Jadili maudhui ya kifo kama yanavyoangaziwa katika Riwaya
Kifo/mauti ni hali ya kutokwa na uhai. maneno marehemu mamake kuwa mwanamume hufumbika hisia na kuwa machozi ya mwanamume hayapaswi kuonekana hata mbele ya majabali ya maisha. Terry na wanawe walikumbana na janga hili la kifo baada ya kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba yao. Kangata na Ndarine waliiaga dunia- mwandishi anatujuvya kuwa kwa sasa, miaka mitano imepita na Kangata na Ndarine wameipa dunia kisogo. Kiriri alikumbwa na mauti- mwandishi ametueleza kuwa Kiriri aliiaga dunia muda mfupi kutokana na kihoro cha kufilisikavna ukiwa aliokuwa ameachiwa na mkewe Annette na wanawe. Subira alikumbana na mauti baada ya Subira kuondoka nyumbani alienda mjini Kisuka na baada ya miezi kadha mumewe alimpata kwenye chumba chake akiwa amejifia, Nduguye Mwangeka alikumbana na mauti. Mwangeka anapomkumbuka Tila anatabasamu kisha tone moto la chozi linamdondoka. Kumbukumbu ya Annatila inavuta taswira ya mnuna wake mkembe aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka sita wakati ile Mwangeka akiwa na umri wa miaka kumi na miwili tonna Ile ilipowafika. Baada ya Lunga kuachwa na mkewe aliiaga dunia mwandishi dhuho wa mwaka alifariki na kuwaacha watoto wake na mikononi mwa wao. Vijana waliofyatuliwa risasi waliiaga dunia tumeelezwa walimiminiwa risasi vif uani mwao na wote wakaiaga dunia kifo cha kishujaa kwani walijitolea mhanga kupigania uhuru tatu. Kaizari alitokwa na machozi na kuwahurumia Vijana hawa waliokufa kifo walichoweza kukiepuka. Lily Nyamvula na mwanawe Becky waliiaga dunia- Mwangeka ameketi mkabala mwa kidimbwi cha kuogelea nje ya jumba lake la kifahari ambalo yeye aliliona kama makavazi ya kumtonesho donda lililosababishwo na kifo cha mke wake Lily Nyamvula, Mgonjwa mmoja aliyejifia ni kijana anayesomea shahada ya uzamili, alikuwa mwathiriwa wa pombe haramu. Wasichana waliokeketwa waliaga dunia. Mgonjwa kwa jina Tuama alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake waliokuwa wamepashwa tohara kama yeye. Tunaeezwa kuwa miezi mitatu baadaye ami yake Mwangeka aliyeitwa Makaa alichomeka asibakie chochote alipokuwa akiwaokoa watu ambao walikuwa wakipora mafuta kutoka kwenye lori lililokuwa lime bingiria. Mwanafunzi aongezee hoja.
1 Comment
Alvin Lemiso
5/7/2022 11:24:46
Nice page. Interesting info.
Reply
Leave a Reply. |
Uchambuzi wa Chozi la Heri na Assumpta K MateiCATEGORY
ARCHIVES
AUTHOR
M.A NYAMOTIB.ed Science [MKU] RSS FEEDS
CHOZI LA HERI
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |