ATIKA SCHOOL
  • Home
    • Atika School Advanced Search
    • News and Opinions
    • Echo
    • Academic Environment
    • How its Done
    • SITEMAP
    • About Us? >
      • About Us
      • Learn more about us
  • TUTORIALS
    • SECONDARY >
      • SCIENCES >
        • FOCUS MATHEMATICS TUTORIALS AND EXAMS FREE
        • KCSE BIOLOGY NOTES
        • FREE KCSE CHEMISTRY NOTES
        • KCSE PHYSICS NOTES, AUDIOVISUALS AND MORE
      • LANGUAGES >
        • ENGLISH >
          • English KCSE Set Books
          • ENGLISH GRAMMAR #KCSE
        • CHOZI LA HERI - MWONGOZO
        • KIGOGO - MWONGOZO
        • KCSE Kiswahili
      • TECHNICALS >
        • KCSE BUSINESS STUDIES NOTES
        • kcse Computer Studies Notes
        • KCSE AGRICULTURE NOTES, SYLLABUS, QUESTIONS, ANSWERS, SCHEMES OF WORK AND OTHERS
      • HUMANITIES >
        • KCSE History Notes Form 1 to 4
        • FREE KCSE CRE NOTES
        • KCSE GEOGRAPHY NOTES
        • IRE NOTES, AUDIOVISUAL, QUESTIONS AND ANSWERS
    • MASOMO VIDEOS
    • PRIMARY >
      • NOTES >
        • KISWAHILI
        • SOCIAL STUDIES >
          • STANDARD 4: SOCIAL STUDIES
        • SCIENCE
        • ENGLISH >
          • KCPE and Primary Level Compositions
        • MATHEMATICS >
          • KCPE Mathematics Notes
      • EXAMINATIONS >
        • DecaTurbo Online Series Examinations
        • TOP INSHA AND COMPOSITION QUESTIONS
        • CBC Kiswahili
        • FOCUS A365 SERIES K.C.P.E EXAMINATIONS FOR PRIMARY
        • Standard 8 (std) English Topical Questions
      • SYLLABUS >
        • Primary Mathematics Syllabus
  • CURRICULUM
    • NEW CURRICULUM DESIGNS >
      • PRIMARY >
        • PRE PRIMARY ONE CURRICULUM WITH SYLLABUS
        • PRE PRIMARY TWO CURRICULUM WITH SYLLABUS
      • SECONDARY >
        • KNEC KCSE SYLLABUS AND COURSE OUTLINES
      • COLLEGE >
        • Regulations for the TIVET Craft and Diploma Business Examinations
  • PRODUCTS
    • All Categories
    • FREE DOCUMENTS
    • PRIMARY CBC BASED RESOURCES
    • PRIMARY 8-4-4 BASED RESOURCES >
      • STANDARD 8 RESOURCES
    • COLLEGE & VARSITY RESOURCES
    • HIGH SCHOOL RESOURCES
    • FREE NOVELS >
      • COURSE BOOKS
      • KCSE KISWAHILI SETBOOKS
    • Backed Up Files and Archives
  • EXAMINATIONS
    • PRIMARY EXAMS >
      • Assignments and Random Exams
      • 8-4-4 >
        • STANDARD 8 PAST PAPERS 8-4-4 BASED
      • CBC
    • TOP SCHOOLS EXAMINATIONS LATEST >
      • Assignments and Random Exams
    • KCPE >
      • KCPE PAST PAPERS AND ANSWERS
    • KCSE >
      • KCSE BY SUBJECT >
        • KCSE PAST PAPERS BY SUBJECT
        • Free KCSE Past Papers Mathematics
        • Free KCSE Biology Questions and Answers
      • KCSE BY YEAR >
        • KNEC KCSE PAST PAPERS, MARKING SCHEMES, QUESTIONS & ANSWERS
    • QUESTIONS & ANSWERS >
      • SECONDARY >
        • LANGUAGES >
          • ENGLISH POETRY QUESTIONS WITH ANSWERS FOR K.C.S.E CANDIDATES
        • TECHNICALS >
          • COMPUTER STUDIES >
            • COMPUTER STUDIES Q & A
            • kcse computer studies paper 2 AND 3 Questions & Answers
          • BUSINESS STUDIES QUESTIONS & ANSWERS
          • KCSE AGRICULTURE TOPICAL QUESTIONS
          • KCSE HOME SCIENCE DIRECT QUESTIONS AND ANSWERS
        • SCIENCES >
          • KCSE Mathematics Topical Questions
          • KCSE Biology Topical Questions and Answers
          • CHEMISTRY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
          • KCSE Physics Topical Questions
          • KCSE physics Practical Sample Quiz
        • HUMANITIES >
          • ISLAMIC RELIGIOUS EDUCATION (IRE) QUESTIONS AND ANSWERS
          • C.R.E (CRE) QUESTION AND ANSWERS
          • KCSE History Topical Questions and Answers
          • GEOGRAPHY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
      • PRIMARY >
        • Standard 4-8 Mathematics Topical Questions from Mocks and KCPE
        • Std 6 Mathematics Notes
  • HIGH INSTITUTIONS
    • EXAMINATIONS >
      • College and Varsity Past Papers online >
        • College and Varsity Past Papers online
    • TUTORIALS
  • PRICING
  • BLOGS
    • Contact
    • Help & Support
    • MPESA FORM
  • Search Free Documents (PDF)

Follow us now to receive the latest updates @schoolatika

DAMU NYEUSI NA KEN WALIBORA (UCHAMBUZI)

15/4/2018

0 Comments

 

DAMU NYEUSI - Dhamira, Maudhui, Maswala ibuka, Sifa za wahusika, Mbinu za lugha na Uchambuzi wa methali

Dhamira

  1. Mwandishi anajaribu kuonyesha ubaguzi ambao hufanywa na wazungu dhidi ya watu weusi, wao hawahesabiwi kama binadamu kamili. Wazungu hawataki kabisa kutangamana na watu weusi.
  2. Ubaguzi huu huwa mkali sana kiasi kuwa wamarekani wenyewe hubaguana kwa misingi ya rangi. Wamarekani weupe huwabagua wamarekani weusi.
  3. Anadhamiria vilevile kuonyesha masaibu yanayowakumba waafrika ambao huenda Marekani wakitafuta kujiimarisha. Wao hudharauliwa, hubaguliwa, hutusiwa nk.
  4. Anajaribu vilevile kuonyesha kuwa kuna tofauti kubwa sana ya kijamii kielimu na kiuchumi na hata kimazingira kati ya Marekani na Afrika Mashariki.
  5. Kupitia kwa hadithi hii mwandishi vilevile anaonyesha matatizo yanayozikumba nchi za Afrika, mfano ulevi, uyatima, umaskini nk.
  6. Pia anataka kuwasuta waafrika ambao wanataka kwenda ng’ambo wakifikiria kuwa maisha ni mazuri huko. Anawaonyesha masaibu mengi ambayo watapitia endapo wataenda kule.
KCSE Past papers
knec kcse past papers, marking schemes and reports
KCPE Past Papers
KCPE PAST PAPERS AND ANSWERS
English Setbooks
English KCSE Set Books

MAUDHUI

Ubaguzi wa rangi
Wazungu wanawabagua waafrika na hata wamarekani wenzao kwa misingi ya rangi na maeneo watokamo ubaguzi wa rangi unajitokeza hivi.
  1. Uk 23 – Fikirini anadharauliwa kwa kuwa yeye ni mwafrika tena mweusi. Anaulizwa maswali ya kudunishwa.
  2. Uk 22 – dereva wa basi anakataa kusimama kwenye kituo cha mabasi na kumwacha Fikirini. Anakataa kusimama kwa kuwa Fikirini ni mweusi na dereva mwenyewe ni mweupe.
  3. Uk 23 – Fikirini anatozwa faini na polisi mzungu kwa kuvuka barabara huku taa za kuelekeza magari zikiwa zimewaka rangi nyekundu.
  4. Uk 24 – vyuoni alama hutolewa kwa kuwapendelea wanafunzi weupe na kuwakandamiza weusi.
  5. Uk 24 – Fikirini aendapo  kununua vitu kwenye maduka makubwa mlinzi humtafutatafuta kana kwamba anashuku atadokoa vitu vya watu.
  6. Uk 24 – jela imeundiwa mtu mweusi. Wanaume weusi hawapati shahada vyuoni na badala yake wanang’ang’ania kula kalenda.
  7. Uk 24 – anapoenda mkahawani anatazamwa kwa jicho la dharau na wateja na wahudumu.
  8. Uk 24 – Fikirini anaposahau kufunga zipu anaitiwa polisi kuliko kukumbushwa tu aifunge. Inadaiwa kuwa amefanya hivyo maksudi ili kuonyesha uchi wake.
  9. Uk 27 – Fiona na Bob wanamfanyia ukatili japo wao pia ni weusi kama yeye. Bob anatisha kumpiga risasi naye Fiona anatishia kumkata nyeti zake.
  10. Uk 27 – hata wazungu weusi wanawaona waafrika kama ambao wameenda huko kuwasumbua kuliko kukaa kwao Afrika.
  11. Uk 27 – wazungu wanawaona waafrika kama tumbiri.
  12. Uk 26 – wazungu wenyewe wanabaguana Fiona anamwambia Fikirini kuwa kwa watu weupe, kila mtu mweusi ni jambazi.
Elimu
  1. Vijana kutoka Afrika mashariki hupata udhamini kusomea vyuo vikuu huko ng’ambo mf. Fikirini anaenda Marekani kupata shahada ya uzamifu katika kiingereza.
  2. Wanafunzi wazungu wanawabagua wanafunzi weusi kwa kuwauliza maswali ya kijinga na ya kuudhi.
  3. Wahadhiri wanatoa alama kulingana na rangi. Mwanafunzi mweupe anapata maki nyingi kuliko mwanafunzi mweusi.
  4. Wamarekani weusi hufungwa jela na wanajipata wakitumikia kifungu kuliko kusoma.
  5. Nchi za kiafrika zinahitajika kumarisha elimu ili wanafunzi wao wapate elimu papa hapa.
  6. Wazungu hawaaamini kuwa waafrika wanaweza kumudu kiingereza. Ndio maana wanamwuliza Fikirini iwapo anajua kiingereza.
  7. Licha ya kusoma elimu ya vitabu, Fikirini analazimika kusoma elimu nyingine inayohusu maisha ya ugaibuni, mfano namna ya kujibu maswali ya upuuzi amabayo anaulizwa na wazungu.
  8. Pindi wanafunzi hawa wanapomaliza masomo yao wanafaa kurudi kwao ili kuiendeleza nchi yao. Fikirini anataka kumaliza masomo arudi nyumbani.
Uhalifu
  1. Visa vya uhalifu ni vingi mno huko Marekani. Wamarekani weusi hujipata wakila kalenda kuliko kusoma. Hii ni kwa sababu wanashiriki sana katika visa vya utovu wa nidhamu.
  2. Fiona anajifanya mhisani wake Fikirini lakini katika maisha halisi yeye ni jambazi na kahaba.
  3. Chumba chao Fiona na Bob hutumika kama mahali pa kuwaibia na kuwanyanyasa watu hasa wageni. Fikirini ananyang’anywa pesa zake na vitabu.
  4. Wahalifu wana silaha kali kama bunduki na visu. Bob anamtishia Fikirini kwa bunduki naye Fiona natishia kumkata nyeti kwa kisu.
  5. Fikirini anavuliwa nguo na kulazimika kutembea uchi wa mnyama.
Upweke
  1. Awapo ugenini, Fikirini anatamani vyakula vya nyumbani – ugali, matoke, mlenda, mihogo, wali na pilau.
  2. Pia anatamani pombe za nyumbani kama waragi, gongo na chang’aa.
  3. Upweke vile vile unamfanya Fikirini akumbuke wasichana wa kwao. Anasema kuwa wanapendeza na vile vile wana roho safi, wakilinganishwa na wale wa Marekani.
  4. Aibu ambazo alipitia zilimfanya atamani kumaliza masomo arudi kwao Afrika.

MASWALA IBUKA

  1. Elimu – Fikirini anapata udhamini kwenda Marekani kusomea shahada ya uzamifu katika kiingereza. Afikapo huko anateswa na kubaguliwa. Nchi za kiafrika hazijaimarisha elimu vilivyo. Ndio maana watu weusi wanalazimika kutafuta masomo ya juu huko Marekani.
  2. Ubaguzi wa rangi – wazungu hawapendi waafrika na huwaona kama wanaoenda huko kuwasumbua. Fikirini anabaguliwa kwa kuwa alikuwa mweusi.
  3. Wizi/ujambazi – Fikirini anadanganywa na Fiona na kuingizwa nyumbani kwao. Anapokataa kulala na Fiona anaporwa kila kitu na kufurushwa nje uchi. Wamarekani weusi hujipata kifungoni kuliko vyuoni.
  4. Hali ya anga/mazingira – kimazingira, ng’ambo ni tofauti na Afrika Mashariki. Uharibifu wa mazingira unasababisha ukame. Kinyume na Afrika Mashariki, ng’ambo kuna baridi kali na theluji. Inambidi Fikirini kuvaa nguo nyingi ili kupambana na baridi.
  5. Pombe haramu -  Fikirini anashiriki ulevi wa chang’aa, gongo na waragi akiwa Afrika Mashariki. Hivi ni vileo haramu.
  6. Ukahaba – Fiona ni kahaba. Anafanya kitendo kile na wanaume kwa malipo. Ajabu ni kuwa haonekani kuwa na ada maalum anayotoza na inategemea makubaliano kati yake na mteja.
  7. Unafiki – Fiona anajifanya rafikiye Fikirini kumbe ana nia ya kufanya ukahaba naye. Alimdanganya kuwa alitaka kumpeleka shuleni lakini alitaka kumwingiza kwa nyumba yao. Anatumia rangi nyeusi kumnasa Fikirini.
  8. Pia wazungu wanawadhamini waafrika kwa masomo ya juu lakini waafrika wafikapo huko wanabaguliwa na kunyanyaswa.
  9. Uyatima – Fikirini alimpoteza mamake akiwa kidato cha pili toka hapo inambidi ajikaze ili ajilee na awalee wengine.
  10. Njaa – mwandishi anasema kuwa watu wa Afrika Mashariki wanang’ang’ana kufikisha mkono kinywani. Hivi ni kusema kuwa kuna upungufu wa chakula. Nacho chakula cha kizungu hakimkai na hivyo anaishia kuwa na njaa.
  11. Umaskini - nchi za Afrika ni maskini zikilinganishwa na nchi za maghabiri. Hata hivyo Fikirini anatamani amalize masomo yake arudi kwao akafaidi utajiri wa umaskini wao.
MTAZAMO WA WAZUNGU KUHUSU WAAFRIKA NA RANGI NYEUSI KWA JUMLA
  1. Waafrika hawavai nguo.
  2. Kuwa kuna magonjwa mengi sana Afrika – mtu anaugua ukimwi, malaria, polio na utapia mlo.
  3. Kuwa waafrika hutembea uchi.
  4. Kuwa kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe.
  5. Waafrika ni weusi sana -  ni weusi wa kuangukiwa na lami au mionzi ya jua?
  6. Afrika ni nchi si bara.
  7. Waafrika wanaishi kwa miti kama tumbiri.
  8. Wasichana wote wa kiafrika wanakeketwa na kushonwa ili kuzuia ukware.
  9. Afrika ni bara lenye uchawi.
  10. Waafrika wakienda Marekani husumbua tu.
Biology Notes
KCSE BIOLOGY NOTES
Chemistry Notes
chemistry notes
KCSE topical questions
​KNEC KCSE TOPICAL ANALYSIS

SIFA ZA WAHUSIKA 

1. FIKIRINI
  1. Ana subira/mvumilivu – anavumilia mateso na madharau anayofanyiwa huko Marekani. Mfano – kuachwa na basi, kutusiwa na Fiona, kuitiwa polisi na anavumilia baridi kali wakati akitembea shuleni na vilevile anapofukuzwa uchi na Fiona.
  2. Anajiheshimu – wakati Fiona anamtaka, yeye anakataa katakata. Hapapii fursaa hiyo eti kwa sababu imetokea.
  3. Mzalendo/mwenye mapenzi kwa nchi yake.
  4. Japo amepata nafasi ambayo wengi wangeihusudu, anatazamia kwa hamu siku atakapomaliza masomo yake ili arudi kwao Afrika Mashariki.
  5. Vyakula vya ng’ambo na maisha kwa jumla havimkai.
  6. Mwenye utu/ubinadamu – haoni ni kwa nini wazungu wambague ilihali yeye ni binadamu pia. Visa vya kubaguliwa vinamkera mfano anapoachwa na basi.
  7. Msomi – kwa sasa anasomea somo la uzamifu katika lugha ya kiingereza. Amepata udhaminii kutoka kwa serikali ya Marekani.
  8. Anashawishika haraka – Fiona anapomwambia kuwa atampeleka chuoni anakubali kuandamana naye eti wachukue gari la Fiona
  9. Anapomwona akija weusi wake unamshawishi kuwa Fiona ni mweusi mwenzake mambo yanabadilika baadaye.
  10. Mlevi – amewahi kushiriki kwenye ulevi katika vitongoji duni mfano Mathare, Kenya, Ubungo Daresalaam na Kibuye Kampala.
  11. Msiri – anaapa kukiweka siri kisa cha kuvulishwa nguo na Fiona. Hata kama atalewa na kileo kipi ameapa hatakifichua kisa hiki kwa yeyote.
  12. Mtani – napotaniwa na wazungu kuhusu waafrika kwenda uchi anawajibu kuwa wazungu wameanza kuwaiga waaafrika hasa wakati wa kiangazi. Kuwa wakati huu wanawake wazungu huwa hawataki nguo tena; zinawakera.
  13. Mnafiki – anapoambiwa na Fiona kuwa angepelekwa chuoni anajifanya hataki lakini anataka “kisebusebu na kiroho ki papo”.
  14. Mwoga – anapotishiwa na Fiona na Bob alimimina mkojo kwenye sakafu ya ukumbi kutokana na hofu na mishemishe.
  15. Mwenye tahadhari – mwishoni mwa hadithi anakuwa na tahadhari na watu weupe, polisi na ndugu zake weusi.
  16. Ana msimamo dhabiti – anakataa vishawishi vyake Fiona. Si kwamba hakuwa na pesa lakini aliona haifai.
  17. Ana tamaa ya wanawake – anapomwona Fiona moyo unamtuta. Uk 25. Anakumbuka dada zake kule nyumbani- wahaya, wanyankole na wakamba.
UMUHIMU WAKE
  1. Ametumiwa kuonyesha vijana wanaofanya juhudi katika masomo – anapopewa udhamini kwenda Marekani kwa sababu ya juhudi zake za kimasomo.
  2. Kuonyesha namna wazungu wanawabagua watu weusi. Anapatwa na masaibu teletele kwa sababu ya weusi wake.
  3. Ametumiwa kuonyesha maafa yanayowakumba waaafrika wanaoenda ulaya kwa masomo ya juu.
  4. Ametumiwa kuonyesha ulinganuzi wa hali ya maisha katika Afrika mashariki na Marekani mf. Hali ya anga, undugu nk.
  5. Ametumiwa kuonyesha sifa za wahusika wengine mfano Fiona.
  6. Ametumiwa kuonyesha jinsi ulevi umeenea katika Afrika Mashariki kwa kila eneo la Afrika Mashariki analoenda kuna vileo haramu mf. Waragi, gongo na chang’aa.
  7. Ametumiwa kuonyesha ukatili wanaopitia waafrika mikononi mwa wazungu mfano kuvulishwa nguo, kufukuzwa uchi, kutishwa nk.
  8. Anaonyeshwa kuwa waafrika wanaenda ng’ambo wasipojiheshimu na kuwa na msimamo dhabiti basi huenda wasiyafikie malengo yao. Analenga tu elimu licha ya kuwa ana masaibu mengi. Anatamani siku atakapomaliza ili arudi kwao.
2. FIONA
  1. Katili – anamwambia Bob ampige risasi Fikirini.
    • Anamwamrisha Fikirini kuvua nguo licha ya baridi kali iliyoko.
    • Anatisha kumkata nyeti na kisu.
  2. Mkware/kahaba/mzinzi – anamtaka Fikirini kimapenzi kwa malipo
    • Hajali kiasi atakachopewa na Fikirini mradi wana makubaliano.
    • Anamwuliza Fikirini ana pesa ngapi.
  3. Mnafiki anajifanya mzuri kwa Fikirini kuwa angempeleka chuo kumbe alitaka kufanya mapenzi naye apate pesa.
    • Anamwambia Fikirini kuwa yeye ndugu yake lakini anaishia kumvulisha nguo na kuamrisha apigwe risasi.
  4. Mwongo – anamwita Bob haraka haraka kwa madai kuwa Fikirini anataka kumbaka ukweli ni kuwa yeye ndiye aliyetaka kumbaka Fikirini.
    • Anamwambia Fikirini atampeleka chuoni japo hizi zilikuwa hila zake. Hakumpeleka. Aliishia kutaka kufanya mapenzi naye na kumtishia maisha.
  5. Mchafu – nyumba yao ni chafu. Maguo machafu yametapakazwa kiholela na makochi yana utando wa vumbi.
  6. Kigeugeu – anapoona kuwa Fikirini hamtimizii haja zake, anabadilika mara moja. Anakuwa katili na hata kumtishia maisha.
  7. Makubaliano yake na Fikirini yalikuwa kuwa angempeleka chuoni lakini pindi tu Firikini anapoingia kwake, anabadilisha lengo.
  8. Mwizi/mnyang’angi/jambazi – anamwibia Fikirini pesa zake zote. Isitoshe pia anamnyang’anya kadi zake za simu na za benki, vitabu, kalamu nk..
  9. Mbaguzi – anambagua Fikirini kwa misingi ya asili yake. Hawathamini waafrika anaona kuwa waafrika wanaenda Marekani kuwaharibia maisha yao na starehe zao.
  10. Mwenye vitisho – anamwambia Fikirini avue nguo au….
    Anamshikia Fikirini kisu na kumwekea ubavuni.
  11. Mkali – Fikirini anapokataa mambo yake, Fiona anamwita Bob kwa ukali na sura yake inabadilika ghafla na kuwa na ukali.
UMUHIMU WAKE
  1. Anatumika kuonyesha ufuska ambao huendelea katika nchi hizi za kimagharibi. Anamtaka Fikirini kimapenzi licha ya kuwa nduguye Bob yuko katika nyumba iyo hiyo.
  2. Uchafu wa nyumba yake unaonyesha uchafu wa tabia zake. Nyumba imejaa vumbi, nguo chafu na makochi yana utando wa vumbi. Fikirini anaiona hali hii kama fujo.
  3. Yeye mwenyewe haoni haya kumtaka Fikirini kimapenzi kwa malipo. Pia anamfukuza uchi.
  4. Anaonyesha jinsi ubaguzi wa rangi unavyoshika mizizi katika nchi za kimagharibi – waafrika hawatakikani huko na wanaonekana kama ambao wanaenda huko kusumbua. Hakushtakiwa japo anaendeleza ukatili huu. Fikirini anashtakiwa kwa makosa madogodogo.
  5. Ni kielelezo cha ukatili unaendelezwa dhidi ya waafrika – kuwatishia kwa kisu, risasi, kuwavulisha nguo, kuwaibia.
  6. Aonyesha kuwa wamarekani weusi wanaishi kwa hali ya umaskini. Wao huishi kwa nyumba na hali duni.
3. BOB
  1. Ni jambazi sugu – anashirikiana na dadake kuwaibia waafrika wageni.
  2. Mbaguzi – hataki akina Fikirini kule Marekani. Hataki kuitwa ndugu na Fikirini.
  3. Mwenye hadhari -  hataki dadake amuue Firikiri eti maafa yangezuka wakati huo.
  4. Amekosa maadili – ana shughuli za ujambazi ambazo anatenda kwa ushirikiano na dadake.
Angalia wahusika hawa
  1. Wanafunzi chuoni
  2. Dereva wa basi
  3. Mteja mzungu aliyeita polisi.

MBINU ZA LUGHA

TASWIRA
  1. Hali ya anga inatupatia taswira kamili kuhusu jinsi mambo huwa wakati wa baridi. Kila kitu ni cheupe kwa sababu kimefunikwa na blanketi kubwa la theluji.
  2. Umbo la Fiona – mwandishi anasema alikuwa jimama lililofungasha si haba uk 26.
    Uk 25 – mwandishi anasema kuwa alikuwa pandikizi la jimama limekula likashiba hapa anatupatia taswira ya ukubwa wa Fiona.
  3. Uk 24 – taswira ya polisi wa 911 wamemzingira Fikirani na kumwelekeza bastola. Magari yao yakimetamesha taa za dharura.
  4. Chumba cha Fiona na Bob
    Uk 26 – makochi yana utando wa vumbi, maguo machafu yametapakazwa kiholela sakafuni, vumbi limetapakaa kwenye kochi aliloambiwa akalie, taswira hii inadhihirisha uchafu wao.
  5. Uk 29 – Fikirini akikimbia tuputupu kama alivyozaliwa.
  6. Ulevi unaotumika kule Afrika Mashariki unaleta taswira ya umaskini. Watu hulewa chang’aa, waragi, na gongo. Ajabu ni kuwa hata wale ambao wamesoma kama Fikirini wanashiriki katika ulevi huu.
MBINU REJESHI
  1. Uk 22 – wakati Fikirini anaachwa na basi na hivyo kuamua kutembea, ananyapinyapia nyapunyapu na kupepesuka pepesu pepesu, kama mlevi chakari. Katika hali hii alikumbuka siku zake za fahari alipofuatia waragi kwenye kitongoji duni cha kibuye, Kampala, gongo kwenye vichochoro vya ubungo Daresalaam na chang’aa kwenye fondogoo la Mathare, Nairobi.
  2. Uk 22 – taswira ya ubaguzi inapomwingia akirini, anafikiria kuhusu kudhalilishwa kwa mtu mweusi. Papo hapo anakumbuka maneno ya Rais Moi “msifikiri kwamba mzungu anatupenda sisi watu weusi” siku hizo hazikuwa na maana lakini kwa sasa anapobaguliwa basi maneno haya yana maana.
  3. Uk 23 – anapotamani nyumbani kwao na kufafanukiwa kuwa “nyumbani ni nyumbani ingawa pangoni”, anakumbuka mara ya kwanza alipojikuta darasani yeye peke yake mtu mweusi na jinsi mhadhiri mweupe na wanafunzi weupe walivyomsaili maswali ya kumdhalilisha na kumdunisha kwa kumwuliza maswali ya kijinga.
  4. Uk 24 – inapomdhihirikia kuwa jela imeundiwa mtu mweusi, kuwa wanaume weusi wanakula kalenda kuliko kusoma, anakumbuka jinsi yeye mwenyewe alivyoepuka jela kimungumungu. Alienda mkahawani na kuagiza chakula. Baada ya kula akaingia msalani lakini akasahau kufunga zipu. Ndipo mwanamke mmoja mweupe alipopiga simu kwa polisi. Lakini alipopelekwa mahakamani jaji mweusi alimpiga tu faini ya dola 200.
  5. Uk 25- Fikirini anapomwona Fiona, anawakumbuka dada zake kule nyumbani Afrika Mashariki – wahaya aliokutana nao alipokuwa anasomea ualimu katika chuo cha walimu cha Mwanza. Wanyankole aliokutana nao alipowahi kuzuru Uganda Magharibi na wakamba aliokutana nao alipokwenda ziara Kitui.
  6. Uk 29 – Fiona anapomwamrisha Bob ampige risasi Fikirini, Fikirini anamsihi Bob asimpige risasi huku akilia machozi kama mtoto mdogo, katika hali hii Fikirini alikumbuka siku ya mamake mzazi kufa huko kwao Afrika. Fikirini alikuwa katika kidato cha pili. Hakulia wakati huo lakini alijipata akilia mikononi mwa Bob na Fiona.
MISEMO
  1. Likija basi lingine ambalo usukani wake umeshikwa na dereva mweupe uk 22.
  2. ..umetokana na kuangukiwa na lami au kupigwa na mionzi ya jua uk 23.
  3. Sharti ajipende yeye mwenyewe, ajienzi, ajionee fahari uk 23.
  4. Mara mbili ametozwa faini na polisi uk. 23.
  5. …wanang’ang’ana kula kalenda uk 24.
  6. …aliona amekaziwa macho vibaya uk 24. Kufumba na kufumbua, polisi .. uk 24.
  7. Moyo ulikuwa ukimtweta kwa fadhaa uk 24.
  8. Alikuwa hata hajajibu alipopigwa pingu mikononi. Uk 24.
  9. Mtu angefanya hisani ya kumwambia uk 24.
  10. Fikirini alipopiga darubini nyuma hakuwa na budi… uk 24.
  11. ….vinginevyo kisomo chake cha juu kingegonga ukuta. Uk 25
  12. Kwa desturi Fikirini huvaa tabasamu uk 25.
  13. Moyo ulimtuta uk 25.
  14. …huona fedheha kuwasabahi ndugu zao weusi uk 25.
  15. Fikirini alisema kwa roho ya kisebusebu na kijoyo ki papo uk 23.
  16. …alijikuta amesakimu amri na anarudi nyuma uk 26
  17. Maji yamezidi unga uk 26
  18. Akajua dunia hii haimweki tena uk 27.
  19. Mimi namkata na liwe liwalo uk 29.
  20. We utazua zani hapa uk 29.
  21. …kuanza kuhisi vyanda vyake vinakufa ganzi uk 29.
TASHBIHI
  1. Alinyapia nyapunyapu na kupepesuka pepesupepesu kama mlevi chakari uk 23.
  2. Weupe wa theluji umehanikiza na kufunika kila kitu kama blanketi uk 23.
  3. Je, mwaishije kwenye miti kama tumbiri? Uk 23.
  4. ..kumwona yule mama mzungu kama hasidi aliyemwitia polisi uk 24.
  5. Mweusi mwingine aliyekuwa kama kisiwa kwenye bahari ya weupe uk 25.
  6. …akitetemeka kama majani ya mgomba kwenye dhoruba uk 27.
  7. Fikirini alihisi huku akilia machozi kama mtoto mdogo uk 29.
  8. Alijitosa nje tuputupu kama alivyozaliwa uk 29.
  9. Hakuhisi mzizimo wa theluji iliyokuwa inaanguka kama matone ya mvua ya mawe. Uk 29.
  10. Mambo mengine yanakuwa kama ndoto uk 30.
  11. …kukimbia kasi na tuputupu kama mtu aliyepagawa pepo mbaya.
  12. Zilikuwa zimeshika baridi na kuzizima kama mwili wake ulivyozizima.
TABAINI
  1. Anatumia tabaini kusistiza kuhusu wingi wa barafu.
    ..si madirisha, si milango, si paa si kuta, si majani ya miti..
TAKRIRI
  1. Uk 22 – theluji na barafu kila mahali. Kila mahali barafu na theluji.
  2. Uk 22… sharti mtu avae safu ya maguo na maguo na soksi nzito pamoja na viatu, viatu vizito.
  3. Uk 23 nyumbani ni nyumbani ingawa pangoni.
  4. Uk 24 mkahawani alikumbana na mitazamo ya dharau…au mitazamo hiyo haikumshtua.
  5. Uk 25 naam wamarekani weusi, ndugu zake weusi…
  6. Uk 25 – mweusi mwenzake. mweusi mwingine alikuwa kama kisiwa kwenye bahari ya weupe, weupe wa mazingira na weupe wa watu.
  7. Uk 30 hasadiki kama bado yuko hai. Hasadiki kama yote…
  8. Uk 30 “ sasa kaazimia hutahadhari na watu weupe, polisi na ndugu zake weusi. Sasa lazima ajihadhari na ndugu zake weusi.
  9. Uk 29-30 mwandishi anatumia takriri kuonyesha kuwa Fikirini alibaki bila chochote baada ya Fiona kumchakura.
    Hana vitabu, hana mkoba wa vitabu, hana pochi, hana vitambulisho, hana makadi yake mbalimbali.
  10. Uk 29 alijitosa nje tuputupu.
METHALI
  1. Uk 23 – nyumbani ni nyumbani ingawa pangoni – Fikirini alikuwa akitamani nyumbani. Hii ni baada ya kukumbuka siku yake ya kwanza alipojikuta mweusi peke yake darasani.
  2. Uk 24 – simba akikosa nyama hula nyasi – Fikirini alibidika kula chakula cha Marekani. Si kitamu kama cha kwao.
  3. Uk 24 – baharia wa pemba kufa maji mazoea. Fikirini alizoea kutazamwa vibaya/kudharauliwa.
  4. Uk 29 – siku ya kufa kwa nyani miti yote huteleza – yaani mambo yakianza kuharibika, hata mtu afanye nini hakuna linalotengenea.
KINAYA
  1. Ni kinaya kuwa wamarekani weusi wanawabagua waafrika kwa misingi ya asili yao (Afrika) ilihali wao wenyewe wana asili yao katika Afrika yenyewe.
  2. Ni kinaya kuwa wamarekani wako mstari wa mbele kushinikiza mataifa ya Afrika kuhusu utekelezaji wa haki za kibinadamu ilihali Fikirini aendapo huko haki zake za kibinadamu zinavunjwa.
  3. Polisi nchini Marekani wana jukumu kubwa sana la kulinda usalama. Hata hivyo wanamdhalilisha Fikirini.
  4. Elimu ya Marekani ni ya kiwango cha juu. Hata hivyo kuna wamarekani ambao wanatumikia vifungo kuliko kusoma.
  5. Uk 24 – Fikirini anafikiria kuwa yule mama mweupe anapiga simu kwa sababu kasonona na mpenziwe au ameolewa na ndoa yake inaelekea kusambaratika. Kumbe alikuwa akiwapigia polisi simu kwa sababu ya Fikirini.
  6. Uk 24 – ni kinaya kwa polisi kumwuliza Fikirini iwapo anazungumza kiingereza. Yeye ni mwanafunzi wa uzamifu katika somo la kiingerza na labda hata anajua kiingereza kuliko askari hawa.
  7. Uk 25 – Fikirini anafurahia sana anapomwona Fiona. Anamfikiria kuwa mweusi mwenzake. Baadaye Fiona anageuka kuwa jambazi na hata kuyahatarisha maisha ya Fikirini.
  8. Ni kinaya kuwa wamarekani weupe wanawabagua wamarekani weusi ilhali wote ni wamarekani ambao wako na haki sawa kama wananchi.
  9. Ni kinaya kuwa Fikirini anabaguliwa na wamarekani ilhali serikali yenyewe imempa udhamini. Walimpa udhamini ili wakambague? Wao ndio waliomwita.
  10. Uk 23 – ni kinaya kuwa wazungu wanawacheka waafrika kuwa hawavai nguo ilhali wazungu wenyewe (wanawake) hawataki nguo hasa wakati wa kiangazi.
DAMU NYEUSI.pdf
View  |  Download 333k

GILASI YA MWISHO MAKABURINI.pdf
View  |  Download

mAONI YA mSOMI

Submit
0 Comments



Leave a Reply.

    Categories

    All
    CHOZI LA HERI
    DAMU NYEUSI
    KIDAGAA KIMEMWOZEA
    TUMBO LISILOSHIBA

    Archives

    January 2020
    August 2018
    April 2018

    RSS Feed

atika school app
Download our Android App

Primary Resources
  • K.C.P.E Past Papers
  • ​Pri - Primary 1 Level
  • Pri  - Primary 2 Level
  • Grade 1
  • Grade 2
  • Grade 3
  • Grade 4
  • Standard 5
  • Standard 6
  • Standard 7
  • Standard 8
  • English
  • Kiswahili
  • Social Studies
  • Science
  • Mathematics
  • Kenya Sign Language
  • I.R.E
  • ​H.R.E
  • Notes
  • Termly Questions
  • Mocks
  • K.C.P.E Past Papers
College Resources
  • E.C.D.E
  • P.T.E
  • D.T.E
  • Technical Diploma
  • Technical Certificate
  • Business Diploma
  • Business Certificate
  • Higher Diploma
  • K.A.S.N.E.B Resources
  • K.M.T.C Resources
  • Varsity Resources
Secondary Resources
  • K.C.S.E Past Papers
  • Form 1
  • Form 2
  • Form 3
  • Form 4
  • Term 1
  • Term 2
  • Term 3
  • English
  • Geography
  • History
  • C.R.E
  • I.R.E
  • ​H.R.E
  • Home Science
  • Computer Studies
  • Business Studies
  • Agriculture
  • Chemistry
  • Biology
  • Physics
  • Mathematics ALT A
  • Mathematics ALT B
  • Kiswahili
  • French
  • Germany
  • Arabic
  • Aviation
  • Art & Design
  • Drawing & Design
  • Building & Construction
  • Metal Works
  • Wood Work
  • Music
  • Kenya Sign Language
  • Electricity
Other Useful Links
  • Academic Environment
  • How its Done
  • News and Opinions
  • Manyam Franchise Support
  • About
  • SITEMAP
  • FOCUS A365 SERIES
  • Membership Details (KCPE/KCSE)
  • Secondary Mocks
  • SYLLABUS
Contact Us

    Send Us a Message

    Max file size: 20MB
Submit
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii
Tel: 0728 450 424
Tel: 0738 619 279
Tel: 0763 450 425
E-mail - sales@manyamfranchise.com
  • Home
    • Atika School Advanced Search
    • News and Opinions
    • Echo
    • Academic Environment
    • How its Done
    • SITEMAP
    • About Us? >
      • About Us
      • Learn more about us
  • TUTORIALS
    • SECONDARY >
      • SCIENCES >
        • FOCUS MATHEMATICS TUTORIALS AND EXAMS FREE
        • KCSE BIOLOGY NOTES
        • FREE KCSE CHEMISTRY NOTES
        • KCSE PHYSICS NOTES, AUDIOVISUALS AND MORE
      • LANGUAGES >
        • ENGLISH >
          • English KCSE Set Books
          • ENGLISH GRAMMAR #KCSE
        • CHOZI LA HERI - MWONGOZO
        • KIGOGO - MWONGOZO
        • KCSE Kiswahili
      • TECHNICALS >
        • KCSE BUSINESS STUDIES NOTES
        • kcse Computer Studies Notes
        • KCSE AGRICULTURE NOTES, SYLLABUS, QUESTIONS, ANSWERS, SCHEMES OF WORK AND OTHERS
      • HUMANITIES >
        • KCSE History Notes Form 1 to 4
        • FREE KCSE CRE NOTES
        • KCSE GEOGRAPHY NOTES
        • IRE NOTES, AUDIOVISUAL, QUESTIONS AND ANSWERS
    • MASOMO VIDEOS
    • PRIMARY >
      • NOTES >
        • KISWAHILI
        • SOCIAL STUDIES >
          • STANDARD 4: SOCIAL STUDIES
        • SCIENCE
        • ENGLISH >
          • KCPE and Primary Level Compositions
        • MATHEMATICS >
          • KCPE Mathematics Notes
      • EXAMINATIONS >
        • DecaTurbo Online Series Examinations
        • TOP INSHA AND COMPOSITION QUESTIONS
        • CBC Kiswahili
        • FOCUS A365 SERIES K.C.P.E EXAMINATIONS FOR PRIMARY
        • Standard 8 (std) English Topical Questions
      • SYLLABUS >
        • Primary Mathematics Syllabus
  • CURRICULUM
    • NEW CURRICULUM DESIGNS >
      • PRIMARY >
        • PRE PRIMARY ONE CURRICULUM WITH SYLLABUS
        • PRE PRIMARY TWO CURRICULUM WITH SYLLABUS
      • SECONDARY >
        • KNEC KCSE SYLLABUS AND COURSE OUTLINES
      • COLLEGE >
        • Regulations for the TIVET Craft and Diploma Business Examinations
  • PRODUCTS
    • All Categories
    • FREE DOCUMENTS
    • PRIMARY CBC BASED RESOURCES
    • PRIMARY 8-4-4 BASED RESOURCES >
      • STANDARD 8 RESOURCES
    • COLLEGE & VARSITY RESOURCES
    • HIGH SCHOOL RESOURCES
    • FREE NOVELS >
      • COURSE BOOKS
      • KCSE KISWAHILI SETBOOKS
    • Backed Up Files and Archives
  • EXAMINATIONS
    • PRIMARY EXAMS >
      • Assignments and Random Exams
      • 8-4-4 >
        • STANDARD 8 PAST PAPERS 8-4-4 BASED
      • CBC
    • TOP SCHOOLS EXAMINATIONS LATEST >
      • Assignments and Random Exams
    • KCPE >
      • KCPE PAST PAPERS AND ANSWERS
    • KCSE >
      • KCSE BY SUBJECT >
        • KCSE PAST PAPERS BY SUBJECT
        • Free KCSE Past Papers Mathematics
        • Free KCSE Biology Questions and Answers
      • KCSE BY YEAR >
        • KNEC KCSE PAST PAPERS, MARKING SCHEMES, QUESTIONS & ANSWERS
    • QUESTIONS & ANSWERS >
      • SECONDARY >
        • LANGUAGES >
          • ENGLISH POETRY QUESTIONS WITH ANSWERS FOR K.C.S.E CANDIDATES
        • TECHNICALS >
          • COMPUTER STUDIES >
            • COMPUTER STUDIES Q & A
            • kcse computer studies paper 2 AND 3 Questions & Answers
          • BUSINESS STUDIES QUESTIONS & ANSWERS
          • KCSE AGRICULTURE TOPICAL QUESTIONS
          • KCSE HOME SCIENCE DIRECT QUESTIONS AND ANSWERS
        • SCIENCES >
          • KCSE Mathematics Topical Questions
          • KCSE Biology Topical Questions and Answers
          • CHEMISTRY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
          • KCSE Physics Topical Questions
          • KCSE physics Practical Sample Quiz
        • HUMANITIES >
          • ISLAMIC RELIGIOUS EDUCATION (IRE) QUESTIONS AND ANSWERS
          • C.R.E (CRE) QUESTION AND ANSWERS
          • KCSE History Topical Questions and Answers
          • GEOGRAPHY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
      • PRIMARY >
        • Standard 4-8 Mathematics Topical Questions from Mocks and KCPE
        • Std 6 Mathematics Notes
  • HIGH INSTITUTIONS
    • EXAMINATIONS >
      • College and Varsity Past Papers online >
        • College and Varsity Past Papers online
    • TUTORIALS
  • PRICING
  • BLOGS
    • Contact
    • Help & Support
    • MPESA FORM
  • Search Free Documents (PDF)