Soma shairi hili kisha ujibu maswali:1. Nikiwa na njaa na matambara mwilini Nimehudumika kama hayawani Kupigwa na kutukanwa Kimya kama kupita kwa shetani Nafasi ya kupumzika hakuna Ya kulala hakuna Ya kuwaza hakuna Basi kwani hili kufanyika Ni kosa gani lilotendeka Liloniletea adhabu hii isomalizika? 2. Ewe mwewe urukaye juu angani Wajua lililomo mwangu moyoni Niambie pale mipunga inapopepea Ikatema miale ya jua Mamangu bado angali amesimama akinisubiri? Je, nadhari hujitokeza usoni Ikielekea huku kizuizini? 3. Mpenzi mama, nitarudi nyumbani Nitarudi hata kama ni kifoni Hata kama maiti yangu imekatikakatika Vipande elfu, elfu kumi Nitarudi nyumbani Nikipenya kwenye ukuta huu Nikipitia mwingine kama shetani Nitarudi mpenzi mama... Hata kama kifoni. Maswali a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka (alama 1) b) Tambua nafsineni katika shairi hili (alama 1) c) Eleza toni katika shairi hili (alama 1) d) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia (alama 4) e) Fafanua dhamira katika shairi hili (alama 2) f) Thibitisha kuwa hili ni shairi huru (alama 4) g) Taja na ufafanue sifa mbili za mshairi (alama 2) h) Fafanua mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika ubeti wa tatu. (alama 3) i) Eleza maana ya maneno yafuatoyo kama yalivyotumiwa katika shiari hili (alama 2) i) Hayawani ii) Nadhari MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
5. (a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka (alama 1) i. Mama nitarudi ii. Nitarudi iii. Kizuizini alama 1 (asizidishe maneno sita) (b) Tambua nafsineni katika shairi hili (alama 1) Nafsineni ni aliye kizuizini. Anauliza iwapo mamake angali anasimama na kusubiri akitazama kule kizuizini aliko nafsineni (atambue na athibitishe alama 1/0) (c) Eleza toni katika shairi hili (alama 1) i. Toni ya masikitiko / uchungu wa moyoni/huzuni kwa mfano, anasikitikia hali yake ya kuvaa matambara, njaa, kufanyiswha kazi tele ii. Toni ya matumaini kwa mfano, mshairi ana matumaini kwamba siku moja atatoka kizuizini (atambue na athibitishe alama 1/0) (d) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia (alama 4) i. Kuachwa njaa ii. Kufungwa iii. Kufukuzwa iv. Kutopewa nafasi ya kupumzika, kulala na kuwaza v. Kuvaa matambara vi. Kufanyizwa kazi kama mnyama (Zozote 4 x 1 = 4) (a) Fafanua dhamira katika shairi hili (alama 2) i. Mshairi anadhamiria kulalamikia/kukashifu namna anatumiwa vibaya kizuizini ii. Mshairi anakashifu madhila na mateso ambayo wafungwa hutendewa iii. Kumpa mamake matumaini kwamba atatoka kizuizini siku moja (Zozote 2 x 1 = 2) (b) Thibitisha kuwa hili ni shairi huru (alama 4) i. Kuna matumizi ya mistari mishata ii. Idadi ya mishororo inabadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi nyingine iii. Silabi za mwisho katika kila mshororo zinatofautiana iv. Idadi ya mizani katika kila mshororo inatofautiana (Zozote 4 x 1 = 4) (c) Taja na ufafanue sifa mbili za mshairi (alama 2) i. Ni mwenye kulalamika kwa mfano, analalamikia hali yake ya kuwa na njaa, kupigwa ii. Mwenye matumaini kwa mfano, anatumai kuwa siku moja atatoka kizuizini iii. Mwenye mapenzi kwa mfano, anampenda mamake na kumwita mama mpenzi (Zozote 2 x 2 = 4) kila sifa itolewe mfano - atuzwe 2/0 (d) Fafanua mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika ubeti wa tatu. (alama 3) i. Takriri kwa mfano, neno nitarudi limerudiwarudiwa ii. Mdokezo kwa mfano, nitarudi mama mpenzi iii. Tashibihi kwa mfano, kupitia mwingine kama shetani iv. Balagha kwa mfano, Ni kosa gani lilotendeka - Liloniletea adhabu hii isomalizika? (Za kwanza 3 x 1 = 3) (e) Eleza maana ya maneno yafuatoyo kama yalivyotumiwa katika shiari hili (alama 2) i) Hayawani - mnyama ii) Nadhari - fikira (Za kwanza 2 x 1 = 1)
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |