Eleza ufaafu wa anwani Chozi la HeriAnwani ya Riwaya hii ni Chozi la Heri. Anwani hii imeundwa kwa maneno mawili yaani CHOZI NA HERI. Kwa mujibu wa matumizi ya neno Chozi katika riwaya hii, limetumika kuashiria tone la maji au uowevu unatoka machoni aghalabu mtu anapolia au kufurahi. Neno HERI limetumika kuonyesha maana ya amani,Utulivu, mafanikio na usalama . Kwa hivyo, chozi la heri ni kirai ambacho kimetumika kuonyesha chozi la mhusika ambaye amepata utulivu, amani na usalama nafsini mwake. Ni wazi kusema kuwa , mwandishi amefanikisha kwa hali ya utendeti kuonyesha ufaafu wa anwani rejelewa kwa kurejelea mifano hii: Kaizari anamsimulia mwamu wake Ridhaa yaliyotokea, kwamba siku ya nne baada ya mapinduzi walisikia hodi na mkewe akaeleke a kufungua mlango. Alisalimiwa kwa kofi na kuulizwa kiko wapi kile kidume chako kijoga? Nasikia ni mmoja wa wale waliotuuza kwa kupigia Mwekevu kura. Ati as for me and my family we will support our mother. Ninyi ndio vikaragosi wanaotumiwa na wasaliti. Kabla hajajaribu lolote alikuwa amekula mikato miwili ya sime, akasirai kwa uchungu. Baadaye genge hili liliwabaka Lime na Mwanaheri . alijaribu kuwapa wanawe huduma ya kwanza na kisha baadaye wanakumbwa na matatizo ya vyakula na maji katika kambi ya wakimbizi walikokimbilia waathiriwa. Mto wa mamba haukuwa safi ila baadaye waliyanywa maji ambayo walidiriki kupata huku wakisema ni heri nusu shari. Bwana kaizari anasimulia namna vita vilivyowaathiri na walipokimbilia kambi za wakimbizi, anasema kuwa waliokuwa wamabahatika kubeba nafaka haba walizitoa zikatumiwa kwa ujima. Sasa matumbo yalianza kudai haki. Ridhaa katika kumbukizi zake katika msitu wa heri, hakukuwa na wakazi wengi, kwa hivyo, alikosa ushirika wa ndugu zake. Aidha anapojiunga na shule siku za awali alitengwa na wenzake kwani hawakutaka ashiriki michezo yao. Kijana mmoja mchokozi alimwita 'mfuata mvua' aliyekuja kuwashinda katika mitihani yote na kwamba ni yet anayewaibia kalamu zao. Ridhaa hakungoja mwenzake amalize dukuduku lake alichukua mkoba wake na akafululiza nyumbani na kujitupa mchangani na kulia kwa kite na shake. Mamake alimliwaza na kumhakikishia kumwona mwalimu siku iliyofuata. Tangu siku hii, huu ukawa ndio mwanzo wa maisha ya heri kwa Ridhaa kwani baada ya mwalimu kuzungumza na wanafunzi umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano,Ridhaa alipata utulivu, amani na usalama shuleni na kungaa kwa elimu hadi kufikia Kilele cha cha elimu na kuhitimu kama daktari huku utendakazi wake ukimletea mbivu. Kaizari anamshukuru Mungu uk1 6 kwa kuwa hai licha ya kwamba aliwatazama mabinti zake wakifanyiwa ukaini na vijana wenzao. Pia anapomtazama mkewe anashindwa kama inahalisi kumwita mkewe kwa sababu ya vile uso wake ulikuwa umevamiwa na majeraha. Amevimbiana kama dongo la unga ngano. Anasema kuwa ametiwa hamira lakini yeye hana hamira ila ni matokeo ya ubahaimu wa binadamu. Licha ya hayo yote anashukuru kuwa wako hai. Ridhaa anajihisi kama yule Ayubu kwenye kitabu kitakatifu ambaye ibilisi aliifakamia familia na mali yake takribani kutwa moja. Hata hivyo, anajihisi nafuu na kiumbe kipya kwani wapwa wake Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu kutoka kwa vijana wenzao ambao walitumwa na mashirika yasiyo ya kiserikali. Mkewe Kaizari yaani Subira alikuwa katibiwa akapona. Uk36 Ridhaa na mwangeka wakiangaliana kila mmoja akitweta kwa mpigo wa kasi wa moyo. Walitaka kukimbiliana ila hakuna aliyetaka kuanza. Ridhaa hakuamini kuwa Mwangeka angerudi akiwa hai. Fahari ya uzazi na ulezi inayeyusha woga na shaka huku Mwangeka akajirusha kifuani mwa babake huku wakiambiana kimoyo moyo ni hai sijafa uk46 Uk 51 Mwangeka anashaangazwa na hali ya babake ya kutozika mabaki ya familia yao. Baba mtu anamkazia tu macho , bila shaka ameelewa anachowazia mwanawe.Mwangeka ana huzunishwa sana na kitendo hicho cha unyama cha kuacha familia yake , mamake na wanuna wake kama majivu. Matone ya machozi yalitunga machoni, Mwangeka. Akayaacha yamdondoke na kumcharaza, yatakavyo. Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa machozi haya uliulainisha moyo wake, ukampa amani kidogo. Moyo wake ukajaa utulivu sasa kwa kujua kuwa wino wa Mungu haufutiki methali hii Mwangeka anaiona wazi ambayo mpinzani wake aliishi kuirudia mara aliposhindwa na Mwangeka.uk 52 Katika Msitu wa Mamba kulikuwa na maelfu ya watu waliogura makwao. Kati ya familia kwao bila matumaini ya kurudi. Kwa Kangata na mkewe Ndarine, hapa palikuwa afadhali kwani hawakuwa na pa kwenda kwa kuwa hata kule walikokuwa wakiishi awali hakukuwa kwao maskwota hivyo wakaamua kukumbuka asali na maziwa ya Kanaan hii mpya . Uk 57 Msimamo wa Lunga wa watu kutopewa mahindi yaliyokuwa hatari hata kwa kipanya unasababisha kupigwa kalamu. Anakuwa mkulima stadi, marafiki zake wanampa jina la msimbo mkulima namba wani. Uk 70 Umu anapojitosa jiji analiona kama bahari isiyo na kikomo . Akiwa jiji baridi ya vuli inamtafuna huku pia akiwa na mkeketo wa njaa kwenye uchango wake. huku akiwa na matumaini ya kukutana na kijana Hazina ailiyemsaidia akiwa anakataswa na mamaake. Wanapokutana Hazina alibahatika na sasa ni mfanyikazi katika hoteli moja pale mjini. Umu anapomweleza juu ya matatizo yake Hazina anamwonea huruma huku machozi yake yakimdodoka kwa mchanganyiko wa furaha na majonzi.uk87 Kukutana kisadfa kwa Dick na Umu katika uwanja wa ndege kulileta utulivu, walikumbatiana kwa furaha. Machozi yaliwadondoka hawa mandugu wawili na wakawa wanalia kimyakimya.Walijua fika kuwa jaala ilikuwa imewakutanisha na kwamba hawatawahi kutengana tena. Maisha sasa yalianza kuwa ya heri kwao.uk128 Baada ya miaka kumi ya kuuza mihadarati Dick alifaulu hatimaye kujinasua kutoka kwa mwajiri wake. Alianza biashara yake mwenyewe ya kuuza vifaa vya umeme. Sasa akaanza kujitegemea kwa kuwa amejiajiri. Alikuwa ameufungua ukurasa mpya katika maisha yake. Maisha yake sasa ni ya heri. Zohali alikuwa mtoto wa nyumba kubwa wazazi wake walikuwa wa hadhi ya juu.Babake alikuwa mkurugenzi katika shir ika la utohaji huduma za simu huku mamake akiwa mwalimu mkuu wa shule ya kitaifa. Anakumbwa na changamoto za ujana na kushindwa kudhibiti matamanio yake huku akipata ujauzito. Wazazi wake wanamdhulumu na kuishia kutoroka nyumbani. Anaokolewa na Mtawa Pacha anapata utulivu uk100 Chandachema anapata utulivu baada ya kuokolewa na shirika la kidini la hakikisho la haki na utulivu. Alikuwa mtoto wa mwalimu wa Fumba na Rehema ambaye alizaliwa nje ya ndoa kati ya mauhusiano ya mapenzi ya mwalimu na mwanafunzi wake. Anakosa malezi mema na madhila ya unyanyasaji wa kijinsia uliosababishwa na bwana Tenge.uk 107 Uk127 Mwangeka wanapomuaga binti yao Umu alimwambia kuwa siku ile tuliyokuja kukuchukua kwa mwalimu Dhahabu ilikuwa siku ya heri kwangu. Dick alimweleza Umu kuwa siku waliokutana katika uwanja wa ndege na wakasafiri pamoja, hiyo ndiyo ilikuwa siku ya heri zaidi kwake. Nasaha alizopewa na Umu zilimfunza thamani ya maisha. Kisadfa, huu ndio wakati Dick alikuwa ameamua kubadilisha maisha ya kuuza dawa za kulevya na kuamua kuuza vitu vya umeme. Baada ya Mwaliko kujitambulisha kwa Umu na Dick na kushukuru pia wao wanashukuru kupata walezi wazuri, umu na Dick hawakungojea alize.Walikimbia wote wakamkumbatia ndugu yao,wakaanza kulia huku wakiliwazana. Sophie na Ridhaa pia walijiunga nao, wote wakalizana na baadaye wakashikana mikono. Ikawa ni hali ya utulivu. Uk 1 89 Mwaliko alimwambia babake kuwa kuja katika hoteli ya Majaliwa kuliwaletea heri kwa kuwa familia yao sasa imepanuka. Sasa amekutana na watu aliokuwa tu anasikia wakitajwa. Anasema kuwa imekuwa heri tena kuwa, uncle Mwangeka ndiye mzazi na mlezi wa ndugu zake. Uk 1 90 Dick alitoa shukrani tele kwa Umu kwa kuwa ni yeye alimpa matumaini kuwa siku moja watampata ndugu yao Mwaliko. Mwaliko hata anapomtazama Umu, macho yake yakiwa yamefunikwa na vidimbwi vya machozi, anajua kuwa familia yao imerudiana japo katika mazingira tofauti. Mwangeka anapomtazama Apondi anamfurahia kwani yeye ndiye anayempa utulivu wa moyoni. Hapo kabla babake aliishi kumwambia aweze kumtafuta mpenzi na kumuoa ila aliishia kusema kuwa alishindwa kumsahau Lily na Becky. Hata hivyo, Ridhaa alijua kuwa wakati ndio mwamuzi, ipo siku atakapotokeza hurulaini wake Mwangeka. Ataifungua kufuli kubwa iliyoufunga moyo wake na hiyo itakuwa siku yakumwaga chozi la heri
5 Comments
|
Uchambuzi wa Chozi la Heri na Assumpta K MateiCATEGORY
ARCHIVES
AUTHOR
M.A NYAMOTIB.ed Science [MKU] RSS FEEDS
CHOZI LA HERI![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
|