Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali.17/12/2023 Jibu makala yafuatayo kisha ujibu maswali.UFUPISHO Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa ama yoyote. Neno huzurn linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto duma imejaa raha, starehe na vcheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya kufurahisha na kustarehesha tu sio kudhikisha na kuhuzunisha. Huyu tunayemzungumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha kitendekacho mkono wake wa kushoto wala idle kinachofanyika hasa katika mkono wake wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo, vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi machungu ambayo huleta huzuni, sb raha. Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, meha mwana kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule. Huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Iii wasome kama inavyotakikana, m sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaacthibu, hasa wale watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ulivyo. Watoto wa ama hii wanapotiwa adabu raha hujitenga na buzuni huwatawala. Huzuni, hivyo basi, maonekana ya kuwa m uso wa pili katika maisha ya wanadamu, uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana, ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa yumo katikati ya kustarehe. Si tu, inajulikana dhahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao. Zingatia mtoto anayezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali, kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote. Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, anayempata bila kupanga. Hata mtoto huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni mievi na analojua ni kurudi nyumbani usiku akiimba nyimbo za kilevi, kuita mkewe kwa sauti kubwa, kuitisha chakula na kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa ama hiyo atakayoijua ni huzuni tu, si raha asilani. MASWALI (a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo. (Maneno-100). (Alama 9) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………… (b) Ukizingatia aya ya mwisho eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto buzuni. (Maneno 40-45) (Alama 4) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………… Majibu
Majibu (a) (i) Mtoto hudhani/hufikiri ulimwengu umejaa raha na hauna huzuni/hauna mateso/haudhikishi. (ii) Mtoto huyu ni yule mdogo ambaye hajajua kubainisha mambo. (iii) Anavyoendelea kukua, anafahamishwaanabainikiwa na mengi yaletayo huzuni. (iv) Nyumbani ingawa hupendwa, huadhibiwa wanapokuwa watundu na kuhuzunika. (v) Shuleni wanapozembea kazi, wanaadhibiwa na hili huwahuzunisha. (vi) Huzuni basi ni uso wa pili katika maisha ya binadamu, uso wa kwanza ukiwa raha. (vii) Kila mtu duniani huzongwa na huzuni / huhuzunika (viii) Raha humjia mwanadamu kwa nadra ilhali huzuni humuvamia wakati wowote. (ix) Wako watu wengi wasiowahi kuonja raha maishani mwao (Hoja 9-al-1 =9) (b) (i) Mtoto anapofiwa na wazazi (ii) Mtoto anayetupwa na mamake kijana baada ya kuzaliwa. (iii) Mtoto anayelelewa na mama wa kambo mwovu. (iv) Mtoto ambaye babake ni mlevi Hoja4-Al-1 —4
0 Comments
Leave a Reply. |
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |