Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswaliHukuja hapa kwa vingi, Vitimbi vya kila namna, Kanambia nikuruzuku, Kimwana awe mwenzio, Hukumtwaa mwananngu, Kisema mno walavu, Vipi wamgeuza ngoma, Mapepo wampigia? Siwe uloandaa, Harusi ya kukata na shoka Masafu ya magari, yakilalama jua kali, Hadi kanisani kungia, mimbari we kusimama Kasema utamuenzi, hadi yenu mauko? Vipi jicho lageukia, mitaani vipaa mwitu? Hukunambia we fidhuli, Mwanangu utamtunza? Taandamana naye daima, Ja chanda na pete? Hukumwonjesha tamu, ya ulaghai huyuno? Midisko wampeleka, kisingizia mapenzi Vipi wamtezea shere. Mwanangu kumliza? Lini taacha dhuluma hizino humfanyiazo, Tachukua lini majukumu Ya kumlea na vifaranga? Huachi kulia u waya. Wanao kitelekeza Nadhiri zako zako za nitakipu promise, Zi wapi mwana balaa? Lini tafumbua maozi, uone huyu nduli, Alotwala wengi wapendi, Kwa jicho la nje kuwangia, Imeanguka miamba mingapi, nayo ng’ang’ania kufia dondani, Zinduka mwana zinduka, Ailaya waangamiza. Maswali (a) Hili ni aina gani ya shairi. Fafanua (alama 4) (b) Mwandishi anaibua maswala kadhaa ya kijamii. Yaandike. (alama 3) (c) Eleza matumizi ya uhuru wa kishairi katika utungo huu. (alama4) (d) Eleza mbinu ya fasihi iliyotumika katika utungo huu. (alama 3) (e) Bainisha matumizi ya: (alama 4) (i) mistari mishata (ii) mistari kifu (f) Ni nini maana ya vifungu vifuatavyo kama ilivyotumiwa kwenye kifungu? (alama 2) (i) vipaa mwitu (ii) kufia kidondani MAJIBU
(a) Hili ni aina gani ya shairi. Fafanua (alama 4) - halizingatii kulingana kwa mistari katika kila ubeti -idadi ya vipande hailingani katika kila mstari -halizingatii mpangilio maalum wa vina -halizingatii ulinganifu wa mizani katika kila mstari. (b) Mwandishi anaibua maswala kadhaa ya kijamii. Yaandike. (alama 3) -dhuluma katika ndoa - ulaghai katika ndoa -haki za watoto -ukosefu wa uaminifu katika ndoa -kutowajibika kwa waume -tatizo la ukimwi (c) Eleza matumizi ya uhuru wa kishairi katika utungo huu. (alama4) (i) kufinyanga sarufi - hadi kanisani kuingia- yakaingia hadi kanisani -hadi yenu mauko-hadi mauko yenu -mwanangu kumliza-kumliz mwanangu (ii) inkisari -kanambia-ukaniambia taacha-utaacha kisema-ukisema we-wewe -kungia- kuingia tachukua-utachukua wanao-wana wao (iii) mazida - Huyuno-huyu (iv) tabdila -twala-twaa wapendi- wpenzi (v) lahaja -wamtezea- wamchezea (vi) kikale/msamiati wa kale -maozi-macho (d) Eleza mbinu ya fasihi iliyotumika katika utungo huu. (alama 3) (i) maswali ya balagha -hukijahpa kwa vingi? -vipi wamtezea shere, mwanangu kumuuliza? (ii) tashbihi -taandama naye daima ja chanda na pete (iii) utohozi -walavu -midisko -nitakipu promise (iv) sitiari/istiari -vipaa mwitu-wasichana wengine vifaranga watoto -nduli-ugonjwa hatari miamba- watu mashuhuri (vi) tashhisi/uhuishaji -masafa ya magari yakilalama jua kali (vii) nahau - kufia kidondani - kupata hasara unapofuata kitu unachokiona ni cha thamani (viii) msemo -u waya- huna pesa/umefilisika (e) Bainisha matumizi ya: (alama 4) (i) mistari mishata -hukuja hapa kwa vingi -siwe uloandaa -kanambia nikuruzuku (ii) mistari kifu/mistari kamilifu -kasema utamuenzi hadi yenu mauko -vipi jicho lageukia mitaani vipaa mwitu -huachi kulia u waya (f) Ni nini maana ya vifungu vifuatavyo kama ilivyotumiwa kwenye kifungu? (alama 2) (I) vipaa mwitu – wasichana wengine (ii) kufia kidondani - kupata hasara unapofuata kitu unachokiona ni cha thamani
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |