KCSE 2018: KISWAHILI PAPER 3 QUESTIONS AND ANSWERSKiswahili Paper 3
SEHEMU A: USHAIRI
1. Lazima
A. Mazrui: Chembe Cha Moyo Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Nimeyaandika maneno haya Kwa niaba ya: Mamilioni wasio malazi wabebao vifurushi vilivyo wazi wazungukao barabarani bila mavazi ...milki yao ya maisha. Kwa niaba ya: Maelfu wanouawa bila haki wiki baada ya wiki leo sumu au spaki leo kamba au bunduki na kwa wale wanosubiri kunyongwa. Kwa niaba ya: Vijana walio mitaani wale mayatima wa maskini wazungukao mapipani kila pembe mjini kuokota sumu kutia tumboni kujiua bila kujua ili kupata kuishi. Kwa niaba ya: Wakongwe wasio jiweza walao chakula kilichooza wachukuao choo wakijipakaza polepole waki jiangamiza katika vyumba vyao baridi na giza kwa sababu hawana watazama wala wauguza. Kwa niaba ya: Waishi na nyingi hofu kwa sababu ya madawa tifutifu yatiwayo vyakulani yakitufanya wafu Bila ya mtu kuona kama kwamba sote tu vipofu, Na kwa niaba yetu sote; Tuliofungwa vifungoni, duniani Tuliosukumwa kingoni, maishani Tuliopokonywa maoni, machoni Tuliotiliwa sumu, malishoni Tuliodidimizwa kinyesini ili ‘maendeleo’ yaendelee kwenda njiani huku yakitema machicha ya roho zetu.
SEHEMU B: RIWAYA
K. WALIBORA: KIDAGAA KIMEMWOZEA JIBU SWALI LA 2 AU LA 3.
2. “Riwaya hii ya ama yake inathibitisha kwa usanii wa kupigiwa mfano jinsi ndoto ya uhuru barani Afrika imegeuka kuwajinamizi.”
SEHEMU C: TAMTHILIAP. Kea: Kigogo
Jibu swali la 4 au la 5.
4. Tusiwaruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kikoloni kuturejesha kwenye utumwa.
Hatuwezi kukubali kutawaliwa kidhalimu tena!”
5. “Si haki! Unayazika matumaini yetu. Unaifukia kesho yetu.”
SEHEMU D: HADITHI FUPIA. Chokocho na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadhithi Nyingine
Jibu swali la 6 au la 7.
Said A. Mohamed: “Tumbo Lisiloshiba”
6. “. . .lakini hakuiruhusu sahau iketi na kutawala kichwani mwake. . .hapoi.. .Angepoaje na ule moto unaomiipukia kila mtu pale mtaani, umeacha mpaka sasa kovu bichi moyoni mwa kila mtu. . .?“
7. Onyeshajinsi maudhui ya utabaka yalivyoshughulikiwa katika Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine kwa kurejelea hadithi zifuatazo:
SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
(A) SOMA UTUNGO UFUATAO IDSHA UJIBU MASWALI.
Nalilitizama jua la kinjano
Likijikokota kwajitimai kutua Mbele ya nguu ya miima uso kikomo likipisha machweo yenye giza la kaniki Likishindilia uzito wa nanga kwenye moyo tepetevu uloonja shubiri ya kwondokewa.
Twalitazamana na hiyo shamsi
ikipotelea kwenye upeo wa macho huku nyuma ikinambia “yamekwisha.”. Naliona kope zake zikimezwa na kiza Nikaliona jua likitoweka pamwe nawe Jagina wa maisha yangu. Nikaliona likikokota aushiyo likabwakura rohoyo kutoka kwenye vyangu vitanga.
Kumbukizi zilikuleta
kwenye jukwaa la akili yangu pazia likafunguka likayaleta mawio ya siku ya kuamkia kuuka kwako. Nalikuona kwenye ruya ukitazamana ana kwa ana na hasidi alokakawana kutuhasiri mi nawe Nalikiona kipaji chako kikitwaa wasiwasi ukawa ni kama wanywea kwa wake mtazamo.
Hata uliponishika
mkono kunambia tukimbile tui iponye nalikuwa nimechelewa ulikuwa keshanipa kisogo, huku nyuma waniita, “Mwanangu, njoo tujisalimishe Mwanangu njoo, nguvu zimenisha.” Kumbe hiyo ilikuwa tahadhari kwamba Iziraili yu karibu moyowe kuchukua? Kumbe wali ukisema,’Buriani mwanangu?”
Siku ya faradhi ilifika, mkono kulazimika kukupungia
Naliutazama mwilio mtukufii Nalilitazama tambolo liloumbuka wali umedhibitiwa shujaa wangu ndani ya chumba chenye kuta na paa la mbao. Hata tulipokukaribisha, kwa lako kaburi Nilijipa kujiambia, “Hajenda popote mtima bado wapiga.” Nalingoja unisalimu Nalingojea tabasamu lako lenye haya Ela hayo hayakutimila Walikuwa kesha kwenda Kuwa milki, ya ardhi isoshiba.
Hata waliponena, “Udongo kwa udongo,”
Nilikusikia ewe yeli uso kifani ukighani ubeti wa wimbo wako pendwa mawazoni mwangu, “Kifo ni hasidi, Ikiwa mimi Gunge Roho yangu nitamkabidhi Iziraili Mimi niliyekaidi bunduki ya Mzungu Katika kitali cha miaka minne Kwetu kukarudi fahari na jina. Mimi niliyeshindana na ndui na tetekuwanga, iliyowapukutisha wana wote wa Ngome Nikabaki mimi, jogoo wa kijiji.
“Kifo ni shujaa,
Ikiwa mimi Gunge mwili wangu huu mtukufu kwa tambo na nemsi nitaukubalia kuwa lengo la dua za kuonewa imani kuwa karamu ya macho ya mahasimu kuvikwa suti na mwosha kufunikwa kwa udongo uliolaaniwa Mimi Gunge, Niliruhusu jabali kubwa Likibinye changu kichwa Likidhibiti changu kidari Linizibe zangu pumzi Gunge niache ktitawala.”
(b) Fafanua mikakati sita ambayo jamii inaweza kutumia iii kuudumisha utanzu wa semi. (alama 6)
0 Comments
|
Archives
December 2019
Categories
All
|