Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.HINI GILASI YA MWISHO! Kazini wanza, kusema na Mama Pima Leo inafika tama, mbele sitoi sukuma Nimezama nimezama, na kwa wengi sikusema Hini gilasi ya mwisho! Hini gilasi ya mwisho, nyingine sitozama Sitaki mchanganyisho, ya vito vya mama pima Si leo katu si kesho, mitaro kulala jama Hini gilasi ya mwisho! Samba nina uhasama, nanyi mlobaki nyuma La heri nitalisema, hadi nitakapokoma Kuishi kwa mama pima, mno ni kubwa gharama Hini gilasi ya mwisho! Tupo tusolipa karo, wana shule kutotuma Kwa sababu ya umero, wetu huja baki nyuma Na kushonwa matakuro, na wenzao wanosoma Hini gilasi ya mwisho! Hini ya mwisho gilasi, nimesema nimesema Afadhali kula nyasi, nisiwe nabaki nyuma Wenzetu waloziasi, uchumi wameuchuma Hini gilasi ya mwisho!. MASWALI
MASWALI 10 YA CHAGUZI ZAIDI
Majibu
0 Comments
Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswaliMungu naomba subira, subira nayo imani Imani iliyo bora, bora hapa duniani Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani Hiani pamwe ukora wenye kuhini. Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli. Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele Muwele wa hitilafu, hitilafu ya nduwele Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale. Vishale vinitomele, vitomele vikwato Vikwato pia maole, maole kufanya mito Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto. Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka Kutamka wazi vino, vino subira kutaka Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka Wahaka wa matukano, matukano na mashaka. Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita Kunikita salamani, salamani nikadata. Maswali
a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani? (al.2) b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia (al.4) (i) Mpangilio wa maneno (ii) Mpangilio wa vina. c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4) d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (al. 4) e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (al.6) Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswaliKama dau baharini, duniya inavyoyumba, Limeshamiri tufani, kila mmoja lakumba, Viumbe tu hali gani! Duniya yatishika, utahisi kama kwamba, Vilima vyaporomoka, na kuvurugika myamba, Viumbe tu hali gani! Tufani hilo la kusi, languruma na kutamba, Linapuliza kwa kasi, hapana kisichoyumba, Viumbe tu hali gani! Mujiwe ni kubwa sana, mfanowe kama nyumba, Yazuka na kugongana, wala hatuna la kwamba, Viumbe tu hali gani! Mibuyu hata mivule, kama usufi na pamba, Inarusha vilevile, seuze hiyi migomba Viumbe tu hali gani! Ni kipi kilotuliya, tuwazeni na kudumba, Mandovu kiangaliya, yagongana na masimba, Fisi wako hali gani! Hata papa baharini, tufani limewakumba, Walioko mikondoni, kila mmoja asamba, Dagaa wa hali gani! Mashehe wa mdaduwa, kwa ubani na uvumba, Tufani hilo kwa kuwa, kusoze kwake kutamba, Itokee afueni! (Shairi la ‘Tufani’ la Haji Gora Haji, katika Tamthilia ya Maisha, uk 62) Maswali;
Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswaliHeri ujue mapema Nasaba yetu haina woga Woga haumei kwetu, humea kwa kina mamako. Tulichinja jogoo na fahali ili uwe mwanaume. Ah! Kisu cha ngariba ni kikali ajabu. Iwapo utatikisa kichwacho. Uhamie kwa wasiotahiri, Ama tukwite njeku. Mpwangu kumbuka hili, Wanaume wa mlango wetu Si waoga wa kisu Wao hukatwa mchana hadi usiku Wala hawalalamiki. Siku nilipokatwa Nilisimama tisti Nikacheka ngariba kwa tashtiti Halikunitoka chozi. Iwapo utapepesa kope Wasichana wa kwetu na wa mbali Wote watakucheka Ubaki ukinuna. Sembe umepokea Na supu ya makongoro ukabugia Sema unachotaka Usije kunitia aibu Maswali;
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuataYamerundikwa machicha, na maganda ya matunda, Na mwiko uliochacha, na mabli uliorunda, Harufu inaposecha, yanukia nipenda, Hakuna inomchusha, bustani ya maua. Mianzi yetu ya pua, imeota pasigaa, Hasia zinobagua, mara mbili zinafaa, Kibaya tunarundua, kizuri kina balaa, Tope ziwe ni halua, na samli imekaa. Macho yameota kungu, ila yanaona yote, Hata likitanda wingu, anga linatanda kote, Ni mzuri ulimwengu, na furaha na wa kite, Na bustani wenzangu, kipita siteme mate. Mahame na maanguko, machoni yanapumbaza, Kifusi na mafuniko, moyoni yanaliwaza, Mapakacha ya rundiko, topasi yanampoza, Hakuna inomchusa, bustani ya maua. Kuku anapara kucha, na bata tope aponda, Mbwa pua inapucha, pipani anamowinda, Taka zimejenga picha, inovutia kushinda, Vitalu vyenye mahaba, ni lazima kuvilinda. Mbu wanazaiana, panya wanadunduiza, Njiani tunapishana, nzi wanatumbuiza, Maradhi huzidiana, twacheka tukipuuza, Liwazo kubwa si haba, bustani yapendeza. Maswali
(a) Ni nini dhamira ya mtunzi katika shairi hili. (al.2) (b) Vitaje vitu vya kuchukiza ambavyo mshairi anavizungumzia katika shairi hili. (al.3) (c) Kwa nini mshairi anasema kuwa macho yameota kungu ubeti wa tatu? (al.2) (d) Ni nini ujumbe wa mshairi hili. (al.3) (e) Eleza muundo wa shairi hili. (al.4) (f) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa shairi hili (al.6) (i) imeota pasigaa (ii) kibaya tunarandua (iii) macho yameota kungi Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatayo.Una moyo gani, ninakuuliza, wangu muhisani? Na kiasi gani, unavyojiweza, ijapo tufani? Ukiwa laini, utajipoteza, usijaribaini, Kusimama pweke kwataka makini. Zitavuma pepo, zitakupuliza, uanguke chini, Ela uwe papo, unajikweleza, na kujiamini, Utikishapo, umejiumiza, pigo la moyoni, Kusimama pweke kwataka makini. Utie migati, ya kukuoteza, hapo ardhini, Kwa nia na dhati, usiogeuza, au kuihuni, Zidata baruti, uwe wapwiza, weleke usoni, Kusimama pweke kwataka makini. Sishike vishindo, na mauzauza, ya kukuzaini, Kita kama nyundo, ukiniuliza, unayoamini, Na uje mkondo, utadidimiza, kujipa mizani, Kusimama pweke kwataka makini. Wengine wasiwe unaoweleza, yaliyo maani, Wewe ndiwe wewe, utawageuza, pindipo mwakani, Ela jichukuwe, pia kujikaza, katika midani, Kusimama pweke kwataka makini. Maswali
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayoNatunga nikiwaasa, msije kujijutia, Mitego sije wanasa, mkaja kuangamia, Tamaa nyingi za pesa, gereza zitawatia, Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza. Jela inakukonyeza, kama hutajizuwia, Haina ndugu gereza, jela si kuchezea, Inajuvya na kupoza, wenye nguvu kutulia, Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza. Rushuwa si kitu chema, walaji jihadharini, Mkila zitawakwama, zitawatoka puwani, Wazilao hulalama, si mimi ila Fulani, Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza. Ridhika na upatacho, kama moja au mbili, Usitaraji mkocho, apatao Bwana Ali, Tamaa zako za macho, zitakuletea mbuli, Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza. Nimeona kemu kemu, wenye vyeo kutimia, Maleba wakiwahimu, rushuwa kuwaletea, Muogopeni Karimu, beba haombwi rushuwa, Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza. Kuna wengi mahakimu, haki wanazopinduwa, Yatima kuwadhulumu, kwa kupapia rushuwa, Kwa kutaka darahimu, aso haki anapewa, Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza. MASWALI (a) Andika anwani mwafaka kwa utungo huu. (alama 2) (b) Taja athari tatu za rushwa kama zilivyoelezwa katika shairi. (alama 3) (c) Ni nini msimamo wa mwandishi kuhusu rushwa? (alama 2) (d) Andika ubeti wa pili katika lugha sufufu. (alama 4) (e) Eleza sifa nne zinazotambulisha utungo huu kuwa ni shairi. (alama 4) (f) Huku ukitoa mifano, onyesha namna uhuru wa mshairi unatanda katika shairi hili. (alama 2) (g) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (alama 3) (i) Kupapia (ii) Nikiwaasa (iii) Inamkonyeza MAJIBU
(a) Ufisadi/Rushwa 1 x 2 = 2 (b) Athari za rushwa Kutiwa gerezani Kutofaidi chochote Kulalamika 3 x 1 = 3 (c) Msimamo wa mwandishi kuhusu rushwa ni kuwa ni jambo lisilofaa tujiepushe nalo 1 x 2 = 2 (d) Ubeti wa 2 – Lugha ya nathari. Usipojizuia na ukaendelea kula rushwa utafungwa. Huko gerezani hakuna ndugu wala mzaha. Tena wenye nguvu hawatambuliwi na nguvu zao ni bure. Yeyote anayekula rushwa hatimaye atajikuta gerezani. 4 x 1 = 4 (e) Sifa nne kuonyesha ni ushairi Limepangika katika beti Lina mishororo minne kwenye ubeti Lina vipande viwili kwenye mshororo Kila mshororo una vina viwili mwishoni mwa vipande (ukwapi na utao) Mshororo wa mwisho umekaririwa (kibwagizo) Lugha iliyotumika ni ya mkato Utoshelezi upo zozote 4 x 1 = 4 (f) Uhuru wa mshairi Inkisari (ufupishaji wa maneno) Mfano sije – msije Aso – asiye Mazida (kurefusha) K.m rushuwa – rushwa Muogopeni – mwogopeni Tabdila k.m. puwani – puani Kuboronga sarufi mfano. Nyingi pesa – pesa nyingi Gereza ziwatia – zitawatia gerezani zozote 2 x 1 = 2 Utohozi – maleba (g) (i) Kupapia – kuendea kitu kwa hamu kubwa (ii) Nikiwaasa – nikiwaonya, nikiwakataza (iii) Inamkonyeza – inamwita/ inatoa ishara ya kuita / inamvuta. 3 x 1 = 3 Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.Bahari 1. Bahari uzuri, wake tawambia, Sifa tabashiri, kuwahadithia, Ambazo ni nzuri, na faida pia. 2. Na faida pia, na kwamba ujue Nakukuelea, nawe utambue, Na sasa sikia, uzifafanue. 3. Uzifafanue, bahari za pambo, Lenye uzuriwe, pia ni urembo, Ni siri ujue, na pia ni tambo. 4. Na pia ni tambo, ni siri yakini, Aidha ni fumbo, haiwezekani, Ina mengi mambo, yenye na thamani. 5. Yenye na thamani, kwa watu wa pwani, Nawapa yakini, nanyi sikizani, Humo baharini, kwanza pulikani. 6. Kwanza Pu1ikani, lulu twaipata, Samaki yakini, faida huleta, Aidha wendani, pia huokota. 7. Pia huokota, ambari zinduna, Munyu na mafuta, vinapatikana, Faida yaleta, pulikiza sana. 8. Pulikiza sana, tia sikioni, Tija ya maana, ilo baharini, Imepatikana, kwa kila ya fani. 9. Kwa kila ya fani, samaki twauza Mapezi yakini, ya papa sikiza, Huleta thamani, yenye muangaza. 10. Yenye muangaza, pia na forodha, Pato huongeza, Ia kuleta fedha, Pia yaangaza, bahari kwa adha. 11. Bahari kwa adha, adhaye upepo, Hapana orodha, na ichafukapo, Huondoka ladha, tena hapo ndipo. 12. Tena hapo ndipo,- chombo hutotoma, Nyote muliopo, hapana msema, Ndipo muliyapo, “Mama, yoo mama!” MASWALI
MAJIBU
(a) Pindu – Kipande cha mwisho cha kituo ndicho kinaanza (ukwapi) katika ubeti unaofuata Tathlitha – mishororo mitatu Ukaraguni – Vina vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine 1 x 2 = 2 Mathnawi – vipande viwili (b) Faida ya bahari Ni pambo ama urembo Ni chanzo cha lulu, samaki, ambari na zinduna Ni chanzo cha fedha samaki wauzwapo Forodha hupatikana kwenye bahari na ni chanzo cha pesa Zozote 2 x 1 = 2 Hasara ya bahari Pepo husababisha usumbufu (kero) wakati bahari inapochafuka Vyombo huzama bahari inapochafuka 2 x 1 = 2 (c) Umbo la shairi Kila ubeti una mishororo mitatu Vipande viwili (ukwapi na utao) Utao unafanywa kuwa ukwapi kwenye beti hizo Kila mshororo una mizani sita sita jumla kumi na mbili kwa beti Vina viwili kwa kila ubeti Ubeti 11 dhe;po ubeti 12 po; ma (alama 4 x 1 = 4) (d) i) Uhuru wa kishairi. Inksari (1) tawambia – nitawaambia Tabashiri – nitabashiri (taja na mfano) (3) uzuriwe – uzuri wake (8) ilo - iliyo Kufinyanga sarufi/kuboronga sarufi; Bahari uzuri wake tawambia badala ya Nitawaambia uzuri wake bahari au uzuri wake bahari nitawaambia Ambari zinduna Ambari na zinduna Lahaja – Pulikeni (lahaja ya kingozi) Tabdila – Sikizani ; Sikizeni zozote 4 x 1 = 4 ii) Ubeti wa tano Iliyo ya maana/umuhimu kwa watu wa pwani, Nawaambia wazi nanyi msikilize. 3 x 1 = 3 Walio baharini wasikize (e) Pulikani - sikilizeni Tija – faida, tijara, manufaa Adhaye – Usumbufu wake/kero zake Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki, Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Wenginea watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago Hadi kwenye wako au, pasipo hata kupesa, walakukupa kisogo Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwato ako tekelezo Tamko lake ‘subutu’, kuondoa tumaini, na kukuliza wazo Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui Hana faida nyumbani, ni mtu akichimbaye, mradi usitumai Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Kwa hakika ni baka, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi, aibarili rowoyo Mipangayo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa Ningetoa azinio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa Ama nitimue mbio, fuadinininanena, akilini nazuiwa Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka. Maswali a) Toa kichwa cha shairi hili (Alama 1) b) Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili (Alama 3) c) Eleza umbo la shairi hili (Alama 4) d) Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari (Alama 4) e) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi hili (Alama 4) f) Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili (Alama 2) g) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyo tumika katika shairi i) Zani ii) Faraghani (Alama 2) Majibu ya ushairi
a) Binadamu hatosheki Tamaa ni hatari (Alama 1) TAMAA b) Mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka Mwenye tamaa ana unafiki / masengenyo Mwenye tamaa anaweza kuua Mwenye tamaa ni mchoyo (hoja zozote 3x1=3) c) Mishororo minne / Tarbia / unne Migao mitatu – ukwapi / utao / mwandamizi Vina vitatu Mizani 8, 8, 8. Kibwagizo Beti sita (hoja zozote 4x1=4) d) Iwapo ukinunua kitu shetani hafurahi bali huwa na chuki. Mtu kama huyo atakasirika moyoni kwa kile ulichokifanya. - Atakuonya ili akuvunje matumaini ya kutekeleza ulichonua. - Mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka (Alama 4) e) Takriri – kibwagizo Tashibihi – hatari kama nyoka Tashihisi – inahadaa Nahau – Kinyesi kimetupiwa kutaja 1 Maelezo 1 (Jumla 2x2=4) f) Inkisari – Ukweliwe, kisu, tajawa, asosema, alo, mpangoyo Tabdila – shaitani (shetani kubadilisha sauti) Mazida sheitani (Kurefush she/ta/ni) (kutaja 1, maelezo 1 jumla 2x1=2) g) Baa – balaa, janga Majivuno, maringo, ujeuri (Alama 1x1=2) Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswaliKwanza matatu muhimu, ni utu uke na ume Pili kwa mwanadamu, awe na kitu atume, Tatu awe na fahamu, ye dini isimhame, Haya ni mambo adhimu, kwa mke na mwanamume, Mambo ye adimu, huyataka kwa. shime. Kwa la kwanza twaanzana, twaendelea kudumu, Na kitu tunaonana, gharama twaweza kimu, Maisha hayani laana, wala hayawi magumu, La tatu shaka halina, humpamba mwenadamu, Kwa fikira na kuoka, mambo yaliyolazimu. Kwa uwezowe Mwenyezi, mdumisha kila kitu, Matatu haya azizi, karibu kwa kila mtu, Yana hawa na mapenzi, katika nafsi zetu, Na katika matembezi, dunia hii yetu, Kuyakasa hatuwezi, na ndiyo utumwa. Ni utumwa madhabuti, hatuwezi kuuvua, Umetushika kifatu, kwa tadi na kwa takua, Katuizi hatujuti, tumo tunachukua, Na nafasi hatujati, kidogo. ya kuumua, Mpaka yaje mauti, uhuru kutuletea. MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini? (alama 2) (b) Taja mambo matatu muhimu ambayo sharti binadamu awe nayo kulingana na Mshairi.(alama 3) (c) Eleza umuhimu wa kila mojawao katika mambo hayo matatu kama yaliyofafanuliwa na mshairi. (alama 6) (d) Taja bahari zmnazojitokeza katika shairi hili. (alama 2) (e) Uandike ubeti wa kwenza katika lugha nathari. (alama 5) (f) Onyesha kwa kutumia namna ambavyo mtunzi ametumia uhuru wa kishairi. (alama 2) SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.Kama wanipenda sana, wangu wamtakiani? Sitaki la kupishana, kama hilo samahani, Penzi watu kupendana, twaingilia nini? Naepuka kupitana, nakusihi kwa hisani, Wanipendani kidada, mke wangu wakuganya. Mke wangu nakuganya, hakuwepo barazani, Vipi mambo wachanganya, si mwizini we kwani, Sije mambo hutafanya, siri tia mvunguni Na bwanako wamfanya, huadhaninuhaini? Kupenda kwa choyo, yoyo halikosekani. Halikosekani yoyo, fikiria mara thani, Waama nakupa onyo, heri tuache utani, Kuzidi ni mtawanyo, nitajiweka pembeni, Lau hutaposa moyo, hubanduka ukumbini, Sidhani unanipenda, mke wangu sitamwacha. Ukimpenda nipende, simkere mhisani, Ukija mweke upande, simfanye kasirani, Kitaka chake kipande, acha inda hadharani, Sema naye umpende, upitie ardhini, Panya huvuvia dada, nyama au punje kila. Maswali a) Toa kichwa mwafaka cha shairi ulilosoma. (alama 1) b) Shairi hili ni la aina gani? Fafanua. (alama 2) c) Eleza ujumbe wa mshairi katika ubeti wa pili. (alama 3) d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4) e) Taja mbinu zozote tatu za lugha katika shairi hili na uzitolee mifano. (alama 3) f) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 5) g) Nakili mloto wa ubeti wa pili kisha ueleze maana yake. (alama 2) majibu
A. - Mke wangu nakuganya / nakukanya - Sitamwacha mke wangu - Mke wangu. 1x1 = 1 B. Takhmisa / utano kwa sababu kila ubeti una mishororo mitano. 2x1 = 2 C. - Anamuonya mpenzi wake asimseme mkewe - Hakuwa walikopendeana na mpenziwe; anaiba pensi - Lazima ahifahdi siri - Kukiwa na wivu katika penzi kutakuwa na uadui. 3x1 = 3 D. Kweli nakuonya tuache mzaha, ukiendelza kuleta shida nitakuacha; lakini huwezi kunishawishi nitoke kwangu. Hata kama wanipenda sitamwacha mke wangu. 4x1 = 4 E) Maswali ya Balagha km Twaingilia nini? Wangu wamtakiani? • Kinaya – ana mpenzi nje lakini anamheshimu mkewe • Takriri – km Mke wangu nakuganya - Halikosekani yoyo - Mke wangu. 3x1 = 3 F) • Shairi lina beti nne • Lina mishororo mitano katika kila ubeti • Vina vya ukwapi vinabadilikabadilika ilhali vya utao vinatiririka (-ni) isipokuwa kimalizio (ukara) • Kituo cha shairi hili ni sabilia / hakirudiwirudiwi • Kila mshororo una mizani 16 (ukwapi 8, utao 8) • Katika ubeti wa pili na wa tatu shairi linadhihirisha sifa za bahari ya pindu (maneno yaliyomalizia ubeti uliotangulia kuanzia ubeti unaofuatia) G) Mloto ni mshororo wa pili katika ubeti k.v. vipi mambo wachanganya, si mwizi ni we kwani – anamwambia asimlaumu mkewe kwa huyu dada kwani ndiye aliyemchukua mumem wa watu. 2x1 = 2 Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Sahiba umenisema, kwa mchana na laili, Munaondoa lazima, muenendo wa kiasili, Kujenga ulipohamaa, mtu huaje aili, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Haiwi mtu mwanawe, na pia usimjali, Ulikataa mwenyewe, kwa ghadhabu na ukali, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Ndipo wewe ushukiwe, ukajifanya mkali, Na sitaki uambiwe, mtu asije kwa hili, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Kwani ulihama, kuhgura hapo mahali, Enenda sinisumbuwe, siniudhi yangu hali, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usukubali, Na hili ujuwe, kwangu hili ni jamali, Siachi ninga kwa mwewe, wala siwezi badili, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Na hapa ndiyo mwishowe, tamati shairi hili, Kaa usinizuzuwe, nasubiri filihali Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Na; Said Karama Maswali (a) Andika kichwa mwafaka cha shairi hili. ( alama 2 ) (b) Mwandishi anadhamiria nini katika shairi hili. ( alama 4 ) (c ) Hili ni shairi la aina gani? Eleza. ( alama 4 ) (d) Ni methali gani inayoafiki maelezo katika ubeti wa kwanza. ( alama 2 ) (e) Ni nini maana ya kifungu “kupewa usikubali, wajataka usipewe.” (alama 2 ) (f) Andika ubeti wa mwisho katika lugha ya nathari. ( alama 4 ) (g) Bianisha maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. ( alama 2 ) (i) Sahiba (ii) Liali majibu
(a) - Kichwa - Kupewa usikubali, wajataka usipewe. ( alama 2 ) - Kadiria majibu ya watahinwa (b) Kuwaonya watu ambao hudharau kitu walichopewa kisha wakihitaji baadaye - Wasiodhamini mahali wanapoishi na kuhama kisha kutaka kurudi. Hoja zilizofafanuliwa 2 x 2 = alama 4 (c ) Aina ya shairi - Tarbia – kila ubeti una mishororo minne. - Ukara – vina vya nje vinafanana na vya ndani vinabadilika badilika. - Shairi pindu – ni mshororo wa mwisho ndio unaoanza ubeti unaofuatia. - Manthnawi – kila mshroro umegawika katika vipande viwili ( zote 4 x 1 = alama 4 ) (d) Methali – Mchana ago haunyeli huenda akarudi papo. - Usiache mbachao kwa msala upitao. Yoyote 1 x 2 = alama 2 (e) Kupewa usikubali, wajataka usipewe. - Ukipewa kasha ukajivuna na kukataa, utakuja wakati usipewe. ( alama 2 ) (f) Utakapotaka kitu – hutapewa kwani ulipopewa ulikataa . Huu ndio mwisho wa shairi hili. Tulia / kaa usinisumbue kwani nangoja / nasubiri kwa vyovyote vile. Ukipewa ukakataa wakati utakapotaka hutapewa. ( alama 4 – kadiria jibu la mtahiniwa ) (g) (i) Sahiba – sababu / rafiki ( 2 x 1 = alama 2 ) (ii) Laili – Usiku Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuataNaujua mwanzo wake, vile ulivyojipuza, Kilofanya mkereke,na kisichowaumiza, Yakuwa sepata mke, katu hakuwapendeza, Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Mwasema matako hana, yako sawa kama meza, Tena pua yako pana, kama ya kubandika, Lakini mimi naona, yenu sitoyazikiza, Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Kipita nae pahali, sakubimbi hubwagiza, Nzitonzitokauli, asengenywazo.Aziza Nywele za kipilipili,hasongi asongomeza Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Munenayo ni mazito,hadi yeye humliza. Bali kwangu ni matoto,muhali kunichukiza. Japo miguuye fito,haitoshi mtembeza? Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Nataka watowa khofu ,kwa munayo mtangaza, Si Yule mpenda pofu,kawambia ni kengeza, Ni mwenyewe nimeshufu ,muhali kunigeuza. Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Tafadhalini mwachie ,musilumbe kumaliza. Unyonge musitumie,kila siku kumaliza. Haya ni yeye na mie,yaaje mukachagiza , Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Hakujiumba mwenyewe, musighafilike wenza, Aloumba mimi nawe,ndiye aliyemtweza, Tusijitie kiwewe,tukakufuru muweza. Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Maswali a)eleza bahari za shairi hili kwa kutoa ithibati kamili. (alama 3) b)kwa kutoa mifano mwafaka ,eleza methali zozozte mbili kwenye shairi. (alama 4) c)bainisha mambo yoyote manne nafsineni anayazungumzia (alama4) d)fafanua idhini ya mshairi(alama4) e)andika ubeti wa tatukatika lugha tutumbi(alama 3) f)eleza maana za vifungu hivi kama vilivyotumika kwenye shairi i)sakubimbi hubwagiza(alama 1) ii)musighafilike wenza(alama 1) MAJIBU
BAHARI ZA SHAIRI -Tarbia-lina mishororo 4 katika ubeti -Mathnawi-Lina pande 2 katika kila mshororo -Ukara-Vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani havitiririki. b) Methali (i)Akipenda, kipofu huita kengeza (ubeti wa tano) -Mwenyewe amekubali alivyo na hawawezi kumgeuza ingawa wanamsengenya. (ii) Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mimi kumbi (ubeti wa saba) -Hakuna aliyejiumba hivyo waache kusema udhaifu wake. iii) Pilipili usioila yakuashani? (ubeti wa 6 mstari wa 3) (zozote 2x2=4) c)Maudhui -Msimulizi anampenda vile alivyo-mwenyewe amemkubali -Wanakerwa kwani hawana mke -Wanayoyasema hayawahusu wao bali ni kati yake nay eye -Anayezungumziwa hakujiumba mwenyewe bali ni mungu (muumba) -Anawaambia wasitumie udhaifu wake kumsengenya -Ingawa wanayoyasema yanamliza Aziza, yeye hajali. -Waduku wanatahadharishwa wasikufuru d) Uhuru/idini ya mshairi -Tabdila k.m. nae –naye -Mutafanya- mtafanya -Nampenda- ninampenda -Kuboronga sarufu k.m.- Hadi yeye humliza – hadi humliza yeye -Lahaja k.m naujuwa –naujua -Khofu-hofu (zozote 2x2=4) e)Lugha nathari /tutumbi -Nikipita naye popote wadaku/wafitini wanamsengenya Asiza na maneno mazito k.m kuwa hatengenezi nywele. Semeni tu mtasita (au mtaacha) mjue mimi ninampenda alivyo) (3x1=3) Msimulizi anasema kuwa akienda na aziza popote wadaku wanatoa maneno mazito ya kumsengenya k.m hatengenezi nywele. Anawaeleza waendelee tu bali yeye anampenda alivyo. (3x1=3) F). (i)Sakubimbi hubwagiza- wadaku (wasengenyaji hutupa maneno ovyo). (ii) Musighafilike wenza- msiumie/msighadhabike Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswaliHukuja hapa kwa vingi, Vitimbi vya kila namna, Kanambia nikuruzuku, Kimwana awe mwenzio, Hukumtwaa mwananngu, Kisema mno walavu, Vipi wamgeuza ngoma, Mapepo wampigia? Siwe uloandaa, Harusi ya kukata na shoka Masafu ya magari, yakilalama jua kali, Hadi kanisani kungia, mimbari we kusimama Kasema utamuenzi, hadi yenu mauko? Vipi jicho lageukia, mitaani vipaa mwitu? Hukunambia we fidhuli, Mwanangu utamtunza? Taandamana naye daima, Ja chanda na pete? Hukumwonjesha tamu, ya ulaghai huyuno? Midisko wampeleka, kisingizia mapenzi Vipi wamtezea shere. Mwanangu kumliza? Lini taacha dhuluma hizino humfanyiazo, Tachukua lini majukumu Ya kumlea na vifaranga? Huachi kulia u waya. Wanao kitelekeza Nadhiri zako zako za nitakipu promise, Zi wapi mwana balaa? Lini tafumbua maozi, uone huyu nduli, Alotwala wengi wapendi, Kwa jicho la nje kuwangia, Imeanguka miamba mingapi, nayo ng’ang’ania kufia dondani, Zinduka mwana zinduka, Ailaya waangamiza. Maswali (a) Hili ni aina gani ya shairi. Fafanua (alama 4) (b) Mwandishi anaibua maswala kadhaa ya kijamii. Yaandike. (alama 3) (c) Eleza matumizi ya uhuru wa kishairi katika utungo huu. (alama4) (d) Eleza mbinu ya fasihi iliyotumika katika utungo huu. (alama 3) (e) Bainisha matumizi ya: (alama 4) (i) mistari mishata (ii) mistari kifu (f) Ni nini maana ya vifungu vifuatavyo kama ilivyotumiwa kwenye kifungu? (alama 2) (i) vipaa mwitu (ii) kufia kidondani MAJIBU
(a) Hili ni aina gani ya shairi. Fafanua (alama 4) - halizingatii kulingana kwa mistari katika kila ubeti -idadi ya vipande hailingani katika kila mstari -halizingatii mpangilio maalum wa vina -halizingatii ulinganifu wa mizani katika kila mstari. (b) Mwandishi anaibua maswala kadhaa ya kijamii. Yaandike. (alama 3) -dhuluma katika ndoa - ulaghai katika ndoa -haki za watoto -ukosefu wa uaminifu katika ndoa -kutowajibika kwa waume -tatizo la ukimwi (c) Eleza matumizi ya uhuru wa kishairi katika utungo huu. (alama4) (i) kufinyanga sarufi - hadi kanisani kuingia- yakaingia hadi kanisani -hadi yenu mauko-hadi mauko yenu -mwanangu kumliza-kumliz mwanangu (ii) inkisari -kanambia-ukaniambia taacha-utaacha kisema-ukisema we-wewe -kungia- kuingia tachukua-utachukua wanao-wana wao (iii) mazida - Huyuno-huyu (iv) tabdila -twala-twaa wapendi- wpenzi (v) lahaja -wamtezea- wamchezea (vi) kikale/msamiati wa kale -maozi-macho (d) Eleza mbinu ya fasihi iliyotumika katika utungo huu. (alama 3) (i) maswali ya balagha -hukijahpa kwa vingi? -vipi wamtezea shere, mwanangu kumuuliza? (ii) tashbihi -taandama naye daima ja chanda na pete (iii) utohozi -walavu -midisko -nitakipu promise (iv) sitiari/istiari -vipaa mwitu-wasichana wengine vifaranga watoto -nduli-ugonjwa hatari miamba- watu mashuhuri (vi) tashhisi/uhuishaji -masafa ya magari yakilalama jua kali (vii) nahau - kufia kidondani - kupata hasara unapofuata kitu unachokiona ni cha thamani (viii) msemo -u waya- huna pesa/umefilisika (e) Bainisha matumizi ya: (alama 4) (i) mistari mishata -hukuja hapa kwa vingi -siwe uloandaa -kanambia nikuruzuku (ii) mistari kifu/mistari kamilifu -kasema utamuenzi hadi yenu mauko -vipi jicho lageukia mitaani vipaa mwitu -huachi kulia u waya (f) Ni nini maana ya vifungu vifuatavyo kama ilivyotumiwa kwenye kifungu? (alama 2) (I) vipaa mwitu – wasichana wengine (ii) kufia kidondani - kupata hasara unapofuata kitu unachokiona ni cha thamani Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayoNyoosha mkono, uviringe ngumi, unyanyuwe kwa hasira. Nyoosha mkono, sema hunitumi, ila haki ujira. Nyoosha mkono, alama ya kukataa. Alama ya nguvu Nyoosha mkono, na macho makali, uwaonyeshe kukerwa Nyoosha mkono , wataka halali , kwamba hutaki kuporwa Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, umekula njama, uyakatae madhila Nyoosha mkono, nyanyua kwa hima, watambue hukulala Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, jiunge umoja, na wateswaji wenzako Nyoosha mkono, mwonyeshe miuja, yaondoke masumbuko Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, ivume sauti, inayojaa kitisho Nyoosha mkono, mumejizatiti kwa mengi maamrisho Nyoosha mkono,alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, mumeshikamana, huo ukuta wa chuma Nyoosha mkono, kitisho hakuna , wao watarudi nyuma Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Maswali a) Bainisha bahari tatu zinazojitokeza katika shairi.(alama 3) b) Andika ujumbe mkuu unaojitokeza katika shairi hili.(alama 4) c) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4) d) Onyesha tamathali mbili za lugha zilizotumiwa. (alama 2) e) Bainisha kwa njia tatu ni vipi mtunzi amefanikiwa kutumia uhuru wa kishairi .(alama 3) f) Tambua toni ya shairi hili (alama 1) g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili. (alama 2) i) Madhila ii) Jizatiti MAJIBU
a) Ukawafi – Mishororo ya kwanza mitatu ina vipande vitatu Msuko- Kibwagigo ni kifupi Tarbia – Mishororo minne kila ubeti Ukaraguni – Vina vinavyoftofautiana Kikwamba kianzio nyoosha mkono b) Msimamo dhabiti katika utetezi wa haki, kataa kudhulimiwa na uungane na wenzako, lazima uwe na usajiri. 2x2 =4 c) Inuka kwa ujasiri kama ishara ya kutoridhika kwa sababu unadai haki yako kwa njia halali. - Simama imara na ukatae kudhulumiwa na utashinda. 4x1 alama 4 d) Taswira – nyooosha mkono -Misemo - Kula njama- - Uhuishi/ tashihisi – Sauti inayojaa kitisho. Inksari jiunge – ujiunge e) Lahaja – Mangi,- Kuboronga- yaondoke masumbuko, masumboko yaondoke f) Toni ya – kutoridhika/kulalamika kuhamasisha/kuzindua. (alama 2) g) i) Mateso, taabu ii) JIkaze/ Jikakamue/Jitolee/Kujibiidisha. 2x1= alama 2 Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali1. Mbiu naipuliza, kwawa hapana ng’ambo, Kwa aningoja ‘mesikia, inaumiza matumbo, Kwa upole sitafyoa, hata kamna kwa kimombo, Yafaa jihadharia, maisha ya s’ende kombo. 2. Maisha ya s’ende kombo, kututoa yetu ari, Zingatia haya mambo, wetu wale zimukiri, Kuwa wana kwa viambo, huwa Baraka na kheri watunzeni na maumbo, msie zusha hatari. 3. Msije zusha hatari, na nyingi hizi zahama, Wazazi haya si siri, mawi mnayoandama Twaelezea kwa uzuri, matendoyo yatuuma Watoto tunayo mori, ni lini mtaja koma? 4. Ni lini mtaja koma, na pombe siso halali? Sio baba sio mama, mbona ny’ hamtajali? Mwafa ja nzi twasema, mwatua chabi la hali Hangaiko acha nyuma, kwani hamuoni hili? 5. Kwani hamuoni hili, kila saa mwapigana Nyumbanizo hatulali, jehanamu tumeona Mwatusumbua akili, twaumia ten asana Achene na ukatili, kwani upendo hamna. 6. Kwani upendo hamna, kamam mbwa mwatuchapa Mwatuchoma sisi wana, mio yetu yatupapa Pa kujificha hatuna, tumebaki tukitapa 7. Tumevujwa na mifupa, hata leo uke wetu, Mwatubaka na kuapa, kutung’ata nyi’ majitu, Hayo makeke na pupa, mtakoma utukufu 8. Mtakoma utukufu, nakutumia miki Na tabia zenye kutu, tumechoka nayo chuki Hatutakubali katu, kutendewa yenye siki Serikali fanya kitu, kwani nasi tuna haki Maswali a) Fafanua tamathali nne za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 2) b) Taja nafsi nne katika shairi hili. (alama 1) c) Eleza bahari mbili zinaowakilishwa katika shairi hili. (alama 4) d) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari. (alama 4) e) Eleza maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 3) f) Eleza umuhimu wa mbinu mbili amabazo mshairi ammetumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 4) MAJIBU YA SHAIRI
a) Maswali balagha- na pombe siso halali? Mbona ny’ hamtajali. Isitiari- kutang’ata nyi majitu Tashbihi- kama mbwa mwatuchapa Mwafa ja nzi. (zozote 1x4) b) Mtoto (mwana) c) Lina mishororo mine hiyo ni Tarbia. Kina cha kubwagiza kimechukuliwa ili kuwa mwanzo wa ubeti unaofuata hivyo huitwa pindu au mkuju/nyoka.(zozote 1x2) d) Nilini wazazi wataacha kutumia pombe haramu na kuwajali watoto wao kwani wanakunywa na kuwaachia mateso na mahangaiko mengi bila kujali. (alama 4) e) Ukatili, malezi, ulevi. Mwanafunzi aeleze ipasavyo. (alama 3) f) Mazida –mshairi amerufusha baadhi ya … ili kuafikia urari wa k.m. nyumbanizo, matendoyo Liksani- mshairi amefupisha baadhi ya maneno pia kuafiki urari wa viua- mio, ny’ Kuburanga sarufi- kwani upendo kamua badala ya kwani hamna upendo-ili kuleta urari wa viua katika mishororo. (mwanafunzi ataje mbili na kueleza.( zozote alama 2x2 SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.Msambe naja kuteta, nina wema wa kalima, Moto wanikatakata, maini yangu yachoma, Ili nipate takata, ukweli wote ‘tasema, Anayekataa pema, pabaya panamuita. Bahati ni kama nyota, humemeta na Kuzima, Sikimbilie mafuta, ukatae Kula sima, Anayekataa pema, pabaya Panamuita. Haraka zina matata, angaza mbele na Nyuma, Tenda mambo kwa kusita, Usije ukalalama, Keti pako ukipata, Kwa muradi wa uzima, Anayekataa Pema, pabaya panamuita. Pema si penye mafuta, au pa wali Na nyama, Pema watu hutafuta, Utulivu na hekima, Si hoja penye Ukata, pa watu hali ya nyuma, Anayekataa pema, pabaya Panamuita Mahali pema ambata, kwa vitendo na huduma, Sikae penye matata, palipojaa hasma, Lau kama pamemeta, hapafai kwa daima, Anayekataa pema, pabaya panamuita Maswali a) Lipe anwani mwafaka shairi hili. (alama 1) b) Bainisha bahari mbili za shairi hili. (alama 2) c) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4) d) Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 1) e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4) f) Onyesha jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake. (alama 3) g) Kwa kutoa mifano, bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2) h) Eleza maana ya msamiati ufuatao. (alama 3) i) Kalima ii) Mafuta iii) Ukata Majibu
a) Lipe anwani mwafaka shairi hili (al 1) Anayekataa pema, pabaya pamuita b) Bahari mbili za shairi hili (al 2) i) sakarani ii) Masivina – halina urari wowote wa vina c) Muundo wa shairi hili (al 4) - Beti nne - Lina kibwagizo ‘Anayekataa pema, pabaya pamuita’. - Halijazingatia mtoshelezo wa mishororo ktk kila ubeti - Halina urari wa vina d) Dhamira ya shairi ni kuhimiza kuhusu umuhimu wa uadilifu na mienendo inayofaa. (al 1) hakiki e) Mahali pema si pale ambapo pana vizuri bali palipo na utulivu na hekima. Hata kama pana umaskini, mtu anapokataa mahali pema huitwa na pabaya. (al 4) f) (i) Inkisan - Tasema - sikimbilie (ii) Msamiati wa kale- mato badala ya macho (iii) Kuboronga sarufi – keti pako ukipata (iv) Tabdila – muradi (zozote 3) g) Tamathali mbili za usemi (al 2) Tashbihi – Bahati ni kama nyota. Jazanda - mafuta, wali na nyama zimetumika kijazanda (zozote 2) h) Maana ya (i) Kalima – usemi (ii) Mafuta – mng’aro (iii) Ukata - umaskini Soma shairi hili kisha ujibu maswali:Jukwaninaingia, hukuhapapasokota, Kwauchunguninalia, hiitumbonitaikata, Msibamejiletea, nimekilakisotakata, We tumbonitakupani, uweumetosheka? Wazeehatavijana,woteumewasubua, Hurumanaohauna, heshimakawakosea, UkambaninaSagana, hatambwawararua, We tumbonitakupani, uweumetosheka? Wahasibuofisini,kibwebwemejifunga, Miakamingivitabuni, iliwasikoseunga, Nadhariwanadhamini, hesabuwanazirenga, We tumbonitakupani, uweumetosheka? Wapenziwakiholela, piawanakuogopa, Baadayaokulala, wanawaowanatupa, Wakihitajichakula, wanachokoramapipa, We tumbonitakupani, uweumetosheka? Wafugaji hatanao, kamadawawakwamini, Hawajalijiranio, wamesusiaamani, Wanaibang'ombewao, nakuzua kisirani, We tumbo nitakupani, uweu metosheka? Nayomizozoyamaji, kaonekanakwamara, Hiyonayo ni dibaji, sababusioharara, Njaa wahepe wenyeji, huondiomkarara, Wetu mboni takupani, uweumetosheka? Ningeweza kukuuza, ingekuwa siku njema, Tena kwa bei ya meza, sokoni nimesimama, Wala tena singewaza, kuhusu wali na sima, We tumbo nitakupani, uwe umetosheka? Hatima umefikika, naenda zangu nikale, Mate yanidondoka, kwamnukiowa wale, Naomba kwenda kukaa, wala sioni kalale, We tumboni takupani, uw eumetosheka? Maswali (i) Lipe anwani mwafaka shairi hili. (alama 2) (ii) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (alama 2) (iii) Eleza umbo la shairi hili. (alama 4) (iv) Andika ubeti wane kwa lugha nathari. (alama 4) (v) Thibitisha kuwepo kwa uhuru wa kishairi. (alama 2) (vi) Taja madhila anayoelezea mtunzi wa shairi hili yaletwayo n atumbo. (alama 4) (vii) Elezea maana ya maneno yafuatayo. (alama 2) (a) Dibaji (b) Harara MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
8.ushairi (i) Tumbo lisilotosheka/matatizo ya tumbo (1 x 2) (ii) Tarbia – mishororo mine 1 – Kutaja (2) 1 – Kueleza (iii) umbo Mishororo mine katika kila ubeti Vina vya kati ni, nga Vipande viwili katika kila mshororo– ukwapi na utao Kibwagizo-we tumbo nitakupani,uwe umetosheka ? Mizani kumi na sita katika mshororo– ukwapi (8) utao (8) (4 x 1) (iv) Lugha nathari Wapendanao mapenzi yasiyo na dhati wanakuogopa. Wapatao mimba, watoto wao hawajali. Watoto watakapo chakula huwa wanatafuta mapipani. Tumbo nikupe nini ili utosheke? (4×1) (v) uhuru wa mshairi. Inkisari mf. We – wewe nitakupani Kuboronga sarufi mf.Wafugaji hata nao – Hata nao wafugaji. Tabdila mf.Umewasubua – umewasumbua. Mazida mf. Mnukio – mnuko (2 x 1) (vi) Kukcsa heshima – hata mbwa wararua. Ufisadi – hesabu wanazirenga. Kutowajibikia wana – wanachokora mapipa. Wizi – wa ng’ombe. Mizozo/kutoelewana – mradi waliepe njaa. (4 x 1) (vii)Dibaji – Thibitisha/shalali. Harara – hasira/hamaki (2 x 1) Soma shairi hili kisha ujibu maswali:Angawa mdogo, dagaa, amekomaa Kaanga kidogo, dagaa, atakufaa Kalia kinaya, dagaa, h’ondoa njaa Wa kwako udogo, kijana, sio balaa Na sio mzigo, kijana, bado wafaa Toka kwa mtego, kijana, sinyanyapaa Nasaha kidogo, kijana, ukubwa jaa Jikaze kimbogo, kijana, acha kukaa Chimbua mhogo, kijana, usibung’aa Na wake udogo, dagaa, ndani hukaa, Kuliko vigogo, dagaa, hajambaa Hapati kipigo, dagaa, hauna fazaa Maisha si mwigo, kijana ushike taa Sihofu magego, kijana, nawe wafaa Kazana kidogo, kijana, kugaaga Maswali (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka (alama 1) (b) Eleza arudhi zilizofuatwa katika kutunga shairi hili (alama 4) (c) Onyesha jinsi malenga alivyotumia uhuru wake (alama 3) (d) Tambua bahari katika shairi hili (alama 3) (e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari (alama 4) (f) Tambua mbinu za lugha zilizotumika katika shairi (alama 3) (g) Eleza toni la shairi hili (alama 2) MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KISW PPR 3 F3 1. (a) Dagaa au Kijana (1 x 2) (b) Kuna urari wa vina − Lina beti tano − Mishororo mitatu katika kila ubeti − Lina pande tatu katika kila mshororo (4 x 1) (c) Matumizi ya lahaja mf. Magego – Meno Inkisari – h’ondoa – huondoa Kuburoga sarufi – Na wake udogo – Na udogo wake (3 x 1) (d) Ukara – Vina vya utao na mwandamizi havitiririki, vya ukwapi vinatiririka. Ukawafi – Pande tatu (2 x 1) (e) Kijana nakupa mawaidha ya kwamba aliye cheoni kuhusishwa na makosa yote, kwa hivyo tia bidii afanyavyo mbogo uache kukaa. Chimbua mihogo utafute riziki (al. 4) (f) Istiari / jazanda mf Jikaze kimbogo Methali – mf ukubwa jaa Msemo mf shika taa (kuwa mwangaza) taja na kutoa mfano (3 x 1) (g) Toni ya matumaini Toni ya kuhimiza Toni ya kuonya (1 x 2) Soma shairi hili kisha ujibu maswali:1. Nikiwa na njaa na matambara mwilini Nimehudumika kama hayawani Kupigwa na kutukanwa Kimya kama kupita kwa shetani Nafasi ya kupumzika hakuna Ya kulala hakuna Ya kuwaza hakuna Basi kwani hili kufanyika Ni kosa gani lilotendeka Liloniletea adhabu hii isomalizika? 2. Ewe mwewe urukaye juu angani Wajua lililomo mwangu moyoni Niambie pale mipunga inapopepea Ikatema miale ya jua Mamangu bado angali amesimama akinisubiri? Je, nadhari hujitokeza usoni Ikielekea huku kizuizini? 3. Mpenzi mama, nitarudi nyumbani Nitarudi hata kama ni kifoni Hata kama maiti yangu imekatikakatika Vipande elfu, elfu kumi Nitarudi nyumbani Nikipenya kwenye ukuta huu Nikipitia mwingine kama shetani Nitarudi mpenzi mama... Hata kama kifoni. Maswali a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka (alama 1) b) Tambua nafsineni katika shairi hili (alama 1) c) Eleza toni katika shairi hili (alama 1) d) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia (alama 4) e) Fafanua dhamira katika shairi hili (alama 2) f) Thibitisha kuwa hili ni shairi huru (alama 4) g) Taja na ufafanue sifa mbili za mshairi (alama 2) h) Fafanua mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika ubeti wa tatu. (alama 3) i) Eleza maana ya maneno yafuatoyo kama yalivyotumiwa katika shiari hili (alama 2) i) Hayawani ii) Nadhari MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
5. (a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka (alama 1) i. Mama nitarudi ii. Nitarudi iii. Kizuizini alama 1 (asizidishe maneno sita) (b) Tambua nafsineni katika shairi hili (alama 1) Nafsineni ni aliye kizuizini. Anauliza iwapo mamake angali anasimama na kusubiri akitazama kule kizuizini aliko nafsineni (atambue na athibitishe alama 1/0) (c) Eleza toni katika shairi hili (alama 1) i. Toni ya masikitiko / uchungu wa moyoni/huzuni kwa mfano, anasikitikia hali yake ya kuvaa matambara, njaa, kufanyiswha kazi tele ii. Toni ya matumaini kwa mfano, mshairi ana matumaini kwamba siku moja atatoka kizuizini (atambue na athibitishe alama 1/0) (d) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia (alama 4) i. Kuachwa njaa ii. Kufungwa iii. Kufukuzwa iv. Kutopewa nafasi ya kupumzika, kulala na kuwaza v. Kuvaa matambara vi. Kufanyizwa kazi kama mnyama (Zozote 4 x 1 = 4) (a) Fafanua dhamira katika shairi hili (alama 2) i. Mshairi anadhamiria kulalamikia/kukashifu namna anatumiwa vibaya kizuizini ii. Mshairi anakashifu madhila na mateso ambayo wafungwa hutendewa iii. Kumpa mamake matumaini kwamba atatoka kizuizini siku moja (Zozote 2 x 1 = 2) (b) Thibitisha kuwa hili ni shairi huru (alama 4) i. Kuna matumizi ya mistari mishata ii. Idadi ya mishororo inabadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi nyingine iii. Silabi za mwisho katika kila mshororo zinatofautiana iv. Idadi ya mizani katika kila mshororo inatofautiana (Zozote 4 x 1 = 4) (c) Taja na ufafanue sifa mbili za mshairi (alama 2) i. Ni mwenye kulalamika kwa mfano, analalamikia hali yake ya kuwa na njaa, kupigwa ii. Mwenye matumaini kwa mfano, anatumai kuwa siku moja atatoka kizuizini iii. Mwenye mapenzi kwa mfano, anampenda mamake na kumwita mama mpenzi (Zozote 2 x 2 = 4) kila sifa itolewe mfano - atuzwe 2/0 (d) Fafanua mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika ubeti wa tatu. (alama 3) i. Takriri kwa mfano, neno nitarudi limerudiwarudiwa ii. Mdokezo kwa mfano, nitarudi mama mpenzi iii. Tashibihi kwa mfano, kupitia mwingine kama shetani iv. Balagha kwa mfano, Ni kosa gani lilotendeka - Liloniletea adhabu hii isomalizika? (Za kwanza 3 x 1 = 3) (e) Eleza maana ya maneno yafuatoyo kama yalivyotumiwa katika shiari hili (alama 2) i) Hayawani - mnyama ii) Nadhari - fikira (Za kwanza 2 x 1 = 1) Soma shairi hili kisha ujibu maswali:Wanaume ni Wanyama Nakumbuka vyema sana, sisahau siku ile Nilipoitwa na nina, akanipa ya kivyele Mwanangu u msichana, nakuasa usikile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Kuwa umevunja ungo, ni hali ya maumbile Bora uwapo na bongo, anasa uzikimbile, Ukijitia maringo, utatungwa mimba mbele Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Ngawa waje na manoti, “Nakupenda” wakwambile Wakuvalie makoti, usiwaachie mbele Hata wapige magoti, wambile mna kelele Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Ngono ni tendo la suna, Amina sikimbile Wala miguu halina, kwamba lingekukimbile Muhimu kwako Amina, kwanza uthamini shule Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Kuzurura mitaani, si tabia njema ile Unapotoka nyumbani, fululiza hadi shule Si kwenda vichochoroni, kuwaona kina wale Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Uwe mwana msikizi, yano uyazingatile Mengine kuhusu penzi, mwanangu taonywa shule Kama mameyo mzazi, nimekuonya kimbile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama Wakaja kina Hamadi, mwana wa Mzee Sule Kwangu wakapiga hodi, hata mkuu wa shule Ila nikajitahidi, kukwepa mitego ile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Na kuna Karisa, mwanafunzi kule shule Akawa hunipapasa, name pia vilevile Mwishowe itakupasa, tugawe tunda tulile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Nani akachovya uto, wa asali tamu vile Na kisha aape kuto, kula asali milele Kuwa mjamzito, wamenifukuza shule Si waone vile, wanaume ni wanyama. Karisa yu vilevile, angali ywaenda shule Na mie kitumbo mbele, ninajikuna upele Yameshatumia yale, niloonywa siku ile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Maswali: (a) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2) (b) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2) (c) Bainsha mambo manne ambayo nafsineni anatoa kama ushauri kwa nafsinenewa. (alama 4) (d) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo ambapo mshairi ametumia kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 3) (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (alama 3) (f) Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4) (g) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2) majibu
(a) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2) i. Ni tarbia (alama 1) ii. Lina mishororo minne katika kila ubeti (alama 1) (b) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
(c) Bainsha mambo manne ambayo nafsineni anatoa kama ushauri kwa nafsinenewa.(alama 4)
(a) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo ambapo mshairi ametumia kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 3)
(b) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (alama 3)
ii. Kuzurura mitaani, si tabia njema ile – ile tabia ya kuzurura mitaani si njema (Za kwanza 3 x 1 = 3) (c) Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4)
(d) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2) Mama yake mshauriwa kwa mfano, mamayo mzazi, nakuonya ukimbile Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.Ndimi Chesirwo, kijana barubaru, Ndume na gwiji, la ukoo mtukufu, Najivunia umahiri, kusakata kandanda. Tazama umbo langu, guu mithili ya jokovu, Kifua cha miraba, weusi wa kijungu, Wenzangu wanienzi, na hata kuduwaa. Misuli ni tinginya, Kijijini nasifika, Wazee kunienzi, Mabinti kunikabidhi. Maswali (a) Tambua utungo huu na uthibitishe jibu lako. (alama 2) (b) Kwa kurejelea hoja zozote nane, jadili sifa za utungo uliotambua katika (a) (alama 8) (c) (i) Eleza maana ya maghani. (alama 1) (ii) Taja na ueleze tofauti za aina mbili za maghani. (alama 4) (d) Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5) majibu
a) Tambua utungo huu na udhibitishe jawabu lako. (Alama 2) Majigambo/vivugo- mwandishi anajisifu kwa umahiri wake binafsi. Kutaja alama 1 kudhibitisha alama 1 b) Kwa kurejelea hoja zozote nane, jadili sifa za utungo uliotambua kwenye swali la (a). (alama 8) Sifa za majigambo 1. Hutungwa na kuganwa na muhusika mwenyewe. 2. Hutungwa kwa usanii mkubwa. Anayejigamba hutumia mitindo tofauti au ishara. 3. Mwenye kujigamba - hujitungia kivugo kufuatia tukio lililowah kuitokea maishani mwake. 4. Mara nyingi majigambo hutungwa na kuganwa na wanaume. 5. Husheheni matumizi ya chuku. 6. Hutolewa kwa nafsi ya kwanza. 7. Anayejigamba huweza kubeba baadhi ya vifaa vyake vya kazi au vinavyoonyesha jambo analojisifia. 8. Majigambo yanaweza kutungwa papo kwa hapo. 9. Anayejigamba huweza kutaja usuli wake wa kinasaba. Anaweza kusifu ukoo wake 10. Anayejigamba huwa mlumbi. 11. Maudhui makuu katika majigambo huwa ushujaa. (Akikosa (a) , atuzwe 0 katika (b) – Z a kwanza 8 x 1 = 8 athibitishe dai) c) i. Maghani ni nini? (Alama 1) Maghani ni ushairi ambao hutolewa kwa kalima badala ya kuimbwa. 1 x 1 = 01 ii. Taja na ueleze tofauti za aina mbili za maghani unazojua. (Alama 4) maghani ya kawaida- tungo za mashairi yenye hubeba masuala ya kawaida; mfano, njaa, mapenzi, elimu nk. Maghani simulizi: mashiri ya kihadithi ambayo husimulia sifa za mtu ,mnyama, kitu, historia au tukio fulani. Kutaja – alama 2, kutofautisha 2/0 d) Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (Alama 5) 1. Tamasha za kimziki. Wanafunzi hukariri, hugana na kuimba mashairi katika tamasha za muziki 2. Sherehe za harusi, jando, mazishi na matambiko bado zinaendelezwa na jamii ya sasa. 3. Utungaji na utegaji wa vitendawili kupitia redio na runinga. 4. Michezo ya kuigiza katika runinga na redio. 5. Tamasha za drama hihifadhi utanzu wa maigizo,mazungumzo na ushairi simulizi. 6. Sarakasi za wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho. 7. Ngoma za kienyeji huchezwa kwenye hafla kama vile harusi au mikutano ya kisiasa. 8. Wapo watafiti ambao huandika na kuhifadhi rekodi za vipera vya fasihi simulizi. 9. Utambaji wa hadithi hutambwa na jamii nyingi za kisasa hasa sehemu za mashambani. ( Zozote 5 x 1 = 05) Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. |
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |