Soma shairi na kujibu maswaliHuketi mahali tuli, nikaaza peke yangu Na niazalo ni hili, lililo moyoni mwangu Naifikiri ajali, siku ya kunyoka kwangu Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke Itakufa initoke, katika jasadi yangu Ndugu zangu niwepuke, kwa kadhwa ya Bwana M’ngu Kitandani waniweke, wanioshe ufu wangu Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke Tanyoshwa sina kauli, waliye wendani wangu Wanitakase muwili, sina langu wala changu Sanda ikisha waswili, wanikafini wenzangu Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke Nikisha sanda kutiwa, iletwe jeneza yangu Nitiwe kwa kupokewa, na mikono ya wenzangu Wende nami sawa sawa, hadi baiti ya M’ngu Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke (A. Nassir, ‘Maskini roho Yangu,’ Malenga wa Mvita, 1971:170) Maswali (a) Kwa kuzingatia vina taja bahari ya shairi hili. (alama 1) Ukara (1x1=1) (b) Orodhesha mifano ya uhuru wa kishairi iliyotumika na sababu zake. (alama 3) ● Lahaja Nikaaza – nikawaza (kudhirisha ubingwa / asili / usuli/utamu/ladha ● Tabdila/tafsida Naliliya – nalilia (kudumisha mdundo/mapigo ya kisauti / ainisha mapigo) ● Inksari Niwepuke – niwaepuke (kudumisha urari wa mizani) ● Kufinyanga lugha kisarufi Nikisha sanda kutiwa – Nikisha kutiwa sanda. (kudumisha urari wa vina) *Mwalimu atathmini jibu la mwanafunzi [3 x 1 = 3] (c) Shairi hili linajitosheleza. Thibitisha kwa kutolea mifano mitatu. (alama 3) [shairi hujitosheleza kimaana na kimuundo] (i) Kimaana – ujumbe kwamba nafsineni analilia roo yake siku atakapokufa umejitokeza wazi katika shairi lote. Kila ubeti wajenga maana hiyo.Ninaililia roho yangu itakapotengana nami baada ya kufa/kifo change. (4 x 1 = 4) (ii) Kimuundo; kila kipengee ni hoja. Kuna urari wa: ● Vina katika ubeti (kivyake) ● Mizani 8:8 ● Mishororo minne minne katika kila ubeti ● Vipande: ukwapi na utao (2 x 1= 2) (d) Andika ya ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 2) Huwa ninakaa pahali peke yangu na kuwaza. Kile ninachofikiria kimo moyoni mwangu. Jambo ambalo huwa ninafikiria juu yake ni kuhusu siku ya kufariki kwangu(bila kutarajiwa / kupangia). [2 x 1 = 2) (e) Changanua vipengele vya kimtindo vyovyote vitatu katika utungo huu. (alama 3) (i) Jazanda: Siku ya kunyoka – siku ya kifo (ii) Uzungumzi nafsia. Matumizi ya nafsi ya kwanza: Huketi mahali tuli, nikaaza peke yangu. (iii) Tashihisi /uhaishaji/uhuishi Sanda ikisha waswili itakufa iyondoke. (iv) Mjalizo [ni matumizi kuleta msisitizo sina langu wala changu, [kama nipe nikupe, nishike nikushike] Sina langu sina changu (v) Takriri Sawa sawa Kibwagizo Silabi (vi) Utohozi Wanikafini – put in coffin (3 x 1 = 3) (f) Dhihirisha matumizi ya taswira. (alama 3) (i) Taswira Mwendo wende nami sawa sawa, hadi baiti ya M’ngu / sanda ikisha waswili. (ii) Taswira oni. Huketi mahali tuli, nikaaza peke yangu. (iii) Mguso Wanitakase muwili Nitiwe kwa kupokewa, na mikono….. (iv) Taswira hisi Naililia roho yangu Wanitakase muwili (3 x 1 = 3) (g) Tolea mifano mitatu ya takriri zilizotumika. (alama 3) (i) Maana Nitiwe kwa kupokewa, na mikono ya wenzangu (ii) fungu la maneno / mshororo Nalilia roho yangu, itakufa iyondoke (iii) Takriri silabi na - naliliya - naililiya - naifikiri nk Takriri ya vina vya mwisho na kati (iv) Takriri ya neno: M’ngu Sanda Sawa sawa (3 x 1 = 3) Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|