Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Sahiba umenisema, kwa mchana na laili, Munaondoa lazima, muenendo wa kiasili, Kujenga ulipohamaa, mtu huaje aili, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Haiwi mtu mwanawe, na pia usimjali, Ulikataa mwenyewe, kwa ghadhabu na ukali, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Ndipo wewe ushukiwe, ukajifanya mkali, Na sitaki uambiwe, mtu asije kwa hili, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Kwani ulihama, kuhgura hapo mahali, Enenda sinisumbuwe, siniudhi yangu hali, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usukubali, Na hili ujuwe, kwangu hili ni jamali, Siachi ninga kwa mwewe, wala siwezi badili, Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Wajataka usipewe, kupewa usikubali, Na hapa ndiyo mwishowe, tamati shairi hili, Kaa usinizuzuwe, nasubiri filihali Kupewa usikubali, wajataka usipewe. Na; Said Karama Maswali (a) Andika kichwa mwafaka cha shairi hili. ( alama 2 ) (b) Mwandishi anadhamiria nini katika shairi hili. ( alama 4 ) (c ) Hili ni shairi la aina gani? Eleza. ( alama 4 ) (d) Ni methali gani inayoafiki maelezo katika ubeti wa kwanza. ( alama 2 ) (e) Ni nini maana ya kifungu “kupewa usikubali, wajataka usipewe.” (alama 2 ) (f) Andika ubeti wa mwisho katika lugha ya nathari. ( alama 4 ) (g) Bianisha maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. ( alama 2 ) (i) Sahiba (ii) Liali majibu
(a) - Kichwa - Kupewa usikubali, wajataka usipewe. ( alama 2 ) - Kadiria majibu ya watahinwa (b) Kuwaonya watu ambao hudharau kitu walichopewa kisha wakihitaji baadaye - Wasiodhamini mahali wanapoishi na kuhama kisha kutaka kurudi. Hoja zilizofafanuliwa 2 x 2 = alama 4 (c ) Aina ya shairi - Tarbia – kila ubeti una mishororo minne. - Ukara – vina vya nje vinafanana na vya ndani vinabadilika badilika. - Shairi pindu – ni mshororo wa mwisho ndio unaoanza ubeti unaofuatia. - Manthnawi – kila mshroro umegawika katika vipande viwili ( zote 4 x 1 = alama 4 ) (d) Methali – Mchana ago haunyeli huenda akarudi papo. - Usiache mbachao kwa msala upitao. Yoyote 1 x 2 = alama 2 (e) Kupewa usikubali, wajataka usipewe. - Ukipewa kasha ukajivuna na kukataa, utakuja wakati usipewe. ( alama 2 ) (f) Utakapotaka kitu – hutapewa kwani ulipopewa ulikataa . Huu ndio mwisho wa shairi hili. Tulia / kaa usinisumbue kwani nangoja / nasubiri kwa vyovyote vile. Ukipewa ukakataa wakati utakapotaka hutapewa. ( alama 4 – kadiria jibu la mtahiniwa ) (g) (i) Sahiba – sababu / rafiki ( 2 x 1 = alama 2 ) (ii) Laili – Usiku
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |