Soma shairi hili kisha ujibu maswali:Angawa mdogo, dagaa, amekomaa Kaanga kidogo, dagaa, atakufaa Kalia kinaya, dagaa, h’ondoa njaa Wa kwako udogo, kijana, sio balaa Na sio mzigo, kijana, bado wafaa Toka kwa mtego, kijana, sinyanyapaa Nasaha kidogo, kijana, ukubwa jaa Jikaze kimbogo, kijana, acha kukaa Chimbua mhogo, kijana, usibung’aa Na wake udogo, dagaa, ndani hukaa, Kuliko vigogo, dagaa, hajambaa Hapati kipigo, dagaa, hauna fazaa Maisha si mwigo, kijana ushike taa Sihofu magego, kijana, nawe wafaa Kazana kidogo, kijana, kugaaga Maswali (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka (alama 1) (b) Eleza arudhi zilizofuatwa katika kutunga shairi hili (alama 4) (c) Onyesha jinsi malenga alivyotumia uhuru wake (alama 3) (d) Tambua bahari katika shairi hili (alama 3) (e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari (alama 4) (f) Tambua mbinu za lugha zilizotumika katika shairi (alama 3) (g) Eleza toni la shairi hili (alama 2) MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KISW PPR 3 F3 1. (a) Dagaa au Kijana (1 x 2) (b) Kuna urari wa vina − Lina beti tano − Mishororo mitatu katika kila ubeti − Lina pande tatu katika kila mshororo (4 x 1) (c) Matumizi ya lahaja mf. Magego – Meno Inkisari – h’ondoa – huondoa Kuburoga sarufi – Na wake udogo – Na udogo wake (3 x 1) (d) Ukara – Vina vya utao na mwandamizi havitiririki, vya ukwapi vinatiririka. Ukawafi – Pande tatu (2 x 1) (e) Kijana nakupa mawaidha ya kwamba aliye cheoni kuhusishwa na makosa yote, kwa hivyo tia bidii afanyavyo mbogo uache kukaa. Chimbua mihogo utafute riziki (al. 4) (f) Istiari / jazanda mf Jikaze kimbogo Methali – mf ukubwa jaa Msemo mf shika taa (kuwa mwangaza) taja na kutoa mfano (3 x 1) (g) Toni ya matumaini Toni ya kuhimiza Toni ya kuonya (1 x 2)
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |