Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)a) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hizi ( alama 3) (i) Juma alikuja akachukua kitabu akaondoka ……………………………………………………………… (ii) Mti ulikatika ukaanguka ……………………………………………………………… (iii) “Nyanya anashona nguo”.Hamisi akasema ………………………………………………………………………… b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (alama 4) Watoto wale wanafanya kazi lakini wazazi wao wanazungumza nyumbani. ……………………………………………………………………………………… c) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi ( alama 2) (i) Onea …………………………………………………………………………… (ii) Umia …………………………………………………………………………………… d) Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2) Tulifika tukaagana na mjomba hamisi aishiye mombasa …………………………………………………………………………………………… e) Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza tofauti baina ya dhana zifuatazo (alama 4) Sauti ghuna na sauti sighuna ……………………………………………………………………………… f) Onyesha kiima, yambwa, na yambiwa, katika sentensi hii (alama 3) Mwanafunzi alimfutia mwalimu ubao ………………………………………………………………………… g) Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2) “Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo. ……………………………………………………………………… h) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya (alama 2) i. Posa ……………………………………………………… ii. Poza ……………………………………………………… i) Andika sentensi zifuatazo katika hali zilizo kwenye mabano (alama 4) i. Kijikombe chake kilivunjika baada ya kuangukia kijiwe (ukubwa) ………………………………………………………………………… ii. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kisiha (udogo) ………………………………………………………… j) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo (alama 4) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka …………………………………………………………………………… k) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha (alama 2) Nguo zote zimekaushwa na jua …………………………………………………………………………… l) Tunga sentensi kudhibitisha mwingiliano wa maneno yafuatayo (alama 2) Nomino kuwa kivumishi …………………………………………………………………………………… m) Andika kwa wingi (alama 2) Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri ……………………………………………………………………………… n) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2) Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia ……………………………………………………… o) Kamilisha methali ifuatayo (alama 1) Asiye na nadhari… ……………………………………………………… p) Eleza maana ya msemo huu (alama 1) Kwenda mbago… …………………………………………………………… MWONGOZO
a) i) Mfululizo wa vitendo wakati uliopita
ii) Hali ya kutendeka / kuwezekana kwa jambo iii) Katika usemi halisi (Alama 3) c) i) Maonevu, kuonea (kitenzi jina) ii) Umio, maumivu (Alama 4) d) Tulifika, tukaagana na mjomba Hamisi aishiye Mombasa. (Alama 2) e) i) Sauti ghuna zinapotamkwa husababisha kutikisika kwa nyuzi za glota km /b/, /g/, /w/. ii) Sauti si ghuna zinapotamkwa, nyuzi za glota hazitisiki kg /ch/, /sh/, /h/, /l/, /n/. (Alama 4) f) Mwanafunzi – Kiima Ubao – Yambwa Mwalimu – Yambiwa (Alama 3) g) Omari alishangaa baada ya kuona kisura yule kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa Baada ya kumwona kisura yule, Omari alishangaa kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa (Alama 2) h) Posa – Maombi ya kuoa Poza – Tuliza / poesha (Alama 2) i) i) Kombe lake lilivunjika baada ya kuangukia jijiwe (Alama 2) ii) Kijitu kile hakiachi kuandamana na kijibwa chake kilichodhoofika kisiha (Alama 2) j) i) Alikimbia kwenda kuona nyoka ii) Alikimbia alipoona nyoka (Alama 4) k) Jua limekausha nguo zote (Alama 2) l) Nomino kuwa kivumishi Kijana mkulima alituzwa (Alama 2) m) Kuwepo kwa washauri wao kuliwafurahisha mawaziri (Alama 2) n) Mtoto alaye ndiye aliaye ( Alama 2) o) Asiye nadhari siandamane naye (Alama 1) p) Kuenda kandokando (Alama 1)
0 Comments
MATUMIZI YA LUGHA(a) Pigia mstari iliko shadda mara mbili kwenye neno hili ili kuleta maana zake mbili tofauti. Eleza maana hizo. (i) Ala …………………………..…… (ii) Ala (alama 2) ……………..…… (b) Unda kitenzi an nomino kutokana na nomino an kitenzi ulichopewa kwa kufuata mfano uliopewa. (c) Andika kinyume cha sentensi ifuatayo ukizingatia maneno yaliyopigiwa mstari. Zilizala ilipotokea wanafunzi walitulia na kuanza kucheka. (alama 1) ..……………………………………………………………………………… (d) Kamilisha jedwali kwa kauli ifaayo. (alama 4 1/2) (e) Tambua na uainishe vitenzi katika sentensi ifuatayo. (alama 2) Kuzaa si kazi, kazi ni kuvyeleza. ......................................................... (f) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vielelezo vya matawi. (alama 4) Wengi wataitwa lakini wachache watateuliwa .................................................................. (g) Onyesha hali katika sentensi zifuatazo (alama 1) 1. Mwizi akamatwa mtaani Kondele. ............................................................... 2. Nyumba hufagiliwa asubuhi. ................................................................... (h) Kanusha sentensi ifuatayo. (alama 1) Nimemwona Fuchingo na paka wake. ........................................................................ (i) Tunga sentensi yenye kuhusishi cha ‘A’-Unganifu katika ngeli ya I-I, wingi. (alama 1) ............................................................... (j) Andika katika wingi (alama 1) Zigo la kuliwa halilemei .................................................................... (k) Tambua na ueleze aina ya yambwa katika sentensi zifuatazo (i) Mtoto alipigwa vibaya sana na mamake (alama 2) ........................................................................... (ii) Osama alipigwa risasi na wanajeshi (alama 2) ............................................................ (l) Tumia vitate vifuatavyo kutungia sentensi moja moja ili kutofautisha maana zake. 1. Pango (alama 1) .................................................. 2. Bango (alama 1) ............................................................... (m) Onyesha silabi funge kwenye maneno yafuatayo 1. Baiskeli (alama 1) ............................................................................ 2. Muhtasari (alama 1) .............................................. (n) Taja na utofautishe vikwamizo vya meno. (alama 2) .......................................................................................... (o) Geuza katika usemi wa taarifa “Sitatoka hapa leo bila kunilipa. Uliniambiajana nije leo utanilipa. Mbona tena unataka nije kesho?” Mwajiriwa aliteta. (alama 4) ............................................... (p) Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2) Mateka wote waliokamatwa leo watafikishwa mahakamani. ................................................................... (q) Tunga sentensi sahihi ukitumia viunganishi vifuatavyo ipasavyo. (alama 2) (i) Lau ............................................ (ii) Waama ................................................. (r) Pambanua viambishi awali, mzizi na viambishi tamati katika kitenzi. (alama 2) Alituwiaje? ............................................ MAJIBU YA MATUMIZI YA LUGHA
3. MAJIBU YA MATUMIZI YA LUGHA
(a) (i) Ala I Ala I Ala - Tamko la mshangao (ii) Ala / Ala / Ala - Mfhko Wa kubeba ala (b) (i) Kuhukumu / hukumu (ii) Riziki (iii) Husudu / Kuhusudu (iv) Rithi / kurithi (c) Zilizala ilipotokea wanafunzi walibabaika na kuanza kulia. (d) (i) Wangapi? wepi / wapi? gani? (ii) Wangapi? wapi / wepi? gani? (iii) Ngapi? zipi? gani? (e) - Kuzaa - kitenzi jina - Si - t/kitenzi kishirikishi kipungufu - Kuvyeleza - kitenzi jina - Ni - kishirikishi kipundufu / t (g) (i) Hali ya - ka / wakati usiodhihirika / wowote. (ii) Hali ya - hu mazoea (h) Sijamwona Fuchingo wala paka wake. (i) Chumvi, sukari, mvua, chai, njia, asali (j) Mjizigo ya kuliwa hayalemei. (k) (i) Mtoto — Yambwa kitondo (ii) Osama — (a) Yambwa kitondo (b) Risasi - Yambwa ala (1) Pango - Tundu, shimo Bango - Maandishi ya kutangaza, tangazo linalobebwa na waandamanaji, tangazo la kampem (m) (i) Baiskeli - bais (ii) Mukhtasati - muh (n) v - ghuna f - sighuna (o) Mwajiriwa aliteta kuwalkwamba asingetoka hapo siku hiyo bila ya kulipwa kwa sababu aliambiwa siku iliyotangulia kuwa aende hapo siku hiyo alipwe I angelipwa. Alitaka kujua sababu ya kumtaka aende siku iliyofuata I keshoye. (p) Tegemezi - Mateka wote waliokamatwa leo Hutu - Watafikishwa mahakamani (q) (i) Kama - Neno lao sharti liwe mwanzoni mwa sentensi (ii) Kwa kweli (r) A — Kiima / mtendo / Nafsi ya 3 — umoja ii — wakati wakati uliopita njeo, tu — Yamwa / watendendewa Nafsi ya — wingi w — mzizi i— kauli kinyambulishi a — kiishio kimalizio je — kiulizi. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (Alama40) a) Tofautisha sauti zifuatazo. (alama 2) /a/ /u/ __________________________________________________________________________ b) i) Ngeli ni nini? (alama 1) __________________________________________________________________________ ii) Maneno haya yamo katika ngeli gani? (alama 2) Tayo __________________________________________________________________________ Kipepeo __________________________________________________________________________ c) Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti kuleta dhana tatu tofauti. (alama 3) Babu alimchapa nyanya __________________________________________________________________________ d) Ainisha mofimu katika neno lifuatalo (alama 3) Sikumkaribisha __________________________________________________________________________ e) Andika katika usemi wa taarifa (alama 3) “Mtapata mwaliko wenu kesho,” alisema Salim __________________________________________________________________________ f) Andika kwa wastani (alama 2) Magoma hayo yatachezwa mawanjani __________________________________________________________________________ g) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari Wanafunzi wenye bidii hufuzu mtihani h) Tofautisha sentensi zifuatazo. (alama 2) i) Ningekuwa na pesa ningenunua simu nzuri ii) Ningalikuwa na pesa ningalinunua simu nzuri __________________________________________________________________________ i) Tunga sentensi ukitumia vihusishi vya: (alama 3) a) Kulinganisha __________________________________________________________________________ b) Sababu __________________________________________________________________________ c) Wakati __________________________________________________________________________ j) Kwa kutoa mifano katika sentensi onyesha matumizi mawili ya parandesi (alama 2) __________________________________________________________________________ k) Tambua kiima, shamirisho, chagizo na kiarifa katika sentensi ifuatayo (alama 4) Nyanya alimjengea mjukuu nyumba kwa matofali mwaka jana. __________________________________________________________________________ l) Eleza tofauti ya kimaana katika sentensi hizi (alama 2) i) Nisimamapo huchekwa ii) Ninaposimama huchekwa __________________________________________________________________________ m) Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia ‘o’ rejeshi na kiambishi ngeli mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo. __________________________________________________________________________ n) i) Eleza dhana ya kishazi tegemezi (alama1) __________________________________________________________________________ ii) Bainisha aina za vishazi (alama 2) Konde iliyopaliliwa ilituletea mazao mengi sana __________________________________________________________________________ o) Tunga sentensi kuonyesha maana mbili za neno chuma (alama 2) __________________________________________________________________________ Mwongozo
a) /a/ ni irabu ya kati (hutamkwa kwa kutumia sehemu ya kati ya ulimi) midomo hutandanzwa inapotamkwa. /u/ ni irabu ya nyuma (ulimi huinuliwa juu na kupindwa nyuma ya inapotamkwa. midomo kuviringwa inapotamkwa. b) i) Ngeli ni kundi la nomino za aina moja ii) Tayo – LI – YA Kipepeo – A – WA c) Babu alimchapa nyanya? (swali) Babu alimchapa nyanya! (mshangao) Babu alimchapa nyanya. (maelezo / taarifa) d) si – kiwakilishi cha ukanushaji ku – kiwakilishi cha wakati uliopita m – kiwakilisha cha mtendwa karib – mzizi ish – kiwakilishi cha kauli a – kiishio e) Salim alisema kwamba wangepata mwaliko wao siku iliyofuata au Salim alisema kuwa tungepata mwaliko wetu siku iliyofuata. f) Ngoma hizo zitachezwa uwanjani g) S – KN + KT KN – N + V + N N - Wanafunzi V – wenye N – bidii KT – T + N T – hufuzu N – mtihani h) i) Nge – huonyesha wakati ujao na kuwa kuna uwezekano ii) Ngali – huonyesha wakati uliopita na hakuna uwezekano / ni majuto i) a) Abunuwasi ni mjanja kama sungura Dhahabu ni ghali kuliko shaba b) Juma ametuzwa kwa uhodari wake c) Jogoo huwika kabla ya saa tisa usiku j) Jona (kijana mpole) anasafiri leo kwenda mjini? maelezo ya ziada Aziza (mhusika mkuu) aliomba talaka Mjomba: (akikohoa) habari? – tamthilia / mazungumzo Kufungia nambari (1) (2) (3) k) Nyanya – kiima Mjukuu – shamirisho kitondo Nyumba – shamirisho kipozi Chagizo – i) mwaka jana ii) kwa matofali Shamirisho ala – matofali Alimjengea – kiarifa l) i) Wakati wowote ii) Wakati maalumu m) Mwanafunzi aliyetumwa nyumbani juzi, hajapata karo hadi leo. n) Kishazi tegemezi – ni kundi la maneno lililo na kiima na kiarifa lakini haliwezi kujisimamia pekee kama sentensi. hutegemea kishazi huru ili kupata maana. o) Watoto hao wanachuma machungwa Nondo za madirisha hutengenezwa kwa chuma Mimi ninafanya kazi ili kuchuma pesa MATUMIZI YA LUGHAa) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hizi ( alama 3)
(i) Juma alikuja akachukua kitabu akaondoka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (ii) Mti ulikatika ukaanguka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (iii) “Nyanya anashona nguo”.Hamisi akasema …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (alama 4) Watoto wale wanafanya kazi lakini wazazi wao wanazungumza nyumbani. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… c) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi ( alama 2) (i) Onea ………………………………………………………………………………………………… (ii) Umia ………………………………………………………………………………………………… d) Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2) Tulifika tukaagana na mjomba hamisi aishiye mombasa …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… e) Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza tofauti baina ya dhana zifuatazo (alama 4) Sauti ghuna na sauti sighuna …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… f) Onyesha kiima, yambwa, na yambiwa, katika sentensi hii (alama 3) Mwanafunzi alimfutia mwalimu ubao …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… g) Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2) “Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… h) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya (alama 2) i. Posa ………………………………………………………………………………………………… ii. Poza ………………………………………………………………………………………………. i) Andika sentensi zifuatazo katika hali zilizo kwenye mabano (alama 4) i. Kijikombe chake kilivunjika baada ya kuangukia kijiwe (ukubwa) ………………………………………………………………………………………………… ii. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kisiha (udogo) ………………………………………………………………………………………………… j) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo (alama 4) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… k) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha (alama 2) Nguo zote zimekaushwa na jua ………………………………………………………………………………………………… l) Tunga sentensi kudhibitisha mwingiliano wa maneno yafuatayo (alama 2) Nomino kuwa kivumishi ………………………………………………………………………………………………… m) Andika kwa wingi (alama 2) Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri ………………………………………………………………………………………………… n) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2) Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia ………………………………………………………………………………………………… o) Kamilisha methali ifuatayo (alama 1) Asiye na nadhari… ………………………………………………………………………………………………… p) Eleza maana ya msemo huu (alama 1) Kwenda mbago… ………………………………………………………………………………………………… |
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |