Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali1. Mbiu naipuliza, kwawa hapana ng’ambo, Kwa aningoja ‘mesikia, inaumiza matumbo, Kwa upole sitafyoa, hata kamna kwa kimombo, Yafaa jihadharia, maisha ya s’ende kombo. 2. Maisha ya s’ende kombo, kututoa yetu ari, Zingatia haya mambo, wetu wale zimukiri, Kuwa wana kwa viambo, huwa Baraka na kheri watunzeni na maumbo, msie zusha hatari. 3. Msije zusha hatari, na nyingi hizi zahama, Wazazi haya si siri, mawi mnayoandama Twaelezea kwa uzuri, matendoyo yatuuma Watoto tunayo mori, ni lini mtaja koma? 4. Ni lini mtaja koma, na pombe siso halali? Sio baba sio mama, mbona ny’ hamtajali? Mwafa ja nzi twasema, mwatua chabi la hali Hangaiko acha nyuma, kwani hamuoni hili? 5. Kwani hamuoni hili, kila saa mwapigana Nyumbanizo hatulali, jehanamu tumeona Mwatusumbua akili, twaumia ten asana Achene na ukatili, kwani upendo hamna. 6. Kwani upendo hamna, kamam mbwa mwatuchapa Mwatuchoma sisi wana, mio yetu yatupapa Pa kujificha hatuna, tumebaki tukitapa 7. Tumevujwa na mifupa, hata leo uke wetu, Mwatubaka na kuapa, kutung’ata nyi’ majitu, Hayo makeke na pupa, mtakoma utukufu 8. Mtakoma utukufu, nakutumia miki Na tabia zenye kutu, tumechoka nayo chuki Hatutakubali katu, kutendewa yenye siki Serikali fanya kitu, kwani nasi tuna haki Maswali a) Fafanua tamathali nne za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 2) b) Taja nafsi nne katika shairi hili. (alama 1) c) Eleza bahari mbili zinaowakilishwa katika shairi hili. (alama 4) d) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari. (alama 4) e) Eleza maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 3) f) Eleza umuhimu wa mbinu mbili amabazo mshairi ammetumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 4) MAJIBU YA SHAIRI
a) Maswali balagha- na pombe siso halali? Mbona ny’ hamtajali. Isitiari- kutang’ata nyi majitu Tashbihi- kama mbwa mwatuchapa Mwafa ja nzi. (zozote 1x4) b) Mtoto (mwana) c) Lina mishororo mine hiyo ni Tarbia. Kina cha kubwagiza kimechukuliwa ili kuwa mwanzo wa ubeti unaofuata hivyo huitwa pindu au mkuju/nyoka.(zozote 1x2) d) Nilini wazazi wataacha kutumia pombe haramu na kuwajali watoto wao kwani wanakunywa na kuwaachia mateso na mahangaiko mengi bila kujali. (alama 4) e) Ukatili, malezi, ulevi. Mwanafunzi aeleze ipasavyo. (alama 3) f) Mazida –mshairi amerufusha baadhi ya … ili kuafikia urari wa k.m. nyumbanizo, matendoyo Liksani- mshairi amefupisha baadhi ya maneno pia kuafiki urari wa viua- mio, ny’ Kuburanga sarufi- kwani upendo kamua badala ya kwani hamna upendo-ili kuleta urari wa viua katika mishororo. (mwanafunzi ataje mbili na kueleza.( zozote alama 2x2
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |