utawala mbaya ni tatizo sugu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika; Jadili kwa kurejelea matukio ishirini katika tamthilia ya kigogo.(al 20)
10x2 Mwalimu akadirie
0 Comments
a) Eleza muktadha wa dondoo hili ( al4)
Mnenaji ni Boza, mnenewa ni Sudi,mahali ni karakanailiyoko sokoni chapakazi.Kenga alikuwa amewaletea keki ya uhuru naye Sudi akakataa kuila kwani anaiona kama masazo kwa sababu ile nzuri imeliwa kwingine
b) eleza tamathali ya usemi uliotumika (al2)
msemo:
shika hamsini zako hatutaki kufunga nira c) uongozi wa majoka umesheheni sumu ya nyoka.Thibitisha kauli hii kwa kudokeza hoja saba (al14)
Mwalimu akadirie jibu “ Do!Do!Si mameni !Si mameni ! leo kutanyesha mawe!“maswali
i . Eleza muktadha wa dondoo hili ( Alama 4)
ii. Fafanua mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo hili ( alama 4 iii . Huku ukitoa mifano jadili hoja sita zinazodhihirisha jinsi mwanamke alivyasawiriwa katikaTamthilia ya Kigogo ( alama 12) majibu
Ni maneno yaNgurumo
Anawaambia walevi wenzake Wako Mangweni kwa Mamapima/Asiya Anayasema maneno haya anapowaonaTunu na Sudi kwa mamapima ,jambo ambalo halikuwa la kawaida. (al 4) i. Nidaa- Do! Do ! Do!
ii.
(zozote 12X1=12) “ Sitaki kazi za uchafu hapa …”(a) Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
(a)
Msemaji- Majoka Msemewa- Ashua Mahali- Ofisini kwa Majoka Kiini- Baada ya Ashua kuoimba msaada kwa sababu wanawe walilala njaa 4x1 (b) Kwa kurejelea hoja kumi, onyesha jinsi kinaya inajitokeza katika tamthiliya (alama 10)
(b)
(i) Soko ni chafu-maji ya povu kwenye mtaro (ii) Anamtaka Ashua mapenzi ilhali ana mke. Huu ni uchafu wa kimaadili. (iii) Wanafunzi wa Majoka and Majoka Academy hawafuzu- kuwa makabeji kutokana na sumu ya nyoka (iv) Ngurumo kuzikwa juu ya maiti wengine (v) Kenga kumsaliti Majoka (vi)Majoka kuwakuta watu achache kwenye lango la soko (vii) Akina Kombe na Boza kupewa makombo ya keki ilhali wao ndio wanazalisha (rasilimali inatumiwa kwingine) (viii) Kulipa kodi na kitu juu yake (ix) Majoka anaamrisha mauaji ya Jabali na raia wengine ( mikono yake ni michafu-ina damu) (x)Mamapima kupewa kibali cha kuuza pombe haramu 10x1 Mwalimu akadirie kazi ya mwanafunzi (c ) Fafanua sifa sita za msemaji (alama 6)
(c)
(i) Katili (ii) Mkware (iii) Mwenye tamaa-mali (iv) Mwenye dharau- zebe wako (v) Mpyoro (vi) Mbinasfi (vii) Mfisadi 6x1 Lazima mwanafunzi aeleze ndiposa apewe alama kamili. Mwalimu akadirie kazi ya mwanafunzi “Asante ya punda kweli ni mateke, sikujua ungekuja kunihangaisha hivi”. a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Al 4)
Eleza muktadha dondoo hili
b) Fafanua tamathali ya usemi katika dondoo hili (Al 2)c) Kauli hii ina maana gani kwa mujibu wa muktadha huu (Al 2)
Kauli hii ina maana gani kwa mujibu wa muktadha huu?
Majoka anajuta kwa kugharamia masomo ya Tunu ambaye sasa amekuja kumhangaisha kwa kupinga utawala wake. d) Onyesha jinsi anayeambiwa maneno haya anavyoangaisha mzungumzaji. (Al 4)
Onyesha jinsi anayeambiwa maneno haya anavyomhangaisha mzungumzaji
e) Jadili jinsi hali ya “Asante ya punda ni mateke” inawaafiki wanasagamoyo.(Al 8)
Jadili jinsi ambavyo hali ya “asante ya punda ni mateke” inawaafiki wasagamoyo
Tathmini maudhui ya ndoa kwa mujibu wa tamthilia ya kigogo. (Al 20)Tathmini maudhui ya ndoa kwa mujibu wa tamthilia ya “Kigogo”
”Hayatapoa…kumewaka na kutateketea tusipouzima moto.Liwalo na liwe!”a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Bainisha vipengele viwili vya kimtindo vinavyojitokeza katika dondoo hili. (alama 3)
c) Tathmini umuhimu wa anayeambiwa maneno haya katika tamthlia. (alama 5)
d) Onyesha jinsi mzungumzaji alivyouzima moto uliokuwa umewaka jimboni Sagamoyo. (alama 8)
Mzungumzaji ni Tunu
SOMA SHAIRI KISHA UJIBU MASWALI.
1. Sidhani ni kichekesho, kesho kuwepo sidhani
Vilivyoko ni vitisho, viwewe na visirani Mimi kupe kwenye josho, la sumu iso imani Kesho yangu imeshaliwa.
2. Kesho yangu imeshaliwa, isibaki hata kitwa
Kwamba hai nitakuwa, kesho na kesho kutwa Hilo haliwezi kuwa, na wakati limepitwa Na i wapi kesho yangu?
3. Sikwambii mtondoo, au ni mtondogoo
Ajapowika jogoo, kesho sipo ng'oo Hata simu za "haloo", hazinipati "haloo" Nitaituhumu kesho.
4. Kesho nitaituhumu, kwa sababu ya hasama
Hasama ya mahasimu, waliolishana njama Kutaka kunihujumu, wanizulie nakama Itokapi yangu kesho?
5. Wa kwanza huyu Ukimwi, daima aniotea
Kwa dawa huyu hazimwi, haachi kuturingia Amekuwa kama zimwi, mtu lisilomjua Ati nipangie kesho?!
6. Nipange yangu matanga, au kujenga nyumba?
Nipange kung'oa nanga, au shairi kuimba? Nipangeni cha kupanga, biashara za mtumba? Kesho si ukoo wangu.
7. Ukimwi nduguze wako, Ebola na Malaria
Kichomi na sekeneko, mno wajifaragua Maadamu wangaliko, vipi kesho kuwazia? Kesho si ndu yangu mwandani.
8. Mimi napangia leo, maana kesho sijui
Usafiri nifanyao, kwenye vyombo anuwai Una mikasa kibao, majanga ya kila nui Salama yangu i wapi?
9. I wapi salama yangu, huku wapo wa kijicho
Ngaa nipatapo changu, waingiwa mpekecho Kunipikia majungu, nikikosa changu hicho Waso nitakia kesho!
10. Kesho wasonitakia, watele kama siafu
Majambazi nasinzia, tapeli na wazinifu Roho yangu wapania, kunipeleka kwa ufu Nipewe jina "Hayati" MASWALIa. Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (4)
Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (alama 4)
b. Hili ni shairi la aina gani? (1)
Shiari hili ni la Tarbia kwa sababu lina mishororo minne katika kila ubeti.
c. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (4).
Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa anaituhumu kesho yake kwa sababu ya uhasama. Anasema uhasama huu unatokana na mahasimu wanaopanga njama ya kumhujumu. Wanataka tu kumsababishia nakama. Mwandishi anamalizia kwa kuuliza kesho yake itatoka wapi na haya mambo yote yanayomzunguka yanaitishia hiyo kesho.
d.. Eleza mbinu nne za lugha zilizotumiwa. (4)
e. Andika bahari kwa kuzingatia vigezo; (2).
|
author
M.A NYAMOTIB.ed Science archives
Archivescategory
rss feeds
|