SURA YA KWANZA
Chini ya mti mmoja kando ya mto Kiberenge, vijana wawili, amani na Imani wanapunga hewa baada ya kukata kiu. Aidha, wamo safarini kuelekea Sokomoko, kila mmoja na haja yake. Kitambo kidogo tu, wawili hawa wamevunja mwiko kwa kuyanywa maji ya mto kiberenge ambao wenyeji wanaamini kuwa haramu. Muda si kitambo, wenyeji hawachelewi kuambizana na kusimuliana juu ya waja wawili, waliovunja mwiko kwa kuyanywa maji haramu ya Kiberenge na wakakosa kuaga dunia. Kwa kweli, wakati mwingine haramu huweza kuhalalishwa kulingana na watendwa. Imani anayo imani kwamba hakuna haja yoyote ya kuogopa kutenda bila kujaribu.
0 Comments
UTANGULIZI
“Kidagaa Kimemwozea” ni kitabu chenye jalada jeusi iliyorembeshwa kwa picha ya mwanamwali mmoja mrembo aliyekuwa akidondoshwa na machozi. Riwaya hii ni aina ya kipekee,inayothibitisha usanii wa kupigiwa mfano jinsi ndoto ya uhuru barani Afrika ilivyogeuka kuwa jinamizi inayowafanya wazalendo kulia, “kidagaa kimetuozea” kwa kutamaushwa na usaliti wa viongozi wa baada ya Uhuru.
|