Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswaliDaima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa hamu Kushika mpini na kutokwa jasho Ili kujikimu kupata malisho. Anapotembea anasikiliza Videge vya anga vinavyotumbuiza Utadhani huwa vimemngojea Kwa usiku kucha kuja kumwimbia; Pia pepo baridi kumpepea Rihi ya maua zikimletea Nao umande kumbusu miguu; Ni miti yote hujipinda migongo Kumpapasa, kumtoa matongo; Na yeye kuendelea kwa furaha Kuliko yeyote ninayemjua Akichekelea ha ha ha ha ha ha ha … Na mimi kubaki kujiuliza Kuna siri gani inayomliwaza? Au ni kujua au kutojua? Furaha ya mtu ni furaha gani Katika dunia inayomhini? Ukali wa jua wamnyima zao Soko la dunia lamkaba koo; Dini za kudhani zamsonga roho Ayalimia matumbo ya waroho; Kuna jambo gani linamridhisha? Kama si kujua ni kutokujua Laiti angalijua, laiti angalijua! Maswali
majibu ya ushairi
(a) – Ukali wa jua unaharibu zao. - Soko la dunia ni mbaya. - Dini za kudhani zamsonga roho. - Analimia waroho au wenye pupa. (4x1) (b) Tashbihi – Katika njia iendayo kondeni - Kama walivyofanya babuze zamani. Balagha - Kuna jambo gani linamridhisha -Kuna siri inayomliwaza. Tanakali za sauti – Alichekelea ha ha ha ha … Taswira - videge vya anga vinavyotumbuiza Tashihisi – Nao umande kumbusu miguu. Msemo - kumkaba koo – kuumiza. Takriri - Laiti angalijua, laity angalijua. (4x2) (c) Mkulima (1x1) (d) Malalamishi/huruma (1x1) (e) Kuboronga sarufi - Kama mtu aliye na hamu kubwa. - Lahaja - kotama. (2x1) (f) Kila asubuhi anapita akiwa na jembe akielekea shambani. Kama walivyofanya babu zake.Ninapomuona huwa ana furaha kama mtu aliye na tamaa kubwa ya kulima na kutokwa na jasho ili apate kujilisha. (4x1)
0 Comments
Joseph Kiponda : Taifa ni UshuruLau kama ingakuwa, madhali tuna uhuru Watu kodi kutotowa, na kuifanya kufuru Vije nchi ingakuwa, taifa bila ndururu Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Hivi taifa kumea, nakuendelea mbele Kwamba lajitegemea, haliwategei wale Yataka kujitolea, ushuru bila kelele Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Wafanyikazi wa umma, mfano mwema walimu Wauguzi mahashuma, daktari wahadimu Bila hizi darahima, vipi wangalihudumu? Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Si vyema kuombaomba, kwa wageni kila mara Huwa twajifunga kamba, na kujitia izara Adha zinapotukumba, kujitegemea bora Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru. Miradi ya maendeleo, yahitaji darahima Ndo tufikie upeo, ulio dunia nzima Wadogo na wenye vyeo, bila kodi tutakwama Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Ushuru si kwa wanyonge, wasokuwa na uwezo Watozwe hata wabunge, na wengine wenye nazo Yeyote asijitenge, kodi akalipa bezo Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru Kwetu kutoa ushuru, ndiko kujitegemea Pasiwepo na udhuru, sio wa kuelea Huwa ni kama kiguru, asenao kutembea Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru. Maswali
MAJIBU
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.Maendeleo ya umma Sio vitu maghalani Kama tele vimesaki Lakini havishikiki Ama havikamatiki Bei juu Maendeleo ya umma Sio vitu gulioni Kuviona madukani Kuvishika mikononi Na huku wavitamani Kama tama ya fisi Kuvipata ng’o Maendeleo ya umma Sio vitu shubakani Dhiki ni kwa mafakiri Nafuu kwa mafakiri Ni wao tu washitiri Huo ni uistimari Lo! Warudia Maendeleo ya umma Ni vitu kumilikiwa Na wanyonge kupatiwa Kwa bei kuzingatiwa Bila ya kudhulumiwa Na hata kuhadaiwa Hiyo ni haki. Maendeleo ya umma Dola kudhibiti vitu Vijapo nchini mwetu Na kuwauzia watu Toka nguo na sapatu Pasibakishiwe na kitu Huo usawa. Maendeleo ya umma Watu kuwa na kauli Katika zao shughuli Vikaoni kujadili Na mwisho kuyakubali Maamuzi halali Udikteta la. Maendeleo ya umma Watu kuwa waungwana Vijakazi na watwana Nchini kuwa hakuna Wote kuheshimiana Wazee hata vijana. Maswali
majibumajibu
Soma shairi kisha ujibu maswali Nizike Ningali Hai!: Hassam Muchai Kipusa Binti Hamadi, siku n’takuwa kimba Nizikwe Kifudifudi, na yoyo kuyumbayumba Takuwa bure biladi, matozi ungayasomba Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Tena ningaumwa ungo, na mapumu kuugua Lioze ini na nyongo, na pua zisipumua Takuwa sina kinyongo, mradi nimeshatua Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Nizike sasa mwenzangu, nizike ningali hai Singojee kufa kwangu, uanze kurairai Kulilia kifo change, ni bure hakukufai Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Nikifa hutonizika, kimwana sanda nunua Manukato ya kupaka, na nguo za kuanua Nivishe sione shaka, Washindwe kupambanua Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika Tena nikande misuli, nikande pande kwa pande Siate kiwiliwili, shingo, miguu ikande Umalizapo kiwiliwili, mwenzangu niende shonde Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika MASWALI
MAJIBU
maswali 10 ya chaguzi zaidiHapa kuna seti ya maswali 10 ya chaguzi zaidi.
MAJIBU YA MASWALI 10 YA CHAGUZI
Hapa kuna majibu kwa maswali yaliyotolewa:
Soma shairi kisha ujibu maswali Ndugu ona mbwa yule, ambaye ananyekenya; Yaone mabuu yale, ambayo yamchezeya; Kuwa leo yuafile, mwili yanautaniya; Jana awile jasiri! Juzi shujaa awile, pasiwe kumfikiya; Kwenye makani yale, alipojisururiya; Leo kuwa yuafile, mainzi yamchekeya; Jana awile Jasiri! Mijino mikubwa ile, ambayo ‘mejitokeya; Yali kiwaliza wale, karibu walosogeya; Tena akibweka yule, waoga walijinyiga; Jana awile jasiri! Kamwe kuishi milele, kupe ukajinyonyeya; Walo chini yako wale, muhali unawaziya; Ameshindwa yule pale,sembuse wewe sikiya; Jana awile jasiri! Kama walo hai wale, yafaa kuzindukiya; Ni dunia maji male, muhimu kujiwaziya; Wazipunguze kelele, na kwingi kujishauya; Jana awile jasiri! Maswali
Majibumajibu
MASWALI 10 YA CHAGUZIHapa kuna seti ya maswali 10 ya chaguzi zaidi.
MAJIBU YA MASWALI 10 YA CHAGUZI
Hapa kuna majibu kwa maswali yaliyotolewa:
Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.
Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani Hiani pamwe ukora wenye kuhini. Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli. Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele Muwele wa hitilafu, hitilafu ya nduwele Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale. Vishale vinitomele, vitomele vikwato Vikwato pia maole, maole kufanya mito Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto. Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka Kutamka wazi vino, vino subira kutaka Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka Wahaka wa matukano, matukano na mashaka. Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita Kunikita salamani, salamani nikadata. Maswali
a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani? (al.2)
b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia (al.4) (i) Mpangilio wa maneno (ii) Mpangilio wa vina. c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4) d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (al. 4) e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (al.6) Majibu
(a) Ili asiwe na wasiwasi ya kutukanwa na huhiniwa aepuke kufanyiwa mabaya. 1 x 2 =2
(b) (i) Pindu/mkufu/nyoka (al.1) Kwa sababu neno la mwisho katika mshororo wa mwisho wa ubeti linatumiwa kuanzia ubeti unaofuata. (al. 1) (ii) Ukaraguni (al.1) Vina vya kati na vya mwisho vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. (al.1) (c) (i) Tashbihi - Hafifu kama muwele - Tele mithili kitoto.(al.2) (ii) Uradidi/Takriri - Subira’ - Bora, kombora, ukora - Kiburi, kudhuri n.k.(al.2) (d) (i) Misuli kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa. (ii) Hasa mgonjwa mwenye tatizo la (iii) Ambao unasumbua sana daima na (iv) usiopona kwa vishale. (zote4 x 1 = 4) (e) (i) Inkisari - kuleta urari wa mizani k.m kilo — kilicho. (ii) Tabdila - kuleta urari wa vina k.m. kudhuri — kudhuru maole — maozi. - Kuleta urari wa mizani k.m nduwele — ndwele muwili — mwili (iii) Mazida - kuleta urari wa vina pia mizani. - Vinitomele - vinitome. Kutaja na matumizi (al.1) Mfano (al.1) Zote 3 x 2 = 6
Mkatanimkatika, harithihatorithiwa
Sinaninalolishika, walaninalochukuwa Mlimwengukanipoka, hata tone la muruwa! Mrithininiwanangu? Sinango’ombesinambuzi,sinakondesinabuwa Sinahatamakaazi, mupasayokuyajuwa Sinamazurimakuzi, jinsinilivyoachiwa Mrithininiwanangu? Sinakazisinabazi, ilawingiwashakawa Sinachembeyamajazi, mnonikukamuliwa Nakwa’cheniupagazi, mgumukwenuku’tuwa Mrithininiwanangu?
Sinasikuachajina, mkatahatasifiwa
Hatanifanye la mana, mnonikulaumiwa Poleniwanangusana, sinakwenu cha kutowa Mrithininiwanangu? Sinaleosinajana, sinakeshokutwaliwa Sinazizisinashina, walatawikuchipuwa Sinawanangu mi sana, la kwacha nakuraduwa Mrithininiwanangu? Sina utu sinahaki, milayangumeuliwa Nyumayanguilidhiki, nambeleimekaliwa N’nawananamikiki, hadin’tapofukiwa Mrithininiwanangu? Sinai la keshokwenu,wenyewekuiongowa Muwanekwanyingi,mbinumwendepasikupuwa Leo siyo, keshoyenu, kamamutajikamuwa Mrithininiwanangu? (Kina cha maisha A.S.Mohammed) MASWALI
MAJIBU
a) Hali yamzungumzaji. (al 4)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Hukuja hapa kwa wingi,
Vitimbi vya kila namna, Kunambia nikuruzuku, Kimwana awe mwenzio, Hukumtwaa mwanangu, Kisema mno walavu, Vipi wangeuza ngoma, Mapepo wampigia? Siwe uloandaa, Harusi ya kukata na shoka, Masafu ya magari, yakilalama jua kali, Hadi kanisani kungia, mimbari wa kusimama, Kasema utamuenzi, hadi yenu mauko? Vipi jicho lageukia, mitaani vipaa mwitu? Hukunabia we fidhuli, Mwanangu utamtunza? Taandamana naye daima, Ja chanda na pete? Hukumwonjesha tamu, ya ulaghai huyuno? Midisko wampleka, kizingizia mapenzi, Vipi wamtezea shere, mwangu kumliza?
Lini taacha dhuluma hizino humfanyiazo,
Tuchukua lini majukumu, Ya kumlea na vifaranga? Huachi kulia u waya Wanao kitelekeza Nadhiri zako za nitakipu promise, Zi wapi mwana balaa? Lini tafumbua maozi, uone huyu nduli, Alotwala wengi wapendi, Kwa jicho la nje kuwangia, Imeanguka miamba mingapi, nayo ngangania kufia dodani, Zinduka mwana zinduka, Ailayo waangamiza. Maswali
majibu
Shairi la pili Majibu
Soma shairi hili kisha ujibu maswali
Naingia ukumbuni,nyote kuwakariria
Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia Mnipe masikioni, shike nachoelezea, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Naaanza kwa usalendo, nchi yetu tuipende, Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuilinde, Wa kila mtu muwendo, usije kawa mpinde, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Wote tuwe na umoja, tuuache ukabila, Kabila lisiwe hoja, mwenza kunyima hela, Taifa letu ni moja, Mkenya ndilo kabla, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Linda demokrasia, uongozi tushiriki, Haki kujielezea, wachotaka na hutaki, Change naweza tetea, demokrasia haki, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili Tena adili usawa, mgao rasilimali, Bajeti inapogawa, isawazishe ratili, Idara zilizoundwa, faidi kila mahali, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Tuwe na uadilifu, twache tamaa ya hongo, Tusiwe na uadilifu, wa kuwa watu waongo, Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Ubinafsi si adili, ila ni kusaidiya, Ukiwa nayo maali, asiyenacho patiya, Kama mtu mswahili, ubinafsi achiya, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Na invyoelezea, katiba ni kielezi, Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi, Kwa hayo nitawachia, hiyo ya ziada kazi, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. MASWALI
MAJIBU
SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI MODEL25122022001
Ulimwengu ulimwengu, ulimwengu naratibu
Yaliyo kichwani mwangu, nataka kuyatubu Wayasome ndu zangu, wa mbali na wa karibu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ulimwengu ni kiwanja, cha wenye raha na tabu
Wengine wanajikonja, kwa wengine ni adhabu Kucha na kutwa twahanja, kutafuta matulubu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa balaa, aliniusia babu
Mna mambo yamejaa, ya faraja na kusibu Na machache ya kufaa, ila mengi ya udubu Cha wenye raha na tabu,ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja cha Amina,Saidi Ali Rajabu
Wengine kitu hatuna, tunaishia kababu Wale wamejaza sana, wanashindwa kuhesabu Cha wenye raha na tabu, Ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa urongo, na kweli pia ajabu
Kichwa hudanganya shingo, tumbo kiuno chasibu Usitumai ubongo, wa nduguyo na swahibu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa walevi, pombe kwao ni dhahabu
Mara vile mara hivi, wakilewa majudhubu Maneno ya kiujuvi, hujipaka hata shabu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja wenye dini, wamtiio wahabu
Mashekhe msikitini, humo humfanya muhibu Mapadiri kanisani, huvihubiri vitabu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa malofa, lofa mtu mwenye tabu
Kusema sana kashifa na moyo kisebusebu Tunakaribia kuja, kwa kushindwa kujimudu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa faraja, alowajali habibu
Na wengine sitotaja, msinambe ninagubu Ni uwanja wa viroja, vigumu kuvikutubu Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja. maswali(a) Lipe shairi hili anwani ifaayo. (alama 1)
Ulimwengu ni kiwanja
Changamoto ulimwenguni 1 x 1 = alama 1 (b) kwa kutoa mfano, eleza mbinu zozote mbili za lugha zilizotumika katika shairi.(alama 2)
(b) Istiara/ jazanda – ulimwengu ni kiwanja
Msemo – kutwa kuchwa Ukinzani/tanakuzi – wenye raha na tabu Uhuishaji – Kichwa kudanganya shingo (zozote 2x1 = alama 2) (c) Eleza jinsi uhuru wa mshairi ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
(c) Inkisari – naratibu – ninaratibu
Ndu zangu – ndugu zangu. Kuboronga lugha – wenye kitu hatuna – wengine hatuna kitu Utohozi – shehe – sheikh Padre – padre (2 x 1 = 2) (d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (alama 4)
(d) babu alimshauri kuwa ulimwengu ni uwanja wa balaa ulionjaa mambo ya faraja na kusibu. Pia alisema kuwa kuna machache ya kufaidi na mengi ya kuudhi. Kwa hivyo ulimwengu ni kiwanja kwa walio na raha na walio na taabu.
(4x1 = alama 4) (e)Taja na ueleze bahari zozote mbili zilizotumika katika shairi hili.(alama 2)
(e) (i) Tarbia – mishororo minne kwa kila ubeti
(ii) Mathnawi – vipande viwili kwa kila mshororo (iii) Pindu – sehemu ya mwisho kuanzia ubeti unaofuata. (iv) Ukara – vina vya mwisho vinatirirka na vya kati havitiririki. (2x1 = alama 1) (f) Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
(f) (i) Mishororo minne kwa kila ubeti
(ii) Vipande viwili kwa kila mshororo – ukwapi na utao. (iii) Lina beti tisa. (iv) Vina vya mwisho vinatiririka na vya kati vinabadilika (v) Lina kibwagizo – che wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja. (vi) mizani ni 8,8 kwa kila mshororo 4x1 = 4 (g) Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
(g) masikitiko (alama 1)
(h) Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 2)
(h) Kufahamisha watu hali ilivyo ulimwenguni. Kwamba kuna mazuri na mabaya ili wajihadhari. (1x2= 2)
(i) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.(alama2)
|
AuthorAtika School Team Archives
December 2023
Categories
All
|
Can't find what you are looking for? Don't worry, Use the Search Box Below.
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |