SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.Kama wanipenda sana, wangu wamtakiani? Sitaki la kupishana, kama hilo samahani, Penzi watu kupendana, twaingilia nini? Naepuka kupitana, nakusihi kwa hisani, Wanipendani kidada, mke wangu wakuganya. Mke wangu nakuganya, hakuwepo barazani, Vipi mambo wachanganya, si mwizini we kwani, Sije mambo hutafanya, siri tia mvunguni Na bwanako wamfanya, huadhaninuhaini? Kupenda kwa choyo, yoyo halikosekani. Halikosekani yoyo, fikiria mara thani, Waama nakupa onyo, heri tuache utani, Kuzidi ni mtawanyo, nitajiweka pembeni, Lau hutaposa moyo, hubanduka ukumbini, Sidhani unanipenda, mke wangu sitamwacha. Ukimpenda nipende, simkere mhisani, Ukija mweke upande, simfanye kasirani, Kitaka chake kipande, acha inda hadharani, Sema naye umpende, upitie ardhini, Panya huvuvia dada, nyama au punje kila. Maswali a) Toa kichwa mwafaka cha shairi ulilosoma. (alama 1) b) Shairi hili ni la aina gani? Fafanua. (alama 2) c) Eleza ujumbe wa mshairi katika ubeti wa pili. (alama 3) d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4) e) Taja mbinu zozote tatu za lugha katika shairi hili na uzitolee mifano. (alama 3) f) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 5) g) Nakili mloto wa ubeti wa pili kisha ueleze maana yake. (alama 2) majibu
A. - Mke wangu nakuganya / nakukanya - Sitamwacha mke wangu - Mke wangu. 1x1 = 1 B. Takhmisa / utano kwa sababu kila ubeti una mishororo mitano. 2x1 = 2 C. - Anamuonya mpenzi wake asimseme mkewe - Hakuwa walikopendeana na mpenziwe; anaiba pensi - Lazima ahifahdi siri - Kukiwa na wivu katika penzi kutakuwa na uadui. 3x1 = 3 D. Kweli nakuonya tuache mzaha, ukiendelza kuleta shida nitakuacha; lakini huwezi kunishawishi nitoke kwangu. Hata kama wanipenda sitamwacha mke wangu. 4x1 = 4 E) Maswali ya Balagha km Twaingilia nini? Wangu wamtakiani? • Kinaya – ana mpenzi nje lakini anamheshimu mkewe • Takriri – km Mke wangu nakuganya - Halikosekani yoyo - Mke wangu. 3x1 = 3 F) • Shairi lina beti nne • Lina mishororo mitano katika kila ubeti • Vina vya ukwapi vinabadilikabadilika ilhali vya utao vinatiririka (-ni) isipokuwa kimalizio (ukara) • Kituo cha shairi hili ni sabilia / hakirudiwirudiwi • Kila mshororo una mizani 16 (ukwapi 8, utao 8) • Katika ubeti wa pili na wa tatu shairi linadhihirisha sifa za bahari ya pindu (maneno yaliyomalizia ubeti uliotangulia kuanzia ubeti unaofuatia) G) Mloto ni mshororo wa pili katika ubeti k.v. vipi mambo wachanganya, si mwizi ni we kwani – anamwambia asimlaumu mkewe kwa huyu dada kwani ndiye aliyemchukua mumem wa watu. 2x1 = 2
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |