Joseph Kiponda : Taifa ni UshuruLau kama ingakuwa, madhali tuna uhuru Watu kodi kutotowa, na kuifanya kufuru Vije nchi ingakuwa, taifa bila ndururu Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Hivi taifa kumea, nakuendelea mbele Kwamba lajitegemea, haliwategei wale Yataka kujitolea, ushuru bila kelele Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Wafanyikazi wa umma, mfano mwema walimu Wauguzi mahashuma, daktari wahadimu Bila hizi darahima, vipi wangalihudumu? Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Si vyema kuombaomba, kwa wageni kila mara Huwa twajifunga kamba, na kujitia izara Adha zinapotukumba, kujitegemea bora Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru. Miradi ya maendeleo, yahitaji darahima Ndo tufikie upeo, ulio dunia nzima Wadogo na wenye vyeo, bila kodi tutakwama Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Ushuru si kwa wanyonge, wasokuwa na uwezo Watozwe hata wabunge, na wengine wenye nazo Yeyote asijitenge, kodi akalipa bezo Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Kwetu kutoa ushuru, ndiko kujitegemea Pasiwepo na udhuru, sio wa kuelea Huwa ni kama kiguru, asenao kutembea Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru. Maswali
MAJIBU
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |