Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Hizi bombo mwaanika, wa ndizini nashtuka,
Peupe mwazianika, kwenye jua kukauka, Zingine zimeraruka, aibu zinatufika, Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.
Nako kule kwenye bafu, mwaziweka hizo chafu,
Hilo nalo nakashifu, mkitoa nitasifu, Kuziweka maji chafu, hilo ndilo ninahofu, Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.
Kwenye meza wazileta, wana wenu wakipata,
Wageni wakijateta, aibu haitatupata? Muondoeni utata, hizo zenu twazipata, Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha. Kwa heshima tudumuni, tufaapo za mwilini, Tamaduni jifunzeni, msiige uzunguni, Za bafuni zi jikoni, zi watoto makononi, Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.
Wino wangu kibindoni, nitatua tamatini,
Za ndani ziwe za ndani,msonyeshe hadharani, Za bafuni si jikono, msiweke kabatini, Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha. MASWALI
a) Pendekeza kichwa mwafaka katika shairi hili. (alama 1)
b) Eleza toni ya shairi hili. (alama 1) c) Tambua nafsineni katika shairi. (alama 1) d) Jadili matumizi ya mitindo ifuatayo ya lugha katika shairi hili. i. Kinaya (alama 2) ii. Usambamba (alama 2) iii. Balagha (alama 1) e) Onyesha kuwepo kwa uhuru ufuatao katika shairi. (alama 3) i. Tabdila ii. Kubananga sarufi iii. Inkisari f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha mjazo. (alama 4) g) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 5) MWONGOZO
1. Pendekeza kichwa mwafaka.
Aibu, Aibu kwetu
2.Eleza toni ya shairi hili
● Toni ya kukasifu/kushtumu/kukejeli mienendo ya kutojali. ● Toni ya kughadhabika Kwa kutojali. ● Toni ya kushauri kuhusu heshima na usiri.
3. Tambua nafsineni wa shairi
Mhusika ambaye amepata aibu kutokana na mienendo ya watu kuanika mavazi ovyo ambayo anahisi ni vibaya.
4. Jadili matumizi ya mitindo ifuatayo
● Ni kinaya kuwa angependa mavazi fulani yafichwe ilhali yamefichwa bafuni. ● Ni kinaya kuwa anataka zikauke bila kuanika /ilhali zimefichwa. ● Ni kinaya kuwa wageni wanaibika ilhali wenyewe huzitumia na huanika kwao Usambamba ● Miundo sawa ya mistari/mishororo-anikeni kwa kuficha,z ndani mkisafisha. ● Urudiaji wa maneno –anika,kuficha. ● Urudiaji wa silabi-ka(ubeti wa kwanza) fu(ubeti wa pil) ta (ubeti wa tatu) Balagha ● Ubeti wa mwisho mshororo wa pili-aibu haitatupata?
5. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya mjazo/Nathari.
Mshairi anasema kuwa nguo za ndani zinazoanikwa ovyo/popote,watoto/wana huzipata na kutembea nazo hata mezani kwa wageni.Hili huleta aibu kubwa na hivyo hushauri watu waanike kwa tahadhari.
6. Onyesha kuwepo kwa uhuru ufuatao katika shairi
● Tabdila –muondoeni badala ya mwondoeni. ● Kubananga sarufi-anikeni kwa kuficha,za ndani mkisafisha. Badala ya mkisafisha za ndani mzianike kwa kuficha. ● Inkisari-tufaapo badala ya tunapofaa.
7. Eleza muundo wa shairi hili
● Shairi hili lina beti tano. ● Kila ubeti una mishororo minne. ● Shairi hili lina kibwagizo ambacho ni :anikeni kwa kuficha , za ndani mkisafisha. ● Idadi ya mishororo inatoshana kaika kila mshororo;kumi na sita. ● Kila mshororo una vipande viwili, ukwapi na utao. ● Vina vyake vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|