Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswaliMungu naomba subira, subira nayo imani Imani iliyo bora, bora hapa duniani Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani Hiani pamwe ukora wenye kuhini. Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli. Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele Muwele wa hitilafu, hitilafu ya nduwele Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale. Vishale vinitomele, vitomele vikwato Vikwato pia maole, maole kufanya mito Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto. Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka Kutamka wazi vino, vino subira kutaka Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka Wahaka wa matukano, matukano na mashaka. Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita Kunikita salamani, salamani nikadata. Maswali a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani? (al.2) b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia (al.4) (i) Mpangilio wa maneno (ii) Mpangilio wa vina. c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4) d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (al. 4) e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (al.6)
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |