Jadili maudhui ya ‘asasi ya ndoa’ kama yalivyoangaziwa riwayani Ndoa ni maafikiano rasmi baina ya mwanamume na mwanamke ili waweze kuishi pamoja kama mke na mume. Ridhaa alikuwa na mke kwa jina Terry. Walibarikiwa kuwa na watoto wafuatao: Mwangeka, Tila na marehemu Dede. Ndoa hii haikudumu kwani janga la moto iliisambaratisha aila hii na ndipo Terry, Tila, Lily na Becky wakaiaga dunia. Ridhaa akabaki mjane. Mwangeka alikuta na Lily Nyamvula katika chuo kikuu na kumwoa. Walibarikiwa na mtoto mmoja kwa jina Becky. Ndoa hii haikudumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto. Baada ya ndoa ya mwanzo kusambaratika, Mwangeka alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa. Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema.Hawakufaulu kupata mwana wao kindakindaki japo walipanga mwana wao kwa jina Mwaliko. Kangata alikuwa na mke wake kwa jina Ndarine. Walibarikiwa na wana wafuatao. Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri. Lucia Kiriri -Kangata — alikuwa ameolewa katika ukoo wa Waombwe ambao awali walikuwa maadui sugu wa ukoo wa Mwongezo mzima lakini kutokana na Msimamo imara wa Kangata halikusimama. Watu wa ukoo wa kina Kangata walishangaapikwo nini mwana wao akaozwa kwa watu ambao huvaa nguo nje na pia huzaa majoka ya mdimu ambayo ni machovo kupindukia. Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira. Walibarikiwa na mabinti wawili, Lime na Mwanaheri. Lunga alikuwa na mke kwa jina Naomi. Walikuwa wa watatu, Umu, Dick na Mwaliko. Ndoa hii haikudumu Naomi alimwacha Lunga na kwenda muni alikokuwa shangingi kwelikweli. Pete na Fungo- tunaelezwa kuwa Pete alipoingia darasa la saba alipashwa tohara nao wajombake wakapokea posa na baadaye’ mahari kutoka kwa buda mmoja kwa una Fungo aliyemuoa kama bibi wa nne. Ndoa hii haikudumu kwani Pete alihiari kumwacha baba huyu.
0 Comments
Leave a Reply. |
Uchambuzi wa Chozi la Heri na Assumpta K MateiCATEGORY
ARCHIVES
AUTHOR
M.A NYAMOTIB.ed Science [MKU] RSS FEEDS
CHOZI LA HERI
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |