ATIKA SCHOOL
  • Start
    • SITEMAP
    • KNEC Portal
    • ZERAKI HELP AND SUPPORT
    • Academic Environment
    • KNEC KCSE PROJECT INSTRUCTIONS
  • BLOGS
    • About Us? >
      • Learn more about us
    • CUSTOMER CARE >
      • PRICING
      • Help & Support
    • News and Opinions
    • JOBS IN KENYA AND ABROAD FOR KENYANS AND BEYOND
    • How its Done
  • OUR PRODUCTS
    • All Categories >
      • MORE PRODUCTS >
        • SECONDARY CRE NOTES
        • COURSE BOOKS
        • KCSE KISWAHILI SETBOOKS
        • Backed Up Files and Archives
        • FREE DOCUMENTS
        • PRIMARY 8-4-4 BASED RESOURCES
        • STANDARD 8 RESOURCES
        • HIGH SCHOOL RESOURCES >
          • Biology Paper 3 Exams
          • Secondary Examinations
        • PRIMARY CBC BASED RESOURCES
        • COLLEGE & VARSITY RESOURCES
      • PRIMARY RESOURCES CBC
      • PRIMARY RESOURCES 8-4-4
      • SECONDARY RESOURCES
      • NOTES & TUTORIALS
      • COLLEGE RESOURCES
      • NOVELS and OTHER BOOKS
    • EXAMINATIONS >
      • MOCKS AND JOINT EXAMS >
        • FORM 1 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 2 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 3 EXAMINATIONS, QUESTION PAPERS AND ANSWERS
        • FORM 4 MOCKS PAST EXAMS BY REGION
        • TOP SECONDARY EXAMS ALL SUBJECTS
      • KPSEA NATIONAL EXAMS
      • KCPE >
        • KCPE PAST PAPERS AND ANSWERS >
          • KCPE 2020 RESULTS, REPORTS, QUESTIONS AND ANSWERS
          • KCPE PAST PAPERS 2019 REPORTS, RESULTS, QUESTIONS AND ANSWERS
        • KCPE PAST PAPERS PER SUBJECT
      • KCSE >
        • KCSE PAST PAPERS BY SUBJECT
        • KNEC KCSE PAST PAPERS, MARKING SCHEMES, QUESTIONS & ANSWERS
        • Free KCSE Past Papers Mathematics
        • Free KCSE Biology Questions and Answers
      • QUESTIONS & ANSWERS >
        • SECONDARY >
          • LANGUAGES >
            • Secondary English Questions and Answers
          • TECHNICALS >
            • COMPUTER STUDIES >
              • COMPUTER STUDIES Q & A
              • kcse computer studies paper 2 AND 3 Questions & Answers
            • BUSINESS STUDIES QUESTIONS & ANSWERS
            • KCSE AGRICULTURE TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE HOME SCIENCE DIRECT QUESTIONS AND ANSWERS
          • SCIENCES >
            • KCSE Mathematics Topical Questions
            • KCSE Biology Topical Questions and Answers
            • CHEMISTRY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE Physics Topical Questions
            • KCSE physics Practical Sample Quiz
          • HUMANITIES >
            • C.R.E (CRE) QUESTION AND ANSWERS
            • ISLAMIC RELIGIOUS EDUCATION (IRE) QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE History Topical Questions and Answers
            • GEOGRAPHY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
        • PRIMARY >
          • Standard 4-8 Mathematics Topical Questions from Mocks and KCPE
          • Std 6 Mathematics Notes
    • TUTORIALS >
      • SECONDARY >
        • SCIENCES >
          • FOCUS MATHEMATICS TUTORIALS AND EXAMS FREE
          • KCSE BIOLOGY NOTES
          • FREE KCSE CHEMISTRY NOTES
          • KCSE PHYSICS NOTES, AUDIOVISUALS AND MORE
        • LANGUAGES >
          • ENGLISH >
            • A GUIDE TO SILENT SONG AND OTHER STORIES
            • English KCSE Set Books
            • ENGLISH POETRY QUESTIONS WITH ANSWERS FOR K.C.S.E CANDIDATES
            • ENGLISH GRAMMAR #KCSE
          • KISWAHILI >
            • Bembea ya Maisha
            • CHOZI LA HERI - MWONGOZO
            • KIGOGO - MWONGOZO
            • MASWALI NA MAJIBU YA TUMBO LISILOSHIBA
            • USHAIRI MASWALI NA MAJIBU
            • KCSE Kiswahili Fasihi
        • TECHNICALS >
          • HOME SCIENCE NOTES
          • KCSE BUSINESS STUDIES NOTES
          • COMPUTER STUDIES NOTES LATEST
          • kcse Computer Studies Notes
          • KCSE AGRICULTURE NOTES, SYLLABUS, QUESTIONS, ANSWERS, SCHEMES OF WORK AND OTHERS
        • HUMANITIES >
          • KCSE History Notes Form 1 to 4
          • FREE KCSE CRE NOTES
          • KCSE GEOGRAPHY NOTES
          • IRE NOTES, AUDIOVISUAL, QUESTIONS AND ANSWERS
      • PRIMARY >
        • STANDARD 4: SOCIAL STUDIES
        • NOTES >
          • KISWAHILI
          • SOCIAL STUDIES
        • EXAMINATIONS
        • DecaTurbo Online Series Examinations
        • KCPE Mathematics Notes
        • KCPE and Primary Level Compositions
      • Other Supportive Documents >
        • SYLLABUS >
          • Primary 8-4-4 based Syllabus, Objectives and Lessons
          • Primary Mathematics Syllabus
        • MASOMO VIDEOS
    • CURRICULUM >
      • NEW CURRICULUM DESIGNS >
        • PRIMARY >
          • PRE PRIMARY ONE CURRICULUM WITH SYLLABUS
          • PRE PRIMARY TWO CURRICULUM WITH SYLLABUS
        • SECONDARY >
          • KNEC KCSE SYLLABUS AND COURSE OUTLINES
        • COLLEGE >
          • Regulations for the TIVET Craft and Diploma Business Examinations
    • HIGH INSTITUTIONS >
      • EXAMINATIONS >
        • College and Varsity Past Papers online
      • TUTORIALS >
        • COLLEGE AND UNIVERSITY NOTES AND TUTORIALS
  • MEMBERS RESOURCES
    • Primary >
      • CBC AND 8-4-4 LATEST EXAMS
      • CBC PROFFESSIONAL TOOLS
      • CBC NOTES PRIMARY
      • CBC KPSEA EXAMS
      • Standard 8 (std) English Topical Questions
      • KCPE MATHEMATICS TOPICAL QUESTIONS FROM 1989 TO LAST YEAR
      • STANDARD 8 PAST PAPERS 8-4-4 BASED
    • Secondary >
      • FORM 1 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 2 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 3 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 4 EXAMS WITH ANSWERS
      • KCSE 2020 QUESTIONS AND ANSWERS
      • NOTES SECONDARY
      • MOCKS SECONDARY >
        • kcse form 2 mathematics questions
    • Free Schemes of Work
    • FOCUS A365 SERIES K.C.P.E EXAMINATIONS FOR PRIMARY
    • ALL GROUPS PRODUCTS
    • PREMIUM PRODUCTS 2

​Soma makala yafwatayo kisha ujibu maswali yafwatayo MODEL25122022002

25/12/2022

0 Comments

 

​Soma makala yafwatayo kisha ujibu maswali yafwatayo

Hapo zamani za kale, paloindokea mtu mmoja kwa jina mzee Kata. Mzee Kata alikuwa na wake wawili. Mke wa kwanza aliitwa Neema na wa pili aliitwa Nduli. Kila mmoja wa wake hawa alikuwa na mtoto mmoja.  Neema alikuwa na mtoto wa kike kwa jina Majaliwa. Majaliwa alikuwa ameumbwa akaumbika.Uso wake ulihimili macho meupe mfano wa theluji. Meno yake ya juu yalipangika kwa njia ambayo iliyafanya kuacha mwanya ambao ulifanya tabasamu yake kuwa ya mvuto wa sumaki. Urembo wa Majaliwa, kama walivyosema wengi, ungemtoa nyoka yeyote pangoni.
Kwa upande mwingine Kutu, bintiye Nduli, alikuwa mwenye sura mbaya ya kutisha.Uso wake usiopendeza ulimfanya kuonekana kama ajuza wa miaka mia moja! Tabia yake ya ukorofi ilikoleza mvuto wake hasi. Vijana wa kijijini walimfanyia inadi kila mara kwa kumkumbusha kuwa hakufaa kuringa. “Sura kama kiboko”, wangemtania
Tofauti za kiumbo kati ya Majaliwa na Kutu zilizua uhasama mkubwa kati ya ndugu hawa, sikwambii mama zao. Hali hii ilizidishwa Zaidi na nongwa za kila siku zilizotokana na ukewenza. Familia yam zee Kata ikawa medaniya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hali ya mtafaruku iliendelea kuikosesha nyumba yam zee kata amani. Asubuhi moja, Mzee Kata aliamka kama kawaida yake, alijikohoza kama isharaya kutangaza kufika kwake. Daima hakupenda kuzungumza na wakeze asubuhi na mapema. Aliamini kuwa wangemletea nuksi. Kinyume na siku nyingine, mzee Kata hakuitikiwa. Ilibidi kujikaribisha nyumbani mwake. Mara tu alipovuka kizingiti cha kijumba hicho, alitupa macho yake juu yakitanda cha mayoweambapo mke wake alijinyosha twaa kakauka kama ukuni; hanapumzi. Weupe wa macho yake na mapovu yaliyomtoka kinywani yalimhakikishia Mzee Kata kuwa Neema kampungia mkono. Harufu kali ya sumu ilihanikiza hewa kumwarifu kuwa Mzee kata kuwa mkewe kafa kwa kutendwa na mkemwenza
Maisha ya Majaliwa yalichukua mkondo mpya baada ya tanzia hii. Mama wa kambo sasa alipata mwanya wa kumhini majaliwa. Kazi zote za nyumbani aliachiwa yeye.Huku Kutu akiachwa huru kucheza. Majaliwa alipewa chakula hapa; wengine wakila biriani yeye alipewa wali wa kawaida. Mavazi yake yaligeuka matambara.Siku zilivyozidi kusonga ndivyo mateso yalivyoongezeka. Mama wa kambo alizidisha wivu wake kwa majaliwa. Hata Majaliwa alipovunja ungo na wachumba kuja kumposa, mama wa kambo aliwafukuzia mbali. Wenine walihimizwa kumposa Kutu. Wachumba waliochachawa kutaka kumuoa majaliwa wakidai kuwa hawamtaki Kutu kwa sababu ya kiburi chake, walinyeshewa matusi, wakahizinika na kujiendea zao.
Siku moja alitokea kijana mmoja makini .alikuja amavalia gwanda jeusi lililojiinamia kwa uchovu. Viatu alivyovaa vilikuwa vimejichokea kwa kupiga lami. Kofia iliokuwa kichwani pake ilitosha kumhakikishia mama wa kambo kuwa huyu alikuwa fakiri. Mama mtu alikubali mara moja posa ya kijana huyu kwa Majaliwa akijua kuwa angeadhibika. Aliamini amemtokomeza Majaliwa ndani ya lindi la ulitima. Mzee Kata naye hakusita kumwoza Majaliwa kwa kiajana huyu maana aliiona hii kama fursa ya pekee ya kumwepusha vitimbi vya mama wa kambo Majaliwa aliandamana na mume wake hadi Kijiji cha peponi ambako kijana huyu allishi. Wallingia katika nyumba ya msonge ambamo Majaliwa alitarajia kuanza Maisha ya ndoa. Walitayarisha chajio, wakala na kulala.
​Asubuhi, Majaliwa aliamshwa na nyimbo za ndege. Alipofunguamacho, alijikuta kalala ndani mya chumba chenye sakafu ya vigae. Ukuta wa chumba hicho ulikuwa wa rangi wa zari. Mapambo ya dhahabu yalitundkwa ukutani. Kumbe kijana aliyemuoa hakuwa maskini kama ilivyodhaniwa! Alikuwa mwana wa mfalme! Na hili lilikuwa kasri hasa! Majaliwa hakueza kuamini! Alikuwa ameamkia Maisha ambayo hakuwahi yawazia.
Alipoingia sebuleni alimpata mama yake mpenzi, akiwa na tabasamu ya milele usoni. Walikumbatiana kwa shauku kuu. Kumbe kijana huyo alikuwa ametumwa na mamake Majaliwa! Mumewe majaliwa alishuhudia kwa umbali. Machozi ya mama mtu na mwanawe yakilovya vifua vyao na kuyeyusha simanzi na kuyeyusha simanzi iliyokuwa imeyaandama Maisha yao. Tangu siku hiyi, watu hawa wallishi kwa raha mstarehe. Hadithi yangu inaishia hapo.

MASWALI

a) Taja na utolee mifano mbinu sita za kimtindo  zilizotumiwa katika utungo huu (al.3)
b) Utungo huu unaweza kuainishwa kama ngamo, toa sababu (al.1)
c) Fafanua umuhimu nne wa formula ya kumalizia katika utungo huu (al. 4)
d) Taja shughuli moja ya kijamii katika jamii ya utungo huu (al. 1)
e) Jadili tatizo moja la ukewenza katika utungo huu (al.1)
f) Taja na ufafanue dhima tano ya utungo huu katika jamii yake (al.5)
g) Taja mambo mawili ambayo fanani anaweza kutekeleza ili kuufanya utungo huu uwe wa kuvutia Zaidi (al. 1)
h) Miviga ni nini? (al.1)
i) Taja hasara tatu za miviga (al.3)

MAJIBU

​​a) MBINU ZA KIMTINDO
i) Tashbihi -Sura kama kiboko
ii) msemo/nahau -Kumtoa nyoka pangoni
iii) Nidaa- Ajuza wa miaka mia moja
iv) Taswira mnuso- Harufu
v) Usimulizi- Hapo zamani za kale
vi) Istiara- Mavazi kugeuka matambara
vii) Majazi-Neema, Majaliwa, Nduli
viii) Tashhisi- harufu kumwarifu
                      ( 1/2x6= alama 3)
b) i) kuna formula ya ufunguzi- hapo zamani za kale
   ii) kuna formula ya kumalizia- Hadithi yangu inaishia hapo (1x1=alama 1)
c) UMUHIMU WA FOMULA YA KUMALIZIA
i) Kurudisha wasikizaji kwa hali ya kawaida
ii) Kubeba wazo au maudhui au ujumbe wa hadithi
iii) Onyesha mwisho wa hadithi
iv) Pahsa mtambali anayefuata. Pisha shughuli inayofuata
v) Kitulizo kwa hadhira baada ya  kumakinika kwa muda
vi) Kutoa changamotomkwa hadhira.
  (4x1=alama 4)
D SHUGHULI ZA KIJAMII
i) Ndoa- Wake wawili, Nduli kukosa kupashashwa, Majaliwa kuolewa
    1x1= alama 1
E MATATIZO YA UKEWENZA
i) Wivu- mamake majaliwa kupewa sumu
ii) Mateso kwa wana wa wake wenza- majaliwa kuteswa na mamake Nduli
  (1x1= alama 1)
F    DHIMA YA UTUNGO
i) Huelimisha
ii) Huburudisha
iii) Huadilisha
iv) Hukuza utamaduni
v) huleta utangamano
vi) Hukuza ubunifu
vii) Hukuza uwezo wa kukumbusha
viii) Hutoa onyo
ix) Ni kitambulisho cha jamii
x) Hukuza ujasiri
xi)Hukuza historia
(5x1=alama 5) mwanafunzi atoe maelezo Zaidi ndiposa apewe
G) MAMBO YA KUFANYA HADITHI KUVUTIA
i) Kutumia Ishara kama miondoko
ii) Kutumia ala za muziki
iii) kutumia maleba
iv) Kushirikisha hadhira
v) kuimba
vi) Kucheka 
(2x1/2=alama 1)
H) MIVIGA- sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi au wakati maalumu wa mwaka                   (1x1=alama 1)
I) HASARA ZA MIVIGA
ii) Zingine zimepitwa na wakati kama vile tohara ya wanawake. Huhatarisha Maisha ya waathiriwa
ii) Zingine hukinzana na malengo ya taifa kama vile ukeketaji wa Watoto wa kike
iii) Zingine hujaza watu hofu kama zile zinazotumia kafara ya binadamu
iv) zingine huleta uhasama kati ya koo hasa zile za kufukuza mapepo
v) Zingine ni ghali kwani huhitaji fedha nyingi na kusababisha umaskini
 (3x1=alama 3)

Read More
0 Comments

FAFANUA MAJUKUMU YOYOTE MANNE YA NYIMBO KATIKA JAMII.   (AL 8)

24/12/2022

0 Comments

 

​b) Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii.   (Al 8) 

Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)
  1. ni hifadhi za matukio muhimu ya kihistoria katika jamii
  2. hutumiwa kama nyenzo ya kupitisha utamaduni 
  3. hutumiwa kama burudani 
  4. huakisi umbuji wa tamaduni mbalimbali
  5. huhamasisha watu kutenda mambo mbalimbali 
  6. huelimisha na kupitisha maarifa mbalimbali miongoni mwa wanajamii
  7. ni kiakisi cha fahari walio nayo wanaohusika katika utamaduni wao. Aina na maana za nyimbo

Read More
0 Comments

Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike

24/12/2022

0 Comments

 

​Tumia kifungu kifuatacho kujibu maswali yanayofuata 

a) Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike.

​I) Bainisha kipera kinachorejelewa  (Al 1).

Kitendawili 

​II) Andika shughuli moja ya Kijamii na moja ya Kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utingo huu.   (Al 2)

  • Kijamii – ndoa (kulichuma/ ndugu wa kiume asimuoe nguye wa kike).
  • Kiuchumi – kilimo – paipai lilioiva

​III) Eleza dhima nne za kipera kinachorejelewa katika jamii yako.   (Al 4) 

Umuhimu
  • Kuburudisha jioni baada ya kazi 
  • Kukuza ubunifu wa kuvitunga kwa kulinganisha vitu katika mazingira ili kuviunda.
  • Kuimarisha uwezo wa kukumbuka.
  • Kukuza uwezo wa kufikiri kwani mfumbiwa huhitaji kufikiri sana ili kupata jibu. 
  • Kuleta umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati vinategwa. 
  • Kuimarisha ujuzi wa kujieleza kwa lugha.
  • Kupanua ujuzi wa mazingira wa mtoto. 
  • Kuendeleza utamaduni wa jamii kama Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – Ndugu wa Kiume asimuoe nduguye wa kike. 
  • Kukejeli au kudharau tabia mbaya kama wazungu wawili wanachungulia dirishani – Makamasi

​IV) Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia katika uwasilishaji wako.  (Al 5)

  1. Kutumia fomyula/muundo maalum. Mifano
    Mtegaji : Kitendawili
    Mteguaji : Tega 
  2. Kutumia ukakamavu wa kuweza kuzungumza hadharani.
  3. Kuwa na uelewa wa mazingira na masuala ibuka katika jamii ili kuweza kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake. 
  4. Ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha kwa wepesi. 
  5. Kuwa mchangamfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai.
  6. Ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na Imani za hadhira.
  7. Kushirikisha hadhira kama vile kuimba, maswali ya balagha ili isikinai.
  8. Kudramatisha ili kuonyesha picha Fulani kama vile kuiga toni, sauti, na kiimbo kulingana na swala analowasilisha. 
  9. Kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kulingana na hali anayoigiza. 
  10. Ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia. 
  11. Kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti unazoigiza kama huzuni. 
  12. Ufaraguzi/kubadilisha uwasilishaji papo hapo kutegemea hadhira na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira. 

Read More
0 Comments

Eleza umuhimu wa ukusanyaji na uhifadhi wa data za fasihi simulizi.  (alama 5)

21/12/2022

0 Comments

 

​Eleza umuhimu wa ukusanyaji na uhifadhi wa data za fasihi simulizi.  (alama 5)

  • Fasihi  simulizi ni hifadhi ya mitazamo ya kitamaduni ya jamii.
  • Ukusanyaji humpa  mwanafunzi wa fasihi simulizi  kushuhudia  na kuathiriwa moja kwa moja  na utendaji wa fasihi simulizi.
  • Husaidia kurekodi na kuhifadhi tamaduni za jamii mbali mbali kwa nia ya kuvipitisha kwa kizazi kijazo.
  • Ukusanyaji huiendeleza  fasihi simulizi,.
  • Husaidia kuziba pengo la utafiti lililopo.
  • Hutumiwa kama kiunzi(msingi) cha uchunguzi wa kulinganishi  wa fasihi simulizi za jamii mbalimbali.
  • Ni muhimu kukusanya data ili kueleza kwa nini, utungo mmoja huwasilishwa kwa njia tofauti na mwingine.
  • Utafiti wa fasihi simulizi humwezeza mwanafunzi kuwa na  ujuzi wa kufanya utafiti katika taaluma nyingine.
  • Utafiti wowote ule husaidia kurekebisha mawazo potovu kuhusu suala  fulani.
  • Umewawezesha  wasomi wengi kutambua  kuwa  tungo nyingi zilizoandikwa zilitokana na fasihi simulizzi.
5x1

Read More
0 Comments

Fafanua matatizo yanayomkabili mkusanyaji wa fasihi simulizi nyanjani. (alama  10)

21/12/2022

0 Comments

 

​Fafanua matatizo yanayomkabili mkusanyaji wa fasihi simulizi nyanjani. (alama  10)

  1. Gharama ya utafiti.
  2. Mtazamo hasi wa wajamii kuhusu ujazaji wa hojaji huenda ukafanya wengi wao kutojaza hojaji hizo.
  3. Wanajamii wengine  huweza kushuku kwamba mtafiti anawapeleleza na wakakataa kutoa habari.
  4. Baadhi ya\ mafanani au wahojiwa huenda wakadai walipwe kabla ya kutoa habari zozote.
  5. Mbinu nyingine za utafiti kama vile  hojaji huhitaji watu ambao wajua kusoma na  kuandika .
  6. Vizingiti vya kidini.
  7. Kupotea au kufisidiwa kwa vifaa  vya kuhifadhi.
  8. Vikwazo kutokana kwa watawala.
  9. Wadhamini  mara nyingi ndio huamua mambo yanayochunguzwa, mahali  pa kuchunguziwa  na mawanda au upeo  wa uchunguzi  wenyewe.
  10. Mtafiti huenda asiwe na wakati  wa kutosha  kuwahoji watu wengi.
  11. Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi.
  12. Matatizo ya kibinafsi . Anayekusanya fasihi simulizi anaweza kushindwa kuidhibiti hadhira.
  13. Ukosefu wa usalama.
  14. Tafsiri ya data .
10x1=10

Read More
0 Comments

Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi.   (alama 5)

21/12/2022

0 Comments

 

​Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi.   (alama 5)

Jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi      
  1. Tamasha za muziki.
  2. Sherehe za arusi  jando, na matambiko/ mifano ya miviga  bado zipo.
  3. Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia redio na runinga.
  4. Mchezo ya kuigiza katika runinga, redio.
  5. Tamasha za drama huendeleza utanzu wa maigizo, mazungumzo na ushairi simulizi.
  6. Sarakasi  zinazofanywa na wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho na kukipokeza.
  7. Ngoma za kienyenji kama Isukuti zinazochezwa katika halfa za kisiasa na harusi.
  8. Watafiti, ingawa wachache,  wanaotafiti na kuandika , kurekodi vipera vya fasihi simulizi.
  9. Utambaji wa hadithi bado hufanyika katika baadhi ya jamii, hasa katika sehemu za mashambani.
   5x1=5

Read More
0 Comments

​Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)

17/12/2022

0 Comments

 

​Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)

  1. Hutolewa kwa watu waliotenda kinyume na matarajio ya jamii zao.
  2. Baadhi yalitolewa kabla ya ulaji wa viapo.
  3. Yanaweza kutolewa moja kwa moja na aliyeathirika.
  4. Huaminiwa yanaleta maangamizi kwa jamii, hivyo wanajamii hushauriwa kuyaepuka kwa kutenda mema.
  5. Hutumia lugha fasaha na mtoaji kwa kawaida huwa mlumbi.
  6. Hutumia lugha kali ya kuonya  na kujaza woga ili watu waache maovu.

Read More
0 Comments

​Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)

17/12/2022

0 Comments

 

​Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)

Matambiko
Sadaka au ada inayotolewa kwa Mungu, mizimu, pepo au miungu ili wasaidie binadamu kutatua mambo magumu, kuomba radhi au kutoa shukrani. Matatizo ni kama vile ukame, magonjwa, kukosa watoto, mafuriko au janga lolote lililomshinda binadamu nguvu na uwezo.
Pembezi
Tungo za sifa za watu wa aina fulani wanaosifika kwa matendo yao au nafasi walizo nazo katika jamii kv matendo ya kishujaa au kujitolea kwao. Km viongozi, walezi wazuri, waganga, nk
Misimu 
Semi zinazozuka na kutumiwa na kundi fulani la wanajamii kama misemo ya mawasiliano baina ya wanakikundi hicho./  Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka tu kutegemea mazingira maalum./ Ni semi ndogo ndogo za kupita. Huzuka katika mazingira fulani  na hufa baada ya kutokuwepo kwa mazingira yale.

Read More
0 Comments

Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)

17/12/2022

0 Comments

 

Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)

Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)
  • Maandalizi_ mada ya utafiti, mawanda ya utafiti, walengwa, kipindi cha utafiti, kibali, mbinu za kukusanya na kuhifadhi na gharama ya utafiti.
  • Utafiti na ukusanyaji wa data yenyewe. Kuhusisha mbinu mbalimbali kama vile kuhoji, hojaji, kushuhudia au kujaza fomu.
  • Kurekodi data kwa kuandika- kunasa habari ama kupiga picha za kawaida ama video au zote tatu.
  • Kuchunguza data – ili kutafsiri na kuandika upya neno kwa neno bila kupotosha maana halisi ya lugha asili.
  • Kuchambua/ kuchanganua na kufasiri data ili kupata matokeo kamili ya utafiti na mapendekezo. 

Read More
0 Comments

Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)

17/12/2022

0 Comments

 

Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)

Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)
  • Zingine hazina faida yoyote
  • Zingine zaweza kusifu tamaduni zinazodhalilisha watu fulani
  • Zaweza kuleta utengano kati ya majirani hasa zile zinahifadhi siri
  • Zaweza kuleta matabaka
  • Zingine huenda kinyume na mabadiliko ya wakati. Baadhi ya matendo wakati wa matanga na unyago yamepitwa na wakati.
  • Huweza kusababisha tofauti ya kijinsia kv jando na ndoa kwani humdhalilisha mwanamke na kumtukuza zaidi mwanamume.
  • Ina gharama – mavazi, chakula, zawadi,nk
  • Baadhi hujaza hofu.

Read More
0 Comments

JADILI SIFA ZOZOTE NNE ZA MTAMBAJI BORA. (ALAMA 4)

17/12/2022

0 Comments

 

Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)

Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)
  • mbunifu – awe na uwezo wa kuwasilisha hadithi kwa namna ya kuwachangamsha. Abuni hadithi upya mara tu anapoitamba.
  • Afahamu lugha- Awe na ufahamu mpana wa lugha husika na utamaduni unaohusika ili awasilishe vyema ngano yake.
  • Afahamu hadhira yake na mahitaji yao- wake , waume, watoto, vijana, nk . apatane vyema na mazingira yake ya kisimulizi.
  • Mcheshi- ili kuinasa makini ya hadhira yake.
  • uwezo wa ufaraguzi na afahamu mbinu zifaazo za sanaa na maonyesho – uwezo wa kuunda, kugeuza na kuwasilisha kazi ya fasihi simulizi papo hapo.
  • Afahamu tabia za binadamu- mambo yanayofurahisha, kuudhi, kuchangamsha, kuvutia au kumpendeza. Pia wafahamu mikondo mbalimbali ya jamii.
  • Sauti yake isikike na ibadilike ipasavyo.
  • Ashirikishe hadhira yake-  anaweza kuwauliza maswali,  waimbe nyimbo nk
  • Jasiri – aweze kuzungumza hadharani bila haya hasa masuala ya aibu.
  • Afahamu utamaduni wa hadhira yake ili atoe ujumbe kwa njia inayokubalika na hadhira na asije akatumia ishara au maneno yasiyokubalika pale.

Read More
0 Comments

ELEZA TOFAUTI KATI YA VITENDAWILI NA METHALI.

15/12/2022

0 Comments

 

Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali.  (Alama 5)

Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali.  (Alama 5)
  • Vitendawili huwa na fomyula ya uwasilishaji ilhali methali haina fomyula mahususi.
  • Vitendawili huwa na fumbo ambalo lazima lifumbuliwe hapo hapo na hadhira ilhali methali fumbo halifumbuliwi papo hapo na huwasilishwa na mwenye kutumia methali.
  • Vitendawili ni maarufu kwa vijana ilhali methali huwa maarufu miongoni mwa wazee na watu wazima.
  • Vitendawili hutolewa kwenye kikao maalum ilhali methali si lazima zitengewe vikao maalum.
  • Vitendawili huwa na hadhira tendi ilhali methali huwa huwa na hadhira tuli.
  • Vitendawili huwasilishwa kwa majibizano ilhali methali huwasilishwa kwa kauli moja tu na msemaji.
(5x1)

Read More
0 Comments

Jadili mifano mitano ya ngomezi za kisasa.

15/12/2022

0 Comments

 

Jadili mifano mitano ya ngomezi za kisasa   (alama 5)

Jadili mifano mitano ya ngomeziza kisasa.     (alama 5)
  • Milio ya ambulensi
  • Toni katika rununu
  • Kengele shuleni
  • Toni katika saa
  • Kengele za milangoni                                                     
(5x1)

Read More
0 Comments

​ELEZA MAANA YA; VITANZA NDIMI TARIHI VIVUGO MATAMBIKO MAAPIZO

15/12/2022

0 Comments

 

​Eleza maana ya;     (alama 5)
i. Vitanza ndimi
ii. Tarihi
iii. Vivugo
iv. Matambiko
v. Maapizo

Eleza maana ya;      (alama 5)
i. vitanza ndimi- ni kauli au sentensi zenye maneno ambayo yana mfuatano wa sauti zinazotatanisha kimatamshi.
ii. Tarihi- ni rekodi za matukio ya kihistoria ambayo hupangwa yakifuatana kiwakati na huwasilishwa kwa njia ya masimulizi bila ya kutolewa ufafanuzi.
iii. Vivugo- ni maigizo ya kujigamba ambayo yanaweza kuambatanishwa na ngoma na maleba.
iv. Matambiko- ni sadaka au  ada inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu, miungu, pepo au mizimu
v. Maapizo- ni maombi maalum ya kumtaka Mwenyezi Mungu , miungu au mizimu ili kumwadhibu mhusika hasidi, mkinzani au mwovu.       (5x1)

Read More
0 Comments

Fafanua sifa za nyimbo za watoto.  (alama 5)

15/12/2022

1 Comment

 

FAFANUA SIFA ZA NYIMBO ZA WATOTO.  (ALAMA 5)

a)  Fafanua sifa za nyimbo za watoto.  (alama 5)
  1. Hujaa urudiaji
  2. Huashiria kazi za jamii husika
  3. Hutumia kiimbo cha juu
  4. Huimbwa kwa toni ya furaha
  5. Huambatanishwa na uchezaji wa viungo vya mwili.
  6. Huhimiza tabia chanya
  7. Hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.

Read More
1 Comment

Fafanua mchakato/fomula ya uwasilishaji wa vitendawili.

15/12/2022

0 Comments

 

​a) Fafanua mchakato/fomula ya uwasilishaji wa vitendawili. (alama4)

a) Fafanua mchakato wa uwasilishaji wa vitendawili. (al.4)
  1. Kitangulizi- Mtegaji: kitendawili
    Mteguaji: tega
  2. Swali lenyewe- kitendawili kutegwa
  3. Majibu kutolewa
  4. Mtegaji asipooridhika huomba kupewa zawadi kisha hutoa jibu.

​b) Linganisha naulinganue vitendawili na methali. (alama10)

​b) Linganisha na ulinganue vitendawili na methali. (al.10)
Mfanano
  1. Zote ni tungo fupi za semi
  2. Zote huwa na maana fiche
  3. Zote hutumia lugha inayojenga taswira
  4. Zote huwa na miundo maalum ya lugha
  5. Zote  hupata maana kulingana na jamii
Tofauti
  1. Vitendawili vina fomyula ilhali methali hazina fomyula
  2. Fumbo la kitendawili hufumbuliwa papo hapo fumbo si lazima kufumbuliwa papo katika methali.
  3. Vitendawili hutumiwa na watoto sana, methali hutumiwa kuonyesha hekima miongoni mwa watu  wazima  na wazee
  4. Vitendawili hutolewa katika vikao maalum, methali si lazima kutengewa vikao maalum.
  5. Vitendawili hutumia lugha ya majibizano , methali aghalabu huwa kauli moja ya msemaji.
  6. Hadhira tendi huwa katika vitendawili , katika methali hadhira si lazima  iwe tendi.

​c) Toa sababu sita za kudidimia kwa fasihi simulizi. (alama6)

C) Uhamaji wa watu huwafanya kuacha utamaduni wao.
  • watu kuwa na mtazamo hasi kuhusu fasihi simulizi 
  • ubidhaaishaji wa fasihi simulizi- kuandika kitabu kama vile cha methali na kubadilisha umiliki 
  • watu kupendelea kusoma
  • mwingiliano wa watu huwafanya kusahau fasihi yao
  • teknolojia yasasa ambayo fasihi simulizi huhifadhiwa badala yaakilini.
  • Utamaduni wa fasihi simulizi umebadilika – babu na bibi hawawatambii watoto hadithi.   Mwalimu akadirie

Read More
0 Comments

FASIHI SIMULIZI - Soma utungo huu na kujibu maswali yanayofuata model14122022002

14/12/2022

0 Comments

 

FASIHI SIMULIZI - Soma utungo huu na kujibu maswali yanayofuata MODEL14122022002

​Zamani sana katika kijiji cha Tima paliondokea sonara mmoja.  Sonara huyu alikuwa na mke mrembo ambaye alihusudiwa na walimwengu wote katika eneo hilo.  Karibu na kibanda chao palikuwa na msitu ambao ulisetiri mazimwi ya kila aina.  Kila jioni ungeyasikia mazimwi hayo yaking’ang’ania mawindo.  Sonara na mkewe hawakwisha kushangaa jinsi viumbe hawa walivyokithiri kwa tamaa.
Siku moja sonara aliondoka kijijini kwenda mbali kwa shughuli za ufuaji.  Alimwacha mkewe akiwa mjamzito.  Mara tu baada ya kuondoka, uchungu wa uzazi ulibisha hodi.  Mama mtu akawa taabani, asiwe na mwombezi.  Katika hali hii ya hamaniko, mama mtu alishutukia kapata mkunga aliyeonekana mzuri na mpole ajabu.  Mama akajawa na furaha tele.  Bahati iliyoje!
Mkunga akaingia kazini.  Baada ya dakika chache, malaika, kitoto kichanga kikahanikiza hewa ya asubuhi mbichi kwa kilio.  Mama mtu alishukuru mkunga kwa usamaria wema.  Laiti angalijua kuwa kajipagaza zigo lisilobebeka!

Mkunga huyu hakukawia.  Akaingia ghalani akachukuwa mtama. Akasaga na kumpikia mwanagenzi fuka.  Mzazi, hamu ya kula hajapata bado, mkunga akamkabidhi bakuli la uji.  “Shika mke mzazi”, akasema.  Hata kabla ya mama kutoa kauli, mkunga akabadilika ghafla.  Ile sauti ya upole ikabadilika kuwa mngurumo wa kutisha: “UKIKATAA, MIMI NAENDA KUUNYWA!”.  Kumbe yule mkunga alikuwa zimwi lililobugia uji pamoja na bakuli!  Mama alipoona hayo, vimbimbi vikamsimama kwa woga.
Kufikia jioni, njaa ilikuwa imemuuma mama na mtoto si haba.  Yule mkunga zimwi akajigeuza binadamu na kumchinja mbuzi ili ampikie mama mzazi.  Baada ya supu kuiva zimwi likaibeba pamoja na minofu na kumpelekea mama mzazi.  Lakini hata kabla ya kutua sufuria, lilikariri maneno yale yale: “UKIKATAA NAENDA KUNYWA”.  Kwa kauli hiyo, likabugia nyama pamoja na sufuria.  Mbuzi mzima akapata makao ndani ya tumbo la zimwi!  Mama na mtoto wake wakalala mataya yakigongana.  Siku tatu zilipita bila ya mama kupewa chakula chochote.  Unyonge wa uzazi ukamvamia, kitoto nacho kikaendelea kudai haki.

Asubuhi moja Kasuku alipatia akitarajia kiamsha kinywa kama kawaida.  Akampata mke wa sahibu yake taabani.  Baada ya mazungumzo mafupi na mama mtu, waliafikiana kuwa ampelekee sonara ujumbe.
“Kasuku alienda akatua juu ya mti uliokuwa karibu na kiwanda cha sonara.  Akaimba:
  
Ewe sonara unayefua
Mke kajifungua
Unyonge wa uzazi wamaliza
Tumbo la uzazi latekenya
Chango zamsokota
 Kisa na maana
Chakula hapati
Mpishi hupikia tumbole
Zimwi huchumia chunguche
Kikawia hasara takufikia
Ya kinda na mamaye
Sonara alisikiliza wimbo huu kwa muda na ujumbe wake ukamgonga ndipo.  Akajihami na kufunga safari kurejea nyumbani.  Alipofika, alimpata mkewe taabani, mwili umenyong’onyea.  Magala yote yalikuwa yamefagiwa na zimwi lililokuwa limejidai kuwa mfadhili na lililala nje ya ghala kwa mavuno ya shibe.  Sonara alilidunga mkuki likafa papo hapo.  Ingawa sonara alijuta kwa kutowazia hali ya mke wake tangu awali aliweza kuliangamiza zimwi.  Hadithi yangu inaiishia hapo. ​

Maswali

(a) (i)   Tambulisha aina ya utanzu huu.    (alama 1)
        Hadithi/masimulizi  (1x1=1)
(ii)  Taja tanzu zingine zinazoingiliana katika kifungu ulichosoma huku ukitolea mifano.       (alama 2)
● nyimbo
● semi
● mazungumzo     (3x1=3)
(b) “Hadithi yangu inaishia hapo”
Eleza umuhimu wa kifungu hiki katika uwasilishaji wa utungo huu.     (alama 4)
Fomyula ya kufunga;
i) Huashiria mwisho wa ngano
ii) Hutangaza funzo kwa wasikilizaji
iii) Kuwapa changamoto ya kuwa watambaji mashuhuri wa ngano.
iv) Humpisha mtambaji anayefuata
v) Kuitoa hadhira ulimwengu wa hadithi (Sanaa) na kuwarudisha katika ulimwengu halisi.
vi) Hupisha shughuli inayofuata
vii) Ni kitulizo kwa hadhira ambayo sasa huacha kuwa makini.  (5 x 1) = 5
(c) Jadili mafunzo yanajitokeza katika usimulizi huu.   (alama 2)
i) Tuwe na mipango madhubuti maishani / tuyape mambo muhimu nafasi ya kwanza. Sonara alimwacha mkewe akiwa karibu kujifungua. (Hakuwajibika). Anajipata akiteseka sonara akiwa mbali naye.
ii) Tutende wema daima. Jitu linauliwa na Sonara kutokana na ukatili walo. (1 x 2 = 2)
(d) Eleza namna ambavyo hadhira inaweza kushirikisha katika usimulizi huu.  (alama 4)
- Kuimba
- Kupiga makofi
- Kuuliza maswali
- Kuigiza
- Kuitikia na kuhimiza 
- Kutoa mifano
- Hisia/ishara za usoni ili mwasilishaji abadilishe uwasilishaji
- Kutoa majibu
- Kutoa mifano ya baadhi ya wahusika katika jamii zao endapo wataulizwa.
- Kuchukua nafasi na kuitamba upya hadithi. (4x1=4)
(e) Kwa kutolea mifano orodhesha tamathali za usemi zilizotumika.    (alama 4)
● Takriri  -   Ukikataa mimi naenda kunywa
● Kupiga chuku/ongezea chumvi   -  mbuzi mzima akapata makao ndani ya tumbo la zimwi.
● Tashihisi  -  unyonge wa mzazi ukamvamia.
● Jazanda  -  kinda kwa maana ya mtoto. 
● Semi  -  chango zamsokota
● Nahau  - funga safari
[Tathmini jibu la mwanafunzi  4x1=4]
(f) Jadili aina za taswira zilizotumika na mtunzi.   (alama 3)
Taswira sikivu
- ungeyasikia mazimwi hayo yaking’ang’ania chakula
- sauti,  “ukikataa mimi naenda kunywa”
Taswira oni
- alikuwa mke mrembo
Taswira mwendo
- akaingia ghalani
- asonara ujumbe
- akajihami na kufunga safari
Taswira hisi
- akapata makao ndani ya tumbo la zimwi
- ujumbe ukamgonga ndipo
- mama akajawa na furaha tele
- hakwisha kushangaa
- uchungu wa uzazi ulibisha  hodi   (3x1=3)

Read More
0 Comments

FASIHI SIMULIZI -soma utungoufuataokishaujibumaswali MODEL14122022001

14/12/2022

0 Comments

 

​FASIHI SIMULIZI - soma utungoufuataokishaujibumaswali model14122022001

​Hapo zamani za kale paliishi mtoto katika kisima kimoja. Siku moja mtoto huyu aliokota kijiwe karibu na soko kuu. Kijiwe kilikuwa kikimeremeta kwa rangi mbalimbali na kilizingirwa na pete ya dhahabu. Mtoto huyu na wenzake walianza kurushiana kijiwe hicho. Baada ya muda kilianza kuongezeka umbo na kuonekana kama kiwiliwili cha binadamu.  Kikaanza kuwakimbiza wale watoto. Kutokana na ukulele wao watu walikuja kutazama nini kilikuwa cha mno. Walipofika walikutana ana kwa ana na dubwana hilo.  Lilizidi kuongezeka umbo na likawameza wote pamoja na mifugo wao. Wachache waliojaribu kukimbia liliwashika kwa mikono yake mipana na mirefu.  Kwa bahati njema alikuwepo mama mmoja aliyeona haya yote.  Alikuwa mbali na hapo. Aliteremka kutoka kilele cha  mlima na kuwapata wakuli mamakondeni na sawia akawajuza kuhusu kitendo kilichomwogofya sana.  Wote wakaacha shughuli zao na wakatwaa silaha zao wakaelekea soko kuu.
​Dude sasa lilikuwa limejilaza baada ya shibe, wakulima wale walichagua watu sita ambao walijulikana kwa ushujaa wao.  Pamoja walilinyemelea lile nyangarika na kulikata mara moja.  Lilitoa mkoromo mkuu kabla halijakata kamba. Punde, wanakijiji kwa uangalifu mkubwa walitoboa tumbo lake wakitarajia kupata maiti za wapenzi wao pamoja na mifugo wao.  Wote walijawa na furaha kuu walipoona wapenzi wao wakijichomoza kutoka tumboni, mmoja baada ya mwingine hadi akatoka Yule wa mwisho.  Mbuzi, kondoo na ng’ombe wote walitoka mmoja mmoja.
Siku hiyo kuliandaliwa sherehe ya kumshukuru Muumba kwa wema wake.  Watoto walishauriwa wasithubutu kuchezea vitu wasivyovijua.

​MASWALI.

a) Ainisha kipera hiki cha fasihi simulizi.    (alama.1)
b) Fafanua mambo matatu yanayodhihirisha kuwa kipera hiki ni sanaa.  (alama.3)
c) Mwasilishaji wa kipera hiki anafaa kuwa na sifa gani?  Eleza.   (alama.4)
d) Onyesha mifano miwili ya fantasia katika hadithi hii.   (alama.2)
e) Eleza majukumu matatu ya tungo hizi kwa wanajamii. (alama.3)
f) Eleza majukumu manne ya mtindo uliotumiwa kuanzisha hadithi hii.  (alama.4)
g) Fafanua aina tatu za taswira zinazojitokeza katika utungo huu. (alama.3)

​MWONGOZO WA FASIHI SIMULIZI

a) Nganoyamazimwi – kunamatumizimengiya fantasia.  Kijiwekuongezeka umbo.  (1x1=1)
b)i Kina umbo maalum, kwamfano kina mwanzo.  Hapozamaniza kale….
ii) Mandahri/mazingirayamesawiriwakwaufundimkubwa.
iii) Wahusikawamejengwakwaufundimkubwailikusawiritabiazawahusikakatikajamii.
iv) Lughaimetumikakwaufundi.  Kwamfanolughayakitamathali.  Kuna tashhisi,Uhuishi, takririn.k (3x3=3)

c)i) Awe mbunifuiliabunihadithiupya
ii) Ajuehadhirayakenamahitajiyakepamojanakiwango cha elimu.
iii) Kuilewanakumudulughayahadhirayake.
iv) Kuwajasiriiliasimamembeleyahadhirayake.
v) Kuwamcheshiilihadhiraichangamke.
vi) Kuwanauwezowakushirikishahadhirayakekwanjiambalimbali.
viii) Awe naujuzinaufasahawalughailikuwasilishamawazokwanjiamwafaka.  (4x4=4)
d)i) Zimwikuwezakumezaumatiwawatupamojanamifugo.
ii) Watunamifugokutokatumbonimwazimwiwakiwahai.
iii) Kijiwekuongezeka umbo nakuonekanakamakiwiliwili cha binadamu.  (2x1=2)
e)i) Kukashifutabiayauovu, ulafinaukatili
ii) Kutahadharishadhidiyakuwanaulafi, ukatilin.k.
iii) Kutiamoyowaliodhulumiwakuwawaliowanyanyasawataadhibiwasikumoja.  (3x1=2)
f)i) Kuvutamakiniyahadhira.
ii) Kumtambulishamtambajikwahadhira
iii) Kuashiriamwanzowahadithi.
iv) Kutoahadhirakutokaulimwenguhalisihadiulewahadithi
v) Kushirikishahadhiranamtambaji.  (4x1=4)

g) Taswiramwendo
✔ kikaanzakuwakimbiza wale watoto.
✔ aliteremkakutokakilele cha mlima.
✔ wakaelekeasokokuu.

Taswirahisi
✔ Kitendokilichomwogofyasana.
✔ Lilitoamkoromomkuu
✔ wotewalijawanafurahakuu.
Taswiramguso
✔ Na kulikatamaramoja
✔ …uangalifumkubwawalitoboatumbo.  (3x1=3
0 Comments
    fasihi simulizi

    Categories

    All
    CHOZI LA HERI
    DAMU NYEUSI
    FASIHI SIMULIZI
    FORM 4
    KIDAGAA KIMEMWOZEA
    Swali Na Jibu
    TUMBO LISILOSHIBA

    Archives

    January 2023
    December 2022
    June 2021
    January 2020
    August 2018
    April 2018

    RSS Feed



Primary Resources
  • K.C.P.E Past Papers
  • ​Pri - Primary 1 Level
  • Pri  - Primary 2 Level
  • Grade 1
  • Grade 2
  • Grade 3
  • Grade 4
  • Standard 5
  • Standard 6
  • Standard 7
  • Standard 8
  • English
  • Kiswahili
  • Social Studies
  • Science
  • Mathematics
  • Kenya Sign Language
  • I.R.E
  • ​H.R.E
  • Notes
  • Termly Questions
  • Mocks
  • K.C.P.E Past Papers
College Resources
  • E.C.D.E
  • P.T.E
  • D.T.E
  • Technical Diploma
  • Technical Certificate
  • Business Diploma
  • Business Certificate
  • Higher Diploma
  • K.A.S.N.E.B Resources
  • K.M.T.C Resources
  • Varsity Resources
Secondary Resources
  • K.C.S.E Past Papers
  • Form 1
  • Form 2
  • Form 3
  • Form 4
  • Term 1
  • Term 2
  • Term 3
  • English
  • Geography
  • History
  • C.R.E
  • I.R.E
  • ​H.R.E
  • Home Science
  • Computer Studies
  • Business Studies
  • Agriculture
  • Chemistry
  • Biology
  • Physics
  • Mathematics ALT A
  • Mathematics ALT B
  • Kiswahili
  • French
  • Germany
  • Arabic
  • Aviation
  • Art & Design
  • Drawing & Design
  • Building & Construction
  • Metal Works
  • Wood Work
  • Music
  • Kenya Sign Language
  • Electricity
Other Useful Links
  • Academic Environment
  • How its Done
  • News and Opinions
  • Manyam Franchise Support
  • About
  • SITEMAP
  • FOCUS A365 SERIES
  • Membership Details (KCPE/KCSE)
  • Secondary Mocks
  • SYLLABUS
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii
Tel: 0728 450 424
Tel: 0738 619 279
Tel: 0763 450 425
E-mail - sales@manyamfranchise.com
  • Start
    • SITEMAP
    • KNEC Portal
    • ZERAKI HELP AND SUPPORT
    • Academic Environment
    • KNEC KCSE PROJECT INSTRUCTIONS
  • BLOGS
    • About Us? >
      • Learn more about us
    • CUSTOMER CARE >
      • PRICING
      • Help & Support
    • News and Opinions
    • JOBS IN KENYA AND ABROAD FOR KENYANS AND BEYOND
    • How its Done
  • OUR PRODUCTS
    • All Categories >
      • MORE PRODUCTS >
        • SECONDARY CRE NOTES
        • COURSE BOOKS
        • KCSE KISWAHILI SETBOOKS
        • Backed Up Files and Archives
        • FREE DOCUMENTS
        • PRIMARY 8-4-4 BASED RESOURCES
        • STANDARD 8 RESOURCES
        • HIGH SCHOOL RESOURCES >
          • Biology Paper 3 Exams
          • Secondary Examinations
        • PRIMARY CBC BASED RESOURCES
        • COLLEGE & VARSITY RESOURCES
      • PRIMARY RESOURCES CBC
      • PRIMARY RESOURCES 8-4-4
      • SECONDARY RESOURCES
      • NOTES & TUTORIALS
      • COLLEGE RESOURCES
      • NOVELS and OTHER BOOKS
    • EXAMINATIONS >
      • MOCKS AND JOINT EXAMS >
        • FORM 1 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 2 QUESTION PAPERS, ANSWERS AND MARKING SCHEMES COLLECTIONS
        • FORM 3 EXAMINATIONS, QUESTION PAPERS AND ANSWERS
        • FORM 4 MOCKS PAST EXAMS BY REGION
        • TOP SECONDARY EXAMS ALL SUBJECTS
      • KPSEA NATIONAL EXAMS
      • KCPE >
        • KCPE PAST PAPERS AND ANSWERS >
          • KCPE 2020 RESULTS, REPORTS, QUESTIONS AND ANSWERS
          • KCPE PAST PAPERS 2019 REPORTS, RESULTS, QUESTIONS AND ANSWERS
        • KCPE PAST PAPERS PER SUBJECT
      • KCSE >
        • KCSE PAST PAPERS BY SUBJECT
        • KNEC KCSE PAST PAPERS, MARKING SCHEMES, QUESTIONS & ANSWERS
        • Free KCSE Past Papers Mathematics
        • Free KCSE Biology Questions and Answers
      • QUESTIONS & ANSWERS >
        • SECONDARY >
          • LANGUAGES >
            • Secondary English Questions and Answers
          • TECHNICALS >
            • COMPUTER STUDIES >
              • COMPUTER STUDIES Q & A
              • kcse computer studies paper 2 AND 3 Questions & Answers
            • BUSINESS STUDIES QUESTIONS & ANSWERS
            • KCSE AGRICULTURE TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE HOME SCIENCE DIRECT QUESTIONS AND ANSWERS
          • SCIENCES >
            • KCSE Mathematics Topical Questions
            • KCSE Biology Topical Questions and Answers
            • CHEMISTRY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE Physics Topical Questions
            • KCSE physics Practical Sample Quiz
          • HUMANITIES >
            • C.R.E (CRE) QUESTION AND ANSWERS
            • ISLAMIC RELIGIOUS EDUCATION (IRE) QUESTIONS AND ANSWERS
            • KCSE History Topical Questions and Answers
            • GEOGRAPHY TOPICAL QUESTIONS AND ANSWERS
        • PRIMARY >
          • Standard 4-8 Mathematics Topical Questions from Mocks and KCPE
          • Std 6 Mathematics Notes
    • TUTORIALS >
      • SECONDARY >
        • SCIENCES >
          • FOCUS MATHEMATICS TUTORIALS AND EXAMS FREE
          • KCSE BIOLOGY NOTES
          • FREE KCSE CHEMISTRY NOTES
          • KCSE PHYSICS NOTES, AUDIOVISUALS AND MORE
        • LANGUAGES >
          • ENGLISH >
            • A GUIDE TO SILENT SONG AND OTHER STORIES
            • English KCSE Set Books
            • ENGLISH POETRY QUESTIONS WITH ANSWERS FOR K.C.S.E CANDIDATES
            • ENGLISH GRAMMAR #KCSE
          • KISWAHILI >
            • Bembea ya Maisha
            • CHOZI LA HERI - MWONGOZO
            • KIGOGO - MWONGOZO
            • MASWALI NA MAJIBU YA TUMBO LISILOSHIBA
            • USHAIRI MASWALI NA MAJIBU
            • KCSE Kiswahili Fasihi
        • TECHNICALS >
          • HOME SCIENCE NOTES
          • KCSE BUSINESS STUDIES NOTES
          • COMPUTER STUDIES NOTES LATEST
          • kcse Computer Studies Notes
          • KCSE AGRICULTURE NOTES, SYLLABUS, QUESTIONS, ANSWERS, SCHEMES OF WORK AND OTHERS
        • HUMANITIES >
          • KCSE History Notes Form 1 to 4
          • FREE KCSE CRE NOTES
          • KCSE GEOGRAPHY NOTES
          • IRE NOTES, AUDIOVISUAL, QUESTIONS AND ANSWERS
      • PRIMARY >
        • STANDARD 4: SOCIAL STUDIES
        • NOTES >
          • KISWAHILI
          • SOCIAL STUDIES
        • EXAMINATIONS
        • DecaTurbo Online Series Examinations
        • KCPE Mathematics Notes
        • KCPE and Primary Level Compositions
      • Other Supportive Documents >
        • SYLLABUS >
          • Primary 8-4-4 based Syllabus, Objectives and Lessons
          • Primary Mathematics Syllabus
        • MASOMO VIDEOS
    • CURRICULUM >
      • NEW CURRICULUM DESIGNS >
        • PRIMARY >
          • PRE PRIMARY ONE CURRICULUM WITH SYLLABUS
          • PRE PRIMARY TWO CURRICULUM WITH SYLLABUS
        • SECONDARY >
          • KNEC KCSE SYLLABUS AND COURSE OUTLINES
        • COLLEGE >
          • Regulations for the TIVET Craft and Diploma Business Examinations
    • HIGH INSTITUTIONS >
      • EXAMINATIONS >
        • College and Varsity Past Papers online
      • TUTORIALS >
        • COLLEGE AND UNIVERSITY NOTES AND TUTORIALS
  • MEMBERS RESOURCES
    • Primary >
      • CBC AND 8-4-4 LATEST EXAMS
      • CBC PROFFESSIONAL TOOLS
      • CBC NOTES PRIMARY
      • CBC KPSEA EXAMS
      • Standard 8 (std) English Topical Questions
      • KCPE MATHEMATICS TOPICAL QUESTIONS FROM 1989 TO LAST YEAR
      • STANDARD 8 PAST PAPERS 8-4-4 BASED
    • Secondary >
      • FORM 1 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 2 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 3 EXAMS WITH ANSWERS
      • FORM 4 EXAMS WITH ANSWERS
      • KCSE 2020 QUESTIONS AND ANSWERS
      • NOTES SECONDARY
      • MOCKS SECONDARY >
        • kcse form 2 mathematics questions
    • Free Schemes of Work
    • FOCUS A365 SERIES K.C.P.E EXAMINATIONS FOR PRIMARY
    • ALL GROUPS PRODUCTS
    • PREMIUM PRODUCTS 2