SOMA SHAIRI KISHA UJIBU MASWALI MODEL23122022002
Nizike Ningali Hai!: Hassam Muchai
Kipusa Binti Hamadi, siku n’takuwa kimba Nizikwe Kifudifudi, na yoyo kuyumbayumba Takuwa bure biladi, matozi ungayasomba Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Tena ningaumwa ungo, na mapumu kuugua Lioze ini na nyongo, na pua zisipumua Takuwa sina kinyongo, mradi nimeshatua Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Nizike sasa mwenzangu, nizike ningali hai Singojee kufa kwangu, uanze kurairai Kulilia kifo change, ni bure hakukufai Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Nikifa hutonizika, kimwana sanda nunua Manukato ya kupaka, na nguo za kuanua Nivishe sione shaka, Washindwe kupambanua Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Tena nikande misuli, nikande pande kwa pande Siate kiwiliwili, shingo, miguu ikande Umalizapo kiwiliwili, mwenzangu niende shonde Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika MASWALI
A) Dhamira ya matunzi wa shairi hili ni gani? (Al 2)
B) Bainisha nafsineni katika shairi hili (Al 2) C) Eleza toni ya shairi hili (Al 2) D) Changanua muundo wa shairi hili (Al 5) E) Fafanua maana ya kibwagizo cha shairi hili (Al 2) F) Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (Al 4) G) Bainisha bahari ya shairi hili (Al 3) MONGOZO / MAJIBU
a) Dhamira ya mtunzi wa shairi hili ni gani?
Kuhimiza watu kutendea wenzao mema wakiwa wangali hai b) Bainisha nafsineni katika shairi hili Kipusa Binti Hamadi – Kipusa Binti Hamadi, siku n’takuwa kimba c) Eleza toni ya shairi hili Toni ya kushauri – Kipusa Binti Hamadi anatoa ushauri kwamba azikwe angali hai. d) Changanua muundo wa shairi hili i) Lina ubeti 5 ii) Kila ubeti una mishororo minne iii) Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa ubeti wa tano , mshororo wa pili wenye vipande vitatu iv) Vina vya ndani na vya nje vinabadilika katika ubeti v) Lina kibwagizo – Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika vi) Kila mshororo una mizani 16
e) Fafanua maana ya kibwagizo cha shairi hili
Nisaidie ningali hai kwa maana nikifa hutaweza kunisaidia f) Eleza mbinu nne amabazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi i) Kufinyanga sarufi
ii) Lahaja
iii)Tabdila
iv) Inkisari
g) Bainisha bahari ya shairi hili i) Tarbia – lina mshororo minnne katika kila ubeti ii)Mathnawi – Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa ubeti wa tano, mshororo wa pili wenye vipande vitatu. iii)Ukaraguni – Vina vya kati na vya nje vinabadilika katika kila ubeti. Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|