Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
1. UFAHAMU (Alama 15) Soma habari iliyopo, kisha jibu maswali yanayofuatia. Kigumba kwa Nguruwe. Kikamilifu methali hii ni: Kigumba kwa nguruwe kwa mwanadamu ki chungu. Kufahamu maana yake, ni lazima tuchunguze kijuujuu maana ya maneno yaliyotumiwa. Kigumba ni chembe cha mshale, mkuki au chusa kinachotumiwa kuchoma na kumjeruhi mnyama. Nguruwe ni mnyama anayesakwa na kufumwa na kufurahikiwa na wasasi anapopatwa. Uchungu ni maumivu yanayoletwa na kitendo hicho cha kufuma. Nguruwe hufisidi mimea ya wakulima. Hapo basi husakwa kwa mishale na mikuki na kuuawa. Watu hupata uhondo wa nyama. Wakati mwingine, katika zile hekaheka za kusaka, huenda mshale au mkuki ukamdunga mtu badala ya yule mnyama.Vivyo hivyo anapaswa afahamu kuwa uchungu anaousikia yeye ndio ule aliousikia nguruwe. Mzee Kisheta alikuwa mraibu wa bangi, na kwa sababu hiyo, hakuweza kumkimu yeyote; si mkewe, si watoto hata mwenyewe na aila yake yote. Kila hela aliyoipata, alilongeza katika vihindo vya wauzaji bangi. Mkewe, Kitete, alikuwa akienda kutafuta vibarua angalau awasitiri wanawe. Chochote kile alichopata, ilimbidi akifiche, kwani mumewe alivisaka vibetini, mitoni na matandikoni, chini ya mivungu ilimradi nyumba nzima aliichakura. Akikipata hukimbilia kwa wachuuzi wake. Asipokiona, humkabili mkewe kwa matusi na magumi. Mkewe, aliyechekelea sana kufufutwa, humtolea nusu ya pesa alizopata ili aipoze ghaidhi ya mumewe. Kisheta huchomoka huyoo! Hapo basi Kitete huepukana na kero. Siku moja, Kitete alirudi na shilanga lake begani huku akitabasamia mwanawe mdogo Kita, aliyeuona uso wa furaha wa mamaye uliobashiri mafanikio aliuliza, “Mama una furaha leo! Je, umetuletea nini?” Mamake alimjibu kuwa alikuwa na furaha sana siku ile kwa sababu bibi aliyemlimia ngwe siku hiyo alimpa bahashishi ya shilingi ishirini kwa kazi yake nzuri. Badala ya shilingi hamsini alipata shilingi sabini. Ilikuwa furaha iliyoje! Alipomaliza kumjibu mwanawe kwa furaha, aliliingiza jembe lake ndani na kutoka haraka haraka awahi kwenda madukani kabla ya Kisheta kufika pale na kumnyang`anya pesa zake alizozipata kwa jasho. Alipotoka nje ya nyumba tu, alikutana na mumewe aliyezuka ghafula, haijulikani kutoka wapi! Papo hapo alimtolea jicho mkewe mkono kaunyosha akitaka kupewa ujira wote alioupata siku hiyo.Mama Kita alikataa katakata akisema hakupata chochote siku ile. Kisheta alikuja juu, akamshika mkewe akitaka kumvunja kama ukuni mkavu. Mkewe alilia kwa uchungu akijaribu kujikwamua, lakini mikono yake Kisheta ilikuwa imemkaba kama koleo. Hakuweza kumtoka. Mwanawe, Kita, alipomwona mamaye alivyokuwa akiteseka alisema, “Mama, kwa nini ufe na pesa unazo? Si umpe baba hizo shilingi sabini ulizozifunga hapo katika pindo la leso?” Kusikia hivyo, Kisheta alimwachilia mkewe kwa kumkita chini na kumwamrisha ampe pesa zile. Bibi huyo hakuwa na la kufanya ila kuzitoa. Kisha akakaa chini na kujiinamia kwa huzuni. Mzee Kisheta alifurahi na kumnyanyua Kita juu na kusema. “Wewe u dume kweli! Unampenda baba yako. Kua mwanangu na uwe kama babako.” Mtoto huyo alisikiza maneno hayo, lakini hakuonekana kuelewa aliyoambiwa. Siku nyingi zilipita na maisha ya Kisheta yalizidi kuzorota. Jumapili moja baada ya kupotea kutwa nzima, asijulikane alikokuwa. Kisheta alirudi akiandamana na watu wawili hadi pale nyumbani kwake. Walipofika mkabala wa ukumbi, Kisheta alisikika akisema, “Mabwana, mimi asilani sivuti hata sigara, lakini ikiwa mwasisitiza kuwa mwataka kuingia ndani basi mwakaribishwa.” Kita aliposikia babake akisema hivyo, alidakia, “Wewe baba huvuta sigara. Hata jana ulinituma sigara sita kubwa dukani kwa Ali.” Kisheta alimrukia Kita akataka kumzaba makofi. Kumbe wale mabwana aliokuwa nao walikuwa askari kanzu. Walimzuia asimpige mtoto; walilisaka banda lake la nyumba na kuona vipande sita vya misokoto ya bangi chini ya sanduku la mbao lililokuwa na suruali moja iliyojaa viraka na fulana moja kuukuu. Kisheta alitiwa pingu na kupelekwa kwenye kituo cha polisi. Alipokuwa akitolewa mle nyumbani, aliropoka laana kwa mwanawe Kita. Mama Kita matumbo yalimsokota akamkabili mumewe na kumsuta. “Msalie Mtume? Usinilaanie mwanangu? Malipo ni hapa duniani. Jambazi we! Umepata stahili yako!” Maswali: 1. Toa fasili ya kigumba katika kisa hiki. (Alama 2) ………………………………………………………………………… 2. Eleza uhusiano kati ya Kisheta na mkewe katika hali yao ya maisha. (Alama 3) …………………………………………………………………… 3. Ni kitu gani kilichopandisha mori Kisheta hata akawa karibu kumwumiza mkewe? (Alama 1) ……………………………………………………… 4. Taja sababu zilizomfanya mtoto Kita kutoboa kuwa mamaye alikuwa na pesa na babaye alivuta sigara? (Alama 2) ………………………………………………… 5. Ni mafunzo gani tunayoyapata kutokana na kisa hiki? (Alama 3) ………………………………………………… 6. “Kutojua ni usiku wa giza.” Fafanua msemo huu ukilinganisha na makala uliyosoma. (Alama 2) …………………………………………………… 7. “Jambazi we! Umepata stahili yako!” Fafanua. (Alama 2) …………………………………………………… MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
1. Ni jambo la kuudhi unalolitendea mtu huku ukidhani huwezi kutendewa (alama 2) 2. • Kisheta alikuwa mkali • Kisheta hakumwamini mkewe • Kisheta hakumsaidia mkewe kwa chochote • Mkewe alikuwa mnyenyekevu kwake. 3. Kukatazwa pesa au pato la siku hiyo. 4. • Mama kita alirudi akitabasamu mpaka huyu mtoto akajua kulikuwa na mafanikio fulani. • Kita alifichua kuwa babake alikuwa amemtuma sigara kubwa dukani kwa Ali. 5. Hakuna siri ya watu wawili. - Kuna hatima ya mateso. - Familia haiwezi kuendelea utengano ukiwepo. 6. Kisheta alimdunisha mwanamke kwa kila alichofanya akidhani hakujua. • Kisheta alimshangilia mwanawe bila kufahamu kuwa ndiye angemtia matatani. 7. Mkewe alifurahia kilichotokea hata kama hakikuwa bora kwa mumewe. - Mkewe Kisheta hakuwa na uwezo wa kumkabili mumewe lakini neema za Mungu zilimwokoa akalipishiwa kisasi. Tanbihi i) Pitia majibu huku ukidondoa makosa ya - Sarufi - hijai ii) Kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza liondolewe nusu alama mpaka upeo wa aina kumi na mbili ½ x 12 alama 6 iii) Kila kosa la hijai liondolewe nusu alama hadi upeo wa aina sita za makosa ½ x 6 alama 6 Mfano J = 10 S = 1 (makosa mawili tofauti) 9 H = 2 (makosa manne tofauti) 07
0 Comments
1. UFAHAMU (ALAMA 15) Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanoyofuatia. Malengo ya maendeleo ya Milenia Malengo ya maendeleo ya Milenia (yajulikanayo kwa kimombo kama Millenium Development Goals (MDG), Ni malengo manane ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa, ambayo nchi hizi zilikubaliana kujitahidi kutimiza kufikia mwaka wa 2015.Azma ya kufikia malengo haya ilizinduliwa rasmi mnamo septemba 2000 katika azimio la millennia la umoja wa mataifa.Wakati wa uzinduzi, mataifa yote 189 wanachama wa umoja wa mataifa yalihusika.Kwa sasa, mataifa wanachama yameongezeka na kufikia 193 na yote yanajizatiti kutekeleza azma hii. Azma ya kwanza ni kukomeza au kupunguza umaskini uliokithiri kwa asili 50 miongoni mwa watu ambao kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku.Aidha lazima hii inalenga kupunguza kwa kiasi hicho idadi ya watu wanaokumbwa na dhiki ya njaa kufikia mwaka wa 2015.Kwa kielelezo, kwa mfano vijiji viitwavyo ‘vijiji vya milenia’vilianzishwa katika nchi sahara,ambazo ni Uhabeshi, Ghana, Kenya, Malawi, Rwanda, Nigeria, Senegal, Tanzania na Uganda vilichaguliwa.Wakazi hawa wanapookolewa kutoka kwa ulitima, hatua zilichukuliwa vijijini humu yanaonyesha athari chanya.Kunayo matumaini. Lengo la pili lilikuwa kutimiza elimu ya msingi kwa wote chini ya wito ‘Elimu kwa wote’, yaani kwa kingereza Eduction for All (EFA) kufika mwaka wa 2015.Nchini Kenya, elimu ya msingi ilifafanuliwa upya katika katiba mpya ya 2010, ikawa yaanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne. Aidha imetajwa kuwa ya lazima, kwamba mtoto sharti ahudhurie masomo.Ina maana kuwa mzazi analazimika kumpeleka mtoto shuleni. Lengo pia lipo, kuhakikisha watoto wote wa jinsia za kike na kiume wanahitimu. Lengo jingine ni kuwania usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha kuna nafasi sawa kwa wote.Katika janibu nyingi za wanachama wa umoja wa mataifa, wanawake kwa miaka ya ayami walionekana kuwa chini ya wanaume kutokana na taasubi ya kiume, mwanamke alifaa kuwa chini ya mwanamume.Hatua ya kwanza ya malengo ya maendeleo ya millennia inanuia kuondoa tofauti ya uwiano wa wasichana na wavulana katika elimu ya msingi hadi sekondari ifikapo mwaka 2005; na katika ngazi zote za elimu ifikapo 2015. Kuondoa utoro miongoni mwa wahudhuriao masomoni hutahakikisha usawa huu. Lengo la nne ni kupuuza vifo vya Watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili kufikia mwaka wa 2015. Jitihada zinatiwa kuhakikisha kuwa kina mama waja wazito hawazai njiti wala watoto wao hawaagi punde baada ya kuzaliwa.Changamoto imekuwa kwamba watoto wengi katika nchi zinazoendelea hufa kabla kufikia umri wa miaka mitano. Mapambano dhidi ya magonjwa kama vile kifaduro, polia na malaria yaliyosababisha vifo hivi pamoja na jitihada za kujizatiti za kufikia lengo hili. Kunayo azma ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za uzi ili kupunguza kwa robo tatu vifo vya uzazi kufikia 2015. Kua kwa wajawazito kunaashiria huduma duni wakati wa kuhimili.Kina mama wengine katika nchi zinazoendelea hawahudhurii kliniki wakati wakati wa kulea mimba.Kwingineko, huduma hizi huwa mbali sana, huku namna za usafiri zikiwa duni.Kina mama huishia ama kuhudumiwa na ‘wakunga’ wasiohitimu au hata kujifungua pweke .Mataifa wanachama wanahimiza kuongezea zahanati na vituo vingine muhimu vya afya.Kadhalika jitihada zinatiwa kuwaelimisha kina mama na jamii kwa jumla kuhusu umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakatiwa ujauzito na kuhakikisha mama yu salama wakati wa kujifungua. Magonjwa sugu yanayotishia kuwamaliza walimwengu ni kikwazo cha jitihada za walimwengu kujiendeleza.Ndiyo maana lengo la sita ni kupambana na Ukimwi, malaria na magonjwa mengineyo.Kampeni zinaimarishwa katika jumuiya hii kuzuia kabisa na kupunguza maambukizo mapya ya Ukimwi.Jitihada zinatiwa kupunguza au kuzuia kabisa ugonjwa wa malaria au magonjwa mengine hatari. Vyombo vya habari, vituo tamba vilivyo na maafisa wa nyanjani vinatumiwa nyanjani katika mataifa wanachama ili kufaulisha kampeni hii. Aidha wanachama wanalenga kuhifadhi mazingira kwa kujumuisha misingi ya maendeleo endelevu katika sera na program za nchi.Zinalenga kuzuia upotevu wa rasilimali ya mazingira kama vile miti na maji.Lengo lipokuhakikisha kuwa katika kipindi hiki wanachama watapunguza kwa asilimia 50 idadio ya watu wanaoshindwa kupata maji safi na salama – hii ni moja wapo ya malengo ambayo, kwa mujibu ya tovuti ya umoja wa mataifa www.un.org/milleniumgoals, kuna matumaini ya kutimiza zaidi ya 2015. Mwisho kuna lengo la kujenga mshikamano wa maendeleo duniani, kwanza kwa kuboresha zaidi mfano wa Fedha na biashara duniani kuhakikisha ni wa usawa, unafuata sheria na kamwe hauna ubaguzi.Utawala bora; kushughulikia mahitaji ya kipekee ya nchi changa kama vile kuziondolea ushuru wa bidhaa muhimu,kuzipunguzia au kuziondolea madeni; kutoa misaada zaidi kwa nchi maskini zinazotia jitihada kutoa umaskini kushughulikia mahitaji muhimu, ya visiwa vidogo na nchi zisizo na bandari miongoni mwa nchi zinazoendelea; kuwapa vijana ajira bora; kushirikiana na sekta za kibinafsi ili kuimarisha teknolojia ya kisasa hasa katika habari na mawasiliano ni baadhi ya yanayozingatiwa kulenga kutimiza mshikamano huu. MASWALI. 1. Malengo ya maendeleo ya milenia ni nini? (Alama 2) ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ 2. Ni wachochole wa kiwango gani wanaolengwa kuinuliwa na hatua za malengo ya maendeleo ya milenia? (Alama 1) ........................................................................................................................................................................ 3. Taja vipengele viwili muhimu kuhusu elimu katika katiba mpya ya Kenya vinavyo changia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia? (Alama 2) ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ ........................................................................................................................................................................ 4. Gusia changamoto tano zinazowakabili kina mama wajawazito katika ulimwengu wa tatu. (Alama5) ....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... 5. Kampeni dhidi ya magonjwa sugu inafanywa kwa namna gani. (Alama 2) ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ 6. Hali ya maji inatarajiwa kuwaje kufikia 2015. (Alama 1) ....................................................................................................................................................................... 7. Eleza maana ya vifungu hivi. (Alama 3) a) Hawazai njiti ............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... b) Vifo vya uzazi. ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
1. Majibu ya Ufahamu. 1. Malengo manane ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa,ambayo nchi hizi zilikubaliana kujizatiti kufikia mwaka wa 2015. (Alama 2) 2. Maskini ambao kipato chao ni cha chini ya dola moja kwa siku. (Alama 1) 3. i) Inaanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne. (Alama 2) ii) Ni ya lazima, yaani mtoto sharti ahudhurie masomo. (Alama 1) 4. i) Kutohudhuria kliniki wakati wa kulea mimba. ii) Huduma kwa wajawazito kuwa mbali sana. iii) Namna za usafiri kuwa duni. iv) Kuhudumiwa na ‘wakunga’ wasiohitimu au hata kujifungua pweke. v) Ukosefu wa kinga muhimu na lishe bora. (zozote 3 alama 5) 5. Kwa kutumia vyombo vya habari na vituo tamba vilivyo na maafisa wa nyanjani. (Alama 2) 6. Kupunguza kwa asilimia 50 idadi ya watu wanaoshindwa kupata maji safi na salama . (Alama 2) 7. i) ‘Hawazai njiti’ – Mimba hazitoki . (Alama 1) ii) ‘Vifo vya uzazi’- vifo vinavyotokea wakati kina mama wanajifungua. (Alama 1) 1. UFAHAMUSoma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za kulitadarukia tatizo ambalo linakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea, unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakipiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yale yaliyoendelea kama vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao. Vyanzo vya umasikini huu ni anuwai mathalan,ufisadi uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemezwa kwenye kilimo kinachotegemea mvua isiyotabirika, idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalohusika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili. Jamii ya ulimwengu inapaswa kuelewa kuwa umaskini, unaoathiri nchi fulani una athari pana sana. Uvunjifu natokana na umaskini unaweza kuwa mboji ambako matendo mabaya huchipuka. Raia maskini huweza kushawishiwa haraka kujitosa kwenye matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina. Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburia madeni mataifa yanayoendelea kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwa muhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umasikini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea. Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharura ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tagemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa hauishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umaskini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima yauzingatie uhalisi wa maisha ya raia wa mataifa hayo. MASWALI a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea? (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… d) Mfumo wa soko huru una madhara gani kwa mataifa machanga? (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… e) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya: (alama 3) i) Kulitadarukia ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ii) Kuatika ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… iii) Kuyaburia madeni ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… 1. UFAHAMU
a) i) Ufisadi ii) Uongozi mbaya iii)Turathi za kikoloni iv) Uchumi kuegemezwa kwenye kilimo kinachotegemea mvua isiyotabirika v) Idadi kubwa ya watu inayoupika uwezo wa uchumi taifa linalohusika vi) Ukosefu wa nyenzo na mali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umasikini vii) Ukosefu wa elimu na nafasi za ajira (4x1=4) b) Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. (1x2=2) c) i) Kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umasikini ii) Pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni masikini iii) Kuzalisha nafasi za kazi kwa dharura iv) Kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi v) Kuendeleza elimu vi) Kuimarisha miundo msingi (4x1=4) d) Ni chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umasikini zaidi (1x2=2) e) i)kulitadarukia – kulishughulikia, kulitatua kulikabili ii) Kuatika - kuanzisha , kutia , kuzua iii) Kuyaburia madeni. Kuyasamehe madeni, kuyaondolea madeni (3x1=3) SWALI LA KWANZA – UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Zamani wanadamu wa kwanza ambao ni mababu wa vizazi vilivyopita waliishi duniani. Habari kuhusu maisha na maumbile yao haikujulikana kwa hakika kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kuandika. Lakini mara kwa mara shughuli za wanakioolojia kama Louis Leakey na wengine hugundua mifupa yao ardhini na michoro yao katika mapango. Wataalamu hawa hufukua mafuvu, vyombo na silaha zao za zamani. Kwa kuchunguza vitu hivi tunaweza kubahatisha viumbe hawa walivyokuwa na jinsi walivyoishi. Moja ya mambo yanayofahamika sasa ni kuwa wanadamu hawa wa awali walifanana na Sokwe. Aidha , walitembea kwa kupinda mgongo kama kibiongo. Chakula au uhai wao ulitegemea kukusanya matunda, kokwe, majani ya miti na mayai ya ndege. Vile vile , walitegemea wanyama wadogo, kufukua mizizi na kubambua magamba ya miti walipokabwa na njaa. Maisha yao yalikuwa ya hatari . Walikuwa wakiwindwa na wanyama wakubwa. Hii ni kwa sababu mwanzoni hawakuwa na silaha za kujihami. Hivyo iliwabidi kujificha katika miti na vilima kuepuka uvamizi. Lakini usalama wao ulitegemea kwa kiasi kikubwa kudura za Mungu au pengine miungu. Kwa taratibu wanadamu hawa walijifunza kutengeneza silaha. Walianza kutumia fimbo nene zenye ncha au mawe ya kutupia. Baadaye walichonga mawe ili kufanya kuwa visu, nyundo au vigumba vya mikuki. Hatimaye waliviomoa au kupasua vipande vya mawe na kuvitumia kama mishale. Hapa ndipo walianza kuwinda wanyama wakubwa mithili ya swara nguruwe nyati na ngiri. Pia walioweza kutumia mikuki kundunga samaki majini. Mababu zetu hawakuwa na nyumba . Kwanza walikuwa wakijisitiri kwa kukaa chini ya vivuli vya miti au kujenga vibanda vya matawi na majani ya miti. Hawakuweza kuingia mapangoni asilani kwa kuchelewa wanyama wapori wakali kama vile chatu , simba na mamba waliokaa humo. Kwa bahati, siku moja mmoja wao aligundua moto alipokuwa akipekecha vijiti. Kabla ya ugunduzi huu, wao pia hawakujua kazi ya moto na walikuwa wakiogopa na kukimbia moto jinsi wafanyavyo wanyama wa mbugani mpaka leo. Ujuzi wao wa kutumia moto ulileta mabadiliko makubwa. Baada ya hapo waliweza kukaa mapangoni na kukoka mioto milangoni mwa mapango ili kuaogofya adui. Hali kadhalika, waliweza kuota moto, Kumilikia maskani yao mpya na kuchoma nyama badala ya kuila mbichi. Wanadamu wa awali hawakuwa na mavazi. Waliwezaje kuzuia baridi? Inadhaniwa kwamba nywele nyingi walizokuwa nazo kwenye mwili zilisaidia kuwapa joto. Uvaaji wa nguo ulianza walipoanza kutumia ngozi kutoka kwa wanyama waliowawinda. Walizisafisha ngozi kwa kuzipaa kwa kombe za mawe kuzianika juani. Zilipokauka walizivaa kwa kujifunga na kuzishikanisha kwa mifupa au mikanda ya ngozi. Wanadamu hawa hakuweza hata kuongea. Waliwasiliana kwa kupiga mayowe, Kutoa milio au kunguruma jinsi wafanyavyo wanyama. Polepole walianza kutumia sauti na baada ya muda walizipanga sauti kuibua mifumo ya maneno yenye maana za kipekee. Uimilisi wa kutumia lugha uliwawezesha kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Lugha pamoja na matumizi ya moto na silaha viliwarahisishia maisha na kuwawezesha kupata muda wa kupumzika mapangoni jioni wakiota moto. Kutokana na hali hii waliweza kutekeleza jambo moja kuu waliloturidhisha. Walitupokeza zinaa.Kutoka kwao tulirithi fasihi simulizi na kupata nakshi za michoro hii inapatikana katika mapango hata leo hii nchini Ufaransa , Uhispania, Africa kusini na hataAfrika mashariki. Maswali a) Msemo “kudura za Mungu au pengine miungu” inadhihirisha hali gani ya wanadamu wa kwanza. (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Kwa nini wanadamu hawakuishi mapangoni mwanzoni? (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… c) Fafanua mambo matatu yaliyomwezesha mwanadamu wa kwanza kupiga hatua kimaendeleo. (alama 6) ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… d) Taja sifa mbili za kimaumbile zilizowatofautisha wanadamu wa awali na wa siku hizi. (alama 2) …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Eleza maana ya (alama 3) (i)Walipokabwa………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (ii) Kijihami……………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………… (iii) Maskani…………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………… SEHEMU A: UFAHAMU
1. a) Hawakuweza kujikinga na haieleweki walivyookoka uvamizi b) Wanyama hatari waliishi humo c) (i) Uwezo wa kutumia silaha kujikinga na kupata chakula (ii) Uvumbuzi wa moto ulimwezesha kuishi pangoni d) (i) Walitembea kwa kuinama (ii) Walikuwa na nywele nyingi mwilini e) (i) Walipohisi, walipoona, walipokumbwa (ii) Kujitetea, kujilinda (iii) Makaazi, makao, nyumbani UFAHAMu 1. UFAHAMU Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Tukilinganisha maisha ya zamani na ya siku hizi tutaona kwamba mambo mengi sana yamebadilika. Si watu wazima, si watoto; sote tumeathirika si haba. Mitindo mipya ya kimaisha na mazingira yanayobadilika kasi ni baadhi tu ya mageuzi haya. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitizamo, mawazo na mielekeo tu bali katika vipengele vingi vingine. Mavazi ya zama hizo yalikuwa yakitengenezwa kutokana na maganda ya mti au ngozi za wanyama kama vile mbuzi, kondoo, punda, ngamia, ng’ombe na hata pengine wanyama wa mwituni. Kwa vile kila mtu alifuga wanyama wengi, hakukuwa na shida ya kuzipata ngozi kama hizo wakati wowote ule haja itokeapo. Magome ya miti yalipatikana mwituni – na kwa kuwa katika enzi hizo hakukuwa na hifadhi za wanyama wa mwitu wala miitu yenyewe, watu waliweza kuingia katika pori lolote na kubambua maganda au kuua wanyama kama walivyohitaji. Mavazi yalikuwa rahisi kupatikana kuliko zama zetu; licha kwa upande wa ndarama, hata kwa upande wa sheria pia. Zaidi, katika enzi hizo watu hawakujali kwenda uchi au walipachika kipande tu cha vazi mwilini. Siku hizi gharama ya maisha imepanda mno. Siku hizi hatuwezi kuwaua wanyama wa mwituni vururu mtende eti kwa chakula, kama walivyofanya babu zetu. Enzi hizo matunda yalining’inia mitini na njaa zilikuwa si nyingi. Chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo. Vinywaji vilikuwa kwa mpango – wazee wa ngambi walikuwa na vinywaji vyao; wazee wa kawaida, wanawake na watoto hirimu hawakusahauliwa. Watu waliheshimiana; vijana walikuwa wenye adabu na walifahamu fika kuwa walipaswa kuwaheshimu wakubwa kwa vyovyote vile. Siku hizi vyakula ni haba na ghali na vingi vyazua magonjwa tata. Siku hizi kuna weledi wengi, hasa wa sayansi. Mja akitaka kwenda safarini huchukua kidubwasha fulani na huyoo! Kaenda zake; barabarani, angani au hata katikati ya kilindi cha bahari. Leo twajivunia ujuzi na maendeleo ya kiafya na madawa yapunguzayo mno unyofu wa binadamu lakini bado kuna pengo kubwa kati ya vikongwe na watu wa makamo, kinyume na zama hizo. Maisha ya karne hii yamekuwa kama zile nguo ziitwazo“bwaga – mtwae’’, ambazo hazibali kufumka au kukwajuka. Hivi leo, mtu akiumwa na kichwa hukimbilia kwa daktari. Mwingine akiumwa na nyoka popote pale, hukimbilia hospitalini akapate sindano ambayo hata jina lake halijui. Zamani ilikuwa mtu achimbechimbe mizizi ya upuzi upuzi, aitafune na alipata nafuu! Wa kisasa twawapuuza wa kale eti hawakujua elimu ya usafi tuijuavyo sisi, ilhali walikuwa wakiichoma miili ya watu waliokuwa wamekufa kwa ukoma au kifua kikuu. Wakati mwingine walikihama kijiji kilichoingiliwa na maafa ya ndui. Hata sasa wagonjwa kama hao hutengwa hospitalini huku maradhi kama vile UKIMWI bado yakikosa tiba. Mengi tuliyonayo sasa, mathalan tarakilishi na eropleni yalivumbuliwa au kugunduliwa na hao wa zamani. Fanaka zetu zote na ustawi tulionao asili yake ni watu hao wa zamani. Akili ni mali na kila mtu ana zake. Kuongezeka kwa watu duniani, mchanganyiko au matumizi mabaya ya madawa mengi pamoja na uchafuzi wa hali ya anga pia yameongezea kuleta hasara kubwa. Kweli sikio haliwezi kushinda kichwa. (a) Kulingana na mwandishi, kwa nini maisha ya kale na ya sasa hayalingani? (alama 3) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (b) Kupata mavazi zama zile kulikuwa nafuu. Toa sababu. (alama 2) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (c) Kwa kusema siku hizo, ’chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo,’ mwandishi anamaanisha nini? (alama 2) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (d) Taja sababu za magonjwa na maafa kukithiri siku hizi licha ya hatua kubwa katika elimu na afya. (alama 3) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (e) Fafanua usemi, ’sikio haliwezi kupita kichwa’ kwa mujibu wa taarifa. (alama 2) (f) Eleza maana ya: (i) Magome – (ii) Vururu mtende – (iii) Hazibali - (alama 3) 1. UFAHAMU
(a) Mabadiliko ya maisha/athari za kigeni/mitindo mipya ya kimaisha;, mavazi, chakula, afya nk. Mazingira yanayobadilika – Sheria zinabadilika Teknolojia, tarakilishi nk. Zozote 3 x 1 = 3 (b) Wanyama walifugwa kwa wingi Misitu ilikuwa kocho Watu walikuwa huru hata kuwinda na kukata miti Zozote 2 x 1 = 2 (c) Chakula kilipatikana kwa urahisi mno na bila malipo au gharama kubwa. 1 x 2 = 2 (d) Idadi kubwa/kuongezeka kwa watu duniani Mazingira yanayobadilika mara kwa mara Mchanganyiko au matumizi ya madawa mengi pamoja Uchafuzi wa hali ya anga Zozote 3 x 1 = 3 (e) Vijana si sawa na wazee; watu wazima wana hekima, busara na tajriba ya maisha Watu wa siku hizi hawawashindi wa zamani kimaisha 2 x 1 = 2 (f) (i) Maganda ya miti (ii) Ovyo ovyo bila woga au vikwazo (iii) Hazikawii; hazichukui muda ; hazihimili 3 x 1 = 3 UFAHAMU1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali. Mtoto anapozaliwa huwa ni malaika wa Mungu, hutaraji kuongozwa kwa kila njia ili awe mwana mwelekea. Jukumu la kulea mtoto huanzia nyumbani. Wako baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa jukumu hili muhimu hutekelezwa bora na mama; wengine husema ni jukumu la baba. Ni kweli kwamba mtoto huwa na mama yake kwa muda mrefu zaidi ya baba lakini kivuli cha baba hakikosi kumwandama na kumwathiri maisha yake. Uongozi wa mama huanzia siku ya mwanawe kuingia ulimwengu kwa hivyo, mama zaidi ya baba huwa ndiye chanzo cha chemichemi ya maisha ya mwanawe. Mtoto wa kawaida ana tabia ya kuiga kila jambo analoliona na kusikia na mambo ya awali ajifunzayo kutokana na mamaye. Je; mtoto huiga kutokana na mama pekee? Kila utamaduni hasa huku kwetu Afrika, una taratibu zake zilizopangwa kuhusu malezi ya watoto. Kwa mfano ; akina baba wengine wanaoishi maisha ya kijadi huonelea kwamba ni jukume lao kuwalea watoto wa kiume. Kwa hivyo mvulana anayekulia katika mazingira haya akishachuchuka kiasi cha kujua lipi zuri na lipi baya huanzia kuwa mtoto wa baba zaidi ya kuwa wa mama. Baba huathiri mtoto wake kwa kushauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume. Hupenda kukaa naye katika uga wake kwa kumshauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume huku akimkataza kukaa jikoni na kumsisitizia kuwa wanawake ni tofauti naye. Aidha, humfunza sifa kama vile ushujaa na uvumilivu kwa namna ambavyo huona kuwa ni ya kiume. Pindi mtoto anapoonyesha tabia za kikekike, baba hujiandaa kuzitadaruki kwa kumkaripia. Baba hutaka kujiona mwenyewe katika hulka ya mwanawe. Baba kama huyu humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wake wa kiume kwa jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. Kwa upande mwingine baba huyu huwa na machache ya kuzungumza na bintiye kwa kuwa huona kuwa sistahili yake kufanya hivyo. Mtoto wa kike huachiwa mamake lakini kutokeapo jambo la kulipima mama huona linampita kimo, humwita baba kuingilia kati na angalabu baba naye humwagiza dadake aje atoe suluhisho mwafaka. Ulezi kama huu una nafasi yake katika jamii, lakini ni lazima tukiri kuwa pia unaendeleza maisha ya fawaishi na kuanzia taasubi ambayo hatima yake ni mwanamke kukandamizwa na mwanaume. Wazazi walio na mwelekeo huu katika malezi yao hufikiri kuwa wataishi na watoto wao katika mazingira finyu na kwa hivyo waendelee kuwapulizia pumzi za kuhilikisha. Lakini ni sharti wakumbuke kuwa wao si walezi peke yao na mtoto hawezi kuishi pekee yake na kuwa na tabia ya kipekee. Leo ataishi kwao lakini kesho itambidi atoke aone ulimwengu. Kila atakapotia mguu ataona mambo mapya yatakayompa tajriba mpya na mawazo mapya ambayo aghalabu yataendelea kuathiri hulka yake. Iwapo tabia alizopata kwa wazazi wake hapo awali zilikuwa na misingi isiyokuwa madhubuti na mielekeo finyu, zinaweza kuwa pingamizi katika maingiliano yake na watu wengine. Mambo haya yanatuelekeza katika kufikiri kwamba maisha ya sikuhizi hayaruhusu ugawaji wa kazi ya malezi ya namna baba na mama wa kijadi. Baba na mama ni walezi wa kwanza ambao kwa pamoja wanapaswa kuelekeza watoto wao katika maisha ya ulimwengu iliyojaa bughudha na ghuhuri. Ni lazima wazazi watambue tangu awali kuwa katika malezi hakuna cha ubaguzi. Hakuna, mambo ajifunzayo mtoto wa kiume ambayo hayamhusu mtoto wa kike. Uvumilivu, bidii, utiifu na kadhalika ni sifa zinazomwajibikia kila mtoto kama vile upishi, ukulima na usafi. Mwanamke tangu azali ameumbwa kuwa mama na haipasi kulazimishwa kuchagua baina ya mtoto wa kike na wa kiume. Mapenzi na wajibu wa wazazi yapaswa yasiwe na mipaka bali yawe maridhawa kwa watoto wote. Maswali (a) Toa kichwa mwafaka cha makala haya. (al.1) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (b) Kulingana na kifungu hiki, taja mambo mawili ambayo yanaweza kuwa hatari kwa malezi ya watoto. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………..…… (c) Kwa nini baba humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wa kiume katika jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (d) Eleza mambo mawili ambayo ni ya manufaa katika ulezi wa jadi. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (e) Kulingana na makala haya, ushahidi gani unaonyesha kwamba kutegemeana katika ulezi jadi? (al.3) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (f) Taja sifa mbili ambazo baba humfundisha mwana wa kiume. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu hiki: (i) chanzo cha chemichemi… …..…………………………………………………………………………………………………… (ii) Akishachuchuka …………………………………………………………………………………………………..…… (iii) Hulka …………………………………………………………………………………………………..…… Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yoteMgomo uliingia siku ya tano. Asubuhi hii ilikuwa mbaya. Watu mbalimbali walikwisha kamatwa mjini na shamba, wakiwemo wote waliohudhuria kikao maalumu kibandani mwa Fumu. Siku ya pili ya mgomo, Makame aliuawa upenuni pa kibanda chake.Alipatikana amechomwa visu vitano vya mbavu. Mauaji ya kikatili lakini hayakuwa ya siri. Boga, yule kijana aliyehudhuria kikao cha pamoja na Fumu, ambaye toka mwanzo hadi mwisho wa kikao hakusema lolote, saa sita za usiku, aliingia kibandani na kumchopeka Makane visu mbele ya mkewe na wanawe, kisha aliikokota maiti na kuitupa upenuni. Asubuhi, Boga alikuwa mtu wa kwanza katika mkumbo mzima. Yeye alikamatwa kwa uuaji, makosa makubwa zaidi kuliko wenzake. Kukamatwa kwa watu hakukusaidia kitu - mgomo uliendelea. Kule shamba, vilio vya wanawake walioachwa pweke vilisikika. ‘Maskini mume wangu ….maskini, bora, bora ungaliwapeleka hao ng’ombe wakapigwa sindano; kufa kwa ng’ombe si kufa kwa nafsi yako,’ alilia bibi mmoja. ‘Ee, kufa kwa wengi arusi ndugu yangu we. Mimi nimelia we, hata macho yamenivimba kwa mume wangu; ati kakataa kupeleka mazao mjini na kuwajibu askari ufidhuli, lakini halafu nimeona haina maana kulia. Bora tufunge vibwebwe na sisi tuwasaidie kucheza ngoma - wafugaji mia wamekamatwa, wakulima mia mbili na hamsini, na bado wanaendelea kukamata, mji umebaki na wanawake tu; lakini watu wenyewe wana vioja, wanapochukuliwa utawaona wanacheka, sisi tulie nini?’ Mjini kulikuwa na vilio vyake. ‘Mwanangu wamemchukua , wanasema watamfunga au watamwua, kafanyaje? Daima kawatumikia , kapoteza nguvu zake juu yao na sasa…’Alimnung’unikia bibi mmoja. ‘Nini bibi we, wachukuzi na makuli watapata haki zao, na wale wanaozurura iko siku wataajiriwa na watakuta mambo mazuri, na wafanyikazi viwandani watachoka kufukuzwa ovyo ; hivyo ndivyo alivyonambia mwanangu alipokuwa akitoka, pingu mikononi. Nililia bibi, uchungu wa mwana unaujua bibi yangu, lakini baadaye nilipofikiri, nikachanganyisha na yale aliyokuwa akaniambia Ali mwanangu, kila siku; niliuhisi uzito wa maneno yake, nikafuta chozi babu.’ Wasaliti walikuwepo, lakini nafasi ya kusaliti haikupatikana. Kwenye lango la bandarini makuli na wachukuzi walisimama imara na marungu na mapanga tayari kuwang’ariba wahaini wowote. Ng’ambo, vikundi vilitawanyika na kufanya kazi; Wengine walitembea mipini mikononi, tayari kumtia adabu yeyote aliyetokwa na imani ya mgomo. Kikundi kingine kiliwekwa sokoni. Hakuna kitu kilichoingia wala kilichotoka. Magari hayakuwa na safari za shamba wala mjini. Askari walitembea ovyo na kumkamata waliyetaka kumkamata, lakini hakukutokea ghasia wala kupigwa mtu. Mgomo uliendelea, ukimuathiri kila mtu, lakini wale waliodai haki zao hawakuvunja kani. ( Dunia Mti Mkavu-Saidi Ahmed Mohamed) MASWALI 1. Toa anwani mwafaka kwa makala haya. (alama 1) ………………………………………………………………… ……………… 2. Thibitisha kuwa asubuhi hiyo ilikuwa mbaya. ( alama 1) …………………………………………………………………… ………… 3. Mauaji ya Makame yalikuwa ya kikatili. Eleza. (alama 4) …………………………………… …………………… 4. ‘Kufa kwa wengi arusi’. Thibitisha ukweli wa methali hii kwa kurejelea taarifa uliyosoma.(alama 4) …………… ………………………………… … 5. Watu walikamatwa kwa nini? (alama 2) ………………………………………………………… 6. Kwa nini wasaliti hawakupata nafasi yao kusaliti ? (alama 2) ………………………………………………… 7. Eleza maana ya (alama 2) i) makuli …………………… ii) Ukimuathiri ………………………… majibu
MAJIBU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.UFAHAMU Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu; ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana. Ung’amuzibwete ni kibinimethali chake; hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi. Baadhi ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung’amuzibwete wake na kutokeza katika ndoto zake usiku. Kwa mujibu na mawazo ya Sigmund Freud, mwanasaikolojia wa jadi anayechukuliwa na wengi kama mwasisi wa taaluma ya saikolojia, mambo yanayopatikana katika ang’amuzibwete yana sifa hasi. Freud alidahuli kuwa binadamu huyaficha na kuyabania kwenye ang’amuzibwete mambo ambayo hawezi kuyasema kadamnasi. Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli zilizobaramishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ang’amuzibwete. Shehena hiyo ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli zinazotutoka bila wenyewe kukusudia, ishara na lugha ya kitamathalu katika uandishi wa kibunifu na kadhalika. Ung’amuzibwete una uwezo mkubwa wa kuathiri matendo ya bmadamu. Huu ndio msmgi unaowafanya wanasaikolojia wengi, ukiwemo Freud, kusema kuwa tajriba ya mtoto maweza kufichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokeza katika utu uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku tunayang’amua tuyafanyayo, ung’amuzi unaotuwezesha kutambua jema na ovu unatawala. Ung’amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung’amuzibwete wake hutawala. Sisi tunaotawaliwa na ung’amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa kutuelewa. Carl Gustav Jung, aliyewahi kuwa mwanafiinzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud na kuungalia ung’amuzibwete kamajaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung’amuzibwete wa kibinafsi na ung’a,izibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya unaomuhusu mtu binafsi hupatikana katika ung’amuzibwete wa kibinafsi. Dhana ya ung’amuzibwete jumuishi aliitumia kuelezea sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo fulani kama binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu wengi wana sherehe za kuzaliwa mtoto, kuoa, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi Fulani wa kila mwanadamu. Urithi huo unaopatikana katika ung’ amuzibwete una uwezo wa kuathiri ung’amuzi na matendo ya binadamu ya king’amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzuhusisha sehemu zote mbili kwa sababu zinaathiriana. MASWALI(a) Kwa nini ung’amuzibwete unaelezwa kama kinyume cha ung’amuzi? (alama 2) .……………………………………………………………………………………………… (b) Eleza mtazamo wa Freud kuhusu ung’amuzibwete (alama 3) ……………………………………………………………………………………………….. (c) Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung’amuzibwete hudhihirika vipi? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………….. (d) Eleza tofauti ya mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung. (alama 4) ……………………………………………………………………………………………….. (e) Taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud. (alama 2) .……………………………………………………………………………………………… Majibu
(a) Ung’amuzibwete hufanya kazi mtu akiwa amelala/usiku kinyume na ung’amuzi ambao hufanya kazi mtu akiwa macho/mchana. 1x2 = 2 (b) Mambo yanayopatikana katika ung’amuzi bwete (i) Yana sifa hasi / hubana sifa hasi (ii) Huficha mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyasoma wazipeupembele ya kadamnasi (iii) Hubana matamanio yasiyokubalika na jamii (iv) Hubania kauli zilizoharamishwa na miiko ya jamii. 1x3= Hojayoyote mojaAl— 3 (c) (1) Kwa ishara za ndoto (ii) Kwa mitelezo ya kauli (iii) Kwa ishara (iv) Kwa matumizi ya lugha ya kitamathali katika uandishi 4x1= 4 AIa,na-4 (d) Freud anawaza kuwa ung’amuzibwete ni jai la mambo hasi ilhali Jung ana dhana mbili kuhusu ung’amuzibwete (i) Ile ya kibinafsi (ii) Ile ya jumuishi au Freud ana mtazamo wa dhana hasi katika ung’amuzibwete ilhali Jung anawaza dhana ya jumuishi. 2x2=4 Mwanafunzi aonyesha dhana zote mbili ya Freud na ya Jung (e) Ung’amuzibwete una uwezo wa kuathiri ung’amuzi na matendo ya binadamu ya king’amuzi. Al-2 Maswali na Majibu ya UFAHAMU (Alama15)Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa msururu wa migomo na maandamano ya raia. Fujo za karibuni kabisa ni zile zinazoshuhudiwa katika miji mikubwa za wachuuzi na wafanyibiashara wakipinga hatua za serikali za kaunti kuwatoza ushuru takribani kwa kila huduma na bidhaa ikiwemo wanyama, kuku na ndege. La kuhuzunisha zaidi katika baadhi ya majimbo imeripotiwa kuwa raia wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti. Wanasiasa wameonekana kuwa na wakati mgumu kutetea mfumo huu mpya wa ugatuzi huku baadhi wakisema kwamba matatizo yanayoshuhudiwa kwa sasa yametokana na ugeni wa mfumo huo. Wengine wameinyoshea kidole serikali ya kitaifa kwamba ndiyo inayosambaratisha muundo huu. Wengine wanahoji kuwa bado ni mapema na kwamba kunatajika muda mrefu ili kufaulu. Ni wazi kwamba kumekosekana nidhamu bora ya kusimamia maisha ya raia nchini Kenya. Matatizo yanayokumba raia kwa sasa ni dalili kuwa mfumo wa serikali ya ugatuzi umeongezea chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu. Swali ni je, hadi lini nidhamu ya kusimamia raia itakuwa ni suala la majaribio na makosa? Hatua ya kuwarundikizia raia ushuru mkubwa ni kitendo cha unyonyaji na cha dhuluma kinachofaa kupingwa. La kufahamishiwa hapa ni kwamba ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serikali zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi wa kibepari ikiwemo Kenya. Asilimia 90 ya mapato ya serikali za kibepari huegemea ushuru. Kwa hivyo hatua ya serikali za kaunti katika kuwanyonya raia kwa kuwalipisha ushuru si ajabu bali ni thibitisho kuwa jamii ya Kenya inaongozwa na nidhamu ya kiuchumi ya ubepari mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji. Ukweli unabakia kuwa ndani ya serikali za kibepari raia ndio hubebeshwa mzigo wa ushuru unaoishia matumboni mwa viongozi! Miito ya mabadiliko ya katiba na ya miundo mipya ya kiutawala si lolote ila ni moja tu ya hatua za mfumo wa kibepari kujipa muda wa kuishi na kuziba aibu zake za kushindwa kusimamia maisha ya watu. Kufeli huku kwa mfumo huu kunashuhudiwa hadi kwenye nchi kubwa za kibepari kama Marekani na Uingereza hivyo nazo zimekumbwa tele na maandamano na fujo za raia wakilalamikia hali ngumu ya maisha. Maswali a) Yape makala haya anwani mwafaka. (alama 1) __________________________________________________________________________ b) Eleza mtazamo wa wanasiasa kuhusu utepetevu wa mfumo huu. (alama 3) __________________________________________________________________________ c) “Ugatuzi nchini Kenya ni mfumo wa kibepari” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea makala. (alama 3) __________________________________________________________________________ d) Migomo ni zao la matatizo yaliyogatuliwa kutoka kuu. Toa sababu nyingine zinazosababisha migomo katika serikali za ugatuzi (alama 4) __________________________________________________________________________ e) Thibitisha jinsi mfumo wa ugatuzi umeongeza chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu (alama 2) __________________________________________________________________________ f) Eleza maana ya maneno yafuatayo (alama 2) i) Ugatuzi __________________________________________________________________________ ii) Kibepari __________________________________________________________________________ MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA (a) Changamoto za Ugatuzi/Matatatito ya tigatuzi/Ugatuzi ( alama 1x1 = 01) (b) - Ugatuzi ni mfumo geni (Alama 3x1=03) - Serikali kuu kutowajibika - Kudai kuwa mfumo huu unahitaji mda zaidi (c) - Mfumo wa ugatuzi nchini umehusisha matendo ya kibepari kama vile; (alama 3x1=03) - Raia kupewa mzigo wa kulipa ushuru ili kuipa serikali mapato - ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serlkal zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi - viongozi kuwanyonya raia walio maskini (d) - Hali mbaya ya muundo msingi (alama 4x1= 04) - Viongozi kuendeza ufisadi - Ukosefu wa usawa katika ugavi wa rasilimali - Viongozi kupuuza mchango wa wananchi (e) - Raia kulazimishwa kulipa ili kuona maiti za jamaa zao katika fuo (alama 2x1=02) - Raia kurundikiziwa mzigo wa kulipa ushuru mkubwa - Ushuru unaolipwa na wananchi hauwasaidii wananchi la huishia mifukoni mwa viongozi (f) (i) Ugavi wa mamlaka na raslimali kutoka serikali kuu hadi mashinani (alama 2x1 =02) (ii) mfumo wa kiuchumi wa watu wachache kumiliki raslilmali kwa kuwapora wengine Ondoa nusu alama kwa kila kosa la sarufi hadi makosa sita. Ondoa nusu alama kwa kila kosa la tahajia hadi makosa sita. UFAHAMUSoma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yote Mgomo uliingia siku ya tano. Asubuhi hii ilikuwa mbaya. Watu mbalimbali walikwisha kamatwa mjini na shamba, wakiwemo wote waliohudhuria kikao maalumu kibandani mwa Fumu. Siku ya pili ya mgomo, Makame aliuawa upenuni pa kibanda chake.Alipatikana amechomwa visu vitano vya mbavu. Mauaji ya kikatili lakini hayakuwa ya siri. Boga, yule kijana aliyehudhuria kikao cha pamoja na Fumu, ambaye toka mwanzo hadi mwisho wa kikao hakusema lolote, saa sita za usiku, aliingia kibandani na kumchopeka Makane visu mbele ya mkewe na wanawe, kisha aliikokota maiti na kuitupa upenuni. Asubuhi, Boga alikuwa mtu wa kwanza katika mkumbo mzima. Yeye alikamatwa kwa uuaji, makosa makubwa zaidi kuliko wenzake. Kukamatwa kwa watu hakukusaidia kitu - mgomo uliendelea. Kule shamba, vilio vya wanawake walioachwa pweke vilisikika. ‘Maskini mume wangu ….maskini, bora, bora ungaliwapeleka hao ng’ombe wakapigwa sindano; kufa kwa ng’ombe si kufa kwa nafsi yako,’ alilia bibi mmoja. ‘Ee, kufa kwa wengi arusi ndugu yangu we. Mimi nimelia we, hata macho yamenivimba kwa mume wangu; ati kakataa kupeleka mazao mjini na kuwajibu askari ufidhuli, lakini halafu nimeona haina maana kulia. Bora tufunge vibwebwe na sisi tuwasaidie kucheza ngoma - wafugaji mia wamekamatwa, wakulima mia mbili na hamsini, na bado wanaendelea kukamata, mji umebaki na wanawake tu; lakini watu wenyewe wana vioja, wanapochukuliwa utawaona wanacheka, sisi tulie nini?’ Mjini kulikuwa na vilio vyake. ‘Mwanangu wamemchukua , wanasema watamfunga au watamwua, kafanyaje? Daima kawatumikia , kapoteza nguvu zake juu yao na sasa…’Alimnung’unikia bibi mmoja. ‘Nini bibi we, wachukuzi na makuli watapata haki zao, na wale wanaozurura iko siku wataajiriwa na watakuta mambo mazuri, na wafanyikazi viwandani watachoka kufukuzwa ovyo ; hivyo ndivyo alivyonambia mwanangu alipokuwa akitoka, pingu mikononi. Nililia bibi, uchungu wa mwana unaujua bibi yangu, lakini baadaye nilipofikiri, nikachanganyisha na yale aliyokuwa akaniambia Ali mwanangu, kila siku; niliuhisi uzito wa maneno yake, nikafuta chozi babu.’ Wasaliti walikuwepo, lakini nafasi ya kusaliti haikupatikana. Kwenye lango la bandarini makuli na wachukuzi walisimama imara na marungu na mapanga tayari kuwang’ariba wahaini wowote. Ng’ambo, vikundi vilitawanyika na kufanya kazi; Wengine walitembea mipini mikononi, tayari kumtia adabu yeyote aliyetokwa na imani ya mgomo. Kikundi kingine kiliwekwa sokoni. Hakuna kitu kilichoingia wala kilichotoka. Magari hayakuwa na safari za shamba wala mjini. Askari walitembea ovyo na kumkamata waliyetaka kumkamata, lakini hakukutokea ghasia wala kupigwa mtu. Mgomo uliendelea, ukimuathiri kila mtu, lakini wale waliodai haki zao hawakuvunja kani. ( Dunia Mti Mkavu-Saidi Ahmed Mohamed) MASWALI
|
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|