Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuataNaujua mwanzo wake, vile ulivyojipuza, Kilofanya mkereke,na kisichowaumiza, Yakuwa sepata mke, katu hakuwapendeza, Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Mwasema matako hana, yako sawa kama meza, Tena pua yako pana, kama ya kubandika, Lakini mimi naona, yenu sitoyazikiza, Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Kipita nae pahali, sakubimbi hubwagiza, Nzitonzitokauli, asengenywazo.Aziza Nywele za kipilipili,hasongi asongomeza Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Munenayo ni mazito,hadi yeye humliza. Bali kwangu ni matoto,muhali kunichukiza. Japo miguuye fito,haitoshi mtembeza? Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Nataka watowa khofu ,kwa munayo mtangaza, Si Yule mpenda pofu,kawambia ni kengeza, Ni mwenyewe nimeshufu ,muhali kunigeuza. Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Tafadhalini mwachie ,musilumbe kumaliza. Unyonge musitumie,kila siku kumaliza. Haya ni yeye na mie,yaaje mukachagiza , Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Hakujiumba mwenyewe, musighafilike wenza, Aloumba mimi nawe,ndiye aliyemtweza, Tusijitie kiwewe,tukakufuru muweza. Nenani mutamaliza, yeye nampenda vivyo! Maswali a)eleza bahari za shairi hili kwa kutoa ithibati kamili. (alama 3) b)kwa kutoa mifano mwafaka ,eleza methali zozozte mbili kwenye shairi. (alama 4) c)bainisha mambo yoyote manne nafsineni anayazungumzia (alama4) d)fafanua idhini ya mshairi(alama4) e)andika ubeti wa tatukatika lugha tutumbi(alama 3) f)eleza maana za vifungu hivi kama vilivyotumika kwenye shairi i)sakubimbi hubwagiza(alama 1) ii)musighafilike wenza(alama 1) MAJIBU
BAHARI ZA SHAIRI -Tarbia-lina mishororo 4 katika ubeti -Mathnawi-Lina pande 2 katika kila mshororo -Ukara-Vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani havitiririki. b) Methali (i)Akipenda, kipofu huita kengeza (ubeti wa tano) -Mwenyewe amekubali alivyo na hawawezi kumgeuza ingawa wanamsengenya. (ii) Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mimi kumbi (ubeti wa saba) -Hakuna aliyejiumba hivyo waache kusema udhaifu wake. iii) Pilipili usioila yakuashani? (ubeti wa 6 mstari wa 3) (zozote 2x2=4) c)Maudhui -Msimulizi anampenda vile alivyo-mwenyewe amemkubali -Wanakerwa kwani hawana mke -Wanayoyasema hayawahusu wao bali ni kati yake nay eye -Anayezungumziwa hakujiumba mwenyewe bali ni mungu (muumba) -Anawaambia wasitumie udhaifu wake kumsengenya -Ingawa wanayoyasema yanamliza Aziza, yeye hajali. -Waduku wanatahadharishwa wasikufuru d) Uhuru/idini ya mshairi -Tabdila k.m. nae –naye -Mutafanya- mtafanya -Nampenda- ninampenda -Kuboronga sarufu k.m.- Hadi yeye humliza – hadi humliza yeye -Lahaja k.m naujuwa –naujua -Khofu-hofu (zozote 2x2=4) e)Lugha nathari /tutumbi -Nikipita naye popote wadaku/wafitini wanamsengenya Asiza na maneno mazito k.m kuwa hatengenezi nywele. Semeni tu mtasita (au mtaacha) mjue mimi ninampenda alivyo) (3x1=3) Msimulizi anasema kuwa akienda na aziza popote wadaku wanatoa maneno mazito ya kumsengenya k.m hatengenezi nywele. Anawaeleza waendelee tu bali yeye anampenda alivyo. (3x1=3) F). (i)Sakubimbi hubwagiza- wadaku (wasengenyaji hutupa maneno ovyo). (ii) Musighafilike wenza- msiumie/msighadhabike
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |