​Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.
Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani Hiani pamwe ukora wenye kuhini. Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli. Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele Muwele wa hitilafu, hitilafu ya nduwele Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale. Vishale vinitomele, vitomele vikwato Vikwato pia maole, maole kufanya mito Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto. Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka Kutamka wazi vino, vino subira kutaka Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka Wahaka wa matukano, matukano na mashaka. Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita Kunikita salamani, salamani nikadata. ​​Maswali
a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani? (al.2)
b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia (al.4) (i) Mpangilio wa maneno (ii) Mpangilio wa vina. c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4) d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (al. 4) e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (al.6) Majibu
​(a) Ili asiwe na wasiwasi ya kutukanwa na huhiniwa aepuke kufanyiwa mabaya. 1 x 2 =2
(b) (i) Pindu/mkufu/nyoka (al.1) Kwa sababu neno la mwisho katika mshororo wa mwisho wa ubeti linatumiwa kuanzia ubeti unaofuata. (al. 1) (ii) Ukaraguni (al.1) Vina vya kati na vya mwisho vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. (al.1) ​(c) (i) Tashbihi - Hafifu kama muwele - Tele mithili kitoto.(al.2) (ii) Uradidi/Takriri - Subira’ - Bora, kombora, ukora - Kiburi, kudhuri n.k.(al.2) (d) (i) Misuli kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa. (ii) Hasa mgonjwa mwenye tatizo la (iii) Ambao unasumbua sana daima na (iv) usiopona kwa vishale. (zote4 x 1 = 4) ​(e) (i) Inkisari - kuleta urari wa mizani k.m kilo — kilicho. (ii) Tabdila - kuleta urari wa vina k.m. kudhuri — kudhuru maole — maozi. - Kuleta urari wa mizani k.m nduwele — ndwele muwili — mwili (iii) Mazida - kuleta urari wa vina pia mizani. - Vinitomele - vinitome. Kutaja na matumizi (al.1) Mfano (al.1) Zote 3 x 2 = 6 Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|