Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.Bahari 1. Bahari uzuri, wake tawambia, Sifa tabashiri, kuwahadithia, Ambazo ni nzuri, na faida pia. 2. Na faida pia, na kwamba ujue Nakukuelea, nawe utambue, Na sasa sikia, uzifafanue. 3. Uzifafanue, bahari za pambo, Lenye uzuriwe, pia ni urembo, Ni siri ujue, na pia ni tambo. 4. Na pia ni tambo, ni siri yakini, Aidha ni fumbo, haiwezekani, Ina mengi mambo, yenye na thamani. 5. Yenye na thamani, kwa watu wa pwani, Nawapa yakini, nanyi sikizani, Humo baharini, kwanza pulikani. 6. Kwanza Pu1ikani, lulu twaipata, Samaki yakini, faida huleta, Aidha wendani, pia huokota. 7. Pia huokota, ambari zinduna, Munyu na mafuta, vinapatikana, Faida yaleta, pulikiza sana. 8. Pulikiza sana, tia sikioni, Tija ya maana, ilo baharini, Imepatikana, kwa kila ya fani. 9. Kwa kila ya fani, samaki twauza Mapezi yakini, ya papa sikiza, Huleta thamani, yenye muangaza. 10. Yenye muangaza, pia na forodha, Pato huongeza, Ia kuleta fedha, Pia yaangaza, bahari kwa adha. 11. Bahari kwa adha, adhaye upepo, Hapana orodha, na ichafukapo, Huondoka ladha, tena hapo ndipo. 12. Tena hapo ndipo,- chombo hutotoma, Nyote muliopo, hapana msema, Ndipo muliyapo, “Mama, yoo mama!” MASWALI
MAJIBU
(a) Pindu – Kipande cha mwisho cha kituo ndicho kinaanza (ukwapi) katika ubeti unaofuata Tathlitha – mishororo mitatu Ukaraguni – Vina vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine 1 x 2 = 2 Mathnawi – vipande viwili (b) Faida ya bahari Ni pambo ama urembo Ni chanzo cha lulu, samaki, ambari na zinduna Ni chanzo cha fedha samaki wauzwapo Forodha hupatikana kwenye bahari na ni chanzo cha pesa Zozote 2 x 1 = 2 Hasara ya bahari Pepo husababisha usumbufu (kero) wakati bahari inapochafuka Vyombo huzama bahari inapochafuka 2 x 1 = 2 (c) Umbo la shairi Kila ubeti una mishororo mitatu Vipande viwili (ukwapi na utao) Utao unafanywa kuwa ukwapi kwenye beti hizo Kila mshororo una mizani sita sita jumla kumi na mbili kwa beti Vina viwili kwa kila ubeti Ubeti 11 dhe;po ubeti 12 po; ma (alama 4 x 1 = 4) (d) i) Uhuru wa kishairi. Inksari (1) tawambia – nitawaambia Tabashiri – nitabashiri (taja na mfano) (3) uzuriwe – uzuri wake (8) ilo - iliyo Kufinyanga sarufi/kuboronga sarufi; Bahari uzuri wake tawambia badala ya Nitawaambia uzuri wake bahari au uzuri wake bahari nitawaambia Ambari zinduna Ambari na zinduna Lahaja – Pulikeni (lahaja ya kingozi) Tabdila – Sikizani ; Sikizeni zozote 4 x 1 = 4 ii) Ubeti wa tano Iliyo ya maana/umuhimu kwa watu wa pwani, Nawaambia wazi nanyi msikilize. 3 x 1 = 3 Walio baharini wasikize (e) Pulikani - sikilizeni Tija – faida, tijara, manufaa Adhaye – Usumbufu wake/kero zake
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |