Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki, Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Wenginea watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago Hadi kwenye wako au, pasipo hata kupesa, walakukupa kisogo Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwato ako tekelezo Tamko lake ‘subutu’, kuondoa tumaini, na kukuliza wazo Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui Hana faida nyumbani, ni mtu akichimbaye, mradi usitumai Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Kwa hakika ni baka, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi, aibarili rowoyo Mipangayo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa Ningetoa azinio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa Ama nitimue mbio, fuadinininanena, akilini nazuiwa Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Maswali a) Toa kichwa cha shairi hili (Alama 1) b) Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili (Alama 3) c) Eleza umbo la shairi hili (Alama 4) d) Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari (Alama 4) e) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi hili (Alama 4) f) Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili (Alama 2) g) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyo tumika katika shairi i) Zani ii) Faraghani (Alama 2) Majibu ya ushairi
a) Binadamu hatosheki Tamaa ni hatari (Alama 1) TAMAA b) Mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka Mwenye tamaa ana unafiki / masengenyo Mwenye tamaa anaweza kuua Mwenye tamaa ni mchoyo (hoja zozote 3x1=3) c) Mishororo minne / Tarbia / unne Migao mitatu – ukwapi / utao / mwandamizi Vina vitatu Mizani 8, 8, 8. Kibwagizo Beti sita (hoja zozote 4x1=4) d) Iwapo ukinunua kitu shetani hafurahi bali huwa na chuki. Mtu kama huyo atakasirika moyoni kwa kile ulichokifanya. - Atakuonya ili akuvunje matumaini ya kutekeleza ulichonua. - Mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka (Alama 4) e) Takriri – kibwagizo Tashibihi – hatari kama nyoka Tashihisi – inahadaa Nahau – Kinyesi kimetupiwa kutaja 1 Maelezo 1 (Jumla 2x2=4) f) Inkisari – Ukweliwe, kisu, tajawa, asosema, alo, mpangoyo Tabdila – shaitani (shetani kubadilisha sauti) Mazida sheitani (Kurefush she/ta/ni) (kutaja 1, maelezo 1 jumla 2x1=2) g) Baa – balaa, janga Majivuno, maringo, ujeuri (Alama 1x1=2)
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |