Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili Vitisho pamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili. Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili. Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili Sihofu kupata mawi, sitajua, kupigania mwili Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili. Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili. Maswali
Majibu ya Ushairi
(a) Ukawafi Tathlitha Ukara (3x1) (b) Anaonyesha vile mfanyakazi mwenye bidii ambaye anaugua na kushindwa kufanya kazi. (1x2) (c) Lina mishororo mitatu kila ubeti Lina beti tano Kila mshororo umegawa vipande vitatu Vina vya kati havifanani lakini vya mwisho vinafanana. Lina silabi hizi 8,4,7 (4x1) (d) Inkisari – ngeushuruti Tabdila - Utimile Kufinyanga lugha - lakini kamwe haiwi. Zozote (2x2) (e) Magonjwa Kazi Bidii Dhuluma kutoka kwa waajiri. (3x1) (f) Ningetaka kufika leo lakini mwili una maumivu. Niweze kufanya kazi lakini mwili unakataa. Ningependa kuwa mmoja wanaohusika lakini mwili umeshindwa. ( 4x1)
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |