Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.Ndimi Chesirwo, kijana barubaru, Ndume na gwiji, la ukoo mtukufu, Najivunia umahiri, kusakata kandanda. Tazama umbo langu, guu mithili ya jokovu, Kifua cha miraba, weusi wa kijungu, Wenzangu wanienzi, na hata kuduwaa. Misuli ni tinginya, Kijijini nasifika, Wazee kunienzi, Mabinti kunikabidhi. Maswali (a) Tambua utungo huu na uthibitishe jibu lako. (alama 2) (b) Kwa kurejelea hoja zozote nane, jadili sifa za utungo uliotambua katika (a) (alama 8) (c) (i) Eleza maana ya maghani. (alama 1) (ii) Taja na ueleze tofauti za aina mbili za maghani. (alama 4) (d) Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5) majibu
a) Tambua utungo huu na udhibitishe jawabu lako. (Alama 2) Majigambo/vivugo- mwandishi anajisifu kwa umahiri wake binafsi. Kutaja alama 1 kudhibitisha alama 1 b) Kwa kurejelea hoja zozote nane, jadili sifa za utungo uliotambua kwenye swali la (a). (alama 8) Sifa za majigambo 1. Hutungwa na kuganwa na muhusika mwenyewe. 2. Hutungwa kwa usanii mkubwa. Anayejigamba hutumia mitindo tofauti au ishara. 3. Mwenye kujigamba - hujitungia kivugo kufuatia tukio lililowah kuitokea maishani mwake. 4. Mara nyingi majigambo hutungwa na kuganwa na wanaume. 5. Husheheni matumizi ya chuku. 6. Hutolewa kwa nafsi ya kwanza. 7. Anayejigamba huweza kubeba baadhi ya vifaa vyake vya kazi au vinavyoonyesha jambo analojisifia. 8. Majigambo yanaweza kutungwa papo kwa hapo. 9. Anayejigamba huweza kutaja usuli wake wa kinasaba. Anaweza kusifu ukoo wake 10. Anayejigamba huwa mlumbi. 11. Maudhui makuu katika majigambo huwa ushujaa. (Akikosa (a) , atuzwe 0 katika (b) – Z a kwanza 8 x 1 = 8 athibitishe dai) c) i. Maghani ni nini? (Alama 1) Maghani ni ushairi ambao hutolewa kwa kalima badala ya kuimbwa. 1 x 1 = 01 ii. Taja na ueleze tofauti za aina mbili za maghani unazojua. (Alama 4) maghani ya kawaida- tungo za mashairi yenye hubeba masuala ya kawaida; mfano, njaa, mapenzi, elimu nk. Maghani simulizi: mashiri ya kihadithi ambayo husimulia sifa za mtu ,mnyama, kitu, historia au tukio fulani. Kutaja – alama 2, kutofautisha 2/0 d) Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (Alama 5) 1. Tamasha za kimziki. Wanafunzi hukariri, hugana na kuimba mashairi katika tamasha za muziki 2. Sherehe za harusi, jando, mazishi na matambiko bado zinaendelezwa na jamii ya sasa. 3. Utungaji na utegaji wa vitendawili kupitia redio na runinga. 4. Michezo ya kuigiza katika runinga na redio. 5. Tamasha za drama hihifadhi utanzu wa maigizo,mazungumzo na ushairi simulizi. 6. Sarakasi za wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho. 7. Ngoma za kienyeji huchezwa kwenye hafla kama vile harusi au mikutano ya kisiasa. 8. Wapo watafiti ambao huandika na kuhifadhi rekodi za vipera vya fasihi simulizi. 9. Utambaji wa hadithi hutambwa na jamii nyingi za kisasa hasa sehemu za mashambani. ( Zozote 5 x 1 = 05)
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |