​Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali.
​​Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa hamu Kushika mpini na kutokwa jasho Ili kujikimu kupata malisho.
​Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza Utadhani huwa vimemngojea Kwa usiku kucha kuja kumwimbia; Pia pepo baridi kumpepea Rihi ya maua zikimletea Nao umande kumbusu miguu; Na miti yote hujipinda migongo Kumpapasa, kumtoa matongo; Na yeye kuendelea kwa furaha Kuliko yeyote ninayemjua Akichekelea ha hahaha ha….
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza? Au nikujua au kutojua? Furaha ya mtu nifuraha gani Katika dunia inayomhini? Ukali wa jua wamnyima zao Soko la dunia la mkaba koo; Dini za kudhani zamsonga roho Ayalimia matumbo ya waroho; Kuna jambo gani linamridhisha? Kama sikujua ni kutokujua Laiti angalijua, laitia ngalijua!. (T. Arege) ​​MASWALI.
a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. (alama.4)
b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili. (alama.2) c) Fafanua aina mbili za taswira ukirejelea ubeti wa pili. (alama.2) d) Maswali ya balagha katika shairi hili yanasisitiza maudhui yapi? (alama.2) e) Bainisha vipengele viwili vya kimtindo katika shairi hili. (alama.2) f) Bainisha aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. (alama.2) g) Eleza toni ya shairi hili. (alama.2) h) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama.1) i) Eleza muundo wa shairi hili. (alama.3) ​MWONGOZO WA USHAIRI.
​a)i) Mwenyetumaini /tamaa – kubwahamu
ii) Mwenyebidii- alfajirina,mapema, kutokwanajasho. iii) Anayefurahiamandhari – anapotembeaanasikilizavidege…. iv) Mtulivu- kunasiriganiinayomliwaza? v) Aliyedhulumiwa – soko la dunialamkabakoo. vii) Aliyeridhika- kunajambogani? (2x2=2) b) Inkisari – babuze – babuzake. ii) Kufinyangasarufi/miundongeuyakisintaksia- kubwahamu – hamukubwa. 2x1=2) c)i) Taswiramnuso/harufu – rihiyamaua ii) Taswiramguso – kumpapasa, kumbusumiguu. iii) Taswirauskivu – anasikilizavidege. iv) Taswirayamwendo – yeyekuendeleakwafuraha. (2x1=2)
d)i) Maudhuiyaunyanyasaji – katikaduniainayomhini?
ii) Ukosefuwahakikwabinadamumaskini – soko la dunialamkabakoo. (2x1=2) e)i) Tashhisi- Umandekumbusu, mitikumpapasa, upepokumpepea. ii) Kinaya- nafsineniinafurahiilhaliduniainamhini iii) Tashbihi – kamamtualiyenakubwahamu (2x1=2) f)i) Urudiajiwamaneno- kama – ubeti 1 -furaha – ubeti 3 ii) Urudiajiwasauti – a, a – ubeti 2, 3 -o,o – ubeti 3 iii) Urudidajiwasilabi – ma, ma, za, za, ha, ha (2x1=2) g)i) Toni yauchungu- furahayamtunifurahaganikatikaduniainayomhini? ii) Toni yakuajabia/kushangazwanajambo- kunajamboganilinamridhisha? iii) Kuhuzunisha/masikitiko/kuhurumia- laitiangalijua. 1x2=2 kutaja-1 kueleza -1 h) Mteteziwahaki/aliyezinduka/anayelalamikiadhulumayawanyonge. ii) Mtuanayemtazamamkulimakipita. (1x1=1) I)i) Linabetitatu ii) Kilaubetiunaidaditofautiyamishororonabetinyingine. iii) Kilamshororounakipandekimojaisipokuwaubetiwapilimshororowatisanamshororowamwishoubetiwamwisho. iv) Shairihalinampangiliomaalumwavina v) Idadiyamizanikatikamishororoinatofautiana. (3x1) Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|