemewa: Ni mfanyakazi wa kutegemewa. Ana uhusiano mwema na mwajiri wake na anaelewa kazi yake barabara. Anamkumbusha Neema kuhusu kazi za shule za Lemi kwa maana kuwa, anaelewa jukumu lake la kuwalea watoto wa Neema, anayeonekana kuwa mtu wa kazi nyingi.
  3. Mlezi mwema. Bela analea watoto wa Neema vizuri na kwa bidii.
  4. Mwenye bidii: Bela anafanya kazi ya kuwalea watoto wa Neema kwa bidii. Pia anasema kuwa mara nyingi yeye hakupatana na watoto wake kwa sababu ya shughuli ya kazi. Maneno hayo yanaonyesha alikuwa mwenye bidii hata kabla ya kuanza kufanya kazi kwa Neema.

Umuhimu wake

Anawakilisha wafanyakazi wa kiwango cha chini wanaowajibika, kuheshimu na kuthamini kazi zao.

Read More
0 Comments

Beni

18/3/2023

0 Comments

 

Beni

Mwanakijiji ambaye ni jirani na rafikiye Yona.

Sifa zake:

  1. Mtamaduni: Anashikilia kuwa mtoto wa kiume ana manufaa kuliko wa kike. Anadai Neema hajali maslahi ya baba yake huku akijua kuwa Neema anamshugulikia mama yake ambaye ni mgonjwa. Hajakengeuka: Beni hajazinduka kwa kuwa hajui tofauti kati ya injinia na fundi wa mitambo.
  2. Mchochezi: Anadai kuwa Yona anafedheheshwa kwa kuachiwa kazi za kujipikia. Ni kama anaelekezwa na mkewe na wanawe. Ukweli ni kwamba mkewe alisafiri mjini kwa matibabu na kukaa kwa wanawe kwa siku chache tu. Beni anatawaliwa na taasubi ya kiume na si jirani mwema kwa Yona kwa kuwa anachangia kumchanganya akili. 

Umuhimu wake

Ni hasidi katika jamii. Watu wa aina hii huwachochea wenzao na mwisho kuwatenganisha na wake na familia zao. Yona anapuuza uchochezi wa Beni na kuonyesha kuwa sasa ameanza kupatwa na mwamko mpya.

Read More
0 Comments

​Luka

18/3/2023

0 Comments

 

​Luka

​Mwanakijiji ambaye ni jirani na rafikiye Yona.

Sifa zake:

  1. Ana busara: Anakiri kwamba siku hizi watoto wa kike wameacha kutegemea waume zao na kuanza kuwajibikia familia zao kiuchumi.
  2. Mshauri mwema: Anamshauri Beni kuhusiana na masuala ya kitamaduni kwamba zamani tamaduni zilikuwa lakini sasa tamaduni zingine zimepitwa na wakati.

Umuhimu wake

Anadhihirisha kwamba hata vijijini mabadiliko ya kimawazo kuhusu mtoto wa kike yameanza kukita mizizi. Anamchora Neema kama "simba wa kike" (uk. 67).

Read More
0 Comments

​Kiwa

18/3/2023

0 Comments

 

​Kiwa

​Kijana wa kiume, mtoto wa Dina. Kama majirani wengine anashangazwa na bidii za watoto wa Sara na Yona.

Sifa zake:

  1. Mwenye heshima: Anamheshimu mama yake na kushirikiana naye licha ya pato dogo analopata. Kupitia pato lake dogo, ameweza kubadilisha hali yao ya maisha pale nyumbani na kuinua maisha ya Dina.
  2. Mwenye roho safi: Anashangazwa na ufanisi wa majirani zake lakini hawaonei gere.
  3. Mdadisi: Kiwa anamuuliza mama yake maswali mengi kuhusu familia ya Yona. 

Umuhimu wake

  • Umuhimu wa Kiwa unatokana na mambo mawili; ni kijana anayewajibika na kubadilisha maisha ya mama yake licha ya pato lake dogo. Kupitia kauli zake, anadhihirisha kuwa ufanisi maishani hautegemei jinsia bali bidii ya mtu binafsi.

Read More
0 Comments

​Dina

18/3/2023

0 Comments

 

​​Dina

​Ni mama wa umri wa makamu na jirani wa Sara na Yona.

​Sifa zake:

  1. Mwenye moyo wa huruma: Sara anapougua, Dina anamsaidia kazi za nyumbani na kumpa moyo kuhusu ugonjwa alionao. Anamsifu Sara kwa bidii aliyonayo iliyomfanya kusomesha watoto wake hadi wakafikia Chuo kikuu licha ya masimango ya wanajamii na mateso ya mumewe.
  2. Mwenye ujirani mwema: Anapoitwa na Sara amsaidie kupikia bwana yake, anafika nyumbani mwa Sara kumsaidia katika shughuli hiyo.
  3. Mwenye roho safi: Hana kinyongo chochote kwa watoto au familia ya Sara. Anafurahia kufanikiwa kwa watoto wa Sara.
  4. Mwenye mapenzi ya dhati: Anamsaidia rakifi yake Sara kwa dhati.

​Umuhimu wake

  • Dina anadhihirisha usemi kwamba "Kidole kimoja hakiui chawa." Hii ni kutokana na kujitolea kwake kumsaidia Sara kazi za nyumbani anapokuwa anaugua. Ni kielelezo cha urafiki wa dhati na ujirani mwema. Ifahamike kwamba Sara asingeishi vyema na majirani, asingepata mtu wa kumsaidia.

Read More
0 Comments

​Bunju

18/3/2023

0 Comments

 

​Bunju

​Bunju ni mumewe Neema.

​Sifa zake:

  1. Mpenda haki: Bunju anamkubalia mke wake kutumia pesa zake kuishughulikia jamii yake ambayo ina uhitaji mkubwa baada ya Yona kufutwa kazi. Pia, mama mkwe anahitaji kutunzwa kwa hali na mali kutokana na hali yake ya kuugua kwa muda mrefu.
  2. Mwenye mapenzi: Bunju anampenda mkewe na wanawe na kutekeleza wajibu wake wa malezi kwa bidii.
  3. Mwenye bidii: Anajitahidi kazini na mara nyingi hata muda wa kustarehe hana. Bidii zake zinamwezesha hata kumnunulia mkewe gari.
  4. Ni mgumu wa pesa: Anajitokeza kama mwenye msimamo thabiti kuhusu matumizi ya pesa na hivyo kusawiriwa kama mtu mchoyo au bahili.
  5. Mtamaduni: Bunju anashikilia mila na desturi za jamii yake. Anapoziishi kwa kumkataza mama mkwe kulala nyumbani kwao, anaonekana kama mtu mchoyo na asiyejali maslahi ya mama mkwe wake. Mila na desturi zinamtawala na kumfanya asitangamane na mama mkwe hata akiwa amelazwa hospitalini. Hili Sio jambo jema.

Umuhimu wake

  • Bunju anadhihirisha umuhimu wa kushirikiana katika ndoa. Anatoa kielelezo chema cha mume anayemjali mke wake. Ana moyo wa kusaidia.
  • Alimsaidia Neema wakati alipopata ajali na kumlipia gharama zote za matibabu. Anamsaidia Neema kwa kumruhusu atumie mshahara wake kusaidia wazazi wake. Kwa hiyo, anampatia Neema fursa ya kusaidia jamii yake bila pingamizi. Pia, Bunju anasimamia wanarika ambao bado wanathamini mila na desturi za kwao kwani mwacha mila ni mtumwa.

Read More
0 Comments

​Asna

18/3/2023

0 Comments

 

​​Asna

Bintiye Yona wa pili. Ni mdogo wake Neema. Asna ni mhusika msaidizi. Anamsaidia msomaji kuelewa baadhi ya masuala yanayojadiliwa katika tamthilia.

Sifa zake:

  1. Mwenye misimamo ya kipekee: Asna anasema kwamba si lazima msichana aolewe mara tu aingiapo utu uzima. Anaonelea kuwa watu wanastahili kupewa nafasi ya kufanya maamuzi. Anasema taasisi ya ndoa ndiyo taasisi pekee inayotolewa vyeti kabla ya watu kupita mtihani. Anazungumzia hali ya watu wawili wanaotoa ahadi za maisha kabla ya kufahamu ikiwa jambo wanalojiingiza litafanikiwa au la.
  2. Mwenye heshima: Hata ingawa msimamo wake kuhusu ndoa ni tofauti na ule wa dadake, bado anamheshimu kama mkubwa wake na kuiheshimu ndoa ya Neema ingawa anajua ina matatizo. Pia, anawaheshimu na kuwapenda wazazi wake.
  3. Amekengeuka: Asna anaelewa fika kwamba kuolewa ni kwa hiari ya mtu binafsi ila si kushinikizwa au kulazimishwa na utamaduni.
  4. Msomi: Asna amesoma na kuhitimu hadi Chuo kikuu.
  5. Mwenye chuki: Asna anachukia tabia za Bunju za kujifanya kuwa hana pesa ilhali anazo. Anachukia ubahili.

​Umuhimu wake

  • Asna anawakilisha vijana ambao hawana azimio la kuolewa. Wao ni sehemu ya jamii na wanastahili kukubalika kama wale wenzao wenye imani kwenye taasisi ya ndoa. Hata hivyo, anavyoeleza Sara, na anavyodhihirisha Neema, vijana hawapaswi kuwa na msimamo mkali kuhusu taasisi ya ndoa kwa sababu changamoto nyingi zilizo katika taasisi ya ndoa zinavumilika kama ilivyo katika taasisi nyingine.

Read More
0 Comments

​Neema

18/3/2023

0 Comments

 

​​Neema

​Neema ambaye ni binti wa Yona na Sara ni mhusika mjenzi. Neema ni mke wa Bunju. Wasifu wa Neema unadhihirika kutokana na kauli zake na za watu wengine pamoja na matendo yake. Neema anadhihirisha sifa kadhaa:

​​SIFA ZAKE:

  1. Mwenye bidii: Anadhihirisha mwelekeo wa mtu mwenye bidii tangu alipokuwa shule. Licha ya kwamba wazazi wake walikuwa hawajiwezi, alisoma kwa bidii na kufaulu katika masomo yake hadi Chuo kikuu.
  2. Mwenye moyo wa kujitolea: Neema aliipenda familia yake hata alipoolewa. Tofauti na wasichana wengine ambao hujitenga baada ya kuolewa, Neema aliendelea kuwa nguzo imara katika familia yao. Alijitolea kumpeleka mama yake hospitali na kugharamia ada iliyohitajika. Pia aliajiri wafanyakazi wa kuwasaidia wazazi wake.
  3. Mwenye busara: Neema alidhihirisha busara katika ndoa yake kwa kumheshimu mumewe na kushirikiana naye katika malezi ya watoto wao tofauti na baadhi ya wake ambao huvuruga ndoa zao kwa mivutano mambo yanapokuwa magumu.
  4. Mwenye upole. Hakujibizana na Asna dada yake wakati alikuwa akizungumza vibaya kuhusu ndoa yake na Bunju.
  5. Amekengeuka: Neema amezinduka kwa kujua kwamba kuna tamaduni ambazo hazifai kutiliwa maanani katika kizazi cha leo. Anamwambia Bunju kwamba kumkataza mama yake kulala kwao ni utamaduni uliopitwa na wakati.
  6. Mwenye heshima: Neema anamheshimu baba yake hata baada ya kuwatesa walipokuwa wachanga. Neema anamheshimu bwana yake pia. Anasema amempa heshima yake tangu walipofunga ndoa.

​Umuhimu wake

  1. Neema anajitokeza kuwa kielelezo chema cha akina mama wenye uwezo wa kiuchumi na kuonyesha kwamba inawezekana kudumisha amani kwenye ndoa bila ya kusababisha ushindani usio na manufaa.
  2. Anadhihirisha na kuthibitisha kuwa hata mtoto wa kike anaweza kuwasaidia wazazi wake wanapotatizika hata akiwa kwenye ndoa. Hivyo basi, anasawiriwa kama nguzo muhimu ya kuupinga utamaduni unaomdhalilisha mtoto wa kike na kumtukuza mtoto wa kiume.

Read More
0 Comments

​Sara

18/3/2023

0 Comments

 

​Sara

Sara ni mke wa Yona. Yeye pia ni mhusika mkuu kwa sababu anahusika na karibu masuala yote ya tamthilia hii. Ndoa yake ilikuwa na changamoto nyingi zikiwemo mahitaji ya kiuchumi, fujo za mumewe ambaye alikuwa akishiriki ulevi na ugonjwa wa moyo uliomkaba.

Sifa zake:

  1. Mvumilivu: Sara alivumilia mateso ya mume wake ambaye alimlaumu kwa kutopata mtoto wa kiume. Mume wake alimtesa kutokana na kosa ambalo kwa hakika halikuwa lake.
  2. Mpatanishi: Sara ni mpatanishi kwa kuwa alimshauri bintiye amwelewe mume wake ambaye alitii utamaduni uliomfanya asimkubali mkwe wake alale nyumbani kwao. Pia, alimshauri bintiye amshukuru mumewe kwa kumruhusu kutumia hela zake kumtibu yeye aliyekuwa anaugua.
  3. Mwenye utu: Sara aliijali ndoa yake na kumpenda mumewe licha ya fujo zake. Alikataa kukaa mjini na binti yake ili kumwepushia mume wake fedheha ya kujifanyia kazi zilizohusishwa na wanawake kama vile kuchota maji kisimani.
  4. Mwenye hekima: Maneno anayozungumza yana wingi wa hekima na busara. Anamweleza Asna asicheze na akili zake ijapokuwa hakupata elimu sawasawa.
  5. Mlezi mwema: Anawalea wanawe kwa kuwapa mawaidha ya busara. Anawanasihi kuheshimu ndoa, utamaduni na baba yao.
  6. Mtamaduni: Neema anatilia maanani tamaduni za jamii yake. Kwanza tunamwona akisema kuwa fimbo hurithiwa na mtoto wa kiume. Tena tunamwona akimtetea bwana yake kuhusiana na suala la kazi za jikoni na kuteka maji kisimani.
  7. Mwenye uhusiano mwema: Sara alikuwa na uhusiano mwema na Dina. Anapougua, Dina anakuja kumsaidia kwa kuwa walikuwa na uhusiano mwema.
  8. Mwenye msimamo thabiti: Hata baada ya kusutwa na kukejeliwa na wanajamii hakuyumbishwa na maneno yao. Aliwapenda mabinti zake kwa dhati. Hata ingawa anachapwa kichapo cha mbwa na bwana yake, hakutoka nyumbani kwake, alisimama kidete na familia yake. 

​​Umuhimu wake

  1. Sara anakuwa kielelezo chema cha wanawake walio katika ndoa zenye misukosuko. Anavumilia na kufaulu kuwalea na kuwasomesha wanawe ingawa mumewe anamdhulumu.
  2. Anaendelea kumtii mumewe na kumshauri bintiye amnasihi baba yake dhidi ya ulevi kwa heshima.

Read More
0 Comments

​WAHUSIKA

18/3/2023

0 Comments

 

​WAHUSIKA

Yona

Ni mume wa Sara na pia ni mmoja wa wahusika wakuu. Anatambulika kama mhusika mkuu kwa sababu anahusika na takriban masuala yote yanayojadiliwa katika tamthilia hii. Ni kama kwamba kila kitu katika tamthilia hii kinamhusu.

Sifa zake:

  1. Mwenye bidii: Alikuwa mwalimu hodari aliyesifika kazini na udumishaji wa nidhamu shuleni. Aliijali kazi yake na hakusita kufunga vitabu kwenye baiskeli yake ili avisahihishe anapofika nyumbani hata siku za wikendi.
  2. Mtamaduni: Licha ya kujaliwa na mabinti waliofanikiwa maishani na kuiletea fahari jamii yake, msukumo wa wanajamii wa kumhimiza apate mtoto wa kiume ulimtikisa. Alikosa furaha kwenyenndoa yake kwa sababu ya kuamini mila na desturi za jamii yake.
  3. Mwenye rabsha: Yona alipoingilia ulevi wa kupindukia alibadilika kwa njia hasi. Alianza kumpiga mkewe hata akazirai na kumwagiliwa maji. Alishindwa kutekeleza wajibu wake kazini na hatimaye akafutwa.
  4. Mwenye majuto: Mwishoni mwa tamthilia anajirudi na kujisuta kuhusu matatizo aliyoisababishia familia yake na hasa mke wake na kuamua kuacha kunywa pombe.
  5. Mlevi: Yona aliposhinikizwa na wanajamii kuoa na kutafuta mtoto wa kiume aliingilia ulevi wa kiwango cha juu.
  6. Katili: Yona ni katili na hana utu kwa sababu hata baada ya kumkuta bibi yake akiwa katika hali mbaya ya ugonjwa, anamuuliza kwa nini hajamwandalia chakula. Hakusaidia bibi yake katika mapishi.
  7. Ni msomi: Amesoma hadi Chuo kikuu. Alikuwa mtu wa kwanza pale kijijini kufuzu kutoka chuoni.

Umuhimu wake

  • Yona anadhihirisha masaibu ya uraibu wa pombe unaoweza kuvuruga maisha ya mtu yeyote pasipo kujali nafasi yake katika jamii. Pia, anadhihirisha kwamba vita dhidi ya uraibu wa pombe vinaweza
  • shindwa ikiwa mikakati bora itatumika. Anadhihirisha ukweli wa methali kuwa muwi huwa mwema.

Read More
0 Comments

​Taharuki

18/3/2023

0 Comments

 

​Taharuki

  • Taharuki ni hali katika kazi ya fasihi inayoibua matarajio au hali ya kutojua kitakachofanyika hatimaye.
  • Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu ya taharuki kuendeleza msuko wa tamthilia yenyewe na kumpa msomaji hamu ya kusoma zaidi kujua kitakachotokea.

Mifano

  • Katika onyesho la kwanza sehemu ya kwanza (uk. 1-2), mwandishi anaeleza kuhusu ugonjwa wa Sara. Pia, Asna anaeleza kuwa Sara ataishia
  • kumeza vidonge maisha yake yote kwa sababu ya ugonjwa huo. Kisha, mwandishi anaonyesha Sara akisafirishwa mjini na kulazwa katika hospitali ya bei ghali iliyo na huduma bora na wataalamu hodari kuliko hospitali za kijijini. Mwandishi anampa msomaji hamu ya kuendelea kusoma kujua iwapo ugonjwa wa Sara utapona.
  • Katika uk. 10, Dina anamweleza Kiwa kuhusu namna Yona alivyoanza kulewa kupindukia na kuanza kumpiga mkewe Sara kipigo cha mbwa. Hali hii ya Yona na Sara pia inamulikwa kupitia kwa mazungumzo ya Asna na mamake Sara. Msomaji anapata hamu ya kutaka kujua iwapo ulevi wa Yona ulipungua au ulifikia kikomo.
  • Katika uk. 28, mwandishi anadokeza kuhusu mgogoro baina ya Neema na mumewe Bunju. Bunju anakataa kumsaidia Neema kulipia gharama ya hospitalini kwa ajili ya matibabu ya Sara. Hata hivyo, katika 
  • uk. 40, Bunju anabadilisha msimamo na kuahidi kusaidia "baadaye", kisha anaondoka. Msomaji anapata hamu ya kutaka kujua iwapo Bunju alitimiza ahadi hiyo.
  • Mfano mwingine wa taharuki unazuliwa na mgogoro baina ya Asna na mamake Sara kuhusu haja ya ndoa (uk. 52-53). Asna anasema kuwa kuolewa ni hiari ya mtu, na kuwa ndoa ni dhuluma. Kwa upande mwingine, Sara anamhimiza Asna kutafuta mchumba aolewe amletee wajukuu na zawadi kutoka kwa mumewe. Msomaji anapata hamu ya kujua iwapo Asna aliishia kuolewa au la.

Read More
0 Comments

​Sadfa

18/3/2023

0 Comments

 

​​Sadfa

Sadfa katika fasihi ni hali ambapo matukio mawili hutokea kwa wakati mmoja bila kupangwa na kwa namna ya kushangaza au inayoashiria bahati. Mbinu ya sadfa imetumiwa mara kadhaa katika tamthilia ya Bembeaya Maisha.
  • Kwanza, mbinu ya sadfa imetumiwa katika (uk. 34) ambapo Sara na Asna wanazungumza kuhusu ndoa ya Neema na Bunju wakiwa nyumbani kwa Asna mjini. Ghafla, na bila kutarajiwa, Neema anaingia bila kubisha. Asna anashtuka.
  • Vilevile, katika (uk. 71) Sara anamweleza Neema aende kuandaa kiamshakinywa. Neema anaitikia wito wa mama yake na kusema kuwa ataandaa kiamshakinywa mara moja. Hata hivyo, Yona anawaeleza kuwa alikuwa ameshaandaa tayari. Hii ni sadfa na pia kinyume cha matarajio. Neema anaonyesha kushangazwa na kitendo hicho cha babake.

Read More
0 Comments

Mbinu rejeshi

18/3/2023

0 Comments

 

​Mbinu rejeshi

  • Mbinu rejeshi ni sehemu katika kazi ya fasihi inayozungumzia matukio katika wakati uliopita. Pia huitwa kiangaza nyuma. Mbinu hii imetumika katika sehemu mbalimbali katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Kimsingi, mbinu hii imetumika kutofautisha maisha ya jana na ya leo, kuendeleza maudhui ya utamaduni na mabadiliko. Dina anaturejesha nyuma kiwakati katika mazungumzo yao na Siwa ambapo anasimulia kuhusu maisha ya awali ya familia ya Yona na Sara (uk. 7). Kupitia mbinu hii, tunapata kuelewa shida ambazo Sara na Yona walipitia, hasa masimango ya watu waliowasema kwa kukosa kupata watoto.
  • Katika (uk. 51) Bunju na Neema wanaturejesha nyuma kwenye ajali iliyompata Neema. Bunju anasema alimpata Neema akiwa mahututi.
  • Neema anakiri kuwa ilikuwa ajali mbaya sana ambayo ilisababisha vifo vingi. Hata hivyo, Neema alinusurika baada ya kupangiwa matibabu na Bunju. Mfano huu unaendeleza sifa ya utu na ukarimu alionao Bunju.
  • Mbinu rejeshi pia imetumika katika uk. 62 kupitia mazungumzo baina ya Beni, Luka na Yona. Hususan, Yona anakumbuka maisha yake ya awali alipokuwa kijana na mwalimu. Yona anaeleza kuwa alikuwa anarauka kwenda shuleni, akiwa na kiboko mkononi na hakupenda wanafunzi kuchelewa kufika shuleni. Vilevile, anakumbuka namna alivyovibeba vitabu kwenye baiskeli yake kwenda kuvisahihisha wikendi. Mfano huu unadhihirisha bidii yake kabla pombe haijamwathiri na kumbadilisha.
  • Mfano mwingine wa mbinu rejeshi umetumika katika uk. 64 ambapo Neema anakumbuka usafiri wa zamani kabla mabadiliko ya kiteknolojia. Anasema kuwa zamani wangechukua siku tatu kupambana na barabara ya vumbi, na mvua ​iliponyesha, kulikuwa hakuendeki mpaka barabara ikauke ndipo safari iendelee. Sara anachangia na kusema kuwa mwendo ulikuwa wa kobe na safari ilikuwa ya kuchosha. Mfano huu unaendeleza maudhui ya mabadiliko ya kiteknolojia na mgogoro baina ya jana na leo.

Read More
0 Comments

​Usemaji-kando

18/3/2023

0 Comments

 

​Usemaji-kando

  • Hii ni mbinu ambayo mhusika mmoja anasema maneno kwa hadhira au mhusika mwingine huku wenzake kwenye jukwaa wakijifanya kutosikia anachosema mhusika huyo.
  • Mbinu hii humsaidia msomaji kuelewa nia na kuibua msimamo wa mhusika kuhusu mhusika mwingine, wazo au kitu fulani kinachozungumziwa katika kazi ya fasihi kinyume na anayosema au kufanya akiwa na wahusika wengine. Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu hii katika kazi yake.
  • Mbinu hii imetumika katika mazungumzo baina ya Bela na Neema (uk. 24). Bela anaposisitiza kumwuliza Neema sababu ya kutowacha Sara alale kwake ili wapige gumzo, Neema anageuka kando na kuuliza kwa nini Bela aendelee kuulizia kuhusu hilo. Ni wazi kuwa Neema hataki kuzungumzia suala hilo lihusulo mila na tamaduni. Ana hisia hasi nalo.
  • Mbinu ya usemaji-kando pia imetumika katika uk. 29-30. Neema anainuka na kuihutubia hadhira. Analalamikia hali ngumu ya maisha yanayokwenda mbio kama gari liendalo kwa kasi. Anashangaa iwapo Bunju anamwelewa kama ilivyokuwa hapo awali kwa kuwa hataki kumsaidia kumlipia mama yake matibabu. Anajiuliza iwapo anaweza kumwacha mamake ateseke kwa sababu ya ugumu wa maisha.

Read More
0 Comments

MBINU ZA KIMUUNDO

18/3/2023

0 Comments

 

MBINU ZA KIMUUNDO

​​Mbinu za kimuundo hutumiwa na mwandishi kuendeleza msuko wa kazi ya fasihi.
Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu kadhaa za kimuundo kujenga msuko wa tamthilia yenyewe.

Mifano

Uzungumzi nafsia

Ni aina ya monolojia itolewayo na mhusika mmoja akiwa jukwaani pekee yake. Mbinu hii hutumiwa kuwasilisha maoni, hisia na fikra za mhusika kuhusu jambo fulani.
  • Mbinu ya uzungumzi nafsia imetumika (uk. 38) ambapo Neema anazungumza pekee yake na kudhihirisha hisia zake kuhusu maradhi yasiyosikia dawa. Anasema maradhi hayo yanamfukarisha mtu. Mtu huwa hana la kufanya ila kumwomba Mungu amwepushie. Ni wazi kuwa maradhi yana uzito usiostahilimika.
  • Mbinu hii pia imetumika katika (uk. 41) kwenye mazungumzo ya kibinafsi ya Neema. Neema anajisemea kuhusu Bunju. Anasema kuwa Bunju ni zawadi kwake kwa kuwa alimsaidia wakati alipatwa na ajali na kuwachwa katika hali mahututi. Tunamwona pia akikumbuka maneno ya mamake kuhusu Bunju, kuwa Bunju ni mmoja wao. Anakiri kuwa zamani hakuona hivyo kwa kuwa mtazamo wake kuhusu mumewe ulikuwa hasi. Sasa, kwa sababu ameahidiwa kusaidiwa kulipa gharama ya hospitalini ya Sara, mtazamo wake kuhusu Bunju unabadilika na anmuona kama zawadi kwake.
  • Uzungumzi nafsia pia unatokea katika mazungumzo ya Yona (uk. 70). Yona anamhurumia mke wake Sara kwa sababu ya ugonjwa uliodhuru. Anasema awali aliona kuwa ni kama mzaha kuwa mkewe anaugua. Anajilaumu kuwa angejua hangemfanyia madhila mkewe, angemtunza na Silesi za maisha wangezila zijavyo. Tunapata nia na mwelekeo wa Yona kwa kurejelea mazungumzo yake.
  • Anasema ni lazima awache njia zake za awali za unywaji pombe na kutoshughulikia familia yake.
  • Mkondo anaochukuwa ni kubadilisha tabia na kuahidi kwamba siku zake za uzeeni atazitumia kumwangalia mke wake Sara.

Read More
0 Comments

​Tanakuzi

18/3/2023

0 Comments

 

​​Tanakuzi

Ni tamathali ya usemi inayolinganua mawazo kwa kutumia mkinzano wa maneno, virai au sentensi kwenye miundo yenye usambamba.
  • Katika uk. 1, Yona anasema kuwa "njaa haileti shibe". Hapa kuna mkinzano baina ya njaa na shibe.
  • Katika uk. 9, Kiwa anasema kuwa dunia imekuwa ngumu kama "mwanga uletao kivuli". Mkinzano upo baina ya mwanga na kivuli.

Read More
0 Comments

​Tabaini

18/3/2023

0 Comments

 

​​Tabaini

Ni mbinu ya fasihi ambapo jambo husisitizwa kwa kutumia kikanushi 'si'. Mbinu hii imetumiwa na mwandishi wa Bembea ya Maisha mara kadhaa. Mifano:
  • Asna: ...nyumbani pakigeuka kuwa kambi ya jeshi nitafanyaje! Amri si amri, masharti si masharti! Asna anasisitiza hali ya ndoa anayoiona kuwa haifai.
  • Sara: Wewe unajua yote yaliyosemwa, hadharani na faraghani. Si makanisani, si magengeni. Sara anasisitiza kuwa watu waliwasema kila mahali, hata makanisani, mahali pasipofaa kusengenywa mtu.

Read More
0 Comments

​Ishara na taashira

18/3/2023

0 Comments

 

​​Ishara na taashira

​Ishara katika fasihi hutumiwa kurejelea kitendo, hali au kitu kinachodokeza au kuonyesha dalili ya kitu kingine. Nayo taashira ni alama mahususi ambazo huhusishwa na hali fulani katika jamii.
  1. Katika uk. 1, Yona analalamika kuwa nyumba haifuki moshi. Kufuka kwa moshi ni ishara ya upishi. Kutokuwepo kwa moshi ni ishara na pia taashira kuwa hakuna kinachopikwa.
  2. Mwangaza hafifu unaotokana na taa ya sola katika chumba cha Asna mjini ni ishara ya maisha ya Asna. Mwangaza huu hafifu unaashiria kuwa ingawa Asna anaona anaishi maisha mazuri na katika mtaa wa kifahari, mazingira anamoishi si mazuri sana. Uzuri wake ni hafifu. Chumbani humo hamna vitu vya thamani vinavyoendana na maisha ya kifahari. Ishara hii ni kama kejeli kwa maisha anayoishi Asna.
  3. Katika uk. 6, Dina anasema kuwa njia, sawa na moyo wa mwanadamu imejaa giza. Mfano huu unatumia giza kama ishara au taashira ya mambo yasiyojulikana au yasiyoweza kutabirika.
  4. Katika uk. 61, Luka anaeleza kuwa kijiji kina mwanga kutokana na ufanisi wa watoto wa Yona. Katika mfano huu, mwanga umetumiwa kuashiria maendeleo yanayotokana na elimu. Baadhi ya maendeleo hayo ni watoto kupata kazi, kuwajengea wazazi wao nyumba na kununua gari na kuenda nalo kijijini.
  5. Vilevile, mbinu ya ishara imetumika katika uk. 15 ambapo Dina anapika kwa kuni mbichi zinazomfanya Sara kuondoka nje kwa sababu ya moshi. Kuni mbichi zinaashiria umaskini na hali ngumu ya maisha ya kijijini. Pia, ni ukosefu wa maendeleo. Hali hii inaweza kutofautishwa na mjini ambako watu wanapika kwa kutumia jiko la gesi.
  6. Ishara pia imetumika pale ambapo tunaelezwa kuwa Salome alipata First Class katika mtihani wake wa Chuo kikuu (uk. 28). First Class imetumika kama ishara ya hekima na bidii masomoni.
  7. Katika uk. 33, Sara anamwambia Asna kuwa Bunju ashanunua leso yake akavaa mpaka ikazeeka. Leso ni ishara ya zawadi au kirimu kwa mama mkwe. Hivyo basi, Sara anamtaka Asna atafute mume amletee zawadi au amkirimu.

Read More
0 Comments

​Mbinu za kishairi

18/3/2023

0 Comments

 

​​MBINU ZA KISHAIRI

Mbinu za kishairi ni sehemu muhimu ya matumizi ya lugha katika tungo za kitamthilia.
Miongoni mwa mbinu hizo muhimu ni takriri.

​Takriri

​Takriri ni urudiaji wa sauti, silabi, neno au sentensi za namna moja zinazofuatana kwa karibu. Takriri hupamba lugha katika fasihi na pia kuvuta nadhari ya msomaji au msikilizaji.
Mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ametumia mbinu ya takriri katika kazi yake. 

​Mifano:

  • Sara: ... Ulikuwa umenila kiasi cha kuniacha chicha. (uk. 2).
  • Kiwa: Dunia ya leo haithamini kimo, inathamini akili. Haitaki kututumua misuli, inataka tambo la fikira. (uk. 5).
  • Dina: Dunia hii sasa tunaishi katika hofu. Tunahofu hata tusichokifahamu. (uk.9).
  • Dina: Wewe unaona rangi, tena rangi ya mwisho wa kinachoelea. Kabla kielee kimepigwa shoka, kimeonja misumeno ainaaina, kimetambaliwa na randa, kimestahimili makali ya patasi, na kukapaswa na mikwaruzo ya msasa. (uk. 10).
  • Sara: Wewe unajua yote yaliyosemwa, hadharani na faraghani. Si makanisani, si magengeni. (uk. 13). Sara: Tena hodari wa misemo na nahau. Wala hawana simile
    • kutuloweka kwenye misemo na nahau zao. Hawana simile mwanangu!
  • Sara: Tumeyaacha maji ya mbizi na kuingia kwenye maji ya mbuzi. (uk. 20).
  • Neerna: Kikijanjaruka hakitakuwa na budi ila kurauka. (uk. 25).
  • Neema: Usingepikika, usingelika. (ul<. 41).
  • Neema: Mwenyewe huyo analipia kila kitu. Ninakwambia kila kitu! (uk. 41).
  • Asna: Ndoa imeyatia doa maisha yako. (uk. 53).
  • Sara: Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. (uk. 54).
  • Asna: Elimu ni muhimu mama. (uk. 55).
  • Sara: Mungu hakupi yote. Akikupa hiki, anakunyima kile.
    • Akikupa yote yatakushinda. (uk. 55).
  • Sara: Watu walituona maskini wa watoto. Maskini wa kizazi. (uk. 55).
  • Sara: Wakatulaumu na kutusema bila simile. Bila simile! (uk. 56).
  • Yona: Malezi yameachiwa yaya. Nyumba ni ya yaya. (uk. 59).
  • Yona: Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri, kiboko mkononi...
    • Jioni darasani tena, kiboko mkononi. (uk. 62).
  • Yona: Nilishindwa kuingia kazini kila siku. Nilishindwa kuishi bila kulewa. (uk.62).
  • Yona: Yabarikiwe mashamba yetu.
  • Beni: Ibarikiwe mimea yetu.
  • Luka: Vibarikiwe vizazi vyetu. (uk. 64).
  • Neema: Kwenye hujuma na kuchimbana, kwenye ugomvi na mivutano, kwenye chuki na uhasama wa kitoto, kwenye tembo na gumzo lisiloisha, penye uchimvi na kusutana (uk.65).
  • Sara: Anza polepole. Anza na baba yenu. Badala ya kumkabili, mshawishi. Atakuelewa. Akikuelewa atauendeleza ujumbe. (uk. 69).
  • Yona: Siku zangu za uzeeni lazima nizitumie kumwangalia mke wangu mgonjwa. Lazima nimshukuru kwa vitendo kwa jinsi alivyojitolea kuijenga familia yetu. Kwaheri pombe. Buriani. (uk. 70).

Read More
0 Comments

​Tashihisi

18/3/2023

0 Comments

 
​Tashihisi ni mbinu ya mwandishi kuvipa viumbe visivyo na uhai sifa za uhai au za kibinadamu. Pia huitwa uhuishi
  • Katika uk. 5, Kiwa anasema kuwa mvua yenyewe imefanya ugeni. Kiwa analinganisha mvua na mgeni, na hivyo kuipa mvua sifa za uhai.
  • Katika uk. 6, Dina anasema kuwa maradhi yamemgeuza Sara kuwa ngoma. Katika mfano huu, maradhi yamesawiriwa kuwa yenye uwezo wa kumpiga Sara kama vile mtu anavyopiga ngoma.
  • Katika uk. 9, Dina anamweleza Kiwa kuwa "dunia mwanangu imetufunza Sisi wazee wenu". Katika mfano huu, dunia imepewa uwezo wa kutoa mafunzo. Hii ina maana kuwa matukio mbalimbali duniani yana uwezo mkubwa juu ya maisha ya mwanadamu.
  • Tashihisi pia imetumika katika uk. 38. Neema analalamika kuhusu maradhi yasiyosikia dawa. Anasema, maradhi "yakitaka huzichezea dawa mwajificho. Dawa zikiingilia huku, maradhi hutokezea pale, hali pesa zinakwenda, shughuli zinasimama". Vitu hivi vitatu: maradhi,pesa na shughuli vinasawiriwa kuwa na uwezo fulani ambapo maradhi yanazidi uwezo wa vyote viwili.
  • Vilevile, tashihisi imetumika katika uk. 39 ambapo Bunju anamwambia Neema kuwa "chumba chenyewe kinajisemea". Hii ni baada ya Bunju kufika nyumbani kwake na kupendezwa na uzuri wa chumba hicho. Mfano huu una athari ya kusisitiza uzuri wa chumba hicho usiofichika.
  • Mbinu hii pia imetumika katika uk. 56 ambapo Sara anasema kuwa agongo liliyamega maadili" ya Yona kimyakimya na taratibu uwajibikaji wake ukawa umemponyoka. Gongo ni aina ya pombe kali.
  • Mwandishi wa Bembea ya Maisha ameisawiri pombe hii kuwa na uwezo juu ya mwenendo wa maisha ya mtu na kuweza kumdhuru mtu huyo.
  • Vilevile, katika uk. 62, Beni anasema kuwa Yona alikuwa mwalimu mwenye bidii kabla "tembo kunyoosha mikono yake na kumdaka". Mfano huu, sawa na ule uliotangulia hapo juu, unadhihirisha uwezo mkubwa wa pombe kumteka na kumyumbisha mtu.

Read More
0 Comments

​Sitiari

18/3/2023

0 Comments

 
​Ni mbinu ya lugha inayotumia ulinganisho wa moja kwa moja wa kitu na kingine. Kitu kimoja husemwa kuwa kingine. Mifano ya sitiari katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
  1. Mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu huitakasa sahani yake akijua itamfaa tena. (uk. 1-2). Yona analinganisha wanawe (Asna na Neema) na mbegu, mazao yake, na mavuno. Pia, anawalinganisha na sahani ambayo aliitakasa imfae.
  2. Katika uk. 2, Sara anasema kuwa Neema ana 'mzigo' wa familia yake. Mzigo umetumiwa kama sitiari ya majukumu mengi au mazito.
  3. Vilevile, kwenye uk. 2, Yona anasema kuwa fimbo ya mzee hurithiwa na mtoto wa kwanza. Fimbo ni sitiari ya nafasi ya mzee katika familia.
  4. Ukurasa wa 3, Sara anasema kwamba wachapakazi hodari ni njozi iliyopotea. Hii ina maana kuwa hawapatikani.
  5. Mimi mzigo (uk. 4) - mtu ambaye ni tatizo kwa jamaa zake, anayetekelezewa majukumu yake yote.
  6. Amekuwa na kimo cha sindano (uk. 5) - amekuwa mwembamba sana.
  7. Neema ni chuma cha reli (uk. 6) - Neema ana nguvu za kustahimili changamoto za maisha.
  8. Katika uk. 8, mvua ya baraka iliwanyea Yona na Sara. Mvua ya baraka ni sitiari ya watoto ambao Yona na Sara walibarikiwa kuwapata.
  9. Dina anaeleza kuwa watu walimtaka Yona kutafuta mtoto wa kiume ili "utambi wa ukoo wake usizime" (uk. 10). Utambi wa ukoo ni sitiari ya kizazi cha ukoo.
  10. Ukurasa wa 11, dunia ni nyumba ya mitihani. Hii ina maana kuwa dunia ni mahali pa changamoto nyingi.
  11. Sara anasema kuwa alipoanza kuugua alikuwa kimbaumbau mwiko wa pilau (uk. 12) - hii ina maana kuwa alikuwa mwembamba na mithili ya mwiko wa kupikia pilau.
  12. Safari hii ni maji ya mbizi (uk. 16) - safari ni ndefu Maisha ya siku hizi si maji ya kunywa (uk. 23). Maisha si rahisi au mepesi.
  13. Mamangu mzazi ni mboni ya jicho kwetu (uk. 30) - mama mzazi ni mwangalizi wao.
  14. Nyumbani, hiki ni kizimba cha kuku (uk. 31) - ni chumba kidogo na duni.
  15. Maisha ni mshumaa usio mkesha (uk. 32) maisha ni mafupi na hayapo daima.
  16. Sara na Bunju ni chanda na pete (uk. 36) - wanalingana katika maoni yao, ni wamoja.
  17. Mifuko inazidi kuwa king'onda (uk. 41) - inaendelea kuishiwa
  18. Akili za Yona zinatajwa kuwa sumaku (uk. 43) - zinashika mambo haraka.
  19. Nina jeshi lake (uk. 46) - nina watoto wake.
  20. Bunju anamweleza Neema kuwa kuwa yeye (Bunju) ni kichwa na Neema ni shingo (uk. 49). Hii ina maana kuwa Bunju ndiye kiongozi wa nyumba naye Neema ni msaidizi wake.
  21. Ujana ni moshi (uk. 52) - ujana ni kitu kinachopita na kikienda hakirudi.
  22. Ndoa ni mtihani mkubwa sana (uk. 53) ndoa ina majaribu mengi.
  23. Luka anamrejelea Neema kama 'simba wa kike anayenguruma' (uk. 61). hii ina maana kuwa Neema ana sauti, usemi au hadhi sawa na ya mtoto wa kiume.
  24. Watoto walikuwa nyota ya jaha (uk. 61) — ina maana kuwa watoto wa Sara na Yona walikuwa bahati kubwa kwao.
  25. Mwanamume ni mto wa kifuu (uk. 67) - ina maana kuwa mwanamume amesawiriwa kama mtu hatari.
  26. Sasa rudini mzalishe mbegu nzuri (uk. 68) - wawasaidie watoto wengine kukua vyema kama wao; wawe mfano kwa wengine.
  27. Shikeni usukani muwe marubani wa kweli ili ndege ipae angani (uk. 68) -chukueni nafasi ya kuleta maendeleo kijijini.

Read More
0 Comments

​Methali

18/3/2023

0 Comments

 
Methali ni aina ya semi ambayo huwa na muundo maalumu. Hueleza ukweli fulani wenye maana pana na unaoweza kufasiriwa kwa njia mbalimbali.
​​Methali hukusudia kuonya, kuelekeza, kuadhibu, kusuta, kulaumu, kushauri na kadhalika. Methali huwa imebeba maana pana kuliko maneno yenyewe.
Tamthilia ya Bembea ya Maisha imetumia mbinu ya methali kwa wingi.

​Mifano:

  1. Mungu hamwachi mja wake (uk. 8).
  2. Kigumba kwa nguruwe kwa binadamu ki uchungu (uk. 63).
  3. Baada ya dhiki faraja (uk. 6).
  4. Njia haimuagulii msafiri (uk. 6).
  5. Binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe (uk. 5).
  6. Mlango mmoja ukifunga, macho huiona mingine mingi (uk. 56).
  7. Mwacha mila ni mtumwa (uk. 58).
  8. Mgala muue na haki yake mpe (uk. 66).
  9. Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi (uk. 67).
  10. Kutoa ni moyo, usambe ni utajiri (uk. 2)
  11. Mtu hujikuna ajipatapo (uk. 2)
  12. Mungu si Athumani (uk. 10)
  13. Mungu hamtupi mja wake (uk. 10)
  14. Leo kwangu kesho kwal<0 (uk. 11)
  15. Mungu hamwachi mja wake (uk. 11)
  16. Safari ya kesho huungwa leo (uk. 16)
  17. Mrina haogopi nyuki (uk. 18)
  18. Papo kwa hapo kamba hukata jiwe (uk. 21)
  19. Mwana wa yungwi hulewa (uk. 21)
  20. Kipendacho roho hula nyama mbichi (uk. 21)
  21. Ya kale hayanuki (uk. 24)
  22. Mapema ina sudi (uk. 25)
  23. Afikaye kisimani mapema hunywa maji maenge (uk. 25)
  24. Samaki hukunjwa angali mbichi (uk. 26)
  25. Msafiri kafiri angawa tajiri (uk. 31)
  26. Mwindaji huwa mwindwa (uk. 32)
  27. Ng'ombe halemewi na nunduye (uk. 35)
  28. Mali ya bahili huliwa na mchwa (uk. 45)
  29. Mgala muue na haki umpe (uk. 66)
Methali katika tamthilia ya Bembea ya Maisha zimetumika kutekeleza yafuatayo:
  • Kupamba lugha na kuipa mvuto wa kisanaa.
  • Kuendeleza maudhui na dhamira ya mwandishi, hasa kuhusu suala Zima la bembea ya maisha.

Read More
0 Comments
<<Previous
    bembea ya maisha

    Author

    Atika School Team

    Archives

    March 2023
    February 2023

    Categories

    All
    ​AINA ZA TASWIRA
    ANWANI YA TAMTHILIA
    Dhamira Ya Mwandishi
    DOWNLOADS
    ​​HATI
    ​JALADA LA BEMBEA YA MAISHA
    Makosa Ya Kisarufi
    Maswali Na Majibu
    MAUDHUI NA DHAMIRA
    MBINU ZA KIMUUNDO
    ​MBINU ZA LUGHA NA MBINU ZA KIMUUNDO
    Mbinu Za Sanaa
    ​MSUKO
    MTIRIRIKO WA MAONYESHO
    Utangulizi
    ​WAHUSIKA

    RSS Feed



Primary Resources
  • K.C.P.E Past Papers
  • ​Pri - Primary 1 Level
  • Pri  - Primary 2 Level
  • Grade 1
  • Grade 2
  • Grade 3
  • Grade 4
  • Standard 5
  • Standard 6
  • Standard 7
  • Standard 8
  • English
  • Kiswahili
  • Social Studies
  • Science
  • Mathematics
  • Kenya Sign Language
  • I.R.E
  • ​H.R.E
  • Notes
  • Termly Questions
  • Mocks
  • K.C.P.E Past Papers
College Resources
  • E.C.D.E
  • P.T.E
  • D.T.E
  • Technical Diploma
  • Technical Certificate
  • Business Diploma
  • Business Certificate
  • Higher Diploma
  • K.A.S.N.E.B Resources
  • K.M.T.C Resources
  • Varsity Resources
Secondary Resources
  • K.C.S.E Past Papers
  • Form 1
  • Form 2
  • Form 3
  • Form 4
  • Term 1
  • Term 2
  • Term 3
  • English
  • Geography
  • History
  • C.R.E
  • I.R.E
  • ​H.R.E
  • Home Science
  • Computer Studies
  • Business Studies
  • Agriculture
  • Chemistry
  • Biology
  • Physics
  • Mathematics ALT A
  • Mathematics ALT B
  • Kiswahili
  • French
  • Germany
  • Arabic
  • Aviation
  • Art & Design
  • Drawing & Design
  • Building & Construction
  • Metal Works
  • Wood Work
  • Music
  • Kenya Sign Language
  • Electricity
Other Useful Links
  • Academic Environment
  • How its Done
  • News and Opinions
  • Manyam Franchise Support
  • About
  • SITEMAP
  • FOCUS A365 SERIES
  • Membership Details (KCPE/KCSE)
  • Secondary Mocks
  • SYLLABUS
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii
Tel: 0728 450 424
Tel: 0738 619 279
Tel: 0763 450 425
E-mail - sales@manyamfranchise.com
  • Start
    • SITEMAP
    • KNEC Portal
    • ZERAKI HELP AND SUPPORT
    • Academic Environment
    • KNEC KCSE PROJECT INSTRUCTIONS
  • BLOGS
    • About Us? >
      • Learn more about us
    • CUSTOMER CARE >
      • PRICING
      • Help & Support
    • News and Opinions
    • JOBS IN KENYA AND ABROAD FOR KENYANS AND BEYOND
    • How its Done
  • OUR PRODUCTS
    • All Categories >
      • MORE PRODUCTS >
        • SECONDARY CRE NOTES
        • COURSE BOOKS
        • KCSE KISWAHILI SETBOOKS
        • Backed Up Files and Archives
        • FREE DOCUMENTS
        • PRIMARY 8-4-4 BASED RESOURCES
        • STANDARD 8 RESOURCES
        • HIGH SCHOOL RESOURCES >
          • Biology Paper 3 Exams
          • Secondary Examinations
        • PRIMARY CBC BASED RESOURCES
        • COLLEGE & VARSITY RESOURCES
      • PRIMARY RESOURCES CBC
      • PRIMARY RESOURCES 8-4-4
      • SECONDARY RESOURCES
      • NOTES & TUTORIALS
      • COLLEGE RESOURCES
      • NOVELS and OTHER BOOKS
    • EXAMINATIONS >
      • MOCKS AND JOINT EXAMS >
        • FORM 1 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 2 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 3 EXAMINATIONS, QUESTION PAPERS AND ANSWERS
        • FORM 4 MOCKS PAST EXAMS BY REGION
        • TOP SECONDARY EXAMS ALL SUBJECTS
      • KPSEA NATIONAL EXAMS
      • KCPE >
        • KCPE PAST PAPERS AND ANSWERS >
          • KCPE 2020 RESULTS, REPORTS, QUESTIONS AND ANSWERS
          • KCPE PAST PAPERS 2019 REPORTS, RESULTS, QUESTIONS AND ANSWERS
        • KCPE PAST PAPERS PER SUBJECT
      • KCSE >
        • KCSE PAST PAPERS BY SUBJECT
        • KNEC KCSE PAST PAPERS, MARKING SCHEMES, QUESTIONS & ANSWERS
        • Free KCSE Past Papers Mathematics
        • Free KCSE Biology Questions and Answers
      • QUESTIONS & ANSWERS >
        • SECONDARY >
          • LANGUAGES >
            • Secondary English Questions and Answers
          • TECHNICALS >
            • COMPUTER STUDIES >
              • COMPUTER STUDIES Q & A
              • kcse computer studies paper 2 AND 3 Questions & Answers
            • BUSINESS STUDIES QUESTIONS & ANSWERS
            • KCSE AGRICULTURE TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE HOME SCIENCE DIRECT QUESTIONS AND ANSWERS
          • SCIENCES >
            • KCSE Mathematics Topical Questions
            • KCSE Biology Topical Questions and Answers
            • CHEMISTRY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE Physics Topical Questions
            • KCSE physics Practical Sample Quiz
          • HUMANITIES >
            • C.R.E (CRE) QUESTION AND ANSWERS
            • ISLAMIC RELIGIOUS EDUCATION (IRE) QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE History Topical Questions and Answers
            • GEOGRAPHY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
        • PRIMARY >
          • Standard 4-8 Mathematics Topical Questions from Mocks and KCPE
          • Std 6 Mathematics Notes
    • TUTORIALS >
      • SECONDARY >
        • SCIENCES >
          • FOCUS MATHEMATICS TUTORIALS AND EXAMS FREE
          • KCSE BIOLOGY NOTES
          • FREE KCSE CHEMISTRY NOTES
          • KCSE PHYSICS NOTES, AUDIOVISUALS AND MORE
        • LANGUAGES >
          • ENGLISH >
            • A GUIDE TO SILENT SONG AND OTHER STORIES
            • English KCSE Set Books
            • ENGLISH POETRY QUESTIONS WITH ANSWERS FOR K.C.S.E CANDIDATES
            • ENGLISH GRAMMAR #KCSE
          • KISWAHILI >
            • Bembea ya Maisha
            • CHOZI LA HERI - MWONGOZO
            • KIGOGO - MWONGOZO
            • MASWALI NA MAJIBU YA TUMBO LISILOSHIBA
            • USHAIRI MASWALI NA MAJIBU
            • KCSE Kiswahili Fasihi
        • TECHNICALS >
          • HOME SCIENCE NOTES
          • KCSE BUSINESS STUDIES NOTES
          • COMPUTER STUDIES NOTES LATEST
          • kcse Computer Studies Notes
          • KCSE AGRICULTURE NOTES, SYLLABUS, QUESTIONS, ANSWERS, SCHEMES OF WORK AND OTHERS
        • HUMANITIES >
          • KCSE History Notes Form 1 to 4
          • FREE KCSE CRE NOTES
          • KCSE GEOGRAPHY NOTES
          • IRE NOTES, AUDIOVISUAL, QUESTIONS AND ANSWERS
      • PRIMARY >
        • STANDARD 4: SOCIAL STUDIES
        • NOTES >
          • KISWAHILI
          • SOCIAL STUDIES
        • EXAMINATIONS
        • DecaTurbo Online Series Examinations
        • KCPE Mathematics Notes
        • KCPE and Primary Level Compositions
      • Other Supportive Documents >
        • SYLLABUS >
          • Primary 8-4-4 based Syllabus, Objectives and Lessons
          • Primary Mathematics Syllabus
        • MASOMO VIDEOS
    • CURRICULUM >
      • NEW CURRICULUM DESIGNS >
        • PRIMARY >
          • PRE PRIMARY ONE CURRICULUM WITH SYLLABUS
          • PRE PRIMARY TWO CURRICULUM WITH SYLLABUS
        • SECONDARY >
          • KNEC KCSE SYLLABUS AND COURSE OUTLINES
        • COLLEGE >
          • Regulations for the TIVET Craft and Diploma Business Examinations
    • HIGH INSTITUTIONS >
      • EXAMINATIONS >
        • College and Varsity Past Papers online
      • TUTORIALS >
        • COLLEGE AND UNIVERSITY NOTES AND TUTORIALS
  • MEMBERS RESOURCES
    • Primary >
      • CBC AND 8-4-4 LATEST EXAMS
      • CBC PROFFESSIONAL TOOLS
      • CBC NOTES PRIMARY
      • CBC KPSEA EXAMS
      • Standard 8 (std) English Topical Questions
      • KCPE MATHEMATICS TOPICAL QUESTIONS FROM 1989 TO LAST YEAR
      • STANDARD 8 PAST PAPERS 8-4-4 BASED
    • Secondary >
      • FORM 1 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 2 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 3 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 4 EXAMS WITH ANSWERS
      • KCSE 2020 QUESTIONS AND ANSWERS
      • NOTES SECONDARY
      • MOCKS SECONDARY >
        • kcse form 2 mathematics questions
    • Free Schemes of Work
    • FOCUS A365 SERIES K.C.P.E EXAMINATIONS FOR PRIMARY
    • ALL GROUPS PRODUCTS
    • PREMIUM PRODUCTS 2