​USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL14122022003
​Eti
Mimi niondoke hapa Niondoke hapa kwangu Nimesaki, licha ya risasi Vitisho na mauaji, siondoki
​Mimi
Siondoki Siondoki siondoki Niondoke hapa kwangu! Kwa mateke hata na mikuki Marungu na bunduki, siondoki
​Hapa
Siondoki Mimi ni Pahame! Niondoke hapa kwangu! Fujo na ghasia zikizuka Na kani ya waporaji, siondoki
​Haki
Siondoki Kwangu siondoki Niondoke hapa kwangu! Nawaje; waje wanaokuja Mabepari wadhalimu, siondoki
​Kamwe
Siondoki Ng’oo hapa kwangu! Katizame chini mti ule! Walizikwa babu zangu, siondoki
​Sendi
Nende wapi? Si hapa kitovu changu Niondoke hapa kwangu Wangawa na vijikaratasi Si kwamba hapa si kwangu, siondoki
​Katu
Siondoki Sihitaji karatasi Niondoke hapa kwangu Yangu mimi ni ardhi hii Wala si makaratasi, siondoki ​Maswali
a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini (alama 2)
b) Taja masaibu anayopitia mzungumzaji (alama 4) c) Eleza toni ya shairi hili (alama 2) d) Eleza muundo wa shairi hili (alama 3) e) Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba (alama 2) f) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4) g) Tambua idhini moja ya mtunzi (alama 1) h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 3) (i) Karatasi (ii) Nimesaki (iii)kitovu majibu / mwongozo
​a. - Ni shairi huru kwa sababu mshairi ametumia (i) mishata mf. katu, eti, niondoke
- Shairi lina umbo la paa la nyumba - Matumizi ya alama za uakifishaji kwa wingi (al. 2)
​b. (i) Anatishwa kwa risasi
(ii) Kupigwa mateke na mikuki (iii) Kuponda mali yake (iv) Kuletewa hatimiliki bandia (mwalimu akubali hoja nyingine yoyote) Al. 4
​c. (i) Huzuni
(ii) Ujasiri (2 x 1) (iii) Uchungu
​d. Shairi lina beti saba
Kila ubeti una mishororo sita Lina umbo la paa la nyumba (3 x 1)
e. Usambamba – Ni urudiaji wa kiwango cha sentensi, kirai (n.k)
mf. ​(i) Niondoke, mimi niondoke hapa, niondoke hapa kwangu (ii) Siondoki, siondoki, siondoki niondoke hapa kwangu (2 x 1)
​f. Mshairi anasema kamwe hatoki kwake. Anaashiria chini ya mti waliozikwa babu zake na kusisitiza kwamba hawezi akaondoka (al. 3)
g. Inkisari –
​(i) Sendi – Siendi Nende wapi – Niende wapi (ii) Kuboroga sarufi mf yangu mimi ni ardhi hii – Ardhi hii ni yangu mimi (1 x 1)
h. Karatasi – Hati miliki
Nimesaki – Nimebaki Kitovu – Asili (al. 3 x 1) Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|