NITAJONGEANitajongea altare yako, furaha yangu na heri siku zote. 1. Peleka mwanga wako na uaminifu wako, viniongoze; vinipeleke kwako, katika hekalu lako takatifu. 2. Nami nitajongea altare ya Mungu, Mungu wa furaha yangu; nami nitakusifu, moyo wangu kwani wasikitika? 3. Nafsi yangu kwa nini kuinama, na kufadhaika; umtumaini Mungu, mbona yeye ndiye nguzu zako.
0 Comments
NIMEONA MAJINimeona maji yakitoka hekaluni upande wa kuume alleluia x2 1. Nao watu wote waliofikiwa na maji hayo wataokoka {nao watasema alleluia} 2. Msifuni Bwana kwa maana ni mwema, msifuni Bwana kwa maana {huruma yake ni ya milele} 3. Atukuzwe Baba pia na Mwana, naye Roho Mtakatifu {kama mwanzo sasa na milele} NINGEKUWA NA MABAWANingekuwa na mabawa ningeruka hadi mbinguni, ningekuwa na ufunguo ningefungua mlango wako, {niingie nyumbani mwako, nikuimbie Mungu wangu, katika makao yako, makao ya milele} x2 1. Malaika wanakuimbia, nyimbo nzuri za furaha, makerubi hata maserafi, wanasifu jina lako {mimi} 2. Ningekuwa mimi ni bahari, ningevuma kwa sauti, ningekuwa mimi ni kengele, ningelia usikie {mimi} 3. Bwana mimi nitakuimbia, siku za maisha yangu, nitaimba sifa zako Bwana, ili watu wasikie {mimi} 4. Naamini kwamba siku moja, nitafika mbele yako, natamani sana kuja kwako, kwenye raha ya milele {mimi} NINYI NIMEWAITANinyi nimewaita rafiki zangu x2 Kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu 1. Ninyi nimewaita rafiki zangu, kama mkifanya niliyosema. 2. Ninyi siwaiti tena watumishi, Mtumishi hajui analofanya Bwana. 3. Niliwachagua ninyi mkazae matunda, Mkazae matunda yanayodumu. NIMEKUJA KWAKO Nimekuja kwako Bwana nimekuja kwako, niwe mtumishi wako nikutumikie, ee Bwana, nimekuja kwako Bwana, nimekuja kwako.1. Tazama Bwana nimekuja kwako, niyatimize mapenzi yako.
2. Ninafurahia ahadi yako, ni kitu chenye dhamani kubwa. 3. Unitengeneze niwe salama, msikivu kwa maongozi yako. 4. Mafuta unipake kwenye kichwa, nami niwe wako hadi mwisho. NIMEINGIA HAPA Nimeingia {kwako} hapa mahali patakatifu. Unipokee {Bwana} unitakase nipate neema.10/10/2022 NIMEINGIA HAPA Nimeingia {kwako} hapa mahali patakatifu. Unipokee {Bwana} unitakase nipate neema.1. Nimeingia kwako nimeingia, hapa mahali patakatifu.
2. Njooni kwake kwa nyimbo na kwa shangwe, tulisifuni jina lake. 3. Ee Bwana mwema wewe mfadhili sana, nakuja kwako kukutukuza. 4. Nakuabudu pia nakusujudu, nisaidie mimi ni wako. NIFUNGULIENI MALANGO Nifungulieni malango ya haki {nifungulieni malango} nitaingia na kumtukuza Bwana x21. Makao ya Bwana yapendeza sana {nitaingia} nitoe asante kwake yeye Bwana {daima}
2. Sifa zake nitazitangaza sana {nitaingia} kwa unyenyekevu nimsifu Bwana {daima} 3. Wema wake Bwana ni ajabu sana {nitaingia} nitoe asante kwake yeye Bwana {daima} 4. Mateso na dhiki vyanisonga sana {nitaingia} kwa matumaini nitamwona Bwana {daima} NDIMI MTUMISHI WAKO Ndimi mtumishi wako Nitafurahi kwako Bwana x21. Nitajongea altare ya Mungu, Mungu wa raha ya nafsi yangu
2. Machoni pangu meza imepangwa, wanatazama adui zangu 3. Malishoni mwa majani mabichi, ananitunza nikiwa naye 4. Sifa ziende kwa Baba na Mwana, na kwake Roho Mtakatifu. NAYATAMANINayatamani {kweli} nayatamani makao ya Bwana, {maskani yako Bwana yapendeza kama nini} x2
1. Nafsi yangu, itazionea shauku, nyua za Bwana. 2. Nitaingia, nyumbani mwa Bwana, kwa shangwe nikimwabudu. 3. Heri yetu, kumwabudu Bwana, tutazipata neema. 4. Pendo lake kwa viumbe vyake kweli halina kikomo. NILIKUWA NIMELALA1. Nalikuwa nimelala, Moyo wangu u macho, sikiliza Yesu wangu, Mpenzi wa moyo wangu.
2. Siku zote nakungonja, we mwanangu uje kwangu, usiogope kunijia nitakupokea tu. 3. Nimemwaga damu yangu, Roho yako kuokoa, Damu hiyo ipotee? We mwanangu rudi tu. 4. Ni mapendo yangu kwako, Kuokoa roho yako, We mwanangu, usiogope, Njoo utubu dhambi. 5. Ni tayari kukupokea, Mpenzi wangu, rudi kwangu,furahi pamoja nami, milele na milele. NAJA KWAKONaja kwako Bwana, unipokee mtumishi wako x2 Kuijongea altare yako ee Bwana unipokee, kukutolea sadaka ya Misa ee Bwana unipokee, {kati ya malango yako Bwana napita, niwekee mkono wako nibariki} x2
1. Roho ya Bwana yu pamoja nami, {kwani ameniteua, niwaletee habari njema} x2 2. Ninakuja kwako kukusujudia, {kukutolea shukrani, sala na maombi yangu} x2 3. Nikusujudie ee Mungu wangu, {nifanye toba ya kweli, katika nyumba hii takatifu} x2 4. Nitakuimbia kwa nyimbo nzuri, {nyimbo nzuri za shangwe, kukuabudu ee Bwana Mungu} x2 NAINUA MOYO1. Nainua moyo wangu, kwako wewe ee Baba, unikinge na uovu, tumaini wewe tu.
2. Nijulishe njia zako, nifundishe ukweli, hekimayo 'niongoze, tumaini wewe tu. 3. Ewe Baba ukumbuke, wema wako milele, nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu. 4. Nitazame kwa huruma, ewe Mungu amini, nitubishe mwenye dhambi, tumaini wewe tu. 5. Shida zangu angalia, niokoe dhikini, nisamehe dhambi zangu, tumaini wewe tu. 6. Njia zako zote Bwana, ni fadhili na kweli, niongoze mtoto wako, tumaini wewe tu. MSHUKURUNI MWOKOZI Mshukuruni Mwokozi enyi mataifa, Pigeni vigelegele pigeni makofi x2Tangazeni rehema zake leo asubuhi Semeni ya kuwa Bwana ni mwenye adili x2
1. Njoni tumwimbie Bwana mwamba wa wokovu wetu, mikononi mwake zimo bonde za dunia. Bahari ni yake ndiye aliyeumba, Na mikono yake ilituumba sisi. 2. Bwana ametamalaki mataifa watetema, ameketi juu ya makerubi Mbinguni. Yeye Bwana katika sayuni ni mkuu katukuka juu ya mataifa yote. 3. Mshangilieni Bwana mwimbieni kwa zaburi, vinanda na baragumu vyote mvipige. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema kwa kuwa fadhili zake ni za milele. MPIGIENI MUNGU KELELEMpigieni Mungu kelele za shangwe nchi yote, imbeni imbeni imbeni imbeni utukufu wa jina lake, tukuzeni, tukuzeni tukuzeni tukuzeni sifa zake alleluya.
1. Mwambieni MunguN mwambieni matendo yake {yanatisha} x2 kama nini, kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, malaika wako watakuja kuzichezea mbele yako. 2. Mwambieni Mungu mwambieni matendo yake {yanatisha} x2 kama nini, kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, adui wako watakuja kunyenyekea mbele yako. 3. Nchi yote ni nchi yote itakusujudia, wala kukuimbia, itakusujudia na kukuimbia naam, italiimbia jina lako jina lako. |
AuthorAtika School Team ArchivesCategories |