Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswaliKwanza matatu muhimu, ni utu uke na ume Pili kwa mwanadamu, awe na kitu atume, Tatu awe na fahamu, ye dini isimhame, Haya ni mambo adhimu, kwa mke na mwanamume, Mambo ye adimu, huyataka kwa. shime. Kwa la kwanza twaanzana, twaendelea kudumu, Na kitu tunaonana, gharama twaweza kimu, Maisha hayani laana, wala hayawi magumu, La tatu shaka halina, humpamba mwenadamu, Kwa fikira na kuoka, mambo yaliyolazimu. Kwa uwezowe Mwenyezi, mdumisha kila kitu, Matatu haya azizi, karibu kwa kila mtu, Yana hawa na mapenzi, katika nafsi zetu, Na katika matembezi, dunia hii yetu, Kuyakasa hatuwezi, na ndiyo utumwa. Ni utumwa madhabuti, hatuwezi kuuvua, Umetushika kifatu, kwa tadi na kwa takua, Katuizi hatujuti, tumo tunachukua, Na nafasi hatujati, kidogo. ya kuumua, Mpaka yaje mauti, uhuru kutuletea. MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini? (alama 2) (b) Taja mambo matatu muhimu ambayo sharti binadamu awe nayo kulingana na Mshairi.(alama 3) (c) Eleza umuhimu wa kila mojawao katika mambo hayo matatu kama yaliyofafanuliwa na mshairi. (alama 6) (d) Taja bahari zmnazojitokeza katika shairi hili. (alama 2) (e) Uandike ubeti wa kwenza katika lugha nathari. (alama 5) (f) Onyesha kwa kutumia namna ambavyo mtunzi ametumia uhuru wa kishairi. (alama 2)
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |