USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL16122022002
​​Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,
Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia, Mnipe masikioni, shike nachoeleza, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
​Naanza kwa uzalendo, nchi yetu tuipende
Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuipende, Wa kila mtu mwendo, usije kawa mpinde, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
​Linda demokrasia, uongozi tushiriki,
Haki kujielezea, wachotaka na hutaki, Changu naweza tetea, demokrasia haki, Taifa sio taifa,pasi kuwa maadili.
​Tuwe na uadilifu, twache tamaa na hongo,
Tusiwe na udhaifu, wa kuwa watu waongo, Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo, Taifa sio taifa, pasi kuwa na maadili,
​Ubinafsi si adili, ila ni kusaidia,
Ukiwa nayo mali, asiye nacho patia, Kama mtu mswahili, ubinafsi mtu achia, Taifa sio taifa , pasi kuwa na maadili.
​Na inavyoelezea,katiba ni kielezi,
Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi, Kwa hayo nitamwachia, hiyo ya ziada kazi, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. maswali​a) Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na maadili. (alama 4)
a) Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na maadili. (alama 4)
​b) Eleza mtindo wowote ule uliotumika katika shairi hili. (alama 2)
a) Eleza mtindo wowote ule uliotumika katika shairi hili. (alama 2)
​c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (alama2)
|
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|