Soma shairi hili kisha ujibu maswali:Wanaume ni Wanyama Nakumbuka vyema sana, sisahau siku ile Nilipoitwa na nina, akanipa ya kivyele Mwanangu u msichana, nakuasa usikile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Kuwa umevunja ungo, ni hali ya maumbile Bora uwapo na bongo, anasa uzikimbile, Ukijitia maringo, utatungwa mimba mbele Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Ngawa waje na manoti, “Nakupenda” wakwambile Wakuvalie makoti, usiwaachie mbele Hata wapige magoti, wambile mna kelele Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Ngono ni tendo la suna, Amina sikimbile Wala miguu halina, kwamba lingekukimbile Muhimu kwako Amina, kwanza uthamini shule Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Kuzurura mitaani, si tabia njema ile Unapotoka nyumbani, fululiza hadi shule Si kwenda vichochoroni, kuwaona kina wale Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Uwe mwana msikizi, yano uyazingatile Mengine kuhusu penzi, mwanangu taonywa shule Kama mameyo mzazi, nimekuonya kimbile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama Wakaja kina Hamadi, mwana wa Mzee Sule Kwangu wakapiga hodi, hata mkuu wa shule Ila nikajitahidi, kukwepa mitego ile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Na kuna Karisa, mwanafunzi kule shule Akawa hunipapasa, name pia vilevile Mwishowe itakupasa, tugawe tunda tulile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Nani akachovya uto, wa asali tamu vile Na kisha aape kuto, kula asali milele Kuwa mjamzito, wamenifukuza shule Si waone vile, wanaume ni wanyama. Karisa yu vilevile, angali ywaenda shule Na mie kitumbo mbele, ninajikuna upele Yameshatumia yale, niloonywa siku ile Si watu waone vile, wanaume ni wanyama. Maswali: (a) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2) (b) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2) (c) Bainsha mambo manne ambayo nafsineni anatoa kama ushauri kwa nafsinenewa. (alama 4) (d) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo ambapo mshairi ametumia kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 3) (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (alama 3) (f) Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4) (g) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2) majibu
(a) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2) i. Ni tarbia (alama 1) ii. Lina mishororo minne katika kila ubeti (alama 1) (b) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
(c) Bainsha mambo manne ambayo nafsineni anatoa kama ushauri kwa nafsinenewa.(alama 4)
(a) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo ambapo mshairi ametumia kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 3)
(b) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (alama 3)
ii. Kuzurura mitaani, si tabia njema ile – ile tabia ya kuzurura mitaani si njema (Za kwanza 3 x 1 = 3) (c) Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4)
(d) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2) Mama yake mshauriwa kwa mfano, mamayo mzazi, nakuonya ukimbile
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |