SOMA SHAIRI KISHA UJIBU MASWALI MODEL23122022001
Ndugu ona mbwa yule, ambaye ananyekenya;
Yaone mabuu yale, ambayo yamchezeya; Kuwa leo yuafile, mwili yanautaniya; Jana awile jasiri! Juzi shujaa awile, pasiwe kumfikiya; Kwenye makani yale, alipojisururiya; Leo kuwa yuafile, mainzi yamchekeya; Jana awile Jasiri! Mijino mikubwa ile, ambayo ‘mejitokeya; Yali kiwaliza wale, karibu walosogeya; Tena akibweka yule, waoga walijinyiga; Jana awile jasiri! Kamwe kuishi milele, kupe ukajinyonyeya; Walo chini yako wale, muhali unawaziya; Ameshindwa yule pale,sembuse wewe sikiya; Jana awile jasiri! Kama walo hai wale, yafaa kuzindukiya; Ni dunia maji male, muhimu kujiwaziya; Wazipunguze kelele, na kwingi kujishauya; Jana awile jasiri! MASWALI
Fafanua ujumbe wa shairi hili (Al 2)
a) Eleza muundo wa shairi hili (Al 5) b) Eleza toni ya shairi hili (Al 2) c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia (Al 3) i) Ruwaza ya mistari ii) Ruwaza ya vipande iii) Ruwaza ya mizani d) Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (Al 4) e) Bainisha sifa mbili za anayezungumziwa katika shairi hili (Al 2) f) Eleza tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili (Al 2) MWONGOZO / MAJIBU
a) Fafanua ujumbe wa shairi hili
Shairi linazungumzia jinsi walio na nguvu wasivyowazia walio chini yao na kuwahimiza watu kuzinduka na kupunguza kelele pamoja na kujishaua a) Eleza muundo wa shairi hili I) Lina beti 5 II) Kila ubeti una mishororo minne III) Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa kibwagizo chenye kipande moja. IV) Lina kibwagizo – jana awile siri! V) Vina vya kati na vya nje vinatiririka isipokuwa ubeti wa kwanza, mshororo wa kwanza wenye kina tofauti VI) Kila mshororo una mizani 16 isipokuwa ubeti wa pili, mshororo wa pili na ubeti wa tano, mshororo wa kwanza yenye mizani 15. VII) Kibwagizo kimekamilika kwa alama hisi! b) Eleza toni ya shairi hili Toni ya kushauri – nafsineni anawashauri watu kuzinduka na kupunguza kelele na hali ya kujishaua/kujisif
c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia:
I) Ruwaza ya mistari Tarbia – Kila ubeti una mishororo mine ii) Mathnawi – Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa kibwagizo chenye kipande kimoja iii) Ruwaza ya mizani Msuko – Kibwagizo kina mizani michache kuliko mishororo mingine d) Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi i) Tabdila Yamchezeya – Yamchezea Yanautaniya – Yautania n.k. ii) Inkisari ‘mejitokeya – imejitokea Walosogoya – waliosogea iii) Kikale – awile – alikuwa iv) Kufinyanga sarufi – kwingi kujishauya – kwingi kujishaua e) Bainisha sifa mbili za anayezungumziwa katika shairi hili i) Mwenye vitisho – alipobweka/alipozungumza waoga walijinyia ii) Mwenye ubinafsi – Hakuwawazia waliokuwa chini yake f) Eleza tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili i) Jazanda – mbwa ii) Taswira – mabuu yakimchezea mbwa iii) Tashihisi- mainzi yamchekea iv) Chuku – Tena akibweka yule, waoga walijinyinya v) Sitiari – ni dunia maji male Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|