UTANGULIZI
“Kidagaa Kimemwozea” ni kitabu chenye jalada jeusi iliyorembeshwa kwa picha ya mwanamwali mmoja mrembo aliyekuwa akidondoshwa na machozi. Riwaya hii ni aina ya kipekee,inayothibitisha usanii wa kupigiwa mfano jinsi ndoto ya uhuru barani Afrika ilivyogeuka kuwa jinamizi inayowafanya wazalendo kulia, “kidagaa kimetuozea” kwa kutamaushwa na usaliti wa viongozi wa baada ya Uhuru.
Hapa twafahamu kuwa kidagaa kilichokuwa kimeoza kiliwaozea wanyonge haswa, kwa kupitia wahusika kama Amani, Imani, Uhuru, DJ, Matuko n.k. wahusika hawa pamoja na wengine ndio wale wanaodhulumiwa na viongozi wao ambao, badala ya kuonyesha uongozi mwema, wanaongoza kwa kuwatesa na kuwanyang’anya na hata kuwaua wananchi wanaofaa kuwalinda.
Hadithi hii imetolewa kupitia safari ya wahusika wawili, Amani na Imani. Wawili hawa wanang’oa nanga kutoka mastakimunini mwao kuelekea mji wa Sokomoko ili kutafuta kazi zitakazowafanya kuishi maisha ya faraja na yenye buheri wa afya. Hata hivyo katika safari yao, wanafika ukingoni mwa mto Kiberenge ambao maji yake yanasitishwa na wenyeji kwa tuhuma kuwa ni maji ya kifo. Amani na Imani wanavunja mwiko huu kwa kuyanywa maji haya. Tendo hili ambalo Imani anadai kuwa ni kuhalilisha yaliyo haramu linawashangaza wenyeji ambao kwa kuogofya matokeo yake, wanagundua kuwa waili hawa hawaathiriki kivyovyote vile.
Msimulizi anapata nafasi nyingine ya kuendeleza masimulizi yake kupitia mto Kiberenge. Kupitia chombo hiki cha mto Kiberenge, msomaji anagundua kwamba ni wale tu wataoyanywa maji haya yaliyo haramu, ndio wanaoweza kuendeleza vita vya kupatia Uhuru. Hili linatimika kwa sababu, mara tu Amani na Imani wanapofika tu Sokomoko, wanaajiriwa na ndugu wawili, Mtemi Nasaba Bora na Mwalimu Majisifu ambao wote ni wanyanyasaji. Kupitia Nasaba Bora, Mwalimu Walibora andhihirisha kuhusu mizozo ya ardhi baada ya Uhuru ambapowanyonge wananyang’anywa mali na mshamba yao kunyakuliwa. Wachochole wananyang’anywa mashamba yao na Mtemi Nasaba na aina yake ambao pia wanatumia vibaya nafasi za uongozi.
Kwingineko, mwandishi anamdhihirisha Majisifu kuwa tapeli aalimu anayewaibia watu miswada yao. Anapokadhibiwa maandishi na wachapishaji wanaomtarajia kuyachambua na kasha kuandika ripoti, anatenda kinyume kwa kuandika ripoti mbovu na kasha hatimaye, kutumia mawazo yao kujiendeleza kiunafiki.
Hili linadhihirisha wazi maovu katika Nyanja za elimu ambapo wanagenzi wetu hutapeliwa ugwiji wao na wale wanaofaa kuwaendeleza.Hata hivo, Amani na Imani wanapigania vita vikali dhidi ya maovu katika jamii baada ya kugundua haki zao. Wanaongoza umati ulio na kiu ya kupata ardhi zao zilizonyakuliwa na Mtemi Nasaba na aina yake. Wanaongoza kikosi takatifu pamoja na wale walio na mawazo kama hayo. Kikosi hiki kinaweza kuwakilisha mabadiliko ya uongozi baada ya Uhuru katika mataifa ya Afrika ambapo hali ya ukosefu wa maendeleo itasitishwa. Riwaya hii bila shaka itawa wa umuhimu kwa wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu. Kando na kazi za awali za Walibora, Kidagaa Kimemwozea inajumuisha utajiri wa usanii, hali kadhalika misemo. Kazi yenyewe kwa kweli inajumuisha vyombo tofauti tofauti vya usanii kama, hadithi ndani ya hadithi,visakale, visaawali na mengineyo, yaliyojumuishwa miongoni mwa waandishi wa riwaya wenye tajriba za juu yalichapishwa hivi majuzi katika nchi za Afrika Mashariki. Ndio upakue, unihitaji kijisajiri kama memba. Bonyeza hapa ... Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |