YALIMWAGIKA
Lilianza kama wazo, nikawaza,
Niwe na watoto, Si vikwazo, ghafla mama yao akapatikana, Kwa rutuba yake, Akavimba Kumbe ni mapacha, furaha!
Majina walishapewa,
Imani kudumu, watazaliwa, Tungo wakatungiwa, Amani na Imani, Baba yao ni malenga Anatayeita maneno. Maneno yanaitika. Nikasubiri.
Wazazi walitamani kupakata,
Amani na Imani Iwe yao burudani, siyo kama zamani Wachezee zuliani. Baba niwaweke kifuani Na migongoni bila susu, kwa mama yao Si mtoto hutizama kisogo cha ninake? Tukangoja!
Furaha kote nyumbani iliwatanda,
Kuyaona makinda yao, kwa kitanda, Wadondokwe udende, wawapende! Mama anyonyeshe, kiwatazama machoni, Kuwagusa mashavuni, waliapo. Watulie Amani na Imani.
Ukutani ni kiwimbo, baba alishawatungia,
Kushotoni ni wa kike, kuumeni kijanadume Watulie, Baba yao aliwazia Wazo likaanza kupokwa. Hospitali wakiwasili.
Wiki zikajenga miezi
Tamati ikajongea Kawanunulia mavazi Walifaa kuvaa Hawakuvaa! Vijulanga miezi saba, pukachaka! Kifo ni mwewe, kikaninyakulia. Amani na Imani. Tunalia! Pema peponi wanetu! MASWALI
a) Eleza jinsi usimulizi ulivyotumika kwenye shairi. (alama 1)
b) Eleza sifa tatu zinazoafiki shairi hili kuwa huru. (alama 3) c) Shairi hili ni la tanzia. Thibitisha. (alama 1) d) Tambua mandhari ta tanzia. (alama 1) e) Tambua nafsineni kwenye ubeti wa kwanza. (alama 1) f) Eleza toni ya shairi. (alama 2) g) Onyesha mifano miwili ya matumizi ya sadfa katika shairi. (alama 3) h) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi. (alama 4) i) Eleza maana ya msamiati huu kulingana na shairi. (alama 4) i.Vijulanga ii.Susu iii. Akavimba iv ..Kiwimbo YALIMWAGIKA MWONGOZO
A).Eleza jinsi usimulizi ulivyotumika kwenye shairi.
Ushairi umesimulia safari kabla ya ndoa na katika ndoa.
b.Eleza sifa tatu zinazoafiki shairi hili kuwa shairi huru.
● Idadi ya mishororo katika kila ubeti si sawa. ● Idadi ya vipande katika kila mshororo si sawa. ● Idadi ya mizani katika kila mshororo inatofautiana. ● Limechukua miundo mbali mbali lilivyoandikwa. ● Shairi hili halina kibwagizo. ● Vina vyake vinachanganywa/halina mtiririko wa vina. ● Shairi hili lina alama nyingi za uakifishaji.
c).Shairi hili ni tanzia
Kuna kifo cha mapacha waliotarajiwa kuzaliwa na walisuburiwa sana na wazazi zao.
d.Tambua mandhari ya tanzia
Hospitalini ndiko walikofia mapacha.
e).Tambua nafsineni kwenye ubeti wa kwanza
Baba / bwana mtarajiwa/mwanamume.
f).Eleza toni ya shairi.
Toni ya huzuni /majonzi kutokana na kifo cha mapacha Amani na Imani.
g).Onyesha mifano miwili ya matumizi ya sadfa katika shairi.
● Baba anawaza kuhusu watoto na kumpata mke papo hapo wa kuoa. ● Msemaji anasema akataka’ watoto’ na ghafla ujauzito unakuwa wa mapacha. ● Watoto wanapewa majina Imani n Amani na baadaye mimba kugundulika ni ya mapacha kiume na kike.
H).Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi.
Muda uliendelea kusonga wakisubiri watoto wao kuzaliwa. Wakanunuliwa mavazi mbalimbali wakitarajiwa kuwapokea japo halikutimia.watoto wakafa mimba ikiwa ya miezi saba na kuombolezwa.
i).Eleza maana ya misamiati ifuatayo.
● Vijulanga -Vitoto ● Susu-kitambaa cha kuzuia haja za mtoto. ● Akavimba-akawa mjamzito ● Kiwimbo.- wimbo mfupi Follow AtikaSchool.Org on our Social ChannelsThis gives you an opportunity to get our latest uodates, changes and firsthand information ushairi questions and answers pdfushairi pdf downloadushairi wa kiswahili pdfushairi noteskiswahili questions and answers pdffasihi simulizi questions and answers
0 Comments
Leave a Reply.Don't give up, Keep Searching for more |
AuthorAtika School Team Archives
January 2023
Categories
All
|