SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI MODEL25122022001
Ulimwengu ulimwengu, ulimwengu naratibu
Yaliyo kichwani mwangu, nataka kuyatubu Wayasome ndu zangu, wa mbali na wa karibu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ulimwengu ni kiwanja, cha wenye raha na tabu
Wengine wanajikonja, kwa wengine ni adhabu Kucha na kutwa twahanja, kutafuta matulubu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa balaa, aliniusia babu
Mna mambo yamejaa, ya faraja na kusibu Na machache ya kufaa, ila mengi ya udubu Cha wenye raha na tabu,ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja cha Amina,Saidi Ali Rajabu
Wengine kitu hatuna, tunaishia kababu Wale wamejaza sana, wanashindwa kuhesabu Cha wenye raha na tabu, Ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa urongo, na kweli pia ajabu
Kichwa hudanganya shingo, tumbo kiuno chasibu Usitumai ubongo, wa nduguyo na swahibu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa walevi, pombe kwao ni dhahabu
Mara vile mara hivi, wakilewa majudhubu Maneno ya kiujuvi, hujipaka hata shabu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja wenye dini, wamtiio wahabu
Mashekhe msikitini, humo humfanya muhibu Mapadiri kanisani, huvihubiri vitabu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa malofa, lofa mtu mwenye tabu
Kusema sana kashifa na moyo kisebusebu Tunakaribia kuja, kwa kushindwa kujimudu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa faraja, alowajali habibu
Na wengine sitotaja, msinambe ninagubu Ni uwanja wa viroja, vigumu kuvikutubu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja. maswali(a) Lipe shairi hili anwani ifaayo. (alama 1)
Ulimwengu ni kiwanja
Changamoto ulimwenguni 1 x 1 = alama 1 (b) kwa kutoa mfano, eleza mbinu zozote mbili za lugha zilizotumika katika shairi.(alama 2)
(b) Istiara/ jazanda – ulimwengu ni kiwanja
Msemo – kutwa kuchwa Ukinzani/tanakuzi – wenye raha na tabu Uhuishaji – Kichwa kudanganya shingo (zozote 2x1 = alama 2) (c) Eleza jinsi uhuru wa mshairi ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
(c) Inkisari – naratibu – ninaratibu
Ndu zangu – ndugu zangu. Kuboronga lugha – wenye kitu hatuna – wengine hatuna kitu Utohozi – shehe – sheikh Padre – padre (2 x 1 = 2) (d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (alama 4)
(d) babu alimshauri kuwa ulimwengu ni uwanja wa balaa ulionjaa mambo ya faraja na kusibu. Pia alisema kuwa kuna machache ya kufaidi na mengi ya kuudhi. Kwa hivyo ulimwengu ni kiwanja kwa walio na raha na walio na taabu.
(4x1 = alama 4) (e)Taja na ueleze bahari zozote mbili zilizotumika katika shairi hili.(alama 2)
(e) (i) Tarbia – mishororo minne kwa kila ubeti
(ii) Mathnawi – vipande viwili kwa kila mshororo (iii) Pindu – sehemu ya mwisho kuanzia ubeti unaofuata. (iv) Ukara – vina vya mwisho vinatirirka na vya kati havitiririki. (2x1 = alama 1) (f) Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
(f) (i) Mishororo minne kwa kila ubeti
(ii) Vipande viwili kwa kila mshororo – ukwapi na utao. (iii) Lina beti tisa. (iv) Vina vya mwisho vinatiririka na vya kati vinabadilika (v) Lina kibwagizo – che wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja. (vi) mizani ni 8,8 kwa kila mshororo 4x1 = 4 (g) Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
(g) masikitiko (alama 1)
(h) Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 2)
(h) Kufahamisha watu hali ilivyo ulimwenguni. Kwamba kuna mazuri na mabaya ili wajihadhari. (1x2= 2)
(i) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.(alama2)
|
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|