Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuataYamerundikwa machicha, na maganda ya matunda, Na mwiko uliochacha, na mabli uliorunda, Harufu inaposecha, yanukia nipenda, Hakuna inomchusha, bustani ya maua. Mianzi yetu ya pua, imeota pasigaa, Hasia zinobagua, mara mbili zinafaa, Kibaya tunarundua, kizuri kina balaa, Tope ziwe ni halua, na samli imekaa. Macho yameota kungu, ila yanaona yote, Hata likitanda wingu, anga linatanda kote, Ni mzuri ulimwengu, na furaha na wa kite, Na bustani wenzangu, kipita siteme mate. Mahame na maanguko, machoni yanapumbaza, Kifusi na mafuniko, moyoni yanaliwaza, Mapakacha ya rundiko, topasi yanampoza, Hakuna inomchusa, bustani ya maua. Kuku anapara kucha, na bata tope aponda, Mbwa pua inapucha, pipani anamowinda, Taka zimejenga picha, inovutia kushinda, Vitalu vyenye mahaba, ni lazima kuvilinda. Mbu wanazaiana, panya wanadunduiza, Njiani tunapishana, nzi wanatumbuiza, Maradhi huzidiana, twacheka tukipuuza, Liwazo kubwa si haba, bustani yapendeza. Maswali
(a) Ni nini dhamira ya mtunzi katika shairi hili. (al.2) (b) Vitaje vitu vya kuchukiza ambavyo mshairi anavizungumzia katika shairi hili. (al.3) (c) Kwa nini mshairi anasema kuwa macho yameota kungu ubeti wa tatu? (al.2) (d) Ni nini ujumbe wa mshairi hili. (al.3) (e) Eleza muundo wa shairi hili. (al.4) (f) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa shairi hili (al.6) (i) imeota pasigaa (ii) kibaya tunarandua (iii) macho yameota kungi
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |