Jadili maudhui ya nafasi ya mwanamke katika jamii
Mwanamke amesawiriwa kwa namna mbalimbali: Mwanamke ni Msomi Tila alikuwa akimudu masuala ya sheria. Hakuna aliyethubutu kuuchangia mijadala kwani katika masuala ya sheria Tila alikuwa ameyamudu kweli kweli. Selume- Ridhaa alimfariji na kumwomba asilie kwani mwana wake yu hai tena ana kisomo na amehitimu kama mkunga, anaweza kujitegemea. Umulkheri pia alisoma na kuhitimu vizuri. Mwanomke ni Mjinga Tuama alikuwa amejipata katika hali mbaya kwa kukubai kupashwa tohara. Alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake. Tuama anaitetea mila hii ya upashaji tohara kwa wanawake eti haijapitwa na wakati kwani bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Huu ni ujinga na upumbavu. Mwanamke ni mwenye bidii- tunaelezwa kuwa Umulkheri alikuwa nyuma yake Dick akiwa amepiga foleni. Anasafiri ng’ambo kwa shahada yake ya uhandisi katika masuala ya kilimo. Umu, baada ya kuchukuliwa na Mwangeka na Apondi alifanya bidii masomoni na kufuzu vyema katika mitihani yake. Mwanamke ni mwenye tamaa ya mali Naomi hakuwekwa na mazingira haya mapya(Mlima wa Simba). Asubuhi moja alimtumia Lunga ujumbe na kumtaarifu kuwa ameondoka; akatambe na ulimwengu na huenda akaambulia cha kumsaidia Lunga kuikimu familia. Akawaacha Lunga na wanawe. Mwanamke ni mwenye huruma- Apondi na Neema walijitwika jukumu la kuwalea wana ambao si wao kwa upendo na imani. Mwanamke ni katili muuaji- Mamake Sauna aimsaidia Sauna kuavya mimba aliyokuwa amepachikwa na babake mlezi. Neema naye alikuwa ameavya mimba nyingi akiwa kwenye Chuo kikuu. Mwanamke ni mwenye majuto- Neema aikuwa mwenye kujuta kwa kupoteza nafasi ya kupanga mtoto. Mwanamke ni mwenye kujiheshimu- Zohai amewahi kupigana na majitu yaiiyokuwo yakitako kuuhujumu utu wake kwa kumnyanyasa kijinsia. Mwanamke ni mcheshi- Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza bali alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini.
2 Comments
Mwaniki Rwamba
17/3/2022 15:28:13
Kindly post them in point form
Reply
Leila matano
7/6/2022 21:15:24
Asanteni sana kwa somo hili limenisaidia sana
Reply
Leave a Reply. |
Uchambuzi wa Chozi la Heri na Assumpta K MateiCATEGORY
ARCHIVES
AUTHOR
M.A NYAMOTIB.ed Science [MKU] RSS FEEDS
CHOZI LA HERI
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |