Maswali
a) Taja na ueleze sifa za mtambaji bora katika fasihi simulizi. (alama 10)
b) Nyimbo zina wajibu gani katika jamii. (alama 4) c) i) Eleza maana ya vitendawili. (alama 2) ii) Onyesha sifa za kitendawili. (alama 4) Majibu
a) Sifa za mtambaji bora
b) Wajibu wa nyimbo
c)
i) Kitendawili ni fumbo/msemo wa kimafumbo ambao hufumbua jambo fulani na hutolewa kwa hadhira au wasikilizaji ili waufumbue. 1 x 2= 2 ii) Hutangulizwa kwa njia maalumu a) Ujumbe wake ni wa kimafumbo b) Ufananisho wa kijazanda c) Ni fupi kwa maelezo d) Hutegemea mazingira/sehemu Fulani 4 x 1 = 4 Maswali
a) Taja na ueleze aina nne za hadithi (alama 8)
b) Eleza mbinu tatu ambazo mtambaji anaweza kutumia kuishirikisha hadhira yake.(alama 6) c) Fafanua vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi. (alama 6) i) Majigambo ii) Mivigha iii) Lakabu Majibu
a)
i) Visasili - Hadithi zinazosimulia asili ya watu, vitu ama tabia Fulani. ii) Ngano za mazimwi - Husimulia kuhusu mazimwi iii) Hurafa - Hadithi ambazo zina wahusika wanyama lakini waliopewa tabia za binadamu. iv) Hekaya - Ngano fupi zinazosimulia matukio ya kushangaza yanayoonyesha hila au ujanja wa mwanadamu v) Mighani - Ngano za ushujaa Mighani huwa na lengo la kueleza visa na mikasa ya watu ama mashujaa wa jamii fulani.( mwalimu akadirie aina nyingine)
b)
c)
i) Majigambo – Mazungumzo yanayotolewa na mtu fulani ili kujitapa ii) Mivigha – sherehe maalum za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi maalum. iii) Lakabu – Majina ya utani au kupanga ambayo watu hujipa au kupewa
0 Comments
Soma maagizo yafuatayo kisha ujibu maswali
(Alfajiri kuu. Vijana wanazunguka kinu, vifua wazi. Nyusoni wamepakwa masizi na aina ya tope jeupe. Wako katikati yam situ. Mzee Jando ameketi kwenye namna yam to wa nyasi.)
Mzee Jando: (Akiwahiza) haraka! Ongezeni kasi! Zunguka! Haya imbeni, barobaro!
Vijana: jua lachomoza! Muda umefika wa mbegu kuatika! Ichipuke na kuzalisha matunda! Ni leo, ni sasa!
Mzee Jando: haya ketini sasa
Vijana: (Vijana wanaketi katika mistari huku wameshikana mikono mabegani) Mzee Jando: tulisema mume nini? Vijana: (kwa pamoja na kwa sauti ya dhati) Mume ni kazi Sio ubazazi Ale jasho lake
Mzee Jando: Sawa kabisa, je mume ni nani?
Vijana: Ni mlinzi wa jamii Ni mfano mwema wa jitihada Apambane na adui Atende wajibu na maadili
Mzee Jando: Jambo linalovunja umoja!
Vijana: Likumbatiwe na kufunzwa hata watoto wachanga! Mzee Jando: Haya, semeni wenyewe leo! Vijana: Leo tumkomaa, si watoto tena Tumetimia barobaro kamili Sisi ni stadi Sisi ni wapevu! Tayari kwa majukumu ya kujenga jamii Sisi ni tegemeo la umma Sisi ndio chimbuko la wema Maadili na upendo
Mzee Jando: Nakubali mko tayari. Haya tuendelee na ada zetu zingine. Kijembe kukidhihaki!
Vijana: (Wanasimama kijasiri na kurindimisha sauti) Tuko tayari kuingia utuuzima! maswali
majibu
“La, Mzee…. Mbio za sakafuni zimefika ukingoni” (al 4) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (b) Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 4) (c) Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al 4) (d) Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa. (al 4) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4) (i) Maneno ya Kenga (ii) Anamwambia Majoka (iii) Nje ya lango la soko la Chapakazi (iv) Baada ya Majoka kulalamika kuwa Kenga alikuwa ameshindwa kazi kwa kuwakubali wapinzani kufika pale sokoni. (b) Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 8)
(c) Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al. 4)
(d) Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa? (al. 4)
Soma makala yafwatayo kisha ujibu maswali yafwatayo
Hapo zamani za kale, paloindokea mtu mmoja kwa jina mzee Kata. Mzee Kata alikuwa na wake wawili. Mke wa kwanza aliitwa Neema na wa pili aliitwa Nduli. Kila mmoja wa wake hawa alikuwa na mtoto mmoja. Neema alikuwa na mtoto wa kike kwa jina Majaliwa. Majaliwa alikuwa ameumbwa akaumbika.Uso wake ulihimili macho meupe mfano wa theluji. Meno yake ya juu yalipangika kwa njia ambayo iliyafanya kuacha mwanya ambao ulifanya tabasamu yake kuwa ya mvuto wa sumaki. Urembo wa Majaliwa, kama walivyosema wengi, ungemtoa nyoka yeyote pangoni.
Kwa upande mwingine Kutu, bintiye Nduli, alikuwa mwenye sura mbaya ya kutisha.Uso wake usiopendeza ulimfanya kuonekana kama ajuza wa miaka mia moja! Tabia yake ya ukorofi ilikoleza mvuto wake hasi. Vijana wa kijijini walimfanyia inadi kila mara kwa kumkumbusha kuwa hakufaa kuringa. “Sura kama kiboko”, wangemtania
Tofauti za kiumbo kati ya Majaliwa na Kutu zilizua uhasama mkubwa kati ya ndugu hawa, sikwambii mama zao. Hali hii ilizidishwa Zaidi na nongwa za kila siku zilizotokana na ukewenza. Familia yam zee Kata ikawa medaniya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hali ya mtafaruku iliendelea kuikosesha nyumba yam zee kata amani. Asubuhi moja, Mzee Kata aliamka kama kawaida yake, alijikohoza kama isharaya kutangaza kufika kwake. Daima hakupenda kuzungumza na wakeze asubuhi na mapema. Aliamini kuwa wangemletea nuksi. Kinyume na siku nyingine, mzee Kata hakuitikiwa. Ilibidi kujikaribisha nyumbani mwake. Mara tu alipovuka kizingiti cha kijumba hicho, alitupa macho yake juu yakitanda cha mayoweambapo mke wake alijinyosha twaa kakauka kama ukuni; hanapumzi. Weupe wa macho yake na mapovu yaliyomtoka kinywani yalimhakikishia Mzee Kata kuwa Neema kampungia mkono. Harufu kali ya sumu ilihanikiza hewa kumwarifu kuwa Mzee kata kuwa mkewe kafa kwa kutendwa na mkemwenza
Maisha ya Majaliwa yalichukua mkondo mpya baada ya tanzia hii. Mama wa kambo sasa alipata mwanya wa kumhini majaliwa. Kazi zote za nyumbani aliachiwa yeye.Huku Kutu akiachwa huru kucheza. Majaliwa alipewa chakula hapa; wengine wakila biriani yeye alipewa wali wa kawaida. Mavazi yake yaligeuka matambara.Siku zilivyozidi kusonga ndivyo mateso yalivyoongezeka. Mama wa kambo alizidisha wivu wake kwa majaliwa. Hata Majaliwa alipovunja ungo na wachumba kuja kumposa, mama wa kambo aliwafukuzia mbali. Wenine walihimizwa kumposa Kutu. Wachumba waliochachawa kutaka kumuoa majaliwa wakidai kuwa hawamtaki Kutu kwa sababu ya kiburi chake, walinyeshewa matusi, wakahizinika na kujiendea zao.
Siku moja alitokea kijana mmoja makini .alikuja amavalia gwanda jeusi lililojiinamia kwa uchovu. Viatu alivyovaa vilikuwa vimejichokea kwa kupiga lami. Kofia iliokuwa kichwani pake ilitosha kumhakikishia mama wa kambo kuwa huyu alikuwa fakiri. Mama mtu alikubali mara moja posa ya kijana huyu kwa Majaliwa akijua kuwa angeadhibika. Aliamini amemtokomeza Majaliwa ndani ya lindi la ulitima. Mzee Kata naye hakusita kumwoza Majaliwa kwa kiajana huyu maana aliiona hii kama fursa ya pekee ya kumwepusha vitimbi vya mama wa kambo Majaliwa aliandamana na mume wake hadi Kijiji cha peponi ambako kijana huyu allishi. Wallingia katika nyumba ya msonge ambamo Majaliwa alitarajia kuanza Maisha ya ndoa. Walitayarisha chajio, wakala na kulala.
Asubuhi, Majaliwa aliamshwa na nyimbo za ndege. Alipofunguamacho, alijikuta kalala ndani mya chumba chenye sakafu ya vigae. Ukuta wa chumba hicho ulikuwa wa rangi wa zari. Mapambo ya dhahabu yalitundkwa ukutani. Kumbe kijana aliyemuoa hakuwa maskini kama ilivyodhaniwa! Alikuwa mwana wa mfalme! Na hili lilikuwa kasri hasa! Majaliwa hakueza kuamini! Alikuwa ameamkia Maisha ambayo hakuwahi yawazia.
Alipoingia sebuleni alimpata mama yake mpenzi, akiwa na tabasamu ya milele usoni. Walikumbatiana kwa shauku kuu. Kumbe kijana huyo alikuwa ametumwa na mamake Majaliwa! Mumewe majaliwa alishuhudia kwa umbali. Machozi ya mama mtu na mwanawe yakilovya vifua vyao na kuyeyusha simanzi na kuyeyusha simanzi iliyokuwa imeyaandama Maisha yao. Tangu siku hiyi, watu hawa wallishi kwa raha mstarehe. Hadithi yangu inaishia hapo.
MASWALI
a) Taja na utolee mifano mbinu sita za kimtindo zilizotumiwa katika utungo huu (al.3)
b) Utungo huu unaweza kuainishwa kama ngamo, toa sababu (al.1) c) Fafanua umuhimu nne wa formula ya kumalizia katika utungo huu (al. 4) d) Taja shughuli moja ya kijamii katika jamii ya utungo huu (al. 1) e) Jadili tatizo moja la ukewenza katika utungo huu (al.1) f) Taja na ufafanue dhima tano ya utungo huu katika jamii yake (al.5) g) Taja mambo mawili ambayo fanani anaweza kutekeleza ili kuufanya utungo huu uwe wa kuvutia Zaidi (al. 1) h) Miviga ni nini? (al.1) i) Taja hasara tatu za miviga (al.3) MAJIBU
a) MBINU ZA KIMTINDO
i) Tashbihi -Sura kama kiboko ii) msemo/nahau -Kumtoa nyoka pangoni iii) Nidaa- Ajuza wa miaka mia moja iv) Taswira mnuso- Harufu v) Usimulizi- Hapo zamani za kale vi) Istiara- Mavazi kugeuka matambara vii) Majazi-Neema, Majaliwa, Nduli viii) Tashhisi- harufu kumwarifu ( 1/2x6= alama 3)
b) i) kuna formula ya ufunguzi- hapo zamani za kale
ii) kuna formula ya kumalizia- Hadithi yangu inaishia hapo (1x1=alama 1)
c) UMUHIMU WA FOMULA YA KUMALIZIA
i) Kurudisha wasikizaji kwa hali ya kawaida ii) Kubeba wazo au maudhui au ujumbe wa hadithi iii) Onyesha mwisho wa hadithi iv) Pahsa mtambali anayefuata. Pisha shughuli inayofuata v) Kitulizo kwa hadhira baada ya kumakinika kwa muda vi) Kutoa changamotomkwa hadhira. (4x1=alama 4)
D SHUGHULI ZA KIJAMII
i) Ndoa- Wake wawili, Nduli kukosa kupashashwa, Majaliwa kuolewa 1x1= alama 1
E MATATIZO YA UKEWENZA
i) Wivu- mamake majaliwa kupewa sumu ii) Mateso kwa wana wa wake wenza- majaliwa kuteswa na mamake Nduli (1x1= alama 1)
F DHIMA YA UTUNGO
i) Huelimisha ii) Huburudisha iii) Huadilisha iv) Hukuza utamaduni v) huleta utangamano vi) Hukuza ubunifu vii) Hukuza uwezo wa kukumbusha viii) Hutoa onyo ix) Ni kitambulisho cha jamii x) Hukuza ujasiri xi)Hukuza historia (5x1=alama 5) mwanafunzi atoe maelezo Zaidi ndiposa apewe
G) MAMBO YA KUFANYA HADITHI KUVUTIA
i) Kutumia Ishara kama miondoko ii) Kutumia ala za muziki iii) kutumia maleba iv) Kushirikisha hadhira v) kuimba vi) Kucheka (2x1/2=alama 1)
H) MIVIGA- sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi au wakati maalumu wa mwaka (1x1=alama 1)
I) HASARA ZA MIVIGA
ii) Zingine zimepitwa na wakati kama vile tohara ya wanawake. Huhatarisha Maisha ya waathiriwa ii) Zingine hukinzana na malengo ya taifa kama vile ukeketaji wa Watoto wa kike iii) Zingine hujaza watu hofu kama zile zinazotumia kafara ya binadamu iv) zingine huleta uhasama kati ya koo hasa zile za kufukuza mapepo v) Zingine ni ghali kwani huhitaji fedha nyingi na kusababisha umaskini (3x1=alama 3) b) Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)
Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike24/12/2022 Tumia kifungu kifuatacho kujibu maswali yanayofuataa) Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike.I) Bainisha kipera kinachorejelewa (Al 1).
Kitendawili
II) Andika shughuli moja ya Kijamii na moja ya Kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utingo huu. (Al 2)
III) Eleza dhima nne za kipera kinachorejelewa katika jamii yako. (Al 4)
Umuhimu
IV) Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia katika uwasilishaji wako. (Al 5)
Eleza umuhimu wa ukusanyaji na uhifadhi wa data za fasihi simulizi. (alama 5)
Fafanua matatizo yanayomkabili mkusanyaji wa fasihi simulizi nyanjani. (alama 10)
Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)Jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi
Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)
Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)Matambiko Sadaka au ada inayotolewa kwa Mungu, mizimu, pepo au miungu ili wasaidie binadamu kutatua mambo magumu, kuomba radhi au kutoa shukrani. Matatizo ni kama vile ukame, magonjwa, kukosa watoto, mafuriko au janga lolote lililomshinda binadamu nguvu na uwezo. Pembezi Tungo za sifa za watu wa aina fulani wanaosifika kwa matendo yao au nafasi walizo nazo katika jamii kv matendo ya kishujaa au kujitolea kwao. Km viongozi, walezi wazuri, waganga, nk Misimu
Semi zinazozuka na kutumiwa na kundi fulani la wanajamii kama misemo ya mawasiliano baina ya wanakikundi hicho./ Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka tu kutegemea mazingira maalum./ Ni semi ndogo ndogo za kupita. Huzuka katika mazingira fulani na hufa baada ya kutokuwepo kwa mazingira yale. Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)
Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)
Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)
Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)
Jadili mifano mitano ya ngomezi za kisasa (alama 5) Jadili mifano mitano ya ngomeziza kisasa. (alama 5)
Eleza maana ya; (alama 5) |
MWONGOZO![]()
MASWALI NA MAJIBU![]()
|
MASWALI NA MAJIBU![]()
MITIHANI YA MWIGO WA KCSE![]()
![]()
|
MASWALI NA MAJIBU![]()
|
UCHAMBUZI/MWONGOZO (GUIDE)![]()
|
SURA YA KWANZA
Chini ya mti mmoja kando ya mto Kiberenge, vijana wawili, amani na Imani wanapunga hewa baada ya kukata kiu. Aidha, wamo safarini kuelekea Sokomoko, kila mmoja na haja yake. Kitambo kidogo tu, wawili hawa wamevunja mwiko kwa kuyanywa maji ya mto kiberenge ambao wenyeji wanaamini kuwa haramu. Muda si kitambo, wenyeji hawachelewi kuambizana na kusimuliana juu ya waja wawili, waliovunja mwiko kwa kuyanywa maji haramu ya Kiberenge na wakakosa kuaga dunia. Kwa kweli, wakati mwingine haramu huweza kuhalalishwa kulingana na watendwa. Imani anayo imani kwamba hakuna haja yoyote ya kuogopa kutenda bila kujaribu.