Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
1. MUHTASARI: (Alama 15) Ponografia na athari zake: Ponografia ni tendo, maandishi, picha au mchoro unaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa ajili ya kuchochea ashiki ya kufanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana kupitia sinema, video, magazeti, vitabu, muziki, televisheni, wavuti, DVD n.k. Ponografia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii ni kwa sababu imeenea ulimwenguni kote mithili ya moto katika mbuga wakati wa kiangazi. Uenezi umechangiwa na mambo kadha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi umetokana na kuimarika kwa vyombo vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Matumizi ya tarakilishi, mdahilishi na viungambali vya picha yamesambaza ponografia haraka na kwa wingi. Haifahamiki barabara jinsi ponografia ilivyoanza. Hata hivyo hubuniwa au kutengenezwa na makundi mbalimbali ya watu. Miongoni mwa hawa ni watu wasiojali maadili. Pili, kuna wale wenye matatizo ya kisaikolojia na kijamii. Wao hutengeneza na kueneza uchafu huu kwa lengo la ama kuvuruga maadili katika jamii au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi lingine ni lile la wanaoichukulia ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Hivi sasa, kundi kubwa ni lile la wanaotumia matusi haya kama njia ya kuchuma. Kwa mfano, kuna wanamziki ambao hutumia ponografia kuvutia wateja na hivyo kuzindisha mauzo yao. Kushamiri kwa wimbi la uonyeshaji ponografia kuna athari kubwa kwa jamii na hasa watoto. Ingawa watu wengine hudai picha hizi haziwaathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wanaotazama picha za ngono hupata matatizo. Lazima ieleweke kuwa kinachoonekana na jicho au kusikika kwa sikio huathiri fikra au hisia. Picha za matusi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia mambo muhimu kama masomo watu huanza kutafakari mambo machafu. Vijana wengi ni kama bendera. Hivyo basi huanza kuiga wanayoyaona na kusikia. Hili ni tatizo linalowafanya kuacha mkondo wa maadili. Kutokana na uchafu huu, watu wengi hushawishiwa kuingilia shughuli za ngono mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni mengi. Haya ni pamoja na ukahaba. Utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya darasani na mambo yasiyotarajiwa. Vijana wengi huacha shule kabisa.Wengine wao huambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo huwaletea mauti. Inasemekana kuwa akili za binadamu hunata zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha. Si ajabu, vijana huyadumisha matusi haya katika kumbukumbu zao na kuyafanya sehemu ya maisha yao. Wengi huanza kuandama tabia mbovu kama ushoga, ubasha na usagaji. Kuna wale ambao huanza kujichua. Kujichua ni hali ya mwanamke au mwanamume kumaliza haja za kimaumbile bila kufanya mapenzi na mtu mwingine. Ponografia imechangia pakubwa kuenea kwa haya. Jambo hili limegeuza mielekeo ya vijana.Wanaiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao. Halikadhalika, huiga lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono. Yote haya yanapingana na desturi za mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kila kuchapo. Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama unywaji wa pombe, matumizi ya dawa za kulevya, uvutaji sigara na utumiaji wa dawa za kuchochea uchu wa ngono. Mambo haya huwapa vijana tabia za unyama. Jambo hatari ni kuwa, kuendelea kutazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu, yaani huondoa makali. Hata katika utu uzima, mtu atapoteza mhemko wa kawaida na kugeuzwa kuwa mtegemezi wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na maenezi haya yasiyo kizuizi. Jambo la kwanza ni kuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi. Kwa namna hii itawezekana kupunguza mahitaji na uuzaji wa ponografia. Aidha ni vizuri watu wazima wawajibike ili wawalinde hasa vijana kutokana na adhari hizi. Inapasa wenye midahilishi, video na sinema wasiwaruhusu vijana kutazama uchafu huu. Tatizo la kuenea kwa ponografia limeendelea kuwepo kwa sababu ya udhaifu wa sheria. Kilicho basi ni kuweka sheria za kuzuia utengenezaji na usambazaji wa upungufu huu. Kuambatana na haya, hatua kali zichukuliwe kwa wanaovunja sheria hizi. Halikadhalika, ushirikiano wa karibu baina ya wadau uimarishwe katika ulimwengu mzima. Serikali na mashirika ya midahilishi yajumuike kutambua chanzo cha taka hizi kisha wanaohusika wakabiliwe ipasavyo. Jamii ingependa kuona michakato ya kuharamisha utengenezaji, usambasaji na utangazaji wa ponografia ikiwekwa. Wazazi nao wasijipweteke tu bali wasaidie. Ni muhimu washikilie kwa dhati juhudi zao za kuwaelekeza na kuwashauri watoto kuzingatia uongofu na kukwepa picha hizi najisi. Watoto lazima waelezwe kuwa haifai kutazama picha au michoro michafu. Itikadi na imani za kidini na utamaduni wa kiafrika unakataza vikali mtu kuona uchi wa mtu mwingine. Matokeo ya kuasi makatazo haya yana madhara makubwa kwa watu na jamii. Maswali: 1. Ponografia hutengenezwa na akina nani na kwa nini?(maneno 20) (Alama 2) ……………………………………… 2. Eleza sababu za ponografia kusambaa ulimwenguni namna ilivyofanywa.(maneno 10) (Alama 2) ………………………………………… 3. Fupisha aya za mwisho tatu kwa maneno 60. (Alama 7) ……………………………………………… (Utiririko. Alama 2 baada ya kupitia kama wavutia la sivyo pima uwezo wa mtahiniwa.) (Alama 2) ………………………………………………… Muhtasari
1. - Watu wanaotosheleza ashiki zao. - Hutengenezwa na watu wasiojali maadili. - Hutengenezwa na makundi mbalimbali ya watu wasiojali maadili yoyote. (Hesabu maneno) (alama 2 ) 2. Sababu za kusambaa • Akili za binadamu kunata yanayowasilishwa kwa picha. • Mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao. • Lugha, ishara na miondoko inayohusu ngono. Sentensi moja au mbili zilizo na hoja hizi (idadi ya maneno iwe kati ya 6-13) (alama 2) 3. Kueleza ubaya wa ponografia kwa umma. • Kuweka sheria za kuzuia ueneaji. • Ushirikiano wa karibu baina ya washika dau uimarishwe. • Wazazi kuwaelekeza na kuwashauri watoto wazingatie uongofu na kuepa picha hizi. (Idadi ya maneno kati ya 56 – 63) Muhtasari Tanbihi i) Pitia majibu yote ii) Dondoa makosa ya sarufi na hijai iii) Ongeza alama 2(mbili) iwapo mtiririko ni mzuri (tathmini utiririko wa mtahiniwa) Mfano J = 13 J = jumla ya alama Ut = 2 Ut = utiririko bora 15 S – 1 ½ S = makosa matatu tofauti ya sarufi 13 ½ h = 2 h = makosa manne tofauti ya maendelezi 11 ½ 12
0 Comments
UFUPISHO: (Alama 15) Soma kifungu kisha uyajibu maswali yanayofuata. Nidhamu ni kitu cha maana sana maishani mwa binadamu. Kila mwanafunzi anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana.Akiwa na nidhamu hiyo, atakuwa mtu mwadilifu, anayeweza kustahiwa na kusadikika katika mambo, shughuli na hali tofauti. Kwanza, mtoto mwenye nidhamu huwa kama anga au nuru nyumbani mwao, shuleni na pia katika jamii.Watu wote wanampenda na kumheshimu. Wazee kwa vijulanga wote wanamtegemea kama msimamizi wa mambo nyeti ya maisha yao. Kwa hivyo, ni dhahiri shahiri kwamba mwadilifu hunufaika sana, kinyume na mkaidi ambaye wahenga walimwambia kwamba atakosa kufaidi hadi siku ya Idi. Pili, huwadia nyakati ambapo huwa kuna jambo la busara, mathalani jukumu ama dhima fulani ambayo huhitaji tu mwakilishi mmoja darasani, shuleni au katika jamii. Watu hapana shaka watamteua yule mwadilifu kuchukua nafasi kama hiyo. Ndio maana viranja wanaoteuliwa shuleni, huwa ni wanagenzi ambao tayari wamekwisha tiliwa katika mizani na kupigwa msasa madhubuti. Vile vile, mwadalifu daima atajiepusha na shutuma na majanja yote yanayoweza kuchipuka. Kuna msemo maarufu, kwa busara yake iliyobusarisha mwadilifu kwamba “aliye kando haangukiwi na mti.”Pia waliambiwa kwamba, “ pilipili usiyoila yakuwashiani?” Ni bayana kutokana na misemo hiyo miwili kwamba mwenye nidhamu hawezi kuhusishwa na majanga hatari yanayoweza kuyakumba watu. Walakini ni vyema kujiuliza, je, nidhamu huanzia wapi, na kwa nini kuna baadhi ya ‘watoro’ ambao ni utovu wa nidhamu? Utovu wa nidhamu huanzia awali sana maishani mwa mja. Mtoto anapozaliwa, anategemea miongozo na mielekeo ya watu wazima ambao wakomazingirani mwake.Ndipo wakale wale waliokaramka walisema kwamba mtoto akibebwa, hutazama kisogo cha nina. Hivi ni kusema kwamba, nidhamu au utovu wa nidhamu huanzia nyumbani hadi shuleni, kisha hupanuka hadi kufikia kiwango ambapo mja anatangamana na watu wote katika maisha yake.Ikiwa sehemu moja ya ukuaji wa nidhamu maishani mwa mja itasambaratika, basi hawezi akawa mkamilifu kinidhamu maishani mwake. Kwa vile ni bayana kwamba mabaya yote ayatendayo duniani hulipwa na Mola papa hapa duniani,watovu wa nidhamu wote huishia kuangamia, ama kujuta mno kwa amali zao potovu.Ni kheri mja kujihidi mwenyewe, kwani uhalifu haulipi chochote. a) Nini umuhimu wa nidhamu? (maneno kati ya 50-55) (al. 1 ya mtiririko) (alama 7) Matayarisho ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ ........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ Jibu ........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ (b) Bila kubadilisha maana, fupisha aya nne za mwisho. (tumia maneno 55-60) (alama 1 mtiririko ) (alama 8) Matayarisho ........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ Jibu ........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ 2. NIDHAMU
(a) Nidhamu (alama 1) (b) Umuhimu wa nidhamu: • Mwenye nidhamu ni nuru nyumbani hata shuleni. • Anakuwa kiongozi wa wote / watu humtegemea • Kiatu humpenda. • Anajiepusha na shutalma na majanga. • Kijumla anastahiwa. • Hupata fursa ya kuteuliwa miongoni mwa wengi kwa dhima fulani. (Hoja 6 1 = alama 6, mtiririko al. 1, jumla alama 7) (c) Muhtasari wa aya nne za mwisho. i) Mwadilifu hajipati katika matatizo mengi. ii) Lakini utovu wa nidhamu huanzia ututoni na mtoto huiga tabia za wazazi wake na huendelea shuleni. iii) Utovu wa nidhamu hulipwa kwa adhabu mumu humu / watu wajirekebishe. Makosa Sarufi ½ x 10 = alama5 Hijai ½ x 6 = alama 3 Adhibu kila kosa la sarufi na hijai linapotokea SWALI LA PILI – UFUPISHO Soma taarifa ifuatayo kisha ufupishe taarifa hii kulingana na maswali yanayofuata. Katika kipindi cha mwongo mmoja, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, radio ndicho chombo cha habari cha kipekee kilichotamalaki kote nchini. Familia nyingi ziliweza kumiliki chombo hiki. Runinga ilikuwa miliki ya wachache, hasa mabwenyenye. Sasa hivi, hata akina yahe nchini na mashambani wanamiliki chombo hiki. Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasiliano kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundishia. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkem kwa mtu wa kila rika. Halikadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingara yao ya duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji wa staidi ya kufundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa kielimu, huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi. Fauka ya hayo, televisheni ni chemichemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa au kuburudishwa. Televisheni ni mojawapo wa vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu huwa ni liwazo kutokana na shinikizo na migogoro tunayokabiliana nayo kila siku. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu. Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usiokuwa na maadili , kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya wa kimavazi na maonevu ya rangi, dini jinsia , kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanayowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka kwa runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga. Mtumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa familia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujijenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii. Ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa na kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao. Hali kadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalani, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa n.k. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaaribika. Huu ni upotovu. Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya madawa ya kulevya kama tembo na sigara.Vitu hivi vinavyotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaotumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine. Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha na matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.. Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya wawaelekeze vujana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepakana na madhara yake. Maswali a) Ukitumia maneno 50-60, fupisha manufaa ya runinga. (alama8) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Fupisha hasara za runinga ukitumia maneno 70-80 (alama 7) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… SEHEMU B: UFUPISHO
a) Manufaa Hutumika kama nyenzo ya kufundishia Hufanya watu kuchua “misuli” ya kibongo na kufanya watu kuwa makini katika shughuli Hutumbuiza na kuchangamsha. Hii hupunguza gharama na wakati wa kuandama chemichemi nyingine za burudani. Huendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Mengi yanayotokea katika runinga huwezi kuakisi mtazamo, mikakati amali za jamii. (alama2 kwa kila hoja na alama 2 kwa muwala) b) Hasara - Wakati mwingi huendeleza hulka ambazo huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na wastaarabu. Hivyo, vijana huziiga na kuzifuata. - Runinga huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano miongoni mwa familia. Haya yanaweza kuwafanya baadhi ya wanafamilia kujitenga. Waliojitenga huwa rahisi kuingisha maovu. -Baadhi ya matangazo ya runinga hupotosha na kuwafanya watu kushiriki katika mambo hatari kama vile ulevi na kuvuta sigara. - Huwafanya watu kuiga tabia ya matumizi za nguvu za mabavu. (alama 2 kwa kila hoja na 2 kwa muwala) UFUPISHO2. UFUPISHO Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali. Ukimwi ni ufupi wa ukosefu wa kinga mwilini. Uwele huu ni wa zinaa ambao hauna tiba, dawa wala kafara. Insi anaweza kupata wiche ya ukimwi kwa njia ainati. Mathalani ni; kujamiiana baina ya mwanamume na mwanamke japo wote au mmoja ana wiche ya virusi vya ukimwi. Nina aliyehimili anaweza kumtia wiche mtotowe akijifungua au kwa kumnyonyesha. Katika harakati na mikakati ya kutoa damu, au ngeu hiyo kuchangamana na jeraha nyevu. Cheche akilia mfiche kuku, ama fisi akimia mwele funga mlango. Tuupige ukimwi vita shadidi, kwani si lelemama. Tutahadharike kabla ya athari kwani hadi sasa hakuna tiba hususan, ya uwele huu. Tarakimu zinabainisha kwa kina kuwa vijana wengi ndio wanaoathirika. Wengi wao wamefufutika na kugugunwa wakabakia mifupa. Hali kama hii ikishitadi kujiradidi nchi hii yetu itakosa viongozi wa mustakabali. Wimbo mui hauongolewi mtoto. Wazazi wanafaa kuwa kielelezo chema kwa wana wao. Mwana akibebwa hutazama kisogo cha ninake. Ni jambo la fedheha na kukereketa mtima kuwaona baadhi ya wazee wakichana mtaani vipara moto. Vijana hutegwa kwa chachu na kunaswa kwa ulimbo. Pengine huingia mitegoni kwa ghiliba chache tu za pesa nane. Enyi vijana jihadharini! Wazee hawa ni vitaange watawatosa demani. Mila na tamaduni nyingine zimepitwa na wakati. Wala hazina nafasi katika dunia ya sasa. Tunafaa kutembea na wakati kwani tusipoukata utatukata. Swala la kuingia mafa wajane wafaruku limekita mizizi miongoni mwa makabila humu nchini. Hili ni swala nyeti linalohitaji kuvuliwa nguo livaliwe nduruga. Serikali sharti iingilie kati na kukata kauli kuukomesha uozo na uvundo wa namna hii. Ukata na uchochole umechangia pakubwa katika kuupalilia mbolea ukimwi. Kwa sababu ya uchechefu wa fulusi za karo, shababi wengi hawamudu kuendelea na masomo. Kitembo cha elimu hakikiuki elimu ya msingi. Zaidi, mwanamume wa kisasa ambaye bado amefungwa pingu na taasubi za kiume hapendezwi na hali hii na huuma kidole akitamani ya kale. Shingo upande analazimika kukubali kuwa mabadiliko ni jambo la aushi. Mla kunde hunya kunde. Vijana lazima watahadharishwe na malimwengu. Wasije kufa na laiti ningalijua, na chanda kili kinywani. Wengi wamezizika mila na tamaduni katika kaburi la sahau. Hawaoni hawasikii kwa sababu hawana ashiki. Wameuvua utu wakajivika uchu. Matongozi yamejaa tadabui tena, masikio yamejaa komango yasiweze kusikia. Ukimwi unawagegeda na kuwakeketa kama umwa. Utamu unapoisha wanatemwa na kutiwa mavani kama makapi. Wanafaa kuaswa waasike kwa maaso yenye adili. Ulimwengu kokwa ya fuu haiishi utamu, anayeisha ni binadamu. Maswali (a) Fupisha ujumbe unaojitokeza katika aya tano za kwanza za makala haya. [Maneno 50 – 60] [Alama 8,2 za utiririko] Matayarisho …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... Jibu …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (b) Katika aya za sita na saba, mwandishi anawashauri waja. Toa nasaha hiyo. (Maneno 35 – 45 ) (Alama 7, 1 ya utiririko) Matayarisho …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... ……………………………………………………………………………………………………… Jibu …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... 2. UFUPISHO
(a) UKIMWI – Ugonjwa wa zinaa usiokuwa na tiba Mama anaweza kumwambukiza mtoto, wakati wa kuzaa au kunyonyesha Damu ikichanganyika baina ya watu ni hatari Watu waepukane na UKIMWI kwa vile ni hatari Vijana waonywa dhidi ya wazee waasherati Mila zingine zimepitwa na wakati Serikali ina sera mbovu kuhusu mila Umaskini huchangia UKIMWI Ni wajibu wa serikali kupambana na janga hili Zozote 6 x 1 = 6 (b) Watu kuelimika/kuelimishwa waepukane na maafa Vijana waonywa kuepuka maovu Vijana waenzi mila za jamii zao; wasitupe tamaduni/desturi Watu watii wanayoambiwa na wakuu Kuzingatia maadili Kujiepusha na tamaa nyingi za ulimwengu Kuwa na utu – kutahadhari na UKIMWI Zozote 6 x 1 = 6 MUHTASARI2. MUHTASARI
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati ya mioyo yetu uweze kupata ufanisi na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke, “Ajizi ni nyumba ya njaa.” Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga. Lazima tofanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima, kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa la watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao shambani, kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka. Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya hayo lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wake. Wengi ni wale wenye mawazo kwamba lazima aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wageni. Mafunzo tunayopata nyumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya mwana Kenya kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayo tumbaza na kufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa siku zijazo tuwe kielelezo chema kwa wengine. Watu wazima washirikiane na kufikiria kwamba wao ni wamoja, “utengano ni uvundo” lugha ya kitaifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuwaza kutuwasilishia mapendekezo, mawaidha na hisia zetu. Kukosa ndiko kibinadamu, wakati tunapokosea na kufanya masahihisho. Mara moja kwani; “usipoziba ufa, utajenga ukuta”. Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu na wenzetu. Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi yetu tukiwa wazalendo halisi. Sisi tukiwa vijana sharti tujishughulishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashtumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Utamaduni wa asili unakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na nyumbani mwetu. Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeeo, amani na upendo; lazima tuwe na bidii, ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo, tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo, basi tutabaki nyuma kama mkia siku zote. Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama utajiri wake. Kwa hivyo basi tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na nasaba au utajiri. (a) Dokeza mambo muhimu yaliyomo katika aya ya kwanza.(maneno 65-70) (al 8,2 utiririko) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… (b) Fupisha aya ya mwisho kwa kuzingatia mambo muhimu yanayopasa vijana kufanya. (maneno 35- 45) (ala 4, 1utiririko) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… UFUPISHO (Alama 15)Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwauwa maelfu ya watu na kuibua mifumo na taratibu za maisha ya watu. Hata hivyo , magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. Neno ‘UKIMWI’ lilitolewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha ukosefu wa kinga mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kicheka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile “umeme” na pia “ugonjwa wa vijana”. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wachanga wasioweza kujimudu. Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufikia mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini. Hivi sasa, inasemekana kuwa takribani watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imedhibitishwa kwamba takriban watu milioni mbili unusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuaambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo, makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao. Ugonjwa huu umeathiri jamii kwa njia nyingi. Hali ya maisha na woga, ukosefu wa matumaini, ongezeko la mayatima na kuzorota kwa uchumi kutokana na kutoweka kwa kizazi chenye nguvu za kutoa huduma kwa jamii, na baadhi ya athari za maradhi haya. Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia.Tuwe na matumaini kwamba siku moja, tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya, tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira hufuta heri. a) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo (maneno 90 - 100) (alama 3 kwa mtiririko) (alama 12 ) Nakala chafu/maadalizi ……………………………………… Jibu ……………………………………………………………… b) Eleza mambo yanayoleta matumaini kwa wagonjwa wa ukimwi kulingana na aya tatu za mwisho (maneno 40- 45) (alama 1 kwa mtiririko) Nakala chafu …………………………………………………… Nakala Safi ………………………………………………………………… MWONGOZO
UFUPISHO a) i) Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu- tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo n.k. ii) Magonjwa haya yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. iii) Magonjwa haya yaliwaua maelfu ya watu na kutibua mifumo na taratibu za maisha ya watu / yaliwaua watu wengi. iv) Magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba. v) Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. vi) Ukimwi unazidi kuenea kwa kasi. Umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni. vii) Ukimwi unazidi kuenea kwa kasi ulimwengu (lazima wazo la kazi litokee). viii) Wengi wa walioambukizwa ni kati ya miaka 15 – 49 ix) Kundi hili lina nguvu / linatunza jamii / wanaosalia ni watoto na wakongwe wanaoachwa. x) Ukimwi uligunduliwa Kenya mwaka wa 1984 (lazima ataje Kenya). xi) Watu zaidi ya 500 hufa kila siku xii) Ukimwi sasa ni janga la kitaifa. b i) Mashirika na makundi ya kujitolea kuwahudumia wagonjwa ii) Makundi hutoa tiba ya kisaikolojia na kuwapa ushauri na hima ya kuishi badala ya kukata tamaa. iii) Wengi hutibiwa nyumbani kwao. iv) Matumaini ya tiba kutokea. Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali.17/12/2023 Jibu makala yafuatayo kisha ujibu maswali.UFUPISHO Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa ama yoyote. Neno huzurn linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto duma imejaa raha, starehe na vcheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya kufurahisha na kustarehesha tu sio kudhikisha na kuhuzunisha. Huyu tunayemzungumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha kitendekacho mkono wake wa kushoto wala idle kinachofanyika hasa katika mkono wake wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo, vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi machungu ambayo huleta huzuni, sb raha. Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, meha mwana kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule. Huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Iii wasome kama inavyotakikana, m sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaacthibu, hasa wale watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ulivyo. Watoto wa ama hii wanapotiwa adabu raha hujitenga na buzuni huwatawala. Huzuni, hivyo basi, maonekana ya kuwa m uso wa pili katika maisha ya wanadamu, uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana, ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa yumo katikati ya kustarehe. Si tu, inajulikana dhahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao. Zingatia mtoto anayezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali, kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote. Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, anayempata bila kupanga. Hata mtoto huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni mievi na analojua ni kurudi nyumbani usiku akiimba nyimbo za kilevi, kuita mkewe kwa sauti kubwa, kuitisha chakula na kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa ama hiyo atakayoijua ni huzuni tu, si raha asilani. MASWALI (a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo. (Maneno-100). (Alama 9) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………… (b) Ukizingatia aya ya mwisho eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto buzuni. (Maneno 40-45) (Alama 4) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………… Majibu
Majibu (a) (i) Mtoto hudhani/hufikiri ulimwengu umejaa raha na hauna huzuni/hauna mateso/haudhikishi. (ii) Mtoto huyu ni yule mdogo ambaye hajajua kubainisha mambo. (iii) Anavyoendelea kukua, anafahamishwaanabainikiwa na mengi yaletayo huzuni. (iv) Nyumbani ingawa hupendwa, huadhibiwa wanapokuwa watundu na kuhuzunika. (v) Shuleni wanapozembea kazi, wanaadhibiwa na hili huwahuzunisha. (vi) Huzuni basi ni uso wa pili katika maisha ya binadamu, uso wa kwanza ukiwa raha. (vii) Kila mtu duniani huzongwa na huzuni / huhuzunika (viii) Raha humjia mwanadamu kwa nadra ilhali huzuni humuvamia wakati wowote. (ix) Wako watu wengi wasiowahi kuonja raha maishani mwao (Hoja 9-al-1 =9) (b) (i) Mtoto anapofiwa na wazazi (ii) Mtoto anayetupwa na mamake kijana baada ya kuzaliwa. (iii) Mtoto anayelelewa na mama wa kambo mwovu. (iv) Mtoto ambaye babake ni mlevi Hoja4-Al-1 —4 Soma makala haya kisha ujibu maswali yafuatayo HAKI ZA BINADAMU Binadamu wana mazoea ya kufikiria kuwa jinsi wafanyavyo, waongeavyo na wafikiriavyo kuhusu vitu ndivyo inavyopasa kuwa. Kama binandamu tunaamini njia yetu ndiyo sahihi, yenye mantiki na inayopasa kufuatwa na kila mtu. Msingi huu huu unakwenda kinyume na kutambua kila binadamu ana haki ya kufikiri, kusema au kuongea na kutenda mradi asikiuke haki ya mwenzake iliyo sawa na yake. Nguzo mojawapo inayogongomelea hoja hii ni Haki za Binadamu. Azimio kutangaza Haki Bia za Binadamu liliafikiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba 1948. Baraza kuu hilo liliyasisitizia mataifa wanachama umuhimu wa kuyasambaza, kuenezea, na kusisitiza kusambazwa kwa azimio hilo katika shule na taasisi za kielimu. Msingi wa uhuru, haki na amani ulimwenguni ni kutambua binadamu wote wana haki sawa. Ingawa kimsingi jamii na mataifa yote ya ulimwengu yanapaswa kuthamini, kusambaza na kuhimiza umuhimu wa Haki za Binadamu zipo jamii ambazo hukiuka haki hizo. Matokeo ya ukiukaji huu yana athari hasi sana kama ilivyotokea nchini Rwanda na Bosnia. Herzegovina kulikotokea mauaji ya halaiki. Azimio la Haki za Binadamu linajumuisha vipengele kadha ambavyo ni mihimili mikuu ya Azimio lenyewe. Kipengele msingi kabisa kinasisitiza kuwa kila kiumbe anazaliwa huru na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine. Ukweli wa kauli hii ulikokotezwa na kauli ya mwanafalsafa maarufu Jean Jacques Rosseau aliyesema kuwa kila kiumbe huzaliwa huru lakini huwa katika pingu ulimwengu mzima. Kauli hii ilitambua ukiukaji huu wa kipengele hiki. Kipengele cha pili kinasisitiza kuwa binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia, utajiri au chochote kile. Vipengele vingine vinatukumbusha kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi. Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa au unyonge wa kutumikishwa kwa namna yoyote ile. Suala hili linasisitizwa na kipengele cha sita kinachokataza kudhalilishwa kwa watu au kutunzwa kwa namna yoyote ambayo inamfedhehesha kama kiumbe. Azimio la Haki za Binadamu linasisitiza kuwa binadamu yoyote nyule ana haki ya kupata ulinzi wa kisheria. Binadamu huyo hapaswi kubaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa. Hata hivyo sio watu wote ulimwenguni ambao wanazifurahia haki hizi za kimsingi. Zipo lukuki za jamii ulimwenguni ambako haki za kimsingi zinakiukwa. Katika nchi ambazo zinaongozwa na watawala wa kiimla, si ajabu kuona haki za binadamu zikikiukwa. Viongozi wa aina hiyo huwa wamegeuzwa ng’ombe wa shemere na tamaa, ubinafsi na ukatili usiojua thamani ya utu. Viongozi wa aina hii wanasahau kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi maisha huru, asipotumikishwa wala kulanguliwa kama bidhaa. Nchi za kiimla aghalabu huongozwa na itikadi kuwa kiongozi ndiye pekee ambaye ana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Watu wengine wanapaswa kumfuata kisilka kama yule mbwa wa Pavlov ambaye alitokwa na mate kila kengele ilipopigwa. Viongozi wa ama hii hawachelei kuwatenza nguvu raia zao: Kuwadhalilisha kwa namna nyingi. Viongozi wa aina hiyo huiona sheria ya nchi kama iliyowekwa kwa watu wengine bali sio wao. Msimamo huu unakwenda kinyume na kipengele cha saba cha Haki Bia za Binadamu kisemacho kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria. Baadhi ya haki zinazokiukwa katika jamii za kimabavu ni haki ya watu kuungana, kuwaza, kushiriki katika maamuzi ya serikali, kuwa mwanachama wa jumuia waitakayo, kumiliki mali, kutembea, kuishi anakotaka kutohukumiwa bila ya kuwako na utaratibu wa kisheria. Ni muhimu hata hivyo kujua ni muhimu kwa raia wenyewe kujielimisha na kuzijua haki zao. Serikali inapaswa kuwa mlinzi wa sheria zenyewe. Lakini muhimu kujua pia kuwa mlinzi naye hulindwa pia. Maswalia) Kwa maneno kati ya 90 – 100 fafanua Haki Bia za Binadamu zilizoafikiwa na Baraza kuu la umoja wa Mataifa. (alama 10) Nakala Chafu __________________________________________________________________________ Nakala Safi __________________________________________________________________________ b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu. (Maneno 50 – 60). Nakala Chafu __________________________________________________________________________ Nakala Safi __________________________________________________________________________ Mwongozo
a) Kwa maneno kati ya 90- 100 fafanua Haki Bia za Binadamu Zilizoafikiwa na Baraza kuu la Umoja wa mataifa Kila kiumbe anazaliwa humu na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine’ • Binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia au chochote kile. • Kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi • Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa, kutumikishwa, kudhalilishwa au kutunzwa kwa namna inayomfedhehesha kama kiumbe. • Haki ya kupata ulinzi wa kisheria • Kutobaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa . Alama 8 utiririko alama 2) b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu • Tamaa ya uongozi • Ubinafsi • Ukatili, hawajui thamani ya utu • Kiburi cha kujiona kuwa wao ndio wanaofahamu mambo zaidi • Husahau kuwa binadamu ana haki ya kuishi maisha huru bila kutumikishwa au kutanguliwa kama bidhaa • Hudhani wao tu ndio wana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda na wananchi wanapaswa kufuata tu • Huona kuwa sheria ya nchi imewekewa wengine na wala sio wao hivyo huwatenza nguvu raia zao Alama 4, utiririko alama 1) UFUPISHOVipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwauwa maelfu ya watu na kuibua mifumo na taratibu za maisha ya watu. Hata hivyo , magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. Neno ‘UKIMWI’ lilitolewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha ukosefu wa kinga mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kicheka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile “umeme” na pia “ugonjwa wa vijana”. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wachanga wasioweza kujimudu. Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufikia mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini. Hivi sasa, inasemekana kuwa takribani watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imedhibitishwa kwamba takriban watu milioni mbili unusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuaambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo, makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao. Ugonjwa huu umeathiri jamii kwa njia nyingi. Hali ya maisha na woga, ukosefu wa matumaini, ongezeko la mayatima na kuzorota kwa uchumi kutokana na kutoweka kwa kizazi chenye nguvu za kutoa huduma kwa jamii, na baadhi ya athari za maradhi haya. Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia.Tuwe na matumaini kwamba siku moja, tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya, tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira hufuta heri. a) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo (maneno 90 - 100) (alama 3 kwa mtiririko) (alama 12 )
Nakala chafu/maadalizi ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Eleza mambo yanayoleta matumaini kwa wagonjwa wa ukimwi kulingana na aya tatu za mwisho (maneno 40- 45) (alama 1 kwa mtiririko) Nakala chafu ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Nakala Safi ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|