Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Hakikisha kuwa insha yako ina mpangilio mzuri na mtiririko unaofuata hoja kuu.Kuandika insha ni mchakato wa kutumia maneno na sentensi kuwasilisha wazo, mtazamo, au maoni juu ya suala fulani. Hapa kuna hatua muhimu za kuandika insha:
0 Comments
1. Insha ya lazima (Alama 20) Kuzorota kwa nidhamu ya wanafunzi katika shule ya upili ya Mramba, kumemlazimu mkuu wa wilaya hiyo ya Mramba kuteua kamati ili kuchunguza kuhusu utovu wa nidhamu. Wewe ulikuwa mmoja wa kamati hii na ulipewa jukumu la kuandika ripoti ya matokeo. Andika ripoti hiyo. 2. Mpango wa elimu bila malipo nchini Kenya umefaulu ingawa umekumbwa na matatizo. Fafanua. (Alama 20) 3. Usipoziba ufa utajenga ukuta. (Alama 20) 4. Andika insha itakayomalizikia kwa:- (Alama 20) ……..nilipojitazama katika kioo, nilijidharau kwa aibu niliyojipa. Niliapa kutorudia kitendo hicho maishani mwangu. MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
1. Lazima mtindo wa uandishi wa Ripoti uzingatiwe: i) Kichwa (mada) ii) Utangulizi iii) Wanakamati walioshiriki iv) Matokeo ya udadisi:- Kila moja wapo wa mfano ufafanuliwe na watahiniwa. Mfano:-
Mfano:-
viii) Sahihi Swali la 2
Matatizo
Swali la 3 Mtahiniwa aelewe na kutafsiri maana ya methali. Aandike kisa kitakachokubaliana na methali. Maudhui Methali inamaanisha kuwa jambo ndogo likipuuzwa hatimaye huketa shida. Kisa kieleze mapuuza na hatimaye madhara yanayoletwa na mapuuza haya. Swali la 4 Mwanafunzi aeleze kisa / matukio / matendo aliyotenda yaliyomletea aibu Mfano – Ulevi wa kupindukia, vita kati ya walevi, masimango katika kijiji / mji n.k
Muhimu i) Insha isiyotimiza maneno 400 iondolewe alama 2 (urefu) baada ya kumtia kiwango chake. ii) Insha isiyozingatia sura kulingana na mada aondolewa alama 4s (sura) 1. INSHA YA LAZIMA Wewe ni katibu wa jopo lililoteuliwa kuchunguza changamoto zinazokabili uchapishaji wa vitabu vya Kiswahili nchini.Andika ripoti hiyo. 2. Samaki mkunje angali mbichi. 3. Serikali za ugatuzi zitakuwa na manufaa kwa maendeleo ya nchi.Jadili. 4. Andika insha itakayomalizika kwa maneno haya......... Niliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu,machozi yalitoka njia mbilimbili.Hayawi hayawi huwa. MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
SWALI LA LAZIMA Ripoti iwe na yafuatayo: a) Kichwa : Kilenge mada kwa kuonyesha ni ripoti ya uchunguzi wa jopo hii. b) Utangulizi : Utangulizi huonyesha aliyeitaka ripoti hii. - Wanajopo. - Sababu za kutaka ripoti hii itolewe. - Malengo ya ripoti. - Utaratibu wa kupata habari kama kuhoji wazazi, wanafunzi washirika wengine. c) Mwili – Ubebe matokeo ya uchunguzi - Yaandikwe kwa vichwa vidogo vidogo. Mapendekezo – kamati itoe mapendekezo kulingana na uchunguzi waliofanya. Hitimisho – Wito wakatibu , sahihi na jina la katibu. HOJA
TANBIHI.
BAADHI YA MAPENDEKEZO.
Mwanafunzi atunge kisa kinachooana na methali ina maana sawa na: usipoziba ufa utajenga ukuta. Maana
SWALI LA TATU.
INSHA MWONGOZO Utangulizi Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahini wa kuwasiliana na msomoji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi, akizingatia mada aliyopewa.Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa .Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutulia mkazo mtindo, mada na uwezo na mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kuikadiria kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivopendekezwa. VIWANGO MBALIMBALI D – ( D YA CHINI ) MAKI 01 - 02 1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile. 2. Kujitungia swali tofauti na kulijibu. 3. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya Ndimi. 4. Kunakili swali au maswahili na kuyakariri. 5. Kunakili swali au kichwa tu. D – WASTANI MAKI 04 – 05 1. Mtiririko wa mawazo haupo. 2. Mtahiniwa amepooka kimaudhui. 3. Matumizi ya lugha ni hafifu mno. 4. Kuna makosa mengi ya kila aina. D+ (D YA JUU) MAKI 04 - 05 1. Insha huwa na makosa mengi ya kila aina, Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha. 2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukazwa vilivyo. 3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha. 4. Mtahiniwa hujirudiarudia. 5. Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa. 6. Insha ya urefu wa robo yaani, isiyozidi maneno 174 isipite kiwango hiki. C- (C YA CHINI) MAKI 06- 07 1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake. 2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo. 3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi , ya hijai na ya msamiati na insha haieleweki kwa urahisi. C WASTANI MAKI 08 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu. 2. Dhana tofauti hazijitokezi wazi. 3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha. 4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa. 5. Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa. 6. Ana shida ya uakifishaji. 7. Anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ua msamiati lakini bado insha inaeleweka. C+ (C YA JU) MAKI 09- 10 1. Anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini bado insha inaeleweka. 2. Dhana tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu. 3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa. 4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu. 5. Anashida ya uakifishaji. 6. Kuna makosa ya sarufi ya msamiati na hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo. 7. Insha ya kiwango cha nusu, yaani maneno 175- 274 isizidi kiwango hiki. B – (B YA CHINI) MAKI 11- 12 1. Anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti akizingatia mada. 2. Ana mtiririko mzuri wa mawazo. 3. Anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia 4. Makosa yanadhihirika / ni kiasi B (B YA CHINI) MAKI 13 1. Anathihirisha hali ya kuimudu lugha. 2. Mawazo yake yanathihirika akizigatia mada. 3. Anateua na kutumia mifano michache ya misamiati mwafaka. 4. Sanja yake ni mzuri. 5. Makosa ni machache. B+ (B YA JUU) MAKI 14 - 15 1. Mawazo yake yanadhihirika na anajieleza waziwazi. 2. Anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada. 3. Ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia. 4. Sarufi yake ni nzuri. 5. Uakifishaji wake wa sentensi ni mzuri. 6. Makosa ni machache ya hapa na pale. 7. Insha ya urefiu wa robo tatu, yaani maneno 274 – 374, isipite kiwango hiki. A- (A YA CHINI) MAKI 16- 17 1. Anadhihirisha ukomavu wa lugha. 2. Mawazo yake yanadhihirika na anaishughulikia mada. 3. Ana mtiririiko mzuri wa mawazo. 4. Msamiati wake ni mzuri na unavutia. 5. Sarufi yake ni nzuri. 7. Makosa ni machache yasikusudiwa. A WASTANI MAKI – 18 1. Anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada. 2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato. 3. Anatoa hoja zilizokomaa. 4. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi. 5. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi. 6. Makosa ni nadra kupatikana. A+ (A YA JUU) 19 – 20 1. Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughuliwa vilivyo. 2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato. 3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi. 4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unavutia zaidi. 5. Sarufi yake ni nzuri zaidi. 6. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi, kiufundi. 7. Makosa yote kwa jumla hayazidi matano. ALAMA ZA KUSAHIHISHA = = = Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu. _ Hupigwa chini ya sehemu au neno ambapo kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza tu. ü Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilika pambazoni kushoto. Hutumiwa kuonyesha kuacha kwa neno / maneno. Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe. X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hutiwa juu ya neno lenyewe. Kila ukurasa uwe na alama ya chini katikati ili kuthibitisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo. Baada ya kutoa tuzo, lazima mtahini aandike udhaifu wa mtahiniwa. Mfano wa kutuza: Robo Tatu C 08/20 Udhaifu Urefu Maudhui Hijai Sarufi Maswali 1. Umechanguliwa kuwa katibu wa Chama Cha Kiswahili shuleni. Andaa kumbukumbu za mkutano uliofanyika hivi majuzi ili kupanga mikakati ya kukiendeleza Kiswahili nchini. 2. Fafanua jinsi teknolojia ya kisasa inavyoathiri maisha yako. 3. Ngozi ivute ingali mbichi. 4. Andika insha itakayoishia kwa maneno haya…nilisimama nikaangalia nyuma, machozi yakanitoka njia mbili mbili nilipokumbuka wosia wa walimu, wazazi na wenzangu. MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
102/1 2010
iii)orodha ya waalikwa ikiwa wapo iv)orodha ya waliotuka udhuru v)orodha ya wasiohudhuria na hawakutuma udhuru vi)Ajenda Maudhui ya kumbukumbu -kuwe na warsha mbalimbali za Kiswahili -vyombo ya habari -masoma zaidi yatumie Kiswahili katika mitaala -vipindi vya Kiswahili shulni viwe sawa na vya Kiingereza katika ratiba -sera kali dhidi ya wanaovuruga matumizi ya Kiswahili -kukipa Kiswahili hadhi muhumu katika shughuli za kiserikali mtahiniwa afikishe hoja tano
Hoja chanya -ajira kwa watu -kuboresha kazi -Kurahisisha mambo -kuunganisha/kutenganisha watu kutoka sehemu mbali mbali -kuongeza mapato -imeboresha utafiti Hoja hasi -kuvunjika kwa maadili -kuongezeka kwa wizi -watu kupoteza wakati – uraibu -kupanda kwa gharama za maisha -Uharibifu wa mazingira (mtahiniwa azifikishe hoja tano) ( Mtahiniwa asipojihusisha aondolewe al. 2) (- 2 H)
-usipoziba ufa utajenga ukuta Maana – ni vizuri kulainisha/kurekebisha mambo kabla hayajaharibika Matumizi – hutumika kuonya, kufunza maadili, kutoa nasaha kwa watu Kisa. Kulenge mtu aliyekosa kurekebisha/lainisha mambo kiasi cha kuharibika. Km kukosa kumwadhibu mtoto halafu mtoto anaharibika baadaye. Mtahiniwa aonyeshe pande zote mbili.
Mtahiniwa aangazie sehemu hizi tatu a)aonyeshe wosia aliopewa mtu fulani b)kupuuza / kutozingatia wosio huo c)kujuta baadaye / majuto NB: mtahiniwa akiongeza maneno yake atakuwa amejitungia swali na apewe D-(02) mahojiano1. Lazima Wewe ni miongoni mwa wanahabari wanaomhoji Inspekta Jenerali wa Polisi katika ofisi yake. Andika mahojiano yenu juu ya hatua ambazo zimechukuliwa kuimarisha viwango vya usalama nchini. 2. Mfumo wa ugatuzi nchini umekuwa na ufanisi na changamoto zake. Jadili. 3. Andika kisa kinachodhihirisha maana ya methali: Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba. 4. Andika kisa kitakachomalizikia kwa maneno haya: ... ilinichukua muda mrefu mno kayaamini yaliyonifika. MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KISWAHILI KARATASI 102/1 2016
1. Wewe ni miongoni mwa wanahabari wanaomhoji Inspekta Jenerali wa Polisi katika ofisi yake. Andika mahojiano yenu juu ya hatua ambazo zimechukuliwa kuimarisha viwango vya usalama nchini. Hii ni insha ya mahojiano na ni utungaji wa kiuamailifu. Vipengele viwili vya utungo wa aina hii vizingatiwe, yaani muundo na maudhui.
Changamoto za mfumo wa ugatuzi
Kadiria hoja zingine zitakazotolewa na mwanafunzi. 3. Andika kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba. Mwongozo Hii ni insha ya methali. Maana – Mti mkubwa uangukapo, wote wanaoutegemea mti huo huumia ama huathirika kwa namna moja au nyingine. Mtahiniwa aandike kisa kimoja kinachodhihirisha pande zote mbili za methali hii. Hali zifuatazo zaweza kujitokeza:
Hii ni insha ya mdokezo. Mtahiniwa ahitimishe insha yake kwa maneno haya. Hali zifuatazo zaweza kujitokeza:
MWONGOZO WA KUDUMU KENYA CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION KISWAHILI 102/1 2011 MWONGOZO WA KUSAHIHISHA INSHA UTANGULIZI Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi, akizingatia mada aliyopewa. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahimiwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini lazima asome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kukadiria viwango mbalimbali vilivyopendekezwa. Viwango vyenyewe ni A,B,C, na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa. VIWANGO MBALIMBALI KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05
D- (D YA CHINI) MAKI 01-02
C- (C YA CHINI) MAKI 06-07
B- (B YA CHINI) MAKI 11-12
A- (A YA CHINI) MAKI 16-17
USAHIHISHAJI NA UTUZAJI KWA JUMLA Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai. MAUDHUI
Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika. Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule. Kutegemea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kufinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao. MTINDO Mtindo unahusu mambo yafuatayo:
Sarufi ndio msingi wa lugha. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:
Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu. Makosa ya tahajia huweza kutokea:
ALAMA ZA KUSAHIHISHIA ==Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu. __Hupigwa chini ya sehemu au neno ambapo kosa la hijai limetokea kwa mara ya kwanza tu.
Maelezo mafupi yanahitajika kuhusu tuzo lilotolewa. Kila ukurasa uwe na alama chini kudhihirisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo. UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA YA PILI Maneno 9 katika kila mstari ukurasa mmoja na nusu. Maneno 8 katika kila mstari ukurasa mmoja na robo tatu. Maneno 7 katika kila mstari kurasa mbili. Maneno 6 katika kila mstari kurasa mbili na robo. Maneno 5 katika kila mstari kurasa mbili na robo tatu. Maneno 4 katika kila mstari kurasa tatu na robo tatu. Maneno 3 katika kila mstari kurasa nne na nusu. Kufikia maneno 174 insha robo. Maneno 175-274 insha nusu. Maneno 275-374 insha robo tatu. Maneno 375 na kuendelea insha kamili.
Majibu
SWALI LA 1. -Mwanafunzi aandike insha yenye kuhusu mazungumzo au majibizano kati ya wahusika hawa watatu -Insha ifuate mtindo wa mchezo wa kuiguza - Azingatie kisa cha utovu wa nidhamu kama vile kupigana na mwanafunzi mwenzake, kuchelewa, kutovaa sare za shule n.k - Mwanafunzi atumie maneno mia nne (400). Asiyefikia maneno mia nne aondolewe maki 2 yaani 2u - Asipozingatia sura aondilewe maki 4 yaani 4s. SWALI LA 2
Faida ya kuelimisha motto wa kike
Maana ya methali SWALI LA 4 -Mwanafunzi atunge kisa ambacho kitaonyesha kuwa anajuta baada ya kutozingatia mawaidha -aliyopewa hapo awali -Mwanafunzi asiyemalizia kwa maneno haya awekwe katika kiwango cha D (alama3) -Akiongeza au kupunguza maneno matano aondolewe alama 2 yaan 2M mazungumzo kati ya Mwalimu mkuu na mzazi1. Andika mazungumzo kati ya Mwalimu mkuu na mzazi kuhusu chanzo, matumizi na athari za dawa za kulevya miongoni mwa vijana wengi wa siku hizi. 2. Hakuna kizuri kisichokosa ila. Thibitisha methali. 3. Fafanua hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa ili kukabiliana na janga la umaskini hapa nchini. 4. Nilikuwa nimelala fo!fo!fo!nilipogutushwa na kishindo kikuu kutoka upande wa mjini…. 1. (a) Chanzo
(i)Mshawasha kutoka vijana wenzao (ii)Kukosa kazi/ajira (iii)Vyombo vya habari (iv)Kuiga wazazi na wakubwa wao (v)Ukosefu wa maelezo yanayofaa kuhusu athari za dawa hizi Matumizi
Athari
2. Mwanafunzi asimuliw kisa kinachoafikiana na methali hii k.m. mtu aliyekuwa mwema sana lakini hatimaye akapatikana na dosari iliyomfedhehesha sana. Aidha mwanafunzi anaweza kusimulia visa mbalimbali vinavyothibitisha methali hii. 3. Hatua zifaazo ni ;
4. Mwanafunzi aendeleze dondoo hili (mdokezo) kusimulia kisa kinachoafikiana na mdokezo huu. KUANDIKA RIPOTI1. Umeteuliwa kama katibu wa tume ya uchunguzi kuhusu vyanzo vya baa la njaa nchini Kenya. Andika ripoti yako. 2. Ufisadi umekuwa saratani katika nchi nyingi zinazoendelea barani Afrika. Jadili mifano mbalimbali ya janga hili na jinsi ya kulitatua. 3. Mchumia juani hulia kivulini. 4. Mlango wa nyuma ulibishwa mara tatu, Ngo! Ngo! Ngo!. Kufungua tu, nikasikia sauti, “ Lala chini¬¬¬......................” (Endelea). MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
1. Insha hii ni ya kiuamilifu kuhusu ripoti, sura ya ripoti kuzingatiwa. (i) Kichwa/Anwani (ii) Utangulizi (iii) Matokeo ya utafiti/uchunguzi/mwili – vijisehemu vidogovidogo (iv) Mapendekezo kuhusu matokeo (v) Hitimisho;maoni ya kamati (si ya Katibu) (vi) Sahihi na tarehe/cheo Vyanzo vya baa la njaa • Ukame • Matumizi/utegemezi wa vyakula vya aina moja • Njia mbovu/duni za kilimo • Uzembe/uvivu • Idadi kubwa ya watu • Watu kuhamia mijini – kupuuza kilimo • Ufisadi – sakata mf – ya mahindi • Njia duni za kuhifadhi vyakula • Hali duni za uchukuzi • Kukosa ardhi (uskwota) Ondoa alama 4 za sura ikiwa haijitokezi – akikosa vipengele 4 kati ya 6 (-4s) Ondoa alama 2 za urefu ikiwa haukuzingatiwa Hoja inapomalizikia ipigiwe mkwaju / ionyeshwe kwa mkwaju. 2. (a). Mifano - Barabarani - Ofisini - Mahakamani - Bungeni - Shuleni - Viwandani - Serikalini - Vijijini - Nyumbani Njia za kutatua - Kuunda tume za kukabiliana na ufisadi - Kulipa mishahara mizuri - Kufunza maadili shuleni - Kutumia dini/mahubiri - Kubuniwa kwa sheria kali - Viongozi wawe mifano mizuri ya uadilifu - Uwajibikaji kazini - Viongozi watangaze mali yao hadharani 3. Maana – Kisawe cha mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Anayesumbuka kufanya kazi fulani atanufaika hatimaye • Iwe na kichwa – ingawa si lazima • Maana na matumizi ya methali – si lazima • Kisa/visa – Lazima • Hitimisho – Si Lazima • Mtahiniwa ashughulikie pande mbili za methali vilivyo. Atakayeshughulikia upande mmoja tu asipite C+ (Alama 10) • Atakayepotoka atuzwe D Alama 3 20 • Akitoa maelezo ya moja kwa moja bila kisa/visa amepotoka: D 03 20 4. Mtahiniwa aanzie maneno aliyopewa • Kisa kioane na maneno - Kisa cha kutisha mf. Jambazi, wahuni au askari • Asiyeanzia maneno aliyopewa amepotoka D 03 20 • Atakayeongeza kianzio chake lakini asizidishe maneno matano aondolewe alama 2. • Mtahiniwa ni lazima atumie nafsi ya kwanza na ajihusishe; asipojihusisha amepotoka:. D 03 INSHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA 1. Mtahiniwa azingatie yafuatayo; Mbinu za kupambana na ufisadi -Kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya ufisadi kupitia kwa redio, magazeti, runinga n.k. -Kuwaadhibu wahusika – wapelekwe mahakamani na wafungwa jela. -Wananchi waadilike (wawe na maadili mema). -Viongozi wawajibike katika kazi zao. -Sheria za kupambana na ufisadi zibuniwe na kutekelezwa. -Kubuni nafasi zaidi za kazi -Kuimarisha elimu -Kuongeza mishahara kwa wafanyikazi -Tume zaidi za kukabiliana na ufisadi zibuniwe. SURA YA MAHOJIANO -Insha iwe na kichwa kinacholenga mada -Kuwe na mhoji na mhojiwa -Njia ya maswali na majibu -Njia ya kitamthilia ufuatiwe kwa mfano; Juma: Bakari: TAHADHARI -Atakayefululiza bila kufuata mtindo wa mahojiano aondolewe alama (4) sura baada ya kutuzwa. 2. i) Kilimo cha mboga ii) Upanzi wa miti iii) Utengenezaji wa matofali na kuyauza. iv) Ukarabati wa barabara v) Kushirikiana na polisi katika kutoa usalama kwa umma. 3. Maana ya methali Ikiwa umekwisha jitayarisha kufanya jambo, basi bora ulikabili / ulifanye na ulimalize. -Mtahiniwa aandike kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali. -Aonyeshe mtu aliyeanza jambo licha ya vikwazo / matatizo, alijibidiisha kulikamilisha. 4. Sharti mtahiniwa aanze insha kwa maneno aliyopewa bila kubadilisha wala kuongeza. Insha ionyeshe harakati za kumtafuta baba mzazi Asimulie jinsi alivyotambua / alivyokutana na babake kwa mara ya kwanza. Hisia alizozipata kv. Furaha / chuki Iwapo mkutano huu ulifaulisha maisha yake ya usoni au la. Ugunduzi wake ulivyoathiri maisha yake TAZ: Kisa kisimuliwe kwa njia ya kuvutia na kusisimua. Insha
Mwongozo huu unatumika sambamba na mwongozo wa kudumu wa Insha [102/1]
1. Andika hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kupambana na Ufisadi nchini kwa washika dau wote katika Kaunti ya Kakamega. -Insha ihusishe hoja zisizopungua sita kati ya hizi na nyingine zinazorejelea maswala yoyote ya ufisadi nchini: --Chanzo cha ufisadi k.m. umaskini, tamaa, kuiga wengine, kutaka kuhepa adhabu, n.k. --Kunakotokea ufisadi, k.m. ofisini, hospitali, shuleni, mahakamani, katika vyombo vya usafiri, n.k. --Athari za ufisadi k.m. ufujaji wa pesa, nchi/mashirika kutoendelea, n.k. --Adhabu kwa ufisadi k.m. kushikwa, kufungwa, kufutwa, kulazimishwa kulipia, n.k. --Hatua zinazochukuliwa na shirika lake kupambana na ufisadi. --Mapendekezo yake kwa umma kuhusu jinsi ya kupambana na ufisadi. SURA Ionyeshe kuwa ni hotuba kutokana na kianzio, kinachotambua au kuiamkua haadhira. Pia kiishio. Insha yenyewe iandikwe kwa mtiririko ikitumia nafsi ya kwanza. Adhabu ya kawaida ichukuliwe kwa insha isiyochukua sura inayostahili (-04s) 2. Eleza chanzo cha ongezeko la bei ya bidhaa nchini mwako, huku ukionyesha athari za ongezeko hili. CHANZO --Ufisadi --Tamaa --Shilingi ya Kenya kukosa nguvu dhidi ya Dola ya Marekani.
ATHARI
3. Aiszfuye mvua imemnyea. Ni methali. Insha iwe na kisa (au visa) kinachoonyesha ukweli wa methali. Methali ina maana kuwa anayelizungumzia jambo, kulieleza au kulisifu ana tajriba nab. Insha ionyeshe sifa itolewayo na pia alivyonyewa. 4. “Karne ya 21 imeleta ongezeko kubwa la vyombo tofauti vya habari nchini, pamoja na athari anuwai” Jadili kauli hii. ONGEZEKO Insha ithihirishe ukweli kwamba vyombo vya habari vimeongezeka kwa kutoa mifano ya magazeti, majarida, stesheni za redio, runinga, n.k. atakayejaribu kuipinga kauli hii atakuwa amepotoka. ATHARI Ni nzuri na mbaya • Habari zinapatikana kwa urahisi. • Hakuna usiri usiofaa wa serikali tena. • Kuna burudani tele. • Vinaelimisha. • Watu (hususan wale mashuhuri) wamekoseshwa siri katika maisha yao. • Vyombo vingine vinachochea makabila, n.k. • Kuna ongezeko la picha/habari za ngono. • Maadili yamezorota. • N.K. Insha ihusishe hoja zozote sita au zaidi katiya hizi na nyingine. ZIADA YA JUMLA Tumia mwongozo wa kudumu wa insha ili kutuza insha katika viwango kati ya A+ na D-. hoja katika maswali 1,3 na 4 itambulike kwa mkwaju (‘f) kushoto, pembezoni mwa aya iliyobeba hoja. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|