Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatayo.Una moyo gani, ninakuuliza, wangu muhisani? Na kiasi gani, unavyojiweza, ijapo tufani? Ukiwa laini, utajipoteza, usijaribaini, Kusimama pweke kwataka makini. Zitavuma pepo, zitakupuliza, uanguke chini, Ela uwe papo, unajikweleza, na kujiamini, Utikishapo, umejiumiza, pigo la moyoni, Kusimama pweke kwataka makini. Utie migati, ya kukuoteza, hapo ardhini, Kwa nia na dhati, usiogeuza, au kuihuni, Zidata baruti, uwe wapwiza, weleke usoni, Kusimama pweke kwataka makini. Sishike vishindo, na mauzauza, ya kukuzaini, Kita kama nyundo, ukiniuliza, unayoamini, Na uje mkondo, utadidimiza, kujipa mizani, Kusimama pweke kwataka makini. Wengine wasiwe unaoweleza, yaliyo maani, Wewe ndiwe wewe, utawageuza, pindipo mwakani, Ela jichukuwe, pia kujikaza, katika midani, Kusimama pweke kwataka makini. Maswali
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |